Saturday, July 2, 2016

SINAGOGI SIO MSIKITI (SEHEMU YA TATU)


Ndugu msomaji
KIGEZO CHA YESU KUINGIA KATIKA SINAGOGI SIYO KIGEZO SAHIHI CHA KUFUNDISHA LA KUWA YESU NI MUISLAM.
Hebu fuatilia fungu hili la Biblia
MATENDO YA MITUME 17:1
Akiisha kupita kati ya amfipoli na Aporonia akafika Thesalonike ambapo palikuwa na Sinagogi la Wayahudi na Paulo akaingia mle walimo akahojiana nao kwa maandiko Sabato tatu.
Endapo umefuatilia fungu hilo kwa makini unaweza kujiuliza swali lifuatalo ………….
Ikiwa kuingia tu kwenye Sinagogi kulimaanisha Yesu ni Muislam je Paulo naye kwa tendo hilo lakuingia humo alikuwa Muislam?
Jambo la kushangaza hata wale wanaotoa fundisho hili humkataa Paulo kwa kadri ya imani yao na huku wakijivisha kitanzi kwa madai hayo kuwa mtu huwa muislam kwa kuingia katika Sinagogi.
Alichofanya Yesu katika Sinagogi hakiwiani na Misikiti ya Waislam
Luka 4:16 – 17 Yesu apewa chuo cha Nabii Isaya je Waislam leo hii wanachuo cha Nabii Isaya Msikitini? (La Hasha ) hii inaonyesha utofauti mkubwa uliopo baina ya Masinagogi na Msikiti ingawa ni vitu vichache tu vianavyolingana baina ya majengo hayo mawili.
Pamoja na hayo chuo hicho Nabii Isaya humtaja Yesu kama Mungu mwenye nguvu Isaya 9:6-10 tendo ambalo linapingwa na Umma wa Kiislam hivi leo hivyo kamwe Sinagogi na Misikiti si Majengo yanayowiana katika tafsiri na pia hata katika matendo kadhaa makuu ya kiimani pamoja na kufanana kwa machache kama yale yahusuyo mavazi n.k.
KUMFANYA YESU NI MUISLAM NI MAKOSA
Yesu alipaa kwenda mbinguni mwaka wa 33 kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamadi mwaka 570 (BK) ambaye ndiye muanzilshi wa Uislam.
Yesu hakufuata kamwe nguzo tano za Uislam na hata hivyo bado hapakuwa na nguzo hizo kwa kuwa muasisi wa imani ya Uislam yaani Muhamadi (SAW) hakuwepo.
Hebu sasa tuchunguze nguzo hizo tano za uislam na kisha upime mwenyewe endapo Yesu alizitekeleza hizo ili kuwepo na usahihi kwa wanaofundisha na kudai kuwa Yesu alikuwa Muislam.
NGUZO (5) ZA UISLAM
1) Shahadat - kushahadia- hili ni tendo la kukili kuwa Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake.
2) Ikhamu Swalat - Kusimamisha swala- hili ni tendo la kufuata utaratibu wa kusali swala mara tano kwa siku.
3) Ita-U Zhakhati - Kutoa zaka- kutoa mali kwaajili ya Masikini.
4) Swaum Shar Ramadhani - Kufunga – hili ni tendo la kufunga kwa kuangalia mwezi linalochukua muda wa siku 29, 30
5) Hijat ila Baitu Llah - Kuhiji Maka- hili ni tendo la ibada yakwenda mji wa Makka linalo ambatana na matukio mbalimbali kama vile kupiga mawe Shetani na kuheshimu jiwe
Jeusi n.k
Je Yesu alifanya hayo ili aitwe Muislam?
Yesu kamwe hakuwa Muislam (Yasuu Laysa Muslimuna).
Barikiwani; Maswali yanakaribishwa
Na Mwalimu Chaka
Edited by Max Shimba
Amended and narrated by Max Shimba
Barikiwa sana ndugu msomaji baada ya kujifunza kuwa Sinagigi sio Msikiti.
Max Shimba Ministries Org

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW