Friday, August 26, 2016

JE! MUHAMMAD ALIKUWA MWANAMKE?

‎Imeletwa kwenu na Frank Danford Noel‎:
Hili ni swali tu ambalo linasumbua kichwa changu kwa siku nyingi sana, hivyo LEO nimeamua kuweka wazi ili niweze kusaidika kwa watu wenye kujua! kwani me sijawahi kumuona Muhammadi kwa sura live, wala kwa picha yake halisi zaidi ya zile za kuchorwa ambazo hazina UHALISIA, hivyo nimemfahamu kupitia Vitabu vilivyoandikwa!
Pengine unaweza kujiuliza, kama vile ambavyo mimi nimejiuliza, kwa nini nimeuliza kuwa, Je! Muhammadi alikuwa mwanamke? wakati waislamu wanaamini kuwa, alikuwa mwanaume, baba wa watoto karibu sita, akiwemo Qasimu, Ibrahimu, na wengineo? mwanaume ambaye wao wanaamini kuwa, alikuwa na wake 11 ambao ni:
1) Bibi Khadija bint Khuwaylid
2) Bibi Sawda bint Zam'a
3) Bibi Aysha bint Abubakari
4) Bibi Hafsa bint Umar
5) Bibi Zaynab bint Khuzayma
6) Bibi Hindi bint Umayya
7) Bibi Zaynab bint Jahsh
8) Bibi Juwayriya bint Al Harith
9) Bibi Ramla bint Abi Sufyan
10) Bibi Safiyya bint Huyay
11) Bibi Maymuma bint Harith
Hao ndiyo wakeze ambao huamimiwa na waislamu kuwa ni wakeze Muhammadi, ambaye wao hawajawahi kumuona! sasa mimi nimetatizika hapa. 👇
KITABU CHA MAISHA YA NABII MUHAMMAD, MWANDISHI SHEIKH ABDULLA SALEH FARSY
Uk. 18 Paragraph ya Pili, Farsy ameandika!
"Akamfikiri Bwana Waraqa bin Naufal ambaye alikuwa amekwisha kufa siku zile. Akafikiri ile ahadi aliyompa kwamba atakuwa mkono wake wa kulia wakati atakaposimama kuwatangazia dini jamaa zake, mara akawaza shauri nyingine akajarejea kwa Mkewe Bibi Khadija akamsimulia habari hii. Pale pale bibi huyu akamwamini akawa ndiye mtu awali kushehedia shahada ya Uislamu. Basi Muislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke. Uso wake ulikuwa mabruki hakuwa ndiye mbwi wala ng'o bali alikuwa ndiye aliyekuwa mfunguzi wa mfuatano wa Uislamu. Hata leo wako Waislamu zaidi kuliko 400,00,000 Duniani"
👆 Hapo Sheikh Abdulla Saleh Farsy anatuambia kuwa, Muislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke, mfunguzi wa Waislamu Duniani neno Kabisa ni mkazo wa kauli kuonyesha kuwa, ni jambo ambalo lipo, lina ukwel, hivyo mtu wa kwanza kusilimu na kuwa muislamu wa kwanza DUNIANI, ni mwanamke kwa mujibu wa kitabu hicho cha Maisha ya Nabii Muhammadi, sasa isikilize Quran nayo inavyosema kwa habari ya muislamu wa Mwanzo.
( ﻗُﻞْ ﺃَﻏَﻴْﺮَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺃَﺗَّﺨِﺬُ ﻭَﻟِﻴًّﺎ ﻓَﺎﻃِﺮِ ﺍﻟﺴَّﻤَﺎﻭَﺍﺕِ ﻭَﺍﻟْﺄَﺭْﺽِ ﻭَﻫُﻮَ ﻳُﻄْﻌِﻢُ ﻭَﻟَﺎ ﻳُﻄْﻌَﻢُ ۗ ﻗُﻞْ ﺇِﻧِّﻲ ﺃُﻣِﺮْﺕُ ﺃَﻥْ ﺃَﻛُﻮﻥَ ﺃَﻭَّﻝَ ﻣَﻦْ ﺃَﺳْﻠَﻢَ ﻭَﻟَﺎ ﺗَﻜُﻮﻧَﻦَّ ﻣِﻦَ ﺍﻟْﻤُﺸْﺮِﻛِﻴﻦَ )
ﺍﻷﻧﻌﺎﻡ ‏( 6:14 ) Al-An'aam
Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.
Hapa tunaona kuwa, Muhammadi anaamrishwa awe wa kwanza kusilimu, ila kule tumeambiwa wa kwanza kusilimu ni mwanamke! Muhammad akaendelea kusema 👇
( ﻗُﻞْ ﺇِﻧِّﻲ ﺃُﻣِﺮْﺕُ ﺃَﻥْ ﺃَﻋْﺒُﺪَ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻣُﺨْﻠِﺼًﺎ ﻟَّﻪُ ﺍﻟﺪِّﻳﻦَ )

ﺍﻟﺰﻣﺮ ‏( 39:11 ) Az-Zumar
Sema: Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia Dini Yeye tu.
( ﻭَﺃُﻣِﺮْﺕُ ﻟِﺄَﻥْ ﺃَﻛُﻮﻥَ ﺃَﻭَّﻝَ ﺍﻟْﻤُﺴْﻠِﻤِﻴﻦَ )
*Na nimeamrishwa niwe wa mwanzo wa Waislamu.*
Hapa anazidi kukazia kuwa, Mola wake amempa amri ya yeye Muhammad kuwa, wa mwanzo wa Waislamu, na hapa akatekeleza amri hiyo kama alivyosema
👇
( ﻟَﺎ ﺷَﺮِﻳﻚَ ﻟَﻪُ ۖ ﻭَﺑِﺬَٰﻟِﻚَ ﺃُﻣِﺮْﺕُ ﻭَﺃَﻧَﺎ ﺃَﻭَّﻝُ ﺍﻟْﻤُﺴْﻠِﻤِﻴﻦَ )
ﺍﻷﻧﻌﺎﻡ ‏( 6:163 ) Al-An'aam
Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa Mwanzo wa Waislamu.
Hapa anatuambia yeye Muhammadi ndiye muislamu wa mwanzo, na kule tumeambiwa kuwa, Muislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke, sasa ndo maana nimeuliza, Ikiwa kweli Muhammadi ndiye muislamu wa Mwanzo, na tumeambiwa kuwa Muislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke, Je! Muhammadi yeye alikuwa mwanamke?
Kwani Muislamu wa pili Duniani baada ya kuambiwa kuwa Muislamu mwanzo ni mwanamke ni Alii Bin Abi Talib, katika hicho kitabu cha MAISHA YA NABII MUHAMMADI UK. 18 paragraph ya 4 sheikh Farsy anaandika: 👇
Sayyidna Ali bin Abi Talib bin Abdul Mutalib: alikuwa akilelewa na Mtume, alipomuona Mtume na bibi Khadija Usiku ule wanafanya mpya, aliwauliza: "Hii ni Ibada gani? "! Mtume alimfahamisha na akamtaka awe pamoja nao lakini yeye alikataa, akasema: "Mpaka nende nikamshauri baba yangu" Mtume akamkataza kuitoa siri ile nje, mara asubuhi ya Usiku ule ule, kijana huyu akaja kwa mtume akampa habari kuwa yeye yu pamoja nao. Akawa ndiye Islamu wa pili Duniani. Aliposilimu alikuwa kijana wa miaka 10 hivi.
👆 Unaona muislamu wa pili Duniani ni Alii, na tumeambiwa muislamu wa kwanza kabisa ni mwanamke, na Muhammadi yeye amesema kuwa ndiye muislamu wa mwanzo, rafiki zangu wa kiislamu hebu nisaidieni hapo.
A) Je! ni kweli Muhammadi ni mwanamke Kwa kuwa muislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke?
B) Kama yeye siyo Mwanamke, Je! ametudanganya kutuambia kuwa yeye ni muislamu wa mwanzo wakati muislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke?
C) Na kama yeye siyo wa mwanzo, Je! alipingana na amri ya Mola wake ya kumtaka yeye awe muislamu wa mwanzo?
Nb. Mada hii haijalenga kumkashifu Muhammadi, bali ni kutaka kujua kutokana na kile ambacho kimeandikwa kwenye Vitabu vya Dini ya kiislamu.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW