Friday, July 29, 2016

ETI YESU NI MWISLAM KWASABABU ALISUJUDU?



Ndugu msomaji,
Kwanza tujifunze maana ya neno au asili ya neno kusujudu:
NINI MAANA YA KUSUJUDU?
Neno la Kiebrania "shachah" lina maana ya kuabudu, KUSUJUDIA, kuinama kwa kuonesha unyenyekevu, kuonesha heshima kubwa au kuanguka kifudifudi. Neno la Agano la Kale proskuneo halikadhalika lina maana ya kubusu mkono, au kupiga magoti na kugusa ardhi kwa paji la uso kwa unyenyekevu mkuu. Maneno mengine mawili ya kuabudu yana maana ya kutumika, kufanya ibada takatifu na kumtolea Mungu sadaka.
Hivyo kusujudu ipo ndani ya hili neno la "SHACHAH" ikimaanisha kuabudu.
ILI KUELEWA KAMA YESU ALIKUWA MUISLAM, ITABIDI TUANZIE NYUMA KIDOGO NA TUMSOME ISHMAEL AMBAYE WAISLAM WANASEMA ALIKUWA MUISLAM NA CHAGUO LA MUNGU.
Je Ishmael ni Agano la Mungu?
Kila mara nimekuwa nikisisitiza jambo hili ambalo namwomba Roho Mtakatifu aweze kuwafunulia ndugu zangu Waislamu ili muweze kutoka kwenye kifungo kilichowafunga.
◆Wapendwa wangu, mnajua kabisa kwamba Mungu ni roho, mbingu ni mahali pa kiroho, na hivyo hata ujumbe wa Mungu ni wa kiroho. Lakini mara zote Waislam wanaishia kuona mambo kimwili na sio kiroho.
Hapo ndipo Allah alipowapiga chenga kubwa sana inayowagharimu uzima wa milele.
◆Waislam hutumia aya ya 136 katika Surat Al Baqara kwa madai kuwa Yesu ni mwislam! Hakikaa huu ni msiba mkubwaa kwa ndugu zetu Waislam!
Surat Al Baqara 136: “Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yaletuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-haaq na Yaaquub na wajukuu zake, na waliyopewa Muusa na Yesu, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.” Qur-aan 2:136
Kiukweli sioni mantiki kutumia aya hii ili kuthibitisha Yesu ni mwislamu! Hii inanisikitishaa na kunihuzunishaaa...
Tukiwasoma Wapagani wa Makka katika Sahih al-Bukhari, Vol 5, #661 tunajifuza kuwa hawa Wapagani walikuwa WANASUJUDIA JIWE JEUSI. Kwasababu Waislam wameegemea KUSUJU NDIO UISLAM. BASI KUMBE HATA WAPAGANI WA MAKKA NI WAISLAM. KUMBE BASI, UISLAM NI UPAGANI.
HOJA KUU ZA WAISLAM NI HIZI HAPA:
◆Harakati za maombi mbalimbali katika Biblia kutoka kwa Yesu: “Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali:” (Biblia, Mathayo 26:39)
Ujinga sio lazima uokote makopo bali maneno na matendo unayotenda yatadhihirisha kuwa wewe ni mjingaa... Kwa Muislam, eti, kusali huku umesujudu ndio teyari umesha kuwa Muislam. Huu ni msiba kwa ndugu zetu. Inamaanisha kuwa hata Mbwa au Nguruwe akiweza kusujudu basi teyari huyo Nguruwe amekuwa Muislam.
◆ Lakini nimeona nifafanue vema aya hii pamoja na hoja zao ambazo hazina kichwa wala miguu kama makala kamili kwa ajili ya faida ya wengi, maana hoja hii inajirudiarudia tena na tena kutoka kwa ndugu zangu Waislamu walio wengi.
◆Kwanzaa napenda kuwajulisha kwambaa Sisi hatumuamini huyu mungu wenu mnayemwamini nyie ambaye ni mungu wa Ibrahim na Ismail na Is-haaq na Yaaquub.
◆Biblia haijasema na au tupa aya inayo litataja na au sema Mungu wa Ismail ambaye aliabudu masanamu na mizimuuu na wala Biblia aitajee Mungu wa ishamael, huo ni uongo dhaihiri mnaojidanganya
◆Mungu kwenye Biblia amejitambulishaa hivi:
Naye akaendelea kusema “Mimi ni Mungu wa baba yako,
Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. ”Kisha Musa akauficha uso wake,kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu wa kweli(kutoka 3;6)
Umeona kwenye hiyo aya hapo juu? Hakuna jina la Ishmael/
Ismaili.
◆Matendo 3:13 Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo, Mungu wa babu zetu amemtukuza mtumishi wake Yesu. Yeye ndiye yuleyule mliyemtia mikononi mwa wakuu na kumkataa mbele ya Pilato hata baada ya Pilato kuamua kumwacha huru.
Unaona tena kwenye hiyo aya hapo juu? Hakuna jina la Ismaili. Ikimaanisha Mungu aliye mtukuza Yesu si wa Ismaili.
◆ Matendo 7:32 ‘Mimi ni Mungu wa babu zako, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo!’ Musa akatetemeka kwa hofu na wala hakuthubutu kutazama zaidi.
SWALI KWA NDUGU ZETU WAISLAMU:
◆Kama Mwenyenzi Mungu amewateremshia kwa Ibrahim na Ismail na Is-haaq na Yaaquub na wajukuu zake ambaye mmesilimu kwake Je huyo ni munga gani?
◆ Kila anayekataa kuingia kwenye uzao wa Isaka, hana nafasi katika mbingu za Mungu aliyeumba mbingu na nchi.
Hana! Hana! Hana!
◆ Lakini Mungu akasema:
Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. (Mwanzo 17:18-20).
Kwa hiyo, agano la milele kati ya Mungu na Ibrahimu halikumhusisha Ishmaeli hata kidogo japokuwa alikuwa naye
ni mwana wa Ibrahimu. Kwa maana hiyo, halimhusu Muhammad.
Agano linatoka kwa Mungu wa– Ibrahimu – Isaka – Yakobo – Yesu. NA SIO Ishmael wala Muhammad!
Maana yake ni nini?
◆Maana yake ni kuwa mwanadamu yeyote akitaka kuingia kwenye agano la kulindwa, kubarikiwa, kuponywa na kupata uzima wa
milele, ni lazima apitie upande wa Isaka na kamwe si upande
wa Ishmaeli.
◆waislam msipogeukaa mtaingiaa motoni.
Tukijaa hoja ya pili kwa madai wanaodai Yesu ni mwislam, hebu tuone madai yao.
◆Kutoka kwa Yesu: “Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali:” (Biblia, Mathayo 26:39) basi hapo wansema kuwa Yesu ni mwislam, kisa, eti kasujudu.
◆Kwa hoja napata hunzuni na majonzi makubwa sana kwa ndugu zangu waislam maana haiwezekani kuleta hojaa hii dhaifu kiasi hiki? Kwa mantiki hii basi kila kiumbe kinacho sujudu ni muislam!
Je, Tunafanyaje Ibada?

Biblia inatufahamisha jinsi watu walivyotumia mioyo yao, mawazo yao, mikono yao, viganja vyao, miguu yao, na midomo yao katika uimbaji. Walipaza sauti zao kwa furaha na kusujudu, kucheza, kusifu, kubariki na kushukuru.
Maneno kama halal na haleluya kutoka katika Zaburi yana maana ya kusifu, kumwinua na kumwadhimisha Bwana. Neno Yadah lina maana ya kunyoosha mikono hewani, na neno barak lina maana ya kupiga magoti katika ibada ya kumbariki Mungu.
Kuitoa miili yetu katika kumhudumia Mungu na mwanadamu ni ibada pia (Rum 12:1). Watu pia humwabudu Mungu katika sanaa zao, katika uandishi wao, katika michezo ya kuigiza, katika muziki, katika usanifu wa majengo, na hata katika utoaji wa fedha zao kwa ajili ya Injili.
SWALI
Ni wapi Yesu alisilimu na kuwaa mwislam? Maana Yesu yeye alibatizwa na Ubatizo sio sifa na au haupo kwenye Uislam.
Basi kama mnasema Yesu mwislam kwanini msimfuate na kubatizwa kama yeye maana yeye ndiyo njiaa ya kweli na uzima (Yohana14;6)
HITIMISHO
◆Na kwa msingi huu, yeyote anayekumbatia Quran,
(ambayo asili yake ni Ishmaeli au Uarabuni), anakumbatia
utumwa na kukataliwa na Mungu. Lakini yule anayekubali Biblia (ambayo asili yake ni Isaka au Yerusalemu), anakumbatia uhuru na kukubaliwa na Mungu.
Tafakari
Hoji mambo
Chukua hatua
Njoo kwa Yesu.
Sheikh Mstaaf Eden H
Imeratibiwa na Max Shimba
For Max Shimba Ministries Org.

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW