Saturday, July 2, 2016

BIBLIA NA QURAN VITABU VYENYE NGUVU SANA


1. BIBLIA NI KITABU CHA MWENYEZI MUNGU "YEHOVA"
2. QURAN NI KITABU CHA ALLAH AMBAYE SIO MWENYEZI MUNGU
Historia ni kama ghala kubwa ambamo kumehifadhiwa kila kitu. Tunapochungulia kwenye ghala hili, tunaweza kujifunza kuhusiana na wapi tumetokea, na hatimaye wapi tuliko na kule tunakoelekea.
Bila shaka Biblia na Quran ni vitabu viwili ambavyo vina umuhimu mkubwa sana kwa wanadamu na ulimwengu. Hivi ni vitabu ambavyo ndivyo vinavyoumba maisha halisi ya idadi kubwa sana ya watu. Haya si tu maisha ya kula, kunywa na kuvaa hapa duniani, lakini pia vinaaminika kuwa vimebeba hatima ya milele yote kuhisiana na kila mwanadamu.
Ni wazi kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kuamini na kutumainia kitu kisicho cha kweli kama anajua kuwa kitamletea hasara, na hasa kupoteza uzima wa milele. [Lakini hata kama atakiamini ilhali anajua kuwa si cha kweli, basi huyo anakuwa anataka faida fulanifulani za muda mfupi; yaani hata huyu naye hawezi kuamini kitu kwa lengo la kupata hasara].
Kwa mtu anayethamini na kuitafuta kweli, bila shaka atakuwa tayari kujifunza kutoka kwenye historia.
******************
Biblia na Quran zinatofautiana katika mambo mengi, lakini napenda nizungumzie machache, ambayo naamini yanaweza kutusaidia kujibu swali hili kwamba: Kati ya Biblia na Quran, kitabu kipi kinastahili kuaminika?
KUHUSU BIBLIA
Zifuatazo ni sifa za Biblia:
Idadi ya waandishi
Biblia ni kitabu kilichoandikwa na waandishi takribani 40. Waandishi 30 waliandika Agano la Kale na waandishi 10 waliandika Agani Jipya.
Nyakati
Waandishi wa Biblia waliishi katika nyakati tofautitofauti.
Kwa muda gani?
Kuanzia wakati wa Musa hadi wakati wa akina Paulo na Yohana, ilichukua miaka zaidi ya 1500 kupata kila kitu ambacho ndicho kimekuja kuwa Biblia hii tunayoifahamu.
Aina ya waandishi

Biblia haikuandikwa na watu wa aina moja. Badala yake kulikuwa na aina mbalimbali za watu. Kulikuwa na wafalme, kwa mfano Sulemani hadi watu wa chini kabisa, kama vile akina Petro ambao walikuwa ni wavuvi waishio kijijini.
Lugha
Kwa asili, Biblia iliandikwa kwa lugha mbalimbali, yaani Kiebrania, Kiaramu na Kigiriki. Baadaye ndipo lugha hizi zikaja kutafsiriwa katika lugha karibu zote duniani hivi leo.
Mitindo ya uandishi
Biblia imeandikwa kwa mitindo mbalimbali ya uandishi. Kwa mfano:
Historia au masimulizi - Kutoka, Hesabu, Yoshua, Nyakati, n.k.
Sheria – Walawi na Kumbukumbu la Torati
Ushairi – Wimbo Ulio Bora na maombolezo
Unabii – Yeremia, Ezekieli, Habakuki, Yoeli, Malaki, Danieli, n.k.
Nyaraka au barua – Warumi, wakorintho, Waefeso, Yakobo, Petro, n.k.
Mafunuo – Ufunuo
Jinsi ujumbe ulivyokuja
Ujumbe wa Biblia ulikuja kwa njia mbalimbali ambazo ni za kawaida kabisa. Kwa mfano:
Mungu kuongea moja kwa moja na wanadamu. Mathalani aliongea na Adamu (Mwa. 2:16-17), Nuhu (Mwa. 6:13-21), Ibrahimu (Mwa. 12:1-3; 22:1-2) na Musa (Kut. 3:4; 4:16).
Kwa njia ya maono. Kwa mfano, alisema kwa njia ya maono na Ibrahimu (Mwa. 12:7; 15:1), Yakobo (Mwa. 46:2; 28:12-17), Isaya (Isaya 6:1-10), Ezekieli (Eze. 1:1-28; 10:1-22), n.k.
Kupitia historia ya kawaida ya maisha ya Waisraeli. Ndio maana historia hiyo imeandikwa na sisi tunajifunza kweli za kiroho kupitia maisha yao ya kimwili.
HII MAANA YAKE NI NINI?
Maana yake ni kuwa, kwa vile Biblia imeandikwa kwa muda mrefu sana, na watu wengi, na watu tofauti, ambao hawakujuana, walioishi nyakati tofauti, walioishi sehemu tofauti, waliokuwa na elimu na vyeo tofauti, basi tungetarajia kuwepo na mgongano, msigano, na tofauti kubwa kabisa katika ujumbe wake. Isingewezekana kabisa kibinadamu:
Kuwepo na ujumbe unaofanana kwa watu wote hao
Kuwepo na mtiririko safi unaoendana kimantiki na kukubaliana kabisa na majira na nyakati
Maana yake nyingine ni kwamba, ukweli huu unatoa ishara ya wazi kwamba Biblia imetoka kwenye chanzo kimoja tu. Wanadamu walioandika walikuwa wanatumiwa kama vyombo tu na huyo Mwandishi halisi ambaye ni Roho Mtakatifu. Ndiyo maana ujumbe wa watu wote unaendana na kukubaliana sawasawa licha ya tofauti zao kubwa namna hiyo.
KUHUSU QURAN
Quran ni kitabu ambacho, kama inavyoshuhudia Quran yenyewe, kilitokana na kushuka kwa aya kutoka kwa Allah. Aya hizi alipewa Muhammad, ambaye sasa kutoka kwake zilifika kwa wanadamu. Kwa hiyo, yafuatayo ni mambo kuhusiana na Quran pamoja na ujumbe wake:
Idadi ya waandishi
Quran imeandikwa na mwandishi zaidi ya mmoja. Kama Muhammad alipokea kweli hicho anachosema au hakupokea ni vigumu kuthibitisha.
Nyakati
Kama mwandishi alikuwa mmoja, basi aliishi kwenye wakati mmoja tu alipokuwa hai.
Kwa muda gani? Madai:
Muhammad alipokea aya za Quran kwa muda wa miaka 23 tu.
Aina ya waandishi
Kwa vile ‘mwandishi’ wa Quran wanadai ni mmoja tu, hatuwezi kuongelea suala la aina za waandishi katika hii mada.
Lugha
Lugha iliyotumika kuandika ujumbe wa mwanzo wa Quran ni moja tu.
Mitindo ya uandishi
Kwa ujumla Quran ina aina moja tu ya uandishi, ambayo ni aina ya kuambiwa.
Jinsi ujumbe ulivyokuja
Ujumbe wa Quran ulikuja kwa njia tofauti na ule wa Biblia.
[Tafsiri: Ubada bin Samit alisema kwamba wakati wahyi alipomshukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yake), alijisikia mzigo kutokana na hali hiyo na rangi ya uso wake ilibadilika. (Sahih Muslim, Vol. 4, 1248)]
[Tafsiri: Hakika, al-Harith Ibn Hisham alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ufunuo huwa unakujaje kwako? Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ambariki, alisema: Wakati mwingine huja kwangu kama vile sauti ya kengele, na hii huwa ngumu sana kwangu; (hatimaye) unakoma na mimi ninakumbuka kile kilichosemwa. Wakati mwingine malaika hunitokea na anaongea na mimi nami hukumbuka yale aliyosema. Ayishah alisema: Nilishuhudia ufunuo ukimjia katika siku ambayo ilikuwa ya baridi kali sana; ulipomalizika, niliona kwamba uso wake unatoka jasho. (Ibn Sa'd, Kitab al-Tabaqat al-Kabir, Vol. 1, uk 228.)]
[Tafsiri: Mtume aliongeza, "Malaika alinikaba (kwa nguvu) na kunikandamiza kwa nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili zaidi. Kisha aliniachia na kwa mara nyingine akaniambia nisome, nami nikamjibu, 'Mimi sijui kusoma.' Hapo alinikaba tena (kwa nguvu) na kunikandamiza kwa nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili zaidi. Aliniachia na kwa mara nyingine akaniambia nisome, nami nikamjibu, 'Mimi sijui kusoma.' Hapo alinikaba tena na kunikandamiza na kuniachia kisha akasema, “Soma kwa jina la Mola wako ambaye ameumba (vyote) Amemuumba mtu kwa bonge la damu. Soma! Na Mola wako ni mwingi wa ukarimu." Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu alirudi na wahyi huku moyo wake ukidunda kwa nguvu. Kisha akenda kwa Khadija binti Khuwailid na akasema, "Nifunike! Nifunike!" Nao wakamfunika mpaka hofu ilipomwishia na baada ya hapo akawasimulia kila kitu kilichomtokea na akasema, "Naogopa kwamba kuna kitu kinaweza kunitokea." Khadija alijibu, "Hapana! Kwa jina la Allah. Allah hawezi kukuaibisha. Una uhusiano mzuri na ndugu zako, unasaidia walio maskini na fukara, unawafanyia ukarimu wageni wako na kusaidia wenye misiba wanaostahili." (Sahih Al-Bukhari, Volume 1, Kitabu 1, Namba 3)]
………………………
Desturi za Kiislamu ziko kinyume na matumizi ya kengele kwani zinatajwa kuwa ni vyombo ya shetani. Desturi hizi hata zinasema kwamba malaika hawawezi kuwasaidia wale wanaobeba kengele. Ona mifano ifuatayo:
Abu Hurairah alisimulia kwamba Mtume (amani iwe juu yake) alisema: kengele ni ala ya muziki ya Shetani. (Sahih Muslim, Kitabu 024)
Imesimuliwa na Umar ibn al-Khattab: Ibn az-Zubayr alisema kwamba mteja wao mwanamke alimpeleka binti wa az-Zubayr kwa Umar ibn al-Khattab akiwa amevaa kengele miguuni mwake. Umar alizikata na kusema kwamba alikuwa amesikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yake) akisema: Kuna shetani katika kila kengele. (Sunan Abu Dawud, Kitabu 34)
Abu Hurairah alisema kwamba Mtume (amani iwe juu yake) alisema: Malaika huwa hawamsindikizi msafiri ambaye ana mbwa na kengele. (Sahih Muslim, Kitabu 024)
Imesimuliwa na Ummu Habibah: Mtume (amani iwe juu yake) alisema: Malaika huwa hawaongozani na watu wanaosafiri huku wana kengele. (Sunan Abu Dawud, Kitabu 14)
…………………………..
Swali linalokuja kwetu ni kwamba, mtume alipoulizwa ni vipi huwa anapokea wahyi (ufunuo), mojawapo ya njia alizozitaja ni kwamba, upo ufunuo ambao huja kwa sauti kama za kengele. Na hapa anasema kuwa kengele zinahusiana na shetani. Hapo inakuwaje?
Hitimisho
Rafiki uliyesoma makala haya, unapolinganisha vitabu hivi viwili (Biblia na Quran), unadhani ni kipi kinastahili kuaminiwa?
Siulizi kwamba unaamini kipi? Maana nadhani tayari unacho kile unachokiamini. Lakini swali langu ni kwamba, Kipi kinastahili kuaminiwa?
Tafakari
Hoji mambo
Jiulize
Chukua hatua.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW