Friday, August 26, 2016

KWANINI MUHAMMAD ALITAKA KUJINYONGA “COMMIT SUICIDE”?



1. MUHAMMAD ALITAKATA KUJINYONGA
2. MUHAMMAD ALIPANDA MLIMANI NA KUJARIBU KUJIRUSHA ILI AFE
3. AISHA ASEMA MUHAMMAD ALIKUWA AMEROGWA
Ndugu msomaji,
Tunaposoma Biblia tunajifunza kuwa Mungu aliwapa Unabii na Utume watu wake kwa njia ya upendo. Lakini nilipo soma vitabu vya Allah nilikutana na mambo ya ajabu sana.
Bila ya kupoteza muda, ngoja niweke vitabu vyake ili na wewe ujisomee mwenyewe. Maana Waislam huwa wanadai eti nawasingizia au namzulia uongo Allah.
KATIKA SAHIHI BUKHARIY TUNASOMA KUWA MUHAMMAD ALIJARIBU KUJINYONGA KWA SABABU YA HUZUNI KWENYE NYOYO YAKE:
Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: Wao watanifukuza? Riwaya inaendelea kwa yanayoshangaza zaidi kuliko hayo Waraqa bin Naufal alipomkuta MTUME AKIJARIBU KUJINYONGA KWASABABU YA HUZUNI yake kwa kukatika Wahyi, kama si Jibril kumtuliza mara hii baada ya kuwa Waraqa bin Naufal akifanya hivyo. Sahihi Bukhariy J:9 uk 93 kita Ta’abiyri
Swali la kujiuliza hapa ni hili: Hivi wapi tunasoma kwenye Taurat au Zaburi au Injili kuwa Mitume wa kwenye Biblia walijaribu kujinyonga kama Muhammad wa kwenye Quran?
Nilipo endelea kusoma vitabu vya Waislam nikagundua kuwa, hilo tukio la kujaribu kujinyonga “commit suicide” halikufanywa mara moja na Muhammad ambaye ni Nabii kipenzi cha Allah.
MUHAMMAD ALIPANDA MLIMANI NA KUJARIBU KUJITUPA ILI AFE, JE HII TABIA YA KUTAKA KUJIUA NI YA KINABII? Soma hiki kisa hapa chini:
Kisha Waraqa hakuchukua muda akafariki na Wahyi ukakatika kwa muda na Nabii (s.a.w.w.) akahuzunika, ambapo katika yaliyo tufikia mara nyingi huzuni ilipelekea kutaka kujirusha kutoka katika vilele vya milima, lakini kila alipopanda mlima ili ajiangushe Jibril alimtokea na akamwambia Ewe Muhammad “Hakika wewe ni Mtume wa kweli wa Mwenyezi Mungu, basi kwa hayo inapoa hasira yake na nafsi yake inatulia na anarudi na unaporefuka muda wa kutopata Wahyi anarudia hayo, na anapofika kwenye kilele cha mlima Jibril anamtokea na kumwambia mfano wa aliyomwambia. J: 8 uk 234 kitabu Daawaati

Umesoma mwenyewe ushahid kutoka vitabu vyao kuwa Muhammad alitaka kujinyonga na au kujiua au kuitoa nafsi yake. Hii ni ishara tosha kuwa yule anaye daiwa kumpa wahai ni Shetani na sio Mungu wa kwenye Biblia ambaye ni wa upendo. Lakini nilipo endelea kusoma vitabu vyao, nikagundua kuwa labda haya matatizo yanatokana na kurogwa kwake Muhammad. Hebu soma kwanza hiki kisa cha Muhammad kama kinavyo simuliwa na mke wake kipenzi Aisha:
Kutoka kwa Aisha amesema:- Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alilogwa hadi alikuwa anapagawa kuwa amefanya kitu kumbe hakukifanya hadi siku moja alipokuwa kwangu alimuomba Mwenyezi Mungu akamjibu, kisha akasema ewe Aisha umehisi kuwa Mwenyezi Mungu amenijibu nilivyomuomba. “ “ J: 8 uk 56 kitabu Adabu
Nabii (s.a.w.w.) alibaki siku kadhaa wa kadha amepagawa kuwa amemwingilia mke wake na wala hakumwingilia. Al –fruqaan 25
UMESOMA MWENYEWE KUWA MUHAMMAD ALIKUWA AMEROGWA na niajabu sana kwa Nabii wa Allah kurongwa huku Allah akimwangalia tu na kuto fanya chochote kile. Nilipo isoma Biblia Takatifu, sikuwai soma kuwa kuna Nabii wa Jehovah ambaye alirogwa kama Muhammad wala ona kuwa kuna Manabii walitaka kujinyonga kama Muhammad wa kwenye Quran.
Nilipo endelea kusoma vitabu vya Waislam, nikagundua kuwa kumbe Muhammad alikiri kuwa yeye ni mwendawazimu: Soma huu ushuhuda wa Nabii wa Allah:
The "Kitab al-Tabaqat al-Kabir", (Book of the Major Classes), by Ibn Sa'd, kimetafsiriwa na S. Moinal Haq, [4], Ukurasa 225 Nabii Muhammad anasema:
O Khadija, ninaona mwanga na kusikia masauti sauti, nafikiri mimi ni Mwendawazimu.
Kwenye tafsiri zingine zinasema kuwa Muhammad alisema anafikiria kuwa yeye ni “KICHAA”
Je, huu ushuhuda inawezakana kuwa ulitokana na kupigwa kwake kabali na Jibril kwenye pango:
MUHAMMAD AKIRI KUPINGWA NA KUBANWA MBAVU ZAKE NA KIUMBE AKIWA PANGONI,
Katika kitabu kiitwacho: Maisha Ya Nabii Muhammad s.a.w uk 16-17 kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy, tunasoma kama ifuatavyo;-
Hata siku moja- katika mwezi wa Ramadhani mwezi 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 ½ wa umri wake- mtume alimwona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumwona wapi katokea, akamwambia; “soma”. Mtume akamjibu; “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujifundisha kusoma.” Akaja akamkamata akambana, akamwambia tena; “soma,” Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tau akamwambia; “soma- Iqraa Bismi Rabbik.” Akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake. Kisha mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika Qur’an, ingawa haijawekwa mwanzo.
Mara, yule mtu (Malaika) akaondoka machoni mwake- asimwone kenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake-khofu imemshika. Alipofika nyumbani, Bibi Kadhija alidhani ana homa, akamfunika maguo gubigubi na akakaa mbele yake akimsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia alimweleza Bibi Kadhija yote yaliyomtokea; na Bibi Kadhija akamtuliza moyo wake, akamyakinishia ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu akaondoka akenda kwa jamaa yake – Bwana Waraqa bin Naufal- akampa habari yote iliyompata mumewe. Naye akamwamrisha amwite. Na mtume akenda akamweleza habari yake yote. Bwana Waraqa akamwambia; “ Huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa. Basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu, nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako; Inshaallah nitakuwa mkono wako wa kulia” Wakarejea kwao na khofu yote imemtoka”.
Alipokuwa pangoni alichezewa na Shetani: Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
Umejisomea mwenyewe visa vya Muhammad aliye tajiribu kwa mara kadhaa kuitoa nafsi yake na au kujinyonga.
Kulingana na Biblia, kujiua si kigezo cha kukufanya uingie mbinguni. Mtu asiyeokoka akijiua huwa amejipeleka moja kwa moja katika ziwa la moto. Biblia inataja watu wanne waliojiua: Sauli (samueli wa kwanza 31:4), Ahithofeli (samueli wa pili 17:23), Zimri (wafalme wa kwanza 16:18), na Yuda (Mathayo 27:5). Kila mmoja wao alikuwa mwovu na mwenye dhambi. Biblia inachukulia kujiua sawa na kuua – na hivyo ndivyo ilivyo – kujiua mwenyewe. Mungu ndiye ni aamue lini na vipi mtu afe. Kuchukua jukumu hilo mkononi mwako kibiblia ni kufuru kwa Mungu.
SASA WAISLAM, NIONYESHENI, wapi kwenye Taurat, au Zaburi au Injili kama kuna Mtume aliye na sifa za ajabu kama za Muhammad, sifa za kujaribu kujinyonga?
Karibuni kwa Yesu ambaye ndie Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 12, 2016
http://www.maxshimbaministries.org/…/kwanini-muhammad-alita…

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW