Saturday, July 23, 2016

ATHARI YA MKRISTO KUOANA NA MUISLAMU



Imekuwa ni jambo la kawaida kushuhudia Wakristo na waislamu wakiishi pamoja kama mke na mume, na wengi wao huona ni jambo sahihi, kwa sababu Mungu wetu ni mmoja, kwa hivyo hata kama ataolewa na muislamu, hakuna tatizo kwake, tena kama ataoneshwa mapenzi ya dhati kwa kipindi fulani, basi hapo atajiona kuwa amefika sehemu salama, na wengine hujitetea kupitia andiko ambalo Paulo alitoa ushahuri kuhusiana na mtu aaminie kuishi na mtu ambae hana imani kama yake:
1 Korintho 7:12 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika
Andiko hili Watu wengi hulitumia vibaya, wakidhani kwamba, limewapa ruhusa ya Mkristo kuolewa na mtu ambae si Mkristo, Kwanza hapo naomba ifahamke kwamba, katika maelezo hayo ya PAULO, hakuna ndoa baina ya mtu asie amini (Asiye Mkristo) na Mkristo ambae ameamini, ndiyo maana Paulo akasema:
1 Korintho 7:15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
Amesema huyo asie amini kama ataamua kundoka, basi ni ruksa kwake kuondoka, na hapo hapatakuwa na kizuizi cha Mkristo kuoa au kuolewa, ushauri huo hakumlenga Mkristo na Muislamu, bali ulilenga juu wa watu ambao Walipelekewa Injili huko Korintho, kuna baadhi ya watu ambao walilipokea neno, wakaamini, lakini wengine hawakukubali, na miongoni mwa wale ambao hawakukubali, walikuwa tayari wanaishi na kama mume na mke na wale ambao wamekwisha kuamini, kwa hivyo Paulo hakutaka kuwatenganisha, akawataka wale walioamini waendelee kuishi nao, kwa ushauri wake Paulo, na si agizo la Yesu, maana aliamini kwamba kupitia jambo hilo, huyo asie amini anaweza kuongoka kupitia mume au mke alie ongoka, ila kwa wale ambao walioana katika ndoa inayokubalika kwa Mungu, aliweka msimamo wa Yesu mwenyewe akasema:
1 Korintho 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
Hapo aliposema kuwa waliokwisha kuoana, maana yake wale ambao ndoa zao zinatambulikana na Mungu, (Hawakuchukuana tu na kuanza kuishi pamoja) bali hao ni wale ambao tayari wameshaunganishwa na Mungu, kwa kufuata taratibu zote, akasema hakuna ruhusa ya kuachana, kama ilivyo kwa mtu asie amini na aaminie, hata kama mmefunga ndoa, ikatokea mmoja akakengeuka, hakuna ruhusa hiyo ya kuachana, mke akae bila kuolewa, na mume nae pia akae bila kuoa.
Mathayo 19:5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Kwa mafundisho haya ya Yesu, ni dhahiri kuwa, hakuna idhini ya Mke kumwacha mumewe, wala mume kumwacha mkewe, kama ulikurupuka, ukaja kumuona mwanamke mwingine ukataka awe mkeo, ukataka umwache mkeo, basi huna idhini hiyo, wala huna ruhusa ya kumpa talaka na kuoa mwingine:
Lakini ukija upande wa pili wa Uislamu, kama kuna mwanamke ambae anaishi na muislamu, hata kama wamekaaa mika 10 akiwa peke yake, asidhani kwamba, ndo dini yao nayo pia ipo kama ya Kikristo kwamba mke mmoja na mume mmoja, yaani Double M, Hapana, yeye ameambiwa hivi:
Quran 4:3. Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, (madam mtawafanyia Insafu) wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja tu, au (wawekeni masuria)wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea kutofanya jeuri.
Hapo anaambiwa kuwa, aanze kuoa wawili, au watatu, au wanne, kama anao uwezo wa kufanya uadilifu, wewe jiulize, moyo wa mtu unaweza kuwapenda watu wanne kwa upendo mmoja? Pia kama hawawezi kufanya uadilifu, basi waoe mke, mmoja, sasa wewe ambae umeishi nae kwa mika 10 au zaidi, au chini ya hapo, usidhani kwamba, dhamira yake ni hiyo ya kuishi na wewe tu la, bali anahitaji kuongeza mke wengine akupangeni kama mafungu ya nyaya, ila bado hela hazijamtembelea, siku zikimtembelea, basi ataoa, na pia ukiwa peke yako, usidhani upo peke yako, ameambiwa akiwa na mke moja, basi ajiweke masuria, (Vimada) ili kukufanya wewe usilete jeuri, kwa hivyo usiku ukimzingua, ameambiwa akupe kichapo
Quran 4:34. Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu, waonyeni, waacheni peke yao katika vitanda na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu.
Mwanume akikuacha peke yako kitandani, unadhani anenda wapi? Ni kule kwa wale vimada wao, pia tambua kuwa anaishi na wewe kama adui yake, pia ujue kuwa, Mwanume wa kiislamu, unaweza kuwa umejifunika shuka moja nae, mnafanya mapenzi, anakuchekea, ukadhani anakupenda kwa dhati, tambua kuwa moyoni mwamke wewe ni adui yake, kama isemavyo Quran
Quran 64:14. Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu
Lakini sisi Wakristo, hatujaambiwa tuwafanye wanawake kuwa maadui zetu, bali tuwapende wake zetu
Waefeso 5:25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Waefeso 5:28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
Hayo ndiyo maagizo ya BIBLIA, tuwapende wake zetu kama miili yetu, maana mwili wako uwezi kuupiga, lakini kwa waislamu, kichao ruksa, jao wanajaribu kupoza kwa kusema eti umpige kwa kipande cha Kanga. Sisi tumeambiwa kuwa, Wanawake ndiyo walinzi wa wanaume,
Yeremia 31:22 Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.
Hapo kuna hekima kubwa sana kwa mwanamke kumlinda mumewe, maana mwanamke ndiye mwenye kutupikia, kutufulia, kwa hivyo wanatulinda, hawatuwekei sumu, wala upupu kwenye nguo zetu, na kwa kutambua kuwa, hawa wanawake ni walinzi wetu, ndiyo maana tukaambiwa tuwapende, tuwajali, ili wafanye ulinzi kwetu, unadhani ukimpiga mwanamke na kumtesa, unamjengea mazingira gani? sasa kwa upande wa pili, mwanaume ndiye anaemlinda mwanamke,
Dada yangu ambae unaishi na Muislamu, usibweteke ukajisahau, ukadhani kwamba, eti ndiyo umefika, wewe ndiye mwanamke pekee wa maisha yake, anakupenda hivyo kwa sababu, bado upo mbichi, kifuani unalipa, (saa 6) wowo lipo, subiri siku umeanza kuchuja, akijisikia kuwa, hana haja nawe tena, ameona kifaa kipya, basi anayo ruhusa ya kukupa Talaka wewe ulie choka, na kuchukua kifaa kingine kipya,
Quran 4:20. Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, (yaani kumwoa mke mwengine na kumwacha huyo wa zamani) na hali mmoja wao (nae ndiye huyo nae mwacha) mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi?
Hapa katika Tafsiri ya Quran ya Sheikh Abdulla Saleh Farsy, imeweka wazi kuwa, muislamu anayo ruhusa ya kuoa mke mwingine mpya, yaani wewe ambae umeishi nae ka mika 10 unakuwa used, anahitaji kitu kipya (New) unakuwa kama Screpa, au gari linalowekwa juu ya mawe, anachukuliwa mwaanamke mwingine, suala kubwa la kujiuliza, ni nani alie kufanya uchakae kama siye yeye? Tena pengine amekuwa anakutumia kingono kwa sana kiasi kwamba anakuzalisha watoto kibao, matunzo unakosa, unachuja, sasa anaamua akuache, aoe mke mwingine mpya, safi, mwenye kupendeza, sasa wewe unae achwa, nani atakuoa tena wakati umeshakuwa Screpa? Hivi anaestahili kuwa wazamani ni nani kati ya mwanamke na mwanaume? Maana mwanaume umri wake huwa ni mkubwa, mzee wa miaka 50, anamwacha mkewe wa miaka 40, anaenda kuoa kifaa kipya cha miaka 18, eti yeye Mwanaume bado mpya, ila mkewe ameshakuwa wa zamani, Lakini kwa Yesu, mambo hao hakuna, maana hata Wayahudi, nao pia walitaka tabia hiyo ya kuwaacha acha ovyo wanawake, kama ilivyokuwa kwa Musa, iendelee, pale walipomkumbushia, wakimwambia:
Mathayo 19:7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
Ni kweli kwamba Musa alitoa ruhusa ya Talaka, kwa wanawake, kama tunavyosoma hapa:
Kumbu kumbu la Torati 24:1 Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake. 2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.
Wayahudi hao ambao waliuliza swali walidhani kwamba Yesu aweza, kutoa idhini ya kumwacha mwanamke, walidhani ule ulikuwa ni mpango wa Mungu, na kumbe sivyo, kama ambavyo
Yesu aliwafafanulia kwa kusema:
Mathayo 19:8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
Yesu akaweka mkazo kuwa, mwanamke atakae achwa, haruhusiwi kuolewa, hata kama ndoa imevunjwa Mahakamani, mwanamke huyo ahana ruhusa ya kuolewa na mwanamume mwingine kama ilivyo kuwa kwa Musa, maana sheria hiyo iliwekwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu, kwa mwanamke yule kama ataaolewa, basi ajue maisha yake yote atakuwa ni mzinzi tu, na hata kama atakuwa anafanya Huduma ya Mungu, matendo yake mema kwa Mungu yatahesabaika kuwa, ni sawa na mavi tu, maana ni mzinzi, na mzinzi sehemu yake ni motoni, pia Yesu hakumpa ruhusa mwanaume amwachae mkewe aoe mke mwingine, kama ataoa, atakuwa anazini, hata kama atakuwa ni Mchungaji, huduma yake haitafaa mbele za Bwana, kwa sababu kwa Mungu huyo ni mzinzi, kwa hivyo hapo kuna tahadhari kwa wale ambao bado hawajaoa na kuolewa, na wanapenda kwenda mbinguni, wawachunguze kwanza hao ambao wanataka kuoana nao kam,a wana ndoa tayari.
Kwani Mwanamke wa Kikristo, yupo katika kifungo cha ndoa, mpaka mume amekufa, na mme pia nae yupo katika kifungo, mpaka mkewe amekufa, Maandiko yakamkataza Mwanamke wa Kikrito kuolewa na mwanaume pindi mumewe atakapofariki.
1 Korintho 7:39 Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.
Pengine unaweza kujiuliza ni kwa nini Ameambiwa aolewe mwanaume amatake katika BWANA tu? Ni kwa sababu kuna athari kama ataolewa na Muislamu, maana atamkengeusha moyo wake aache kumwabudu BWANA, na kuigeukia miungu mingine, kama waliyo onywa wana wa Israeli.
Kumbukumbu la Torati 7:2 wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;
3 binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake.
4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.
Mataifa hayo ambayo Mungu aliwakataza wana wa israel kuoana nao, ni wale ambao walikuwa wakiabudu miungu mingine kwa hivyo Mungu alijua wazi kuwa kama atawaruhusu kuoana nao, watawakengeusha, na kuwafanya wakaiabudu miungu mingine, kwa hivyo akasema, usimpe binti yako aolewe na mtu ambae hamwambudu Mungu wa Israeli, wala mwanao mume usimtwalie binti kule, maana katika mapenzi anaweza kukolea, na ukashangaa tayari amesha iacha imani, kwa mzazi ambae atamruhusu mwanae aolewe na muislamu, basi ajue kuwa, damu ya mwanae ambae ataenda kusilimishwa na kwenda kuiabudu miungu mingine, Mungu atakuja kumdai mzazi huyo, ngoja nikupe mfano mmoja wa Mfalme Suleman, pamoja na hekima yake aliyokuwa nayo, kupitia wanawake wa kigeni ambao Mungu aliwazuia kuonanao, yeye alipowaoa wanamgeuza moyo wake:
1 Wafalme 11:1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,
2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.
3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.
4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.
6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
Hiyo ndiyo athari ya Mkristo kuoana na muislamu Suleman yalimkuta, wanawake wa Kigeni ambao Mungu aliwazuia waoane nao, wao kwa shingo ngumu, alioana nao, kwa Hivyo Ukamilifu katika Kumwabudu Mungu, haukuwepo tena, kwa hivyo Mkristo usidanganyike kamba, eti Ukiolewa na muislamu, wewe ukabaki kuwa Mkristo wewe yeye akaendelea kuwa Muislamu, basi utakuwa salama, hapana, lazima vikwazo katika kumtumikia Mungu utavipata tu, hutamwabudu Mungu katika hali ya ukamilifu, huwezi kufanya maombi ya nguvu ambavyo Mumeo muislamu atayafurahia, lazima atainua vikwazo kwako, maana kuna nguvu ambazo unaziharibu:
kama sisi Wakristo tutapuuza agizo la Mungu angalia Mungu anavyosema, juu yetu sisi.
Yoshua 23:12 Lakini mkirudi nyuma kwa njia yo yote na kushikamana na mabaki ya mataifa, yaani, mataifa haya yaliyobaki kati yenu, na kuoana nao, na kuingia kwao, nao kuingia kwenu;
13 jueni hakika ya kuwa Bwana, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hata mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo Bwana, Mungu wenu, amewapa ninyi.
Kwa hivyo usione waislamu wanavyowatesa Wakristo katika Nchi nyingi, na mnafanya maombi Ili Mungu alete amani, ana amani haiji, mkadhani kwamba, Mungu amewasahau, hapana Mungu ameamua kuachia adha hiyo, Wakristo wachinjwe, walipuliwe kwa Mabomu, makanisa yachomwe moto, maana hao ambao ametuzuia kuoana nao, tumeoana nao, kwa hivyo wamekuwa mitego kwetu, wamekuwa tanzi na Jeledi mbavuni mwetu, Mungu anatupiga kupitia wao, wamekuwa ni miiba machoni petu, hata hatuwezi kuutazama Wokovu wa BWANA,
Kwa hivyo dada zangu ambao mnapena kuuona ufalme wa Mungu, msizuzuke na mali ambazo waislamu wanazo, mkaamua kukimbilia huko, mjue kuwa adhabu ya Mungu ni kubwa sana na isiyo na kikomo, maana utaadhibiwa milele, Wanawake wa kiislamu, siyo rahisi kubadili dini ili waolewe, sasa iweje ninyi mjirahisi? Hata wanume nanyi, acheni kujirahisi, kusilimu kisa umuoe Mwanamke wa kiislamu, ambae anakukengeusha moyo wako, nanyi pia wazazi, msiwape ruhusa wana wenu kuoana na watu ambao si Wakristo, kwa sababu tu ya tamaa ya mali.
MWISHO: waislamu wana amini kwamba eti kuoa kwao wawake wengi ndo kuwafanya wawe wengi, wanadahani sisi Wakristo kuwekewa sheria ya kuoa mke mmoja, hatuwezi kuongezeka kama wao walivyo na wanawake wanne, wamesahau kuwa, Ng’ombe huzaa mtoto mmoja tu kwa mwaka, na Ng’ombe kila siku wanachinjwa, lakini hawaishi, Lakini Mbwa, anazaa mpaka watoto nane, na Mbwa hana machinjio, wala hana zizi, lakini Mbwa siyo wengi kama Ng’;ombe, kwa nini Ng’ombe wanaochinjwa kila siku na wanazaa mtoto mmoja, ni wengi kuliko Mbwa ambae anazaa watoto kibao na hachinjwi?
Hosea 4:10 Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka; kwa sababu wameacha kumwangalia BWANA..
Kwa hivyo kuoa wanawake wengi, na kuzaa watoto wengi, hakumaanishi kwamba, eti wao watakuwa wengi, Mungu amesema, Waislamu watafanya zinaa sana lakini hawataongezeka kwa sababu wamemuacha BWANA. Kwa hivyo BWANA nae amewaacha, kwa hivyo hata kama kuna Manabii na watu ambao waliwahi kuoa wake wengi, Yesu ameshasema kuwa, ni ugumu wa mioyo yao, lakini si mpango wa Mungu, zama zile za Ujinga zimeshapita, kwa sasa hivi Mungu anatutaka tutubu
Matendo 17: 30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.
31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
MUNGU AKUBARIKI WEWE AMBAE UTACHUKUA HATUA, NA KUYAONA MAISHA YA MBINGUNI NI BORA ZAIDI.
Imeletwa kwenu na Abel Suleiman Shiriwa
By permission
Max Shimba Ministries Org.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW