Saturday, June 18, 2016

UTHIBITISHO WA KIMAANDIKO KUHUSU MWILI WA ALLAH

Ndugu zanguni,
Natanguliza kwa kusema huu ni Msiba Mkubwa sana kwa ndugu zetu kwa kupitia Adam wanao pinga kuwa Allah hana mfano.
Leo nitawawekea mifano kadhaa kama ushahid kuwa Allah ni kiumbe.
Haya, ungana nami moja kwa moja na tujifunze kuhusu huyu Allah kiumbe.
ALLAH ANA-VAA NGUO KAMA VIUMBE
الكبرياء ردائي والعظمة إزاري
Allah ansema katika Hadithi hii Qudsi "Ukuu ndi vazi langu la juu na utukufu ndio vazi langu la chini".
Sasa kama Allah anavaa nguo inamana kuwa Allah ana mwili kama viumbe?
Msiba huu ni mkubwa sana ndugu wasomaji.
Katika Hadithi nyengine Qudsi, Allah anasema: "….Na mja wangu hajikurubishi kwangu kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko yale niliomfaradhishia juu yake. Na mja huwa anaendelea kujikurubisha kwangu kwa nawafil (ibada zisizo za lazima) mpaka nampenda: "فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به، وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله) (التي يمشي بها" Basi nikimpenda nakuwa (Mimi ndio) sikio lake analosikia kwalo, na jicho lake analoonea na mkono wake anaoshikia na mguu wake anaoendea."
Hapo Allah kesha kiri kuwa yeye ana masikio, mikono na macho.
ALLAH ANAKAA KWENYE KITI KAMA VIUMBE
Katika Sura 69:17 Surat al-Haaqqah tunasoma maneno haya:
“Na malaika watakuwa kandoni mwake na malaika wa namna nane watachukua kiti cha enzi cha Mola wako juu ya…”
Tena katika Sura 85:15 Syrat Buruj inamtaja Mungu wa Waislamu aitwaye Allah kuwa yeye ndiye mmiliki wa kiti cha enzi.
Swali ambalo napenda kuwauliza Waislamu wote Allah kumiliki kiti cha enzi. Je, kiti hicho anakifanyia nini? Huenda watu wakanishangaa. Nasema hivyo nikiwa na maana ya je, Allah naye anakaa katika kiti kama wakaavyo wanadamu? Je, ana miguu kama mwanadamu kama anakaa kama mwanadamu katika kiti cha enzi, basi haikosi hana tofauti na mwanadamu.
Angalia katika Sura ya 69: 44-45 Surat Al-haqqah twasoma.
“Na kama (mtume) angelizuia juu yetu baadhi ya maneno tu bila shaka tungalimshika kwa mkono wa kuume”.
Aya hii inaonesha kuwa Allah ana mkono wa kuume. Na kama Allah ana mkono wa kuume atakosaje mkono wa kushoto? Na kama Allah anasema atakosaje mdomo? Basi ondoeni dhana ya kwamba Allah hana mfano.
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW