Saturday, June 18, 2016

KWANINI KWENYE QURAN HAKUNA JINA LA LUSIFA?

ALLAH AMBAYE SIO YEHOVA YAHUH ( يهوه ) HALIJUI JINA LA SHETANI
NDIO MAANA NAENDELEA KUSEMA KUWA ALLAH SIO MWENYEZI MUNGU.
Swali la kwanza la kujiuliza: KWANINI KWENYE QURAN HAKUNA JINA LA LUSIFA?
Ndugu msomaji,
Tunapofikiria juu ya shetani, Je tunakuwa tunafikiria juu ya kitu gani au shetani ni nini? Au ni nani? Je alikuja kutokea wapi? Madhumuni na makusudi yake ni nini? Je, Anatuathiri kwa namna gani? Na ni kwa nini shetani yupo? Je Ana mahusiano gani na Mungu?
NINI MAANA YA SHETANI NA AU SHETANI NI NANI?
Tangu mwanzo Shetani hakuwa anaitwa Shetani, yaani hapakuapo na kiumbe kilichoumbwa na kuitwa Shetani kama ambavyo Quran inadai katika Surat Al Araaf aya ya 11-12.
Lusifa ambalo ndilo jina la Shetani alikuwa ni “mwana wa asubuhi” (Isaya 14:12) yeye pamoja na jeshi lingine la mbinguni,waliumbwa wote wakiwa wakamilifu katika njia zao zote ( Ezekieli. 28:14-19). Kulikuwa na amani na umoja Mbinguni. Kisha mambo yakaharibika. Biblia haiko wazi sana juu ya swala hili ni nini hasa kulitokea na kwa namna gani, ila uovu au kutokumtii Mungu kulioneka kwa Lusifa. Mwishowe alifukuzwa kutoka Mbingini, pamoja na jeshi lake lote lililoasi, wakafukuziwa mbali kabisa kutoka mbinguni na kutupwa, na wanazunguka zunguka katika nchi (duniani).
LAKINI ALLAH ANASEMA HIVI:
Katika Quran Allah anasema alimuumba Shetani kama Shetani tena akiwa na maouvu yake yote:
Surat Al Araaf 11. Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu. 12. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo.
1. Kwanini kwenye Quran hakuna jina la Lusifa?
2. Kwanini Allah aliogopa kuweka jina la Lusifa kwenye Quran?
Allah anadai kuwa eti alimuumba Shetani kama alivyo dai kwenye Surat Al Araaf 11-12 huku YEHOVA anasema kuwa HAKUMUUMBA SHETANI KAMA SHETANI bali alikuwa LUSIFA "Malaika wa Mungu" Kabla ya kuasi.
SHETANI SIO JINA BALI NI WASIFA/MATOKEO WA KAZI/KITENDO ALICHO FANYA. NDIO MAANA NASEMA ALLAH HALIJUI JINA LA SHETANI MAANA KWENYE QURAN HAKUNA JINA LA LUSIFA.
Allah ambaye anaajiita mjuzi wa kila kitu, kwanini ameshindwa kutuambia jina halisi la huyu ADUI MKUBWA WA BINADAMU aitwaye Lusifa?
Waislam wao wanafikiria kuwa eti Neno Shetani ni jina, la hasha. Shetani sio jina bali ni kama wasifa wa kazi anayo itenda Lusifa.
DARASA FUPI KWA WAISLAM:
Mfano: Neno Polisi sio jina bali ni wasifa wa jina/kazi ya mtu fulani ambaye analo jina lake. Vivyo hivyo NENO Mwalimu sio jina bali ni wasifa wa jina/kazi anayo ifanya mtu fulani, wakati huo huyo neno JAMBAZI sio jina la mtu bali ni wasifa wa jina/kazi anayo ifanya mtu fulani anayeweza itwa Abdallah au Juma au Muhammad. Ndio maana inashangaza tunaposoma katika Quran kuwa eti, SHETANI ni jina huku ikifahamika kuwa SHETANI sio jina bali ni matokeo/kazi/tabia/wasifa wa Lusifa alio upata baada ya kuasi mbinguni.
Quran hiyo hiyo inawaitwa watu wanao fanya mambo mabaya ni MASHETWAIN huku ikifahamika kuwa hao watu wana majina yao halisi kama Abdulah au Saidi. Hivyo basi, hata Ibilisi naye analo jina lake ingawa Allah anaogopa kulitaja kwenye Quran.
NINI KILITOKEA MPAKA KUKAWA NA SHETANI?
Inaonekana Lusifa hakufahamu Mpango wa Mungu, na alifikiri ya kwamba yeye Lusifa angeweza kufanya vizuri zaidi kuliko Mungu. Hii ndiyo ilikuwa dhambi kuu ya Shetani. Kwa kufikiri hivi hakumwabudu wala kumsujudia Mungu, lakini anamwona Mungu kama sawa na yeye (Filipo. 2:6)
Isaya 14:14. Nitapaa kupita vimo vya mawingu. Nitafanana na yeye Aliye Juu.
Isaya. 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka Mbinguni. Ewe nyota ya alifajiri, mwana wa asubuhi ! Jinsi ulivyokatwa kabisa. Ewe uliyewaangusha mataifa !(KJV imetumika wakati wote)
Kazi zote za Yehova ni kamilifu; yeye siye mwanzilishi wa ukosefu wa uadilifu; kwa hiyo hakumuumba yeyote akiwa mwovu akama Waislam na Quran yao inavyo dai. (Kum. 32:4; Zaburi 5:4) Yule aliyekuja kuwa Shetani hapo mwanzoni alikuwa mwana mkamilifu wa kiroho wa Mungu. Aliposema kwamba Ibilisi “hakusimama imara katika kweli,” Yesu alionyesha kwamba wakati mmoja huyo alikuwa “katika kweli.” (Yohana 8:44)
Lakini, kama walivyo viumbe wote wa Mungu wenye akili, mwana huyo wa kiroho alipewa uhuru wa kuchagua. Alitumia vibaya uhuru wake wa kuchagua, akaruhusu maoni ya kujitafutia umashuhuri yasitawi moyoni mwake, akaanza kutamani ibada iliyokuwa ya Mungu peke yake, na kwa hiyo akamshawishi Adamu na Hawa wamsikilize yeye kuliko kumtii Mungu. Basi kupitia matendo yake, yeye mwenyewe akajifanya Shetani, jina linalomaanisha “mpinzani.”—Yakobo 1:14, 15;
Swali la kujiuliza:
1. Kwanini hakuna jina la Lusifa kwenye Quran?
2. Kwanini Allah analiogopa jina la Lusifa?
3. Kwanini Quran inafundisho tofauti na Taurat, Zaburi na Injili kuhusu mwanzo wa Shetani?
Kama Mwenyezi Mungu analo jina "Yehova". Vivyo hivyo Malaika wanayo majina mfano "Mikaeli" au "Gabrieli". Hata alipo umbwa Binadamu alipewa jina, "Adam na Hawa", kwanini Allah anashindwa kutuambia jina la shetani?
Hayo maswali ni kwa ajili ya kukufumbua macho kuwa Allah sio Yehova "YAHUH" Hivyo basi Allah sio Mwenyezi Mungu aliye muumba Lusifa kama Malaika mkamilifu.
Ni mimi Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW