HAKIKA YESU NI MUNGU
Ndugu msomaji:
Jambo hili si mzaha wala uzushi bali ni kweli; Yesu Kristo anakuja kuhukumu ulimwengu wote pamoja na Muhammad na Waislam wote. Yesu Kristo ametutamkia kwa kiywa Chake kwa kusema kwamba;
“Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.” (Yohana 5:22,23)
Hukumu ya mwisho ambayo itakuja baada ya ufufuko. Mungu Baba, kupitia Yesu Kristo, atamhukumu kila mtu ili kuamua utukufu wa milele atakaoupokea. Hukumu hii itategemea utiifu wa kila mtu kwa amri za Mungu, ikiwa ni pamoja na kukubali kwake kwa dhabihu ya upatanisho Yesu Kristo ya kutulipia dhambi.
Baba amekabidhi hukumu yote kwa Mwana "Yesu Kristo": Yohana. 5:22.
Hapa tunajifunza kuwa atakaye toa hukumu ya nani kupokea taji la uzima wa Milele na nani kutumbukizwa Jehannam ni Yesu na sio Allah wa Waislam.
Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo: Warumi. 14:10.
Sisi sote inamaanisha PAMOJA NA MUHAMMAD NABII WA ALLAH.
Wafu walihukumiwa kutokana na mambo yale yaliyokuwa yameandikwa: Ufunuo. 20:12.
Katika hukumu siku ya kiyama hatutegemei kumwona YEHOVA akija kuhukumu ulimwengu, bali, Yesu Kristo ndiye ajaye kuhukumu ulimwengu. Hii itakuwa hivyo ili WATU WOTE WAMHESHIMU Yesu sawa sawa na jinsi ambavyo wanamheshimu YEHOVA. Hapo ndipo viumbe vyote watathibitisha kuwa Yesu ni Mungu. Biblia Takatifu inasema kwamba:
“...kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA...” (Wafilipi 2:10,11)
“...kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA...” (Wafilipi 2:10,11)
Kama unataka kuokoka sasa hivi; Tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa kutamka kwa kinywa chako sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu yote. Ninatubu kwa dhati ya kweli kutoka rohoni mwangu. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho Wako – Uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Nakuomba unifanye niwe vile utakavyo mimi niwe. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina."
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zote zimesamehewa kabisa.
Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Mungu awabariki sana,
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
No comments:
Post a Comment