Hili ni swali nyeti sana na huenda ndilo msingi wa sababu hasa za
baadhi ya watu katika ulimwengu wa dini kupinga fundisho hili la
kweli la Kibiblia juu ya Utatu Mtakatifu na Uuungu wa Bwana Yesu.
Hoja kubwa katika sehemu hii inaonekana kuwa ni ya kimahesabu
zaidi ambapo jamii ya wale wanaopinga utatu mtakatifu hudai kuwa
haiwezekeni Baba, Mwana na Roho mtakatifu yaani mamlaka tatu
kuwa Mungu mmoja. Yaani hiyo ni sawa na kusema 1 + 1 + 1 = 3
na siyo 1’ kwa hiyo Baba + Mwana + Roho Mtakatifu = Miungu
watatu.
Kwa mtazamo huu ninalazimika katika sehemu hii kushughulika na
dhana ya kimahesabu zaidi ili kuona kama madai hayo ni sahihi na
kama yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa kifarsafa katika maandiko. Katika kulipatia swala hili ufumbuzi ni vyema tukaongozwa na mtazamo
wa kimaandiko kupitia fungu la kitabu cha ISaya…
Isaya 55:8
Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia
zangu; asema Bwana
Hiyo ni tahadhari ya msingi sana katika kushughulika na mada hii,
Mungu mwenyewe katika kitabu hicho cha Isaya anaweka bayana
kuwa katika utendaji wake njia anazozitumia hutofautiana sana na
njia zetu za kibinadamu na hata mawazo yetu yako tofauti na mawazo
yake. Ukweli wa tamko hilo la Isaya tunaweza kushuhudia katika
kipengele hiki cha uchambuzi ambapo kama utakumbuka hoja ya
msingi ya upinzani juu ya Utatu mtakatifu imejengwa katika kile kinachoonekena
kuwa nafsi tatu haziwezi kuwa Mungu mmoja kwa kuwa
moja jumlisha moja jumlisha moja jumlisha moja ni sawa na tatu
(1+1+1 = 3).
‘Hebu tuichunguze hesabu hiyo (Nafsi tatu - Mungu Mmoja)
katika maandiko’
Baba Mwana/Neno
Roho Mtakatifu Mungu mmoja
Elohim’
Mafundisho na mifano mbalimbali ya kimaandiko katika Biblia vinaweka
bayana juu ya usahihi wa fundisho hili la kweli na la msingi
katika Ulimwengu wa imani ambapo kama hatua ya juu zaidi ya uwazi
wa fundisho hili maandiko ya Biblia yanaweka bayana usahihi wa jibu
la Mungu mmoja toka katika hesabu ya nafsi tatu za Mungu .
Fuatilia mifano na uchambuzi huu:
-
Umoja katika wingi ‘A’
Ushahidi wa kwanza wa msingi juu ya Mungu mmoja katika nafsi tatu
ni ule unaotoka katika kimya cha Mungu mwenyewe kama
tunavyosoma katika andiko la kitabu cha Mwanzo;-
Mwanzo 1:26-27
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani,
na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi.
Sehemu hiyo ya kwanza ya andiko hilo Mungu kwa kutumia tamko la mfumo wa uwingi yaani utatu mtakatifu kama tulivyoona hapo awali
anasema ‘Natuumbe mtu kwa mfano wetu’. Ni wazi kuwa tamko
hilo linatoa taswira ya uwingi, lakini kile kinachoonyesha kuwa uwingi
huo hubeba tu dhana ya upana wa utendaji wa Mungu mmoja katika
nafsi tatu na si miungu watatu, ni tamko linalofuata katika aya ya 27
ya kitabu hicho cha Mwanzo..hebu tuisome:-
(27 ) Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa
Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Haya hebu ona sasa’, tamko la awali lilibeba dhana ya wingi pale
Mungu aliposema ‘Na tuumbe mtu kwa mfano wetu’ lakini tamko
linalofuatia linarejesha dhana ya umoja wa Mungu kwa kusema
‘Mungu akaumba mtu kwa mfano wake’.
Ni wazi kuwa kile kinachomaanishwa katika aya hizo mbili ni kuonyesha
kuwa uwingi au upana huo wa otendaji wa Mungu uko ndani ya
umoja wake na si badala yake kwamba nafsi tatu huzalisha aina
nyingine ya miungu na kuongeza idadi toka ile ya Mungu mmoja na
sasa kuwa miungu watatu.
“Uelewa juu ya Mungu katika zama za Wayahudi - Israel”
Ni vyema ikumbukwe kuwa tangu kipindi cha Wayahudi huo ndio
ulikuwa uelewa wa Wayahudi (Israel) juu ya Mungu.
Wayahudi walimtambua Mungu kwa jina la “Elohim” jina linaloonekana
kutumika zaidi ya mara 2.602 katika maandiko ya Biblia ambapo
jina hili ni la mfumo wa uwingi wa neno “Eli “(Mungu) hivyo neno
Elohim linabeba dhana ya uwingi ndani ya umoja. (It has connotations
of plurality).
Pamoja na uelewa huo bado mtazamo wa Wayahudi ulikuwa ni juu ya
ukweli wa Mungu mmoja tu na si zaidi, ambapo hapa tena Wayahudi
walikuwa na fundisho lililotawala sana la “Monotheistic” – Mono
kwa kiyunani humaanisha Moja’ na Theistic humaanisha Mungu.
Dhana hii ya Mungu hujengwa katika Biblia kupitia fungu ambalo
Wayahudi huliita Shema’ toka asili ya Kiebrania lenye maana Sikia”
ambalo ni:-
Kumbukumbu 6:4
Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja
Kupitia andiko hilo jamii ya Wayahudi ilijenga msingi wa imani usiotikisika
juu ya Mungu mmoja.
Lakini pamoja na hayo ikumbukwe kuwa dhana hii ya Mungu mmoja
pia ilizingatia asili ya Mungu katika utendaji wake wa nafsi tatu za milele kama tulivyoona msingi wake. Na hata katika fungu hilo la
shema’(kumb 6:4) tunaona dhana ya Mungu mmoja inatajwa kupitia
tamko ….”Bwana ndiye mmoja” ambapo neno lililotumika kumaanisha
‘mmoja’ ni neno la lugha ya asili ya Kiebrania
Echad’(mmoja).
Neno hilo ‘Echad’yaani ‘mmoja’(muunganiko – to be united) bado
hubeba dhana ileile ya umoja ndani ya uwingi kwa kile kinachoonekana
kuwa neno hilo hilo Echad’ ndilo lililotumika kumaanisha umoja
katika farsafa ya muunganiko wa wanandoa wa jinsia mbili yaani
mume na mke kama tunavyosoma katika:-
Mwanzo 2:24
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake
naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja
(echad’).
Neno hilo’..watakuwa mwili “mmoja’ neno ‘mmoja’ hapo limetafsiriwa
toka kwenye neno lilelile la Kiebrania lililotumika kueleza umoja
wa Mungu (Echad), hivyo kwa mtazamo huo ni kumaanisha kuwa
dhana ya umoja huu hujengwa katika matokeo ya muunganiko wa
vitu zaidi ya kimoja na hivyo hueleza utendaji wa upana wa nafsi zaidi
ya moja za Mungu.
Katika kuendelea kujibu swali hili hebu tuone mifano mingine kadhaa
juu ya uwezekano wa nafsi tatu kuwa Mungu mmoja, ambapo kama
tulivyoona upande unaohoji swala hili umejikita kwenye dhana ya
kimahesabu zaidi, kuwa je’ moja jumlisha moja jumlisha moja
jumlisha moja yaweza kuwa moja?, hebu sasa twende mbele zaidi
kwa kungalia ushahidi mwingine wa kimaandiko utakaotusaidia kwa
uwazi kupata jibu la msingi juu ya umoja katika nafsi tatu.
Umoja wa Mungu katika nafsi tatu ‘B’
2Petro 3:8
Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana
siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku
moja
Hili ni andiko muhimu sana katika mchakato wa kujibu hoja hii yenye
sura ya kimahesabu, kama ilivyo hoja yenyewe andiko la Petro nalo
linavunja dhana hiyo kwanza kwa kuonyesha kuwa mahesabu ya
Mungu na ya mwanadamu ni tofauti sana, yani kile tunachoona kuwa ni wingi kwetu kama wanadamu kwa Mungu siyo wingi. Rejea upya
sehemu ya kati hadi mwishoni ya andiko hilo la 2Petro 3:8‘…kwa
Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama
siku moja.
Ili kupata urahisi wa ufumbuzi wa hoja yetu tunaweza tukageuza
kidogo maneno hayo kwa kusema’ “kwa Bwana’ Mungu mmoja ni
kama na nafsi tatu, na nafsi tatu ni kama Mungu mmoja”.
Ni imani yangu kwa mfano huo ndugu msomaji wangu umeanza
kupata pambazuko la ufahamu juu ya hoja hii na kwa kadri
tunavyoendelea na uchambuzi huu kupitia maandiko na mifano
mbalimbali tutakayopitia ninaamini hutakuwa na shaka tena juu ya
uelewa wa fundisho hili muhimu la imani.
‘Muunganiko wa vitu zaidi ya kimoja unaozaa
kimoja’(plurality in unity)
Biblia inayo mifano mbalimbali juu ya uwezekano wa kuwepo kwa
muunganiko wa vitu zaidi ya kimoja lakini vikatengeneza kitu kimoja
kama tunavyoweza kuona katika aya zifuatazo:-
Mwanzo 1:5
Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa
jioni ikawa asubuhi, siku moja
Andiko hilo la Mwanzo linaeleza juu ya kanuni inayofanya kupatikana
siku moja’ kuwa ni muunganiko baina ya usiku na mchana au kwa
lugha nyingine nuru na giza ndivyo vinazaa siku inayoitwa siku moja
na siyo siku mbili.
Hivyo kwa maana nyingine haitakuwa sahihi kuchukulia kuwa muunganiko
wa nafsi tatu za Mungu unafanya miungu watatu na huku tukikubali
kuiita moja siku inayozaliwa na muunganiko wa hali mbili ya
giza na nuru katika mzunguko wa majira.
Hebu tufanye hesabu hii...,Usiku + Mchana = Siku
moja’ (Mwanzo 1:5)
Sasa tufanye nahii tena …. ,
Baba + Mwana +Roho = Mungu
mmoja’(1Yoh 5:8)
Nina amini kuwa sasa unaendelea kupata pambazuko juu ya mada hii
na hivyo hofu na mashaka yako vinaanza kutoweka. Hebu tupitie
andiko jingine kidogo;-
Ezekieli 37:17
Ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti
kimoja, viwe kimoja katika mkono wako.
Hilo ni agizo lililowahi kutolewa na Mungu kwa nabii Ezekieli ambapo
Mungu anamwambia Ezekieli achukue vijiti viwili na kuviunganisha ili
apate kijiti kimoja mkononi mwake.
Hivyo kwa msingi wa maelekezo hayo tunaona Biblia ikiweka mkazo
juu ya uwezekano wa kuzaliwa kitu kimoja au umoja toka kwenye
muunganiko wa vitu zaidi ya kimoja lakini kile kinachozaliwa kikaitwa
kimoja, hivyo dhana ya kutowezekana kwa nafsi tatu kumhusu Mungu
mmoja inaondolewa kabisa na maandiko haya ya haki ya Biblia takatifu.
Mifano rahisi
Utatu katika Yai’ – endapo utachukua yai na kulichemsha na
kisha baada ya hapo ukaanza kulimenya’ utagundua
kuwa ndani yake kuna vitu zaidi ya vitatu yaani
“Nganda gumu kiasi la nje, “Nyama laini nyeupe ya
ndani na “Kiini ambavyo kimsingi havijawahi kupelekea
mtu yeyote baada ya kumenya Yai hilo kudai
kuwa hayo ni mayai matatu, badala yake wote tunakiri
kuwa ni Yai moja tu pamoja na utatu uliyomo ndani
yake.
Hivyo mifano hiyo midogo itusaidie kurahisisha tafakuri zetu na
ugumu wa kuamini katika fundisho hili sahihi na la kweli la Utatu
Mtakatifu.
Lenzi mbili toka chanzo kimoja cha Jicho’ Pamoja na mfano huo
lakini mara kadhaa katika mahubiri yangu nimekuwa
nikitumia pia mfano wa macho kufafanua dhana ya
umoja katika katika wingi, katika mfano huu kwanza
nimekuwa nikihoji watu kuwa uwezo wao wa kuona
unatokana na asili ya macho mangapi! Ambapo wengi
wao wamekuwa wakijibu kuwa wanaona kwa asili ya
mambo mawili’ baada ya jibu hilo huwa ninawaomba
wale wanaodai kuona kwa asili ya macho mawili
watumie macho hayo mawili kuangalia kushoto na
kulia kwa wakati mmoja’ tendo ambalo hushindakana.
Kwa tafakari hiyo ndipo tunagundua kuwa
mwanadamu yeyote ana asili moja ya jicho au chanzo
kimoja lakini Mungu ametuwekea lenzi mbili ili kuwa
na upana wa kuona lakini chanzo au kontroo ya jicho ni
moja tu.
Kwa hiyo Mungu mmoja anaweza kujifunua katika nafsi zaidi ya moja
lakini bado hudumu kuwa Mungu mmoja lakini anayetenda katika
wigo mpana zaidi wa mamlaka.
Dunia ya Utatu’
Ni jambo linalonistua binafsi kwa jinsi Mwenyezi Mungu alivyoweka
ushahidi mwingi wa utatu hata katika muundo wa Kisayansi na wa
Kijografia wa Ulimwengu na hivyo ninachelea kwamba wale wanapinga
fundisho hili huenda hata sayansi ikawahukumu katika siku ya
kiyama juu ya mantiki ya upinzani huo.
Hebu ona jinsi nyanja mbalimbali za kisayansi na kijografia zilivyotawaliwa
viashiria au ushahidi wa kielelezo cha utatu:-
Ili kupata ’ World muungano wa Earth + Air + Sky
Ili kupata ’Universy muungano wa Mass + Space + Time
Ili kupata ‘Atom muungano wa Proton + Electron + Neutron
Ili kupata ‘Time muungano wa Present + Past + Future
Ili kupata ‘Sphere muungano wa Lithosphere+Hydrosphere
+Atmosphere
Ili kupata ‘ Number muungano wa Positive + Zero + Negative
Ili kupata ‘ Air muungano wa Nitrogen +Oxygen +Water
Ili kupata ‘water muungano wa Hydrogen x2’ na + 0xygen
Ili kupata ‘Music muungano wa Melody+ Harmon +Reazim
Kwa hali hiyo kile kinachoonekana ni kuwa’ farsafa ya utatu imetawala
sehemu kubwa ya jografia na uumbaji kwa jumla tendo ambalo binafsi
ninaliona kama kielelezo cha ushahidi wa uhalisia wa fundisho
hili la utatu mtakatifu,na kwa kwanamna nyingine ni jibu la vitendo
dhidi ya hoja za mtazamo wa kutowekana kuzaliwa umoja toka
kwenye wingi.
Utatu Mtakatifu katika ibada za viumbe wa mbinguni’
Ushahidi mwingine wenye nguvu ambao kimsingi ndiyo unaohitimisha
kipengele hiki cha uchambuzi ni ule unaohusu mfumo wa ibada za
mbinguni ambapo matamko yanayotolewa na viumbe hao
wanaoabudu huko mbinguni yanaweka bayana juu ya msingi mzima
wa Utatu wa Mungu hebu tusome katika andiko hili la Ufunuo wa
Yohana”-
Ufunuo 4:8
Na hawa wenye uhai wanne,
kila mmoja alikuwa na mabawa
sita; na pande zote na ndani
wamejaa macho, wala hawapumziki
mchana wala usiku,
wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu,
Mtakatifu, Bwana
Mungu Mwenyezi, aliyekuwako
na aliyeko na atakayekuja.
Hivyo ndivyo maandiko ya Biblia yanavyoweka wazi juu ya ibada hiyo
ya mbinguni ambapo viumbe hao wanaoabudu mbele za Mungu hutoa
matamko hayo yanayoweka uthibitisho na ushahidi wa wazi juu ya
utatu wa Mungu kwa kusema mara tatu Mtakatifu,Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na
atakayekuja.
Licha tu ya kutamka Mtakatifu mara tatu, lakini pia viumbe hao
wanaweka wazi sifa za walengwa wa utatu huo kwa kuwataja’ aliyekuwako
na aliyeko na atakayekuja. Kwa tafakari isiyo na ugumu
wowote utagundua kuwa sifa hizo husimamia nafsi hizo za Mungu ambapo
ile ya kwanza aliyekuwako – huonekana kumlenga Mungu
Baba, aliyeko - humlenga Roho Mtakatifu ambaye kimsingi ndiye
anayetawala sasa, atakayekuja - humlenga Yesu ambaye dunia inangoja kuja kwake mara ya pili na hata mbingu nayo inangoja kushuka
kwake duniani baada ya kumaliza kazi yake ya ukuhani wa
upatanisho katika hekalu la mbinguni na hatimaye kurejea na wateule
aliowakomboa mbinguni. Mungu akubariki kwa kuanza upya kujenga
ufahamu wako baada ya kupata ufafanuzi huu wa msingi toka katika
ushahidi wa neno la Mungu.
DARUBINI YA IMANI Na. Mchungaji Dominic Mapima
DARUBINI YA IMANI Na. Mchungaji Dominic Mapima
1 comment:
Hii article ilikosa hata comments, maana kama ulitoka yumbishwa kiimani Unakuta umerud Tena na Imani thabiti
Post a Comment