Wednesday, August 10, 2016

ALLAH SIO MWENYEZI MUNGU (SEHEMU YA TANO)


KUMBE ALLAH ANA MIKONO NA MACHO KAMA VIUMBE
Ndugu msomaji,
Tunaendelea na mada kuhusu Allah ambaye ni kiumbe kama sisi. Leo ninawaletea ushahidi kuwa, Allah ana MIKONO kama binadamu. Haya ungana nami na tuanze kusoma ushahid kutoka vitabu vya Kiislam.
وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ {67}
“Na hawakumheshimu Mwenyezi Mungu heshima ipasayo, na siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kulia, …” (Az-Zumar; 39: 67)
“Mikono” Ya Mwenyezi Mungu Kama Ilivyosimuliwa Na Madhehebu Ya Makhalifa.
Wanazuoni wa madhehebu hiyo hapo juu wamesimulia ndani ya vitabu vyao kutoka kwa Abu Huraira ambaye amesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama ifuatavyo:
“Adamu na Musa walikuwa na mazungumzo yafuatayo: Musa alisema: ‘Ewe Adamu! Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mikono Yake Mwenyewe… Lakini uliwateremsha wanadamu kutoka kwenye bustani kwa sababu ya dhambi yako.’
Adamu akajibu: ‘Ewe Musa, Mwenyezi Mungu kwa hakika amekutukuza wewe, na akaandika Taurati kwa ajili yako kwa mikono Yake Mwenyewe.’”
KUMBE ALLAH ALIANDIKA TAURATI KWA MIKONO YAKE MWENYEWE.
Katika hadithi nyingine iliyosimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, tunakuta:
“Mwenyezi Mungu huwa anashuka mpaka kwenye mbingu ya kwanza, na ananyoosha mikono Yake miwili na anasema…”
Halafu anaendelea kunukuu Ayah zifuatazo kwa ithibati ya madai yake:

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنْفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ {64}
“Na Wayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndio iliyofumba, na wamelaaniwa kwa sababuya yale waliyoyasema. Lakini mikono ya Mwenyezi Mungu iwazi, hutoa apen- davyo …” (Al-Maida; 5: 64)
فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ {83}
“Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo ufalme wa kila kitu, na kwake mtarejea.” (Yaasin; 36: 83)
قُلِ اللَّهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {26}
“Sema: Ewe Mola Mwenye kumiliki ufalme, humpa ufalme umtakaye, na humnyang’anya ufalme umtakaye. Na humtukuza yule umtakaye na kumdhalilisha umtakaye. Kheri yote imo mikononi mwako. Hakika wewe ni Mweza juu ya kila kitu.” (Aali Imraan; 3: 26)
Muhammad bin Muslim alimuuliza Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) kuhusu Ayah ifuatayo:2
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَنْ تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ {75}
“Akasema: Ewe Iblis, ni nini kimekuzuia kumtii yule niliyemuumba kwa mikono yangu?... (Swaad; 38: 75)
Swali ningependa kuwauliza Waislam, hivi kwanini mnasema kuwa Allah hana mfano wakati teyari Allah anajidhihirisha kuwa ana MIKONO? Je, Mikono so mfano wa binadamu? Kwanini mnamzulia Allh uongo kuwa hana Mikono?
ALLAH ANA MIKONOTunaamini kuwa Allaah Anayo mikono miwili mitukufu.
Anasema:
بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاء
"Bali mikono yake (miwili - yadaahu) iwazi. Hutoa Apendavyo."
Al-Maaidah – 64
Na Akasema:
وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالأرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى عَمَّا يُشْرِكُونَ
"Na wala hawakumhishimu Allaah kama Anavyostahiki kadiri Yake. Na Siku ya Qiyaamah ardhi yote itakuwa mkononi Mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono Wake wa kuume. Subhaanahu wa Ta’ala Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo."
Az-Zumar – 67
(Siku ya Ridhwaan Waislamu walipofungamana na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) chini ya mti kwa kumpa mkono wote kwa pamoja, mmoja baada ya mwengine, na Allaah Akateremsha kauli Yake:
إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّهَ يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ
"Bila Shaka wale wanaofungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Allaah. Mkono wa Allaah uko juu ya mikono yao."
Al-Fat-h – 10
Ieleweke kuwa Allaah Anaposema Anayo mikono au macho, ina maana kuwa mikono Yake ni sawa na mikono yetu, au macho Yake ni sawa na macho yetu - AstaghfiruLlaah. Meza inayo miguu na viti vina miguu, lakini miguu ya viti na ya meza ni tofauti na miguu ya mwanaadamu aloitengeneza meza ile, kwani sifa ya mtengenezaji lazima iwe tofauti na sifa ya kilichotengenezwa, ama sivyo mtengenezaji na kilichotengenezwa watakuwa kitu kimoja. Na Allaah Ndiye mwenye kupigiwa mifano bora, sifa Zake Subhaanahu wa Ta’ala haziwezi kufananishwa na sifa zetu. Lakini wakati huo huo lazima tukikubali kila Alichojinasibisha nacho Subhaanahu wa Ta’ala.)
ALLAH ANA MACHO Na tunaamini kuwa Allah Anayo macho mawili kikweli, na hii inatokana na kauli Yake Subhaanahu wa Ta’ala Aliposema kumwambia Nuuh (‘Alayhis-Salaam):
وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا
"Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu."
Huud – 37
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
"Pazia yake ni nuru, na lau kama Ataiondoa basi nuru ya Wajihi Wake ingeunguza kila kilichokifikia."
Na alipokuwa akihadithia juu ya Ad-Dajjaal alisema:
"Dajjaal ana chongo na Mola wenu Hana chongo."
Na tunaamini kuwa macho yetu hayamfikii kumuona Allaah.
Allaah Anasema:
لاَّ تُدْرِكُهُ الأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الأَبْصَارَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ
"Macho hayamfikilii, bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari."
Al-An’aam – 103
Ndugu wasomaji, teyari mmesha elewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu kwasabau ana Mikono.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW