Vichwa vya habari vinasema dini ya kiislamu itakuwa dini kubwa kuliko zote duniani. Lakini uislamu unakutana na matatizo kwa sasa. Vitendo vya kinyama vinavyofanywa na kundi linalojiita la Kiislamu la ISIS kwa kutumia jina la Allah (Mungu wa Kiislamu) na kufuata mfano wa vitendo vya vurugu vya Muhammad, vimewafanya kuwaogopesha Waislamu walio wengi na kuanza kujiuliza kuhusiana na imani yao.
Wamisionari wanaofanya kazi katika nchi za kiislamu wanasema waislamu wengi zaidi wamebadili dini na kuwa Wakristo katika kipindi cha miaka 14 iliyopita toka tukio la ugaidi la Marekani la september 11 kuliko karne 14 zilizopita katika historia ya Kiislamu.
Wengi wamekuwa wakificha siri kuhusu imani wakiogopa maisha yao kuwa hatarini. Jijini London Uingereza, kituo cha CBN kilizungumza na Imran (ambaye hakutoa jina la ukoo, kujilinda ili asijulikane), ni mwanafunzi wa chuo ambaye ametokea Pakistani na familia yake kama wahamiaji nchini Uingereza. Imran aliachana na Uislamu baada ya kujifunza kwa muda mrefu na kujihakikishia kwamba Quran inawezekana si ya ukweli. Kuacha uislamu inaweza kuwa kazi nzito. "Ikiwa mtu ameacha uislamu anakuwa muasi, anafukuzwa kwenye familia, familia yake itakuwa ya kwanza kumtenga", Imran amesem na kuongeza kwamba rafiki zake wataachana naye na atauwawa au atafungwa. Marafiki zangu wengi wameniambia "hii ni mara ya mwisho nazungumza na wewe kwasababu umemdhalilisha Mtume Muhammad, umeudhalilisha Uislamu.
Imran bado hajawa Mkristo, lakini amesema amesoma Biblia na kugundua Ukristo unafaa kuliko Uislamu. Baadhi ya Waislamu baada ya kuachana na dini yao wanakuwa watu wasionadini na wengine wanapata wasaa wa kupatana na Mungu. Kutoka Sweden, Mchungaji Fouad Rasho wa kanisa la 'Angered Alliance ambaye ni mkimbizi kutoka Syria, amesema amewabatiza zaidi ya waislamu 100 akidai waislamu wengi wanaikana dini yao kwasababu ya vitendo vya ISIS.
"Kila wiki nakutana na mtu mmoja au zaidi wanaokuja kwangu wakitaka kujua zaidi kuhusu Ukristo na Biblia kwasababu wanakasirishwa sana na Uislamu. Hawataki kuendelea na dini yao ya kiislamu" alisema Imran, linapokuja suala la dini, bara la Ulaya limekuwa giza, baadhi ya waislamu wa Ulaya wanahisi kuachwa njia panda kati ya wasioamini kabisa mambo ya dini au wameathirika na Uislamu, lakini baadhi yao wamepata tumaini ndani ya Ukristo.
Wakati Nassim Ben Iman alipokwenda Ujerumani akiwa kama mkimbizi pamoja na familia yake wakitokea moja ya taifa la kiislamu, alikumbuka kwamba alikuwa akiwaza kwamba Ujerumani ni taifa la Kikristo, kumbe Ukristo ulikufa, dini ya wenye dhambi "Kuonekana nusu utupu kwenye runinga ni kwasababu ya dini ya Kikristo, kuishi pamoja kwa mwanaume na mwanaume bila ndoa ni kwasababu ya dini ya kikristo" alisema Nassim akikumbuka alichokuwa akikiwaza.
Lakini pia Nassim amegundua Ukristo wa kweli na leo uinjilisti unawafikia waislamu na wasio Waislamu kumjua Kristo. "Watu wanapogundua Yesu ni nani, watampenda na kumfuata yeye kila siku, na Waislamu wanapomuelewa zaidi na zaidi Muhammed ni nani, Quran ni nini, historia yake, watakwenda tofauti mbali zaidi na Uislamu" alisema Nassim.
Muandaaji wa kipindi cha Kikristo cha kuwafikia waislamu amekiambia kituo cha CBN News kwamba Uislamu utakufa. Kaka Rashid ni mtoto wa imam nchini Morocco ambaye ameishi kama Mkristo kwa kificho kwa miaka 15 sasa. Kwa sasa ni muandaaji wa kipindi cha Kikristo kwa lugha ya kiarabu kinachoitwa "Daring Questions" ambacho kinawapa changamoto waislamu kujiuliza kuhusu imani yao.
"Waislamu wengi wanasema, kama ISIS ni uislamu, ninatoka. Baadhi wanakuwa wapagani, alisema Kaka Rashid. Kuna wimbi kubwa la wapagani kwenye dunia ya Waarabu siku hizi. Wengi wanakuwa wakristo. Uislamu haujawahi kupatwa tatizo hili mwanzoni. Nassim amesema uislamu unaonekana upo imara, ila ni kwa nchi ambazo ukristo ni dhaifu. "Uimara wa Uislamu ni udhaifu wa Wakristo, na ndio kinachotokea Ujerumani na Marekani pamoja na nchi nyingine za magharibi. hata ikionekana Uislamu kama unataka kutawala nchi za magharibi, Rashid amesema Wakristo wasiwaogope Waislamu, kwa kuwa anawiwa kusema kwamba dini hiyo inakufa taratibu.
"Uislamu sio chombo cha Mungu kuhukumu nchi za Magharibi, nadhani watu wanaogopa kwasababu ya wanachoona kwenye habari, lakini hata mapigano inaonyesha ni dalili ya kufa kwa dini hiyo.
Makala hii imetafsiriwa na GK kutoka Charisma News
No comments:
Post a Comment