Tuesday, August 2, 2016

JE, UNAZIFAHAMU KAFARA ZA KIMASHETANI?



Utangulizi:
Kwa akili zawatu zilivyo, wakisikia neno kafala wanakimbilia kwenye waganga wa kienyeji, lakini neno hili kafara kwenye Biblia ndio linaitwa dhabihu kwenye Biblia, kuna maadiko kadhaa yanayo taja kafara kwenye Biblia kama ifuatavyo :- Mambo ya Walawi 2 :2, 9, 16; Mambo ya Walawi 10:13, 14, maandiko haya yanataja neno kafara kwenye Biblia na limeonekana mara nyingi, hii ni kukuonyesha kuwa neno kafala lipo kwenye Biblia na lina maana sahihi, kwahiyo Kafara ni Sadaka inayotolewa kwa ajili ya kupokea jambo fulani kutoka ulimwengu wa roho aidha kwa Mungu au kwa Shetani.
Maana ya Kafara:
KAFARA NI SADAKA INAYOTOLEWA KWA AJILI YA KUPOKEA JAMBO FULANI KUTOKA ULIMWENGU WA ROHO, AIDHA KWA MUNGU AU SHETANI.
KUWA MAKINI NA KAFARA ZILIZOTOLEWA KWA MASHETANI
Kumbe shetani anaweza kutolewa kafaraza aina mbalimbali inaweza kuwa ya vinywaji, uji, nafaka, harufu, watoto au watu wazima; na ni muhimu kuwa makini sana na kuhudhuria sherehe ambazo si za ki Mungu kwasababu waweza kujikuta unashiriki kwenye sadaka hiyo. Kuna watu ambao matatizo yao yamewaanza baada ya kushiriki chakula cha kafara jambo hili Biblia imekataza kwasababu ya madhara yake.
Ufunuo 5:8; 8:3 hapa Biblia inataja Sadaka ya harufu, na ndio maana ukienda kwenye maduka mengi utakuta wameweka vitu vinaitwa ubani; Hii ni Sadaka au Kafala ya kuteketezwa kwa majini, Isaya 43:23; Yeremia 6:20; 17:26, Ubani na Udi ni Sadaka ya kuteketezwa, kimsingi; ile harufu ndiyo inayoifanya iitwe Sadaka ya kuteketezwa, kwahiyo mtu unayemuona anachoma ubani ni anakuwa anatoa kafara ya ubani. Nehemia 13:9. Sadaka za unga na Sadaka za ubani. Kimsingi watu tuliookolewa hatutoi sadaka za ubani kwasababu Biblia inasema maombi ya watakatifu ndio sadaka ya harufu kwa Mungu, Yohana 19:39.
Kumbe unapoona mahali au duka ukakuta wanachoma udi kimsingi ni kwamba wanaita Mashetani ambayo yanawasaidia kuleta wateja. Na ndio maana maduka mengi yana kuwa na vitu hivi ambavyo ni kafara au sadaka ya harufu; ili majini yaite wateja. Na ndio maana watu wengi wenye majini wanapenda ubani kwasababu kile ndio chakula chao.
WATU WENYE WIVU WANAWEZA KUKUTOA KAFARA
Ndugu zangu kuna watu hata hawapendi kukuona unakula vizuri, au unapika vizuri au unasomesha.. na akiona huo wivu anaamua kwenda kukufanyizia kwa mganga wa kienyeji..ambapo ataambiwa atoe kafara kwa ajili ya kukuangamiza wewe..
1 Wakorintho 10:20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
Zaburi 126:38 kumbe kuna uwezekano wa watu kutoa kafara kwa mashetani. Na biblia inalikubali hili kupitia maandiko hayo tuliyoyaona hapo. unaweza kuwekewa pepo la udhaifu kupitia kafara.
Luka 13:10 Pepo wa udhaifu.. mtu anaweza kukutolea kafara ili ufe kifo cha Ghafla.
KWELI KUHUSU KAFARA:
Mtoto au mtu akitolewa kafara anakuwa ameuwawa Mwili na kupewa majini au mashetani, katika Biblia shetani anayehusika na mambo ya kafara, Mambo ya Walawi 18:21; ukisoma Biblia ya Kiswahili unaweza ukahisi moleki ni mtu lakini tuangalie kwenye Biblia ya kingereza “do not give out your children to be sacrifices..” Mambo ya Walawi 20:2 “who sacrifices.. kumbe inawezekana unaumwa na upo kwenye ugonjwa kumbe ndio unatolewa kafara hivyo..
Kumbe sasa waweza kumwona mtu amekufa na ugonjwa Fulani kumbe ni kafara, mwingine anatoa kafara kwa ajili ya utajiri. Mambo ya Walawi 20:3, pia tunaona kuwa kumbe wachawi hawa wanatoa ndugu na si mtu ambaye hamjui. Yaani kama una ndugu wa karibu au wa mbali ambaye ni mchawi, Yule ndiye anayeweza kukutoa kafara, na kwenye kitabu cha Mambo ya walawi shetani aliyekuwa anahusika na kafara aliitwa Moleki. Walawi 20:4,5 2Wafalme 20:10
Hayo maandiko ni ya agano la kale lakini pia katika agano jipya jambo hili limetajwa pia; 2 Wakorintho 10:20 “.”
NGUVU YA KAFARA:
Unaweza ukajiuliza kafara inafanyaje kazi; kimsingi; sadaka au kafara ya vinywaji, damu au vyote tulivyoona ni chakula cha Mashetani. Na kimsingi mashetani yapo katika ngazi mbalimbali kuanzia majoka mpaka kwenye majini majini madogo; kwahiyo wachawi au washirikina huita mashetani kulingana na ukubwa wa kafara kama ikitolewa kafara ya kuku anakuja shetani wa ngazi ndogo. Na ikitolewa kafara kubwa kama ya mtu inaliita shetani la ngazi ya juu sana. Hivyo kama mtu hajaokoka ni rahisi kutolewa kafara kwasababu anakuwa hana ulinzi wa Mungu.
Unapomkubali Yesu unakuwa umejiunganisha na mauti ya Yesu hivyo hakuna haja ya kutoa kafara tena. maana Yesu alifanyika kafara kwa ajili yetu na damu ya Yesu ilimwagika ili kutufungua wote na Yesu alipigwa na kufa ili sisi kutookoa kama kafara kwaajili yetu.. watu wa dunia wanaweza kwenda kwa waganga na kutoa kafara lakini sisi tuna Damu ya Yesu ambayo ni nguvu ya madhabahu yetu..
Hivyo sasa kwa kutumia damu ya Yesu unaweza sasa kuharibu kafara na madhabahu zao zote, ukishughulikia madhabahu na kafara unakuwa umeiangamiza nguvu ya madhabahu nza kishetani na tatizo ulilonalo litakwisha .. kwahiyo ni muhimu kuharibu makuhani wa madhabahu yaani wachawi na waganga, madhabahu yenyewe yaani wanapokusanyikia, inatubidi kubomoa kafara yao, nguvu yao na pia Mungu wa madhabahu zao ambazo ni shatani.. na hapo utapata ushindi mkamilifu..
Mathayo 17:14 utajiuliza inakuaje, Yesu anaamua kumtoa pepo wakati tatizo lake lilitajwa ni kifafa, hapo utagundua kuwa matatizo ya watu wengi yanatoka na mapepo au majini yanayo tumwa na kumfanya awe vile alivyo.. lakini unatakiwa ushughulikie madhabahu na mambo yanayofuatana nayo.
Barikiwa sana,

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW