Friday, July 8, 2016

ADAM, MUSA, IBRAHIM, ISMAIL, NA DAUDI HAWAKUWA WAISLAM


Ndugu msomaji,
Waumini wa dini ya Kiislam wamekuwa na tabia ya kusema kuwa, eti, Adam, Musa, Ibrahim, Ismail, na Daudi walikuwa ni Waislam. Madai haya ya Waislam yamekuwa yakisemwa katika mihadhara yao ya kidini bila ya kuwa na ushaidi yakinifu na wa aya ili kusaidia madai yao.
Leo nitajibu madai haya kwa kutumia Biblia na Koran kama ifuatavyo:
ADAM, MUSA, IBRAHIM DAUDI HAKUWAI SEMA SHAHADA
Kufuatana na sharia za Kiislam, ili mtu awe Muislam lazima aseme na au afanye shahada. Adam, Musa, Ibrahim, Ismail na Daudi hawakusema SHAHADA (la ilaha illallah muhammadur rasulullah) na hakuna ushaidi wa Kibiblia, Historia au Koran unao sema kuwa Adam, Musa, Ibrahim, Ismail, na Daudi walisema SHAHADA. Hivyo basi, Adam, Musa, Ibrahim, Ismail, na Daudi hawakuwa Muislam.
SASA NITAANZA KUHOJI UISLAM KWA KUPITIA QURAN, KAMA KWELI ADAM, MUSA, IBRAHIM, ISMAIL, NA DAUDI WALIKUWA WAISLAM:
ALLAH ANASEMA KILA UMMA AMEUPA KITABU NA MTUME:
Soma;
Quran 10: 47. Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
Angalia hii aya pia
Quran 14: 4. Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Dhana hii ya Allah kushusha Kitabu kwa kila lugha ni muhimu sana kwasababu imejirudia mara nyingi na ndio msingi wa hili somo.
ALLAH ANASEMA KILA UMMA ALIUTUMIA MTUME:
Quran 16: 36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
NABII ADAM::::::::::::::::::::
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA ADAM NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:
Kama kweli Allah aliteremsha Kitabu kwa kila Umma, na Adam ni Nabii wa Allah, basi ningependa mnijibu maswali yafuatayo:
1. ADAM alipewa kitabu gani, naomba mtuwekee nakala yake hapa na mtuambie jina la hicho Kitabu.
2. ADAM alikuwa Nabii wa Umma gani, wakati yeye ndie alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa? [Naomba mtutajie jina la Umma wa Nabii Adam]
3. Tuleteeni ushahidi wa aya kwenye hicho kitabu cha ADAM kuwa ADAM alisema shahada.
NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya hakupewa Adam.
NABII MUSA:
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA MUSA NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:
Allah anaendelea kusema kuwa aliteremsha Taurat kwa Nabii wake Musa.
Surat Al Baqara 136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.
Kama kweli Musa alipewa na au teremshiwa kitabu na Allah, basi naomba mnijibu maswali yafuatayo:
1. Kipo wapi na au ipo wapi NAKALA YA TAURAT ambayo Allah aliiteremsha kwa Musa kabla ya Quran?
2. MUSA alikuwa Nabii wa UMMAH gani? Naomba muutaje huo Ummah kwa jina.
3. Tuleteeni ushahidi wa aya kwenye hicho kitabu cha MUSA kuwa MUSA alisema shahada.
NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya sio Taurat ya Musa iliyo teremshwa kabla ya Quran.
NABII IBRAHIM:
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA IBRAHIM NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:
Quran 10: 47. Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
Angalia hii aya pia
Quran 14: 4. Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
S. 3:67 Shakir: Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.
Allah amesema kila Umma ulipewa Nabii na ujumbe "Kitabu" na Ibrahima alikuwa Muislam, SASA BASI.
1. Waislam, Nitajieni jina la kitabu ambacho Ibrahim alipewa na Allah?
2. Nileteeni ushahid wa aya kutoka hicho kitabu kuwa Ibrahim alisema Shahada.
3. Nitajieni jina la Ummah ambao Ibrahim alikuwa Nabii wake?
4. Allah anasema kuwa Ibrahim hakuwa Yahudi wa Mkristo, kama hayo madai ni kweli, KWANINI WAISLAM WANASEMA KUWA UKRISTO ULIANZISHWA NA PAULO, huku ALLAH ANAKIRI KUWA HATA WAKATI WA IBRAHIM KULIKUWA NA UKRISTO?
NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya sio Kitabu ambacho Ibrahim aliteremshiwa kabla ya Quran.
NABII DAUDI:
ALLAH NA WAISLAM WANASEMA KUWA DAUDI NI NABII NA ALIKUWA MUISLAM:
ALLAH ANASEMA "NA DAUDI TUKAMPA ZABURI :
Surat An Nissai aya 163, Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi. S. 4:163
Kama ni kweli Allah aliteremsha Zaburi kwa Daudi, basi maswali yafuatayo lazima yapewe majibu:
1. Daudi alikuwa Nabii wa Ummah upi, naomba Waislam muutaje huo ummah kwa jina.
2. Ipo wapi NAKALA YA ZABURI ambayo Allah aliiteremsha kwa Daudi kabla ya Quran?
3. Daudi alipokea hiyo Zaburi akiwa Mji gani?
4. Leteni aya kutoka Zaburi aliyo iteremsha Allah kabla ya Quran ambayo DAUDI anasema SHAHADA.
NOTE: Aya za Quran sina muda nazo maana hizo aya sio ZABURI ambay iliteremshiwa kabla ya Quran.
MKINILETEA UTHIBISHO WA MASWALI YANGU HAPO JUU,
BASI LEO HII NITASILIMU NA KUWA MUISLAM
Katika huduma yake,
Max Shimba Ministries

2 comments:

Unknown said...

ukiona hujibiwi ujue watu wamekupuuza maana huna hoja unajikanyaga mwenyewe kukujibu mtu kama ww ni kupoteza muda ni heri kutumia muda kuelimisha wanataka kuekimika ww ni mtu wa motoni kwahyo hakuna haja ya kukupatia maarifa malizia kula Hela za kabisa alafu ukakae jahannam

Unknown said...

ukiona hujibiwi ujue watu wamekupuuza maana huna hoja unajikanyaga mwenyewe kukujibu mtu kama ww ni kupoteza muda ni heri kutumia muda kuelimisha wanataka kuekimika ww ni mtu wa motoni kwahyo hakuna haja ya kukupatia maarifa malizia kula Hela za kabisa alafu ukakae jahannam

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW