Sunday, June 19, 2016

YESU ANAKIRI KWA MDOMO WAKE KUWA YEYE NI MUNGU

Ndugu zanguni, leo YESU anawajibu Waislam kwa mara nyingine tena kuwa yeye ni Mungu, "YESU NI MUNGU".
Hii aya hapa chini katika kitabu cha Ufunuo ni ya Yesu mwenyewee akiongea na Yohana. Yesu anakiri kuwa yeye ni Mungu. Hebu tuisome kwanza:
Ufunuo 21: 6 Yesu Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yo yote. 7 Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, NAMI NITAKUWA MUNGU WAKE, naye atakuwa mwanangu.
Mara nyingi kumekuwa na mtanashi kutoka Waislam kuwa eti Yesu hakuwai sema yeye ni Mungu. Mara zote wamekuwa wakidai kuwa, tuwaletee aya ambayo Yesu anasema yeye ni Mungu. Ingawa, Biblia imewajibu kuwa Yesu ni Mungu kutoka sehemu mbalimbali, lakini wamekuwa wabishi na kung'ang'ania waletewe aya, ili wabatizwe na kuwa Wakristo. Kwasababu Biblia imekamilika na haina shaka ndani yake. Leo Biblia inawajibu tena kuwa Yesu ni Mungu.
Aya ya 7 inasema kuwa, NUKUU: [Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, NAMI NITAKUWA MUNGU WAKE, naye atakuwa mwanangu.]
Yesu amekiri kuwa mtu yeyote yule atakaye urithi ufalme wake, basi ifahamike kuwa.
Moja: Yesu atakuwa Mungu wake
Pili: Wewe utakuwa Mwana wake.
Huu ni ushaidi mwingine kuwa Yesu ni Mungu. Waislam, ningependa mfahamu kuwa, Yesu ni Mungu kama ilivyo andikwa kwenye Ufunuo Sura 21 na aya ya 7.
Je, Upo tayari kumfuata Yesu ambaye ni Mungu? Kumbukeni kuwa, Yesu ndie Njia pekee ya kwenda Mbinguni. Dini haita wapeleka popote pale, lakini Yesu Kristo aliye hai ambaye sasa tunasoma kukiri kwake kuwa yeye ni Mungu, ndie njia pekee ya Uzima wa Milele.
Mpokee Yesu leo ili upate uzima wa milele.
Katika Huduma yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Kwa Max Shimba Ministries Org 2014

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW