Sunday, August 28, 2016

Je, Kanisa ni Kiti cha Enzi cha Shetani?




Biblia inasema: “Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani…” (Ufunuo 2:13)


Waislamu “WAHUBIRI WA BIBLIA”, kama kawaida ya “injili” yao potofu hawaachi kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka; lakini kama hawataki kutubu, hukumu yao inakimbia mbio kuwajilia. Wahubiri hawa hutumia andiko hilo hapo juu kuonyesha eti Kanisani ni mahali akaapo shetani, wakimaanisha kuwa Wakristo wote tunapoenda kuabudu Kanisa, basi tunakuwa kwa shetani!

Lakini andiko hili maana yake ni nini?


Maneno haya yamo kwenye ujumbe wa Bwana Yesu kwa Kanisa la Pergamo. Kwa kuwa Bwana Yesu anatoa ujumbe kwa Makanisa kadhaa, hebu tuanzie nyuma kidogo ili tuweze kuona MUKTADHA wa matumizi ya maneno haya kwa usahihi. Siku zote nasisitiza umuhimu wa kuangalia maandiko katika MUKTADHA wake kwa kuwa bila kufanya hivyo, utadanganywa, utadanganywa tu na watumishi wa shetani na roho yako itaangamia milele!!

Mstari wa nane wa sura ya pili ya Ufunuo unasema:
“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.” (Ufunuo 2:8).


Bwana analiambia Kanisa hili:  “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.”  (Ufunuo 2:9).

Haihitaji ufahamu wowote mkubwa kutambua kuwa hapa kuna pande mbili – tena zinazopingana. Kuna upande wa Kanisa la Smirna linalomwamini Yesu Kristo; na kuna upande unaopingana vikali na Kanisa hilo, yaani upande wa Sinagogi la Shetani.

Kwa maneno mengine, Bwana Yesu anasema: “Wewe Kanisa uko Smirna, lakini shetani na kundi lake nao wapo hapohapo Smirna. Yaani hawa wana wa ibilisi ambao wanajidai kuwa wanahubiri neno la kweli la Mungu kumbe ni ujumbe utokao kuzimu kwa shetani, ambao kwa nje unaonekana kama ni maneno ya Mungu lakini ni ujumbe wa mauti.

Ufunuo 2:10 inasema: “Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”

Hapa Bwana anasema kwa hilo Kanisa la Smirna, “Wewe Kanisa, kwa kuwa hapo Smirna ulipo kuna pia kundi la shetani, kaa ujue kuwa shetani amepanga mabaya juu yako na atayatekeleza. Lakini pamoja na uovu wake huo, VUMILIA HATA KAMA ATAWAUA (angekuwa allah angesema, “Msikubali, chukueni mapanga mjilipize kisasi!”).

Hilo ni Kanisa la Smirna. Hebu sasa tugeukie Kanisa jingine kuhusiana na andiko linalotumiwa kwa hila na wahubiri wa ‘injili’ ya kiislamu. Hilo ni Kanisa la Pergamo.

Kwa mantiki ileile ya Kanisa la Smirna, mstari wa 13 unatoa maelekezo ya Bwana Yesu kwa Kanisa la Pergamo. Anasema:
 “Napajua ukaapo, NDIPO PENYE KITI CHA ENZI CHA SHETANI; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.” (Ufunuo 2:13).

Hapa tunaona kuwa, Bwana anatoa tahadhari kwa Kanisa hili. Anachosema ni kuwa: “Wewe Kanisa la Pergamo, hapo Pergamo ulipo ndipo pia yaliko makao makuu ya shetani.”

Kwa kila Kanisa, Bwana anakuwa anaeleza uzuri wa Kanisa husika kisha upungufu wake. Kwa Kanisa la Pergamo, uzuri wao ni huu: “walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu.”

Kwa hiyo, ukitazama mtiririko ulivyo kupitia makanisa haya tu mawili, unaona kuwa Bwana Yesu anatenganisha WAZIWAZI kati ya Kanisa lake na kundi la shetani ambalo linaleta upinzani kwa Kanisa.

Kwa kifupi ni kuwa, Kanisa la Kristo SI MAHALI PA SHETANI HATA KIDOGO bali shetani ni mpinzani anayeingia Kanisani ili kuwaangusha watakatifu kupitia  wale wanaoikana Injili ya kweli ya uzima ya Bwana Yesu!!

Ushauri wangu kwako Mwislamu ‘unayehubiri’ Biblia: kama unadhani ni muhimu kupinga Ukristo, fanya hivyo kwa kutumia hoja ZA KWELI (kama zipo) na sio kutumia hoja ZA UONGO; mambo ambayo Biblia hata haiyasemi!

Mgonjwa wa ebola akitumainia uongo wa kusema, “Mimi sina kabisa ebola mwilini mwangu” wakati anayo, kwanza hamdanganyi yeyote bali ni yeye mwenyewe!! Pili, ATAKUFA yeye mwenyewe na sio wale anaowaambia uongo huo.

Hoji mambo

Uongo unaua

Na ujinga (ignorance) ni barabara ya kwenda kuzimu

Tafakari

Chukua hatua!!

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW