Friday, August 26, 2016

INJILI INATHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU

Utangulizi
Tafadhali angalia Biblia Takatifu au Fungua Bibilia Takatifu iliyo bure na tamatisho zifuatazo kutoka Taurah (Mwanzo), Zabur (Zaburi) na Ijil (Injili).
Injili inathibitisha ya kwamba Yesu alizaliwa kutoka kwa bikira, hakuwa na makosa, alipelekwa mbinguni na Mungu na atarudi tena. Kulingana na Injili Yesu ni zaidi ya nabii. Yeye ni zaidi ya mtu aliye heshimiwa zaidi, utakatifu na baraka. Umuhimu wake kwa mwanadamu ni zaidi ya mponyaji mkubwa wa wagonjwa.
Utetezi wa Yesu kuwa Mwana wa Mungu:
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi (Yohana 5:39).
Somo la kweli na Injili sio mafundisho au filosofia, ila ni mtu: Yesu Kristo. Yesu anatupa sisi msingi wa uhusiano wa dharura na uwiano kati yetu na Mungu. Huu uhusiano unafanya kazi kama chanzo cha uhakika na ujasiri.
Kwanini mwanishutumu kwa sababu nilisema ‘Mimi ni Mwana wa Mungu? (Yohana 10:36).
Wakati Injili inazungumza juu ya Yesu kuwa mwana wa Mungu, haisemi ya kwamba Mungu na Mariamu walipata mwana kwa njia ya kibaolojia. Hii ni dhihaka. Hii haiko katika Injili. Mariamu alikuwa bikira (Mathayo 1:18, Luka 1;34-35) Yesu ni mwana wa Mungu, aliyekuwepo toka mwanzo.
Vitu vyote vimekabidhiwa mikononi Mwangu na Baba. Wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia (Luka 10:22).
Mungu Baba ni Bwana wa mbingu na dunia. Kwa hili dai kamili kama kwa ufahamu wa Baba, Yesu ana onyesha uungu wake. Mstari huu unaonyesha asili ya Yesu inayoweza kufikiwa na kwamba hatuwezi kuwa na ufahamu ulio sawa na Mungu ila ni kupitia ufunuo. Kwa hivyo tunaweza kuwa na ufahamu wa Yesu lakini hatuwezi kumjua kikamilifu
Nilitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni, sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba (Yohana 16:28).

Yale Yesu anasema hapa ni kwamba alikuwa na Baba mwanzoni kabla hajazaliwa. Mwana wa Mungu alingia katika habari zetu za utu akijiweka yeye mwenyewe na Baba kabla hajazaliwa kama mtoto. Yeye alikuwa na asili ya utu na asili ya uungu.
Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna ye yote anayekubali ushuhuda Wake (Yohana 3:31-32).
Yesu alitoka mbinguni katika utu wa uungu, sio kwa kubatilisha mahali, ila kwa kuchukua asili ya mwanadamu, aliyeuchukuwa ili kufanya katika mapenzi ya Baba, kazi ya Wokovu wetu.
Hakuna mtu ye yote aliyemwona Mungu wakati wo wote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha (Yohana 1:18).
Yesu kifuani mwa Baba. Sauti ya Mungu Baba haikuwa hai, wala umbo lake kuonekana na malaika au watu. Baba asiyeonekana, asiyeonekana kwa macho ya mwili; wala hata macho ya ufahamu, kana kwamba unaweza kukiona wala hapo na hapo. Mwanadamu hajui chochote kuhusu Mungu hata mwanzo. Neno pekee laonyesha hakuna anaye mstahimili kamaYesu na uhusiano wake na Mungu.
Wakiwa huko, Yesu alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho. Ghafula wakawatokea mbele yao Musa na Eliya, wakizungumza na Yesu. Ndipo Petro akamwambia Yesu, Bwana, ni vema sisi tukae hapa. Ukitaka, nitafanya vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Eliya. Petro alipokuwa angali ananena, ghafula, wingu linalong’aa likawafunika na sauti ikatoka kwenye Hilo wingu ikisema, Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye sana, msikilizeni Yeye. Wale wanafunzi, waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu. Lakini Yesu akaja na kuwagusa, akawaambia, ’Inukeni na wala msiogope’. Walipoinua macho yao, hawakumwona mtu mwingine ye yote isipokuwa Yesu (Mathayo 17:2-8).
’Yesu alibadilika sura mbele yao’. Yaani, kubadilisha, kubadilishwa katika sura kufunulia wanafunzi wake utukufu wa Mungu. Yesu aling’aa kama jua, anapo ng’aa katika nguvu zake (Mathayo 17:2). Ulio nenwa mbele ya manabii Musa na Eliya ilimpa nafasi iliyo ya mwana juu ya watumishi. Yeye yafaa asikike.Haya maneno yana nafasi juu ya maneno ya manabii. Huyu ni mwana wangu mpendwa wa Baba; msikilize yeye. Hiki ni kitu cha utukufu wa Yesu, kama ule wa mwana aliye zaliwa na Baba.
Yesu akawaambia, ’Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia Kwangu. Kama mngenijua Mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu sasa mnamjua Baba Yangu tena mmemwona’ (Yohana 14:6).
Yesu ni zaidi ya mwalimu mkubwa, zaidi ya mponyaji mkubwa, zaidi ya nabii mkubwa. Yesu ni mwana wa Mungu na siye mojawapo wa njia za kufika kwa Mungu, ila Yeye ni njia ya pekee ya kwenda kwa Mungu. Yesu ndiye njia ya kufikia baraka zote za Mungu. Yesu siye tu kweli, ila yeye mwenyewe ni ukweli. Yesu ndiye njia iliyo hai, kinyume cha dini ingine yoyote.
Yesu amefufuka ni kweli
Ni kweli Bwana amefufuka, naye amemtokea (Luka 24:34).
Wakati Mohammed na manabii wengine wangali ndani ya makaburi yao hata leo hii. Yesu amefufuka toka wafu na yeye yu hai. Yesu alifufuka toka wafu jinsi alivyotabiri na ni mwokozi wa ulimwengu. Kwa hivyo tunaweza kuinuka kwa maisha mapya na yaliyo kamilifu, akawaacha nyuma mashindano yote ya ndani, tamaa, na kutoridhika.Yesu yu hai na anataka wewe umwaamini yeye na kumjua yeye. Mlango unaweza kuwakilisha ufunguzi wa maisha mapya au uwezekano wa maendeleo mapya. Kuingia katika kitu ambacho bado hakijatambulikana. Njia ya wokovu ni uponyaji na ukamilifu. Yesu akawambia: Mimi ndimi lango, ye yote anayeingia zizini kwa kupitia Kwangu ataokoka, ataingia na kutoka, naye atapata malisho (Yohana 10:9).
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16).
Huu mstari ni funzo katika upendo wa Mungu: Mungu alimtoa mwana wake wa pekee kwa ulimwengu huu wenye dhambi. Katika Uislam na katika maeneo mengine, wokovu wa mwanadamu unategemea matendo mema na jitihada njema. Lakini Mungu ni wa neema na pia mwenye haki. Sababu Mungu ni mwenye haki, kwa urahisi hawezi kupuuza dhambi za mwanadamu. Ni lazima ahukumu dhambi. Wewe ni mwenye dhambi. Hauwezi kuondoa dhambi zako, sababu Mungu ni mwenye haki. Tangu mwanadamu alikuwa ametenda dhambi, sheria ya Mungu inahitaji yeye afe. Lakini Mungu pia ni mwenye rehema. Yesu alikuja kufa badala yake mwanadamu, ili kwamba mwanadamu awe kihalali huru. Amani ya kwamba Yesu alikufa kwa ajili yako sababu ya dhambi zako. Uki mwaamini yeye kama aliye sulubiwa, akazikwa na kufufuka kama mwokozi kwa ajili yako, uta pokea msamaha kwa ajili ya dhambi zako zote na ana kipawa chake cha uzima wa milele kwa imani. Kumkataa Yesu kama mwokozi wa ulimwengu huleta hukumu ya Mungu. Kumjua Yesu ni kujua kitu kilicho kizuri katika ulimwengu.
Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele (Yohana 10:10).
Yesu alikuja katika ulmwengu huu katika asili ya binadamu, kutoa mwili wake, mwili, asili yake ya binadamu, nafsi, mwili kwa ajili ya maisha ya wote. Kupitia maisha ya Yesu, wanadamu wemeingia katika mtindo wa maisha yaliyo kweli.
Yesu atakusaidia wewe:
Yesu alitenda miujiza isiyo ya kawaida. Watu wengine katika maandiko pia wali tenda miujiza lakini wali abudu na kumwomba Mungu. Kwa uhakika Mungu alitenda miujiza. NaYesu? Alikuwa ndiye mwenye hizo nguvu mwenyewe. Kujibu maswali haya, kwanza mtizamo wa nguvu za BWANA, Mungu mwenyezi. Hakuna aliye kama yeye kwa ajili ya nguvu na uweza wake mkuu, kwa hizo ame umba mbingu na nchi (Mwanzo 2:4), anazishikilia katika kuwepo:
Ee BWANA Mwenye Nguvu, ni nani aliye kama Wewe? Ee BWANA, Wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka. Wewe unatawala bahari yenye msukosuko, wakati mawimbi yake yanapoinuka, Wewe unayatuliza (Zaburi 89:8-9).
Wakari mawimbi yake yanapoinuka, BWANA huyatuliza ,wakati bahari ina msukosuko na yote ina inua sauti zao na kunguruma, BWANA uyatuliza, kama vile mzazi kwa mtoto wake anapo lia au bwana na wanafunzi wake wanapofanya kelele na ghasia.
Walakini je Yesu ana uweza wa kukulinda wewe katika uhusiano wake mpya na Yeye? Je kuna mtu anayeweza kutoa katika mikono ya Yesu? Na tusome mistari ifuatayo:
Walimlilia Bwana wakati wa msiba wao (Zaburi 107:26-30).
Yakainuka juu mbinguni yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka. Walipepesuka Na kuyumbayumba Kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo. Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao, naye akawatoa kutoka kwenye taabu yao. Akatuliza dhoruba kwa mnong’ono, mawimbi ya bahari yakatulia. Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi kwenye bandari waliyoitamani.
Walimlilia Yesu katika msiba wao (Marko 4:37-5:1).
Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji. Wanafunzi Wake wakamwamsha, wakamwambia, ’Mwalimu, hujali kama tunazama?’ Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, ’Uwe kimya! Tulia!’ Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa. Yesu akawaambia wanafunzi Wake, ’Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?’ Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, ’Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?’ Wakafika upande wa pili wa bahari.
Tunaona katika Injili wanafunzi walikuwa na shida zile kama hali ya Zaburi 107:27-29. Wanafunzi walimlilia Yesu wakati wa shida zao. Walakini, wanafunzi hawakuwa na imani katika Yesu, kama kulala, ili awakomboe wao. Walikuwa tu na imani ndogo katika yeye. Yesu alionyesha ya kwamba yeye ni mwenye nguvu zote. Upepo ukakoma, kukawa na utulivu mkubwa. Pia upepo na mawimbi yakatulia, mtii Yesu kwa neno lake (Ona pia (Marko 1:27) na (Luka 17:6). Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii? Hawezi kuwa mwingine ila ni Mungu mkuu, ambaye upepo na bahari vinamtii: ambayo hayawezi kusemwa kwa mtu mwingine, ila ni Mungu aliye juu sana: Hakuna jambo ambalo liliwahi kusikika kwamba,upepo na bahari zinaweza kukemewa na viumbe tu, na vikatii, Yesu siye tu mwenye nguvu zote, lakini yeye ni chanzo cha nguvu zote na mamlaka. Basi mwanadamu lazima awe mtaifa kwa ufunuo au aliye danganywa, ambaye anaweza kusoma maelezo haya, na kuukana ukweli wa matukio na hali, au kuamini ya kwamba Yesu ni hakika na kweli ni Mungu, kama vile wanafunzi walivyofanya.
Kwa hivyo, rafiki mpendwa, natumai mwisho wa huu ukurasa utaamini kuna ushahidi kwamba Yesu ana uweza wa kukusaidia wewe. Hii inaweza kueleweka katika hali ingine: ya bahari ya ulimwengu huu ikiwa na mambo mabaya ndani yake, yaliyo kama bahari iliyochafuka, na haiwezi kutulia, inayopanda tuu chuki na hakuna upendo na kumdhihaki Mungu. Haswa viongozi wa mabavu na kiimla, walio kama maji ya kiburi na mawimbi yanayo vuma baharini. Lakini Yesu ni mkuu kuliko wao wote, na anaweza na hata anazuia ghadhabu na hasira yao, ili kwamba watu wake wasiwe na chochote cha kuogopa toka kwa hicho.
Wewe pia unaweza kujua ukweli na kufurahia baraka hizo wakristo walizo nazo na Utajua ukweli na utakuweka wewe huru (Yohana 8:32).
Njoo kwa Yesu, ili tufurahi na wewe.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW