Saturday, July 23, 2016

UTATA MKUBWA KUHUSU UTUME WA MUHAMMAD


Ndugu msomaji,
Katika Biblia shetani ametajwa kuwa anaweza kujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
2 Wakorintho 11:13-15 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu, maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakajigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao”.
Muhammad akiwa Medina aliulizwa na Wayahudi ikiwa ufunuo wake umetoka kwa Mungu wa Kweli kwa kumtaka atoe sifa za manabii. Akijibu swali hilo alisema:
Mkweli Mwaminifu Juzuu 3-4 Uk.63. Hadithi Na. 880. “Kasema Mtume (s.a.w):- (Mambo) mane ya sheria za mitume (Kuwa na) na haya,na kujipaka mafuta mazuri,na kuowa (wake),na kupiga mswaki.
Hizi si sifa za Ki-Mungu kwa nabii na mtume bali ni za kibinadamu tu.
Manabii na watu mbalimbali katika Biblia hawakuona haya. Soma Isaya 50:7 “ Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimeukaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya”. Zaburi 34:5 “ Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya” Zab 119:46 “ Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu” Warumi 1:16 “ Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye kwa Myahudi kwanza , na kwa Myunani pia” 1Petro 4:16 “ Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
Zaidi ya hayo tunaona Muhammad alirogwa. Kurogwa ni hali ya mtu kuathirika na nguvu za giza yaani uchawi.. Je nabii au mtume wa Mwenyezi Mungu wa Kweli anaweza kurogwa?
Katika Qur’an Suratul Ban-Israel, 17:47 “ Tunajua sana, sababu wanayosikiliza, na wanaponong’ona, wanaposema hao madhalimu. Nyinyi hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa”
Pia katika Suratul Falaq, 113:1-5 “ Ninajikinga kwa mola wa ulimwengu wote na shari ya Alivyoviumba, na shari ya giza la usiku liingiapo, na shari ya wale wanaopulizia (vivia) mafundoni (wakavunja) mashikamano yaliyo baina ya watu yaani shari ya mafatani, Na shari ya hasidi anapohusudu”

Tunasoma tukio hilo katika ufafanuzi wake uliyomo ndani ya Qur’an chapa ya nane uk.977 unaofafanua Sura ya 113-114 “Athari ya uchawi juu ya mtume (s.a.w). Swali la pili lijitokezalo kuhusu sura mbili hizi ni kwamba kwa mujibu wa hadithi uchawi ulifanywa dhidi ya mtume (s.a.w) naye akawa mgonjwa, na ili kuiondoa athari hiyo ya uchawi Jibril (a.s) alikuja na kumpa maelekezo Mtume (s.a.w) ya kusoma sura mbili hizi. Watafiti wengi zamani na wa sasa wamelifanyia upinzani jambo hilo, kwamba ikiwa hadithi zitakubaliwa, basi mfumo wote wa sharia utakuwa ni wa kutiliwa shaka, kwa sababu kama mtume (s.a.w) aliweza kuathirika kwa uchawi, na kwa mujibu wa hadithi hizi kweli uchawi huo ulionesha athari yake, basi hatuwezi kukaidi au kukana hadi kiwango gani maadui waliweza kumfanya Mtume (s.a.w) aseme na atende mambo kwa nguvu ya uchawi, na katika mafundisho yake mambo mangapi yatoka kwa Allah na mangapi yatokana na athari ya uchawi juu yake. Si hiyo tu, bali pia wasema kuwa baada ya kuyatambua hayo kuwa ni kweli katu haitawezekana hata kule kukaidi kuwa (s.a.w) alishawishiwa kudai utume kwa mauzauza ya kinjozi kuwa alimjia malaika. Pia wanasema hadithi hizi zapingana na Qur’an, na kama ilivyo katika Qur’an kuwa tuhuma hiyo batili kwa makafiri ilivyotajwa kuwa mtume s.a.w amerogwa naye ameathirika na uchawi: wanaposema hao madhalimu, ‘Ninyi hamumfuati isipokuwa mtu aliyerogwa’.” (17:47), lakini hadithi hizi zinathibitisha madai ya makafiri kuwa kwa kweli aliathirika na kuongozwa na uchawi……Kadri historia inavyohusika,ukweli kuwa kiasi fulani cha athari ya uchawi juu ya Mtume (s.a.w) ni hakika iliyothibiti; na kama kwa ustadi wa ubishi inawezekana kuthibitisha kuwa kweli. Limesimuliwa jambo hilo na Bukhari, Muslim, Nasai, Ibn Majah, Ahmad, ‘Abdur Razzaq, Humaid, Baihaqi, Tabarani, Ibn Sa’d, Ibn Marduyah, Ibn Abi Shaibah, Hakim, Abd bin Humaid na Muhadithina wengine toka kwa Bi. ‘Aisha (r.a), Zaid bin Arqam, Ibn ‘Abbas kupitia silsila nyingi mno kiasi kwamba jambo lenyewe limefikia hali ya ufululizo kamili, isipokuwa kila Hadithi, yenyewe ni ripoti kamili.
Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha kuwa utume wa Muhammad una utata. Ikiwa na wao Waislamu kwa mujibu wa hadithi hizi hawajui ni mambo mangapi Muhammad aliyoyasema yanatoka kwa Allah na mangapi aliyasema akiwa ameshinikizwa na wachawi , Je ufunuo na utume wake utakuwa umetoka kwa Mungu wa Kweli? Tafakari !!
Ndani ya Biblia Takatifu hakuma kurogwa kwa mtu wa Mungu. Hesabu 23:23 “ Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israel. Sasa habari za Yakobo na Israel zitasemwa , Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!”
Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia Takatifu, manabii na mitume wa kweli wa Bwana Mungu wanatoka katika taifa la Israel.
Kitabu cha Ezekiel 13:9 “ Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii wanaoona ubatili, na kutabiri uongo;hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israel, wala hawataingia katika nchi ya Israel; Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU” .
Pia kwa mujibu wa kitabu cha Qur’an manabii na mitume ni lazima watoke kwa Yakobo ambaye ni mtoto wa Is-haqa ambaye naye ni mtoto wa Ibrahim. Qur’an Suratul Al-Ankabuut, (Buibui), 29:27 “ Na tulimpa (kumzaa nabii) Is-haqa na (kumjukuu nabii) Yakubu na tukauweka katika kizazi chake unabii na (kupata) kitabu, na tukampa ujira wake katika dunia; naye katika akhera kwa yakini atakuwa miongoni mwa watu wema”.
Aya hii, inaendelea kusisitiza kuwa ni kupitia kizazi cha Yakobo ndiko uliko unabii na kupata kitabu. Kwa bahati mbaya Muhammad ibn Abdullah, hatoki katika kizazi hicho wala kwa Ishmael kama wanavyodai Waislamu . Kwa sababu Ishmael ni Mwebrania kama baba yake mzee Ibrahim alivyo Mwebrania (Mwanzo 14:13) na Muhammad ni mwarabu kutoka kabila la Maqureysh. Kwa kutambua hilo ndipo tunamwoma Muhammad akiwaonya watu wengine wajiepushe na watu wa kabila lake.
Sahih Al-Bukhari Vol.1.Hadithi Na. 801 na Al-Lu’lu Kitabu cha 3. Uk.1089.Hadithi Na.1846 inasomeka“Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema ,“Mtume wa Allah (s.a.w) amesema, Kabila hili la Makuraish litawateketeza watu.’ Wakauliza, ‘Unatushauri nini?’ Akasema, Nashauri watu wajitenge nalo.”
Kumzamisha nzi kwenye kinywaji
Bukhar vol. 4 Hadith 537 “ Narrated Abu Huraira: The Prophet said: If a house fly falls in the drink of any one of you, he should dip it (in the drink) for one of its wings has a disease and the other has the cure for the disease”
Tafsiri: Ilisimuliwa na Abu Huraira: Nabii alisema kama nzi akiangukia ndani ya kinywaji cha mmoja wenu, anapaswa kumzamisha kabisa (ndani ya kinywaji) kwa kuwa bawa lake moja lina ugonjwa na bawa lake jingine lina dawa
Mitume wa Yesu ndani ya Biblia Takatifu walikwisha kutuonya kuhusu uchafu huo. Katika 2 Kor 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries Org.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW