Friday, August 26, 2016

JINA LA ISA BIN MARYAM HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA AU KUPONYA MAGONJWA

SHALOM TENA,
Kwa mara nyingine twamshukuru Yehova Mungu kwa kutupa neema hii tena ili tuweze kukufikishia ujumbe huu wa Biblia na kweli zake.
Kwa muda wa miaka mingi sana pia duniani pote imekuwa ni kawaida kuwasikia waislamu wakifundisha watu wao na kuwadanganya bila ya wao kujuwa ao wengine wakiwa wanakijuwa wanachokifanya kuwa ISA bin Maryam’ Kama Qurani inavyofundisha ndiye “YESU KRISTO”.
Mafundisho haya hivi sasa yanaendeshwa kwa kulinganisha aya za Biblia na Qurani. Ma sheihk, ma Imam na wahubiri wengi wa dini ya kiislamu wanaendesha mihadhara kwa uwingi duniani. Wahadhiri hao pia hutumia mbinu zingine mbali-mbali kama majarida na kurekodi kanda za audio na video, ambazo zimesababisha baadhi ya wakristo nusu au wakristo wajinga waamini kuwa Isa Bin Maryamu ndiye Yesu Kristo. Swali la msingi kwa wakristo wote;Je, ni kweli Isa bin Maryam ndiye Yesu Kristo?
Katika hadithi Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu namba 1, Hadithi namba 104 ukurasa 64 “Hadithi ya Ibn Abbas kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema:
“Nilimuona Musa katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa, naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua. Na nilimuona Isa, naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……”
Lakini YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU.
Mdo 4:9-10, 12
“kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya vipofu na mmoja wao ni Batromayo.

Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao? Yesu Kristo alimfufua Lazaro.
Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa bin Maryam lisilokuwa hata mbegu moja ya wokovu limehusishwa na jina la Yesu Kristo wetu namna gani?
Mdo 16:31 “Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.”
Naamini wengi wenu hapo wawe ni waislam au siyo tumeshakubaliana na maandiko toka pande zote mbili kwamba ISA BIN MARYAM WAO SI MWANA WA MUNGU kama tulivyopata ushahidi katika Suratul Al An-Am 6:101 “Yeye ndiye Mwumba wa mbingu na ardhi. Inawezekanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu”.
Qurani Suratul At-Tawba (Kutubu), 9:30 “Na Mayahudi wanasema “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu” na “Wakristo wanasema “Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu” Haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!
Fundisho la Uwana wa Mungu kama Biblia inavyofundisha, halimo katika mafundisho na itikadi ya dini ya Kiislamu kwa hiyo Isa wao siyo mwana wa Mungu.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW