Saturday, June 18, 2016

KWANINI ALLAH ANAAPA KWA YEHOVA "YAHUH" ALIYE UMBA KILA KITU?


1. Kumbe Allah sio Yahuh-Yehova.
2. Kumbe Allah hakuumba.
3. Kumbe Yesu ni Mungu.
Ndugu msomaji,
Kwanza tujifunze maana ya kuapa ili tuweze elewa kwanini Allah aliapa kwa Yehova.
Nini maana ya kuapa?
Kuapa, au Kula kiapo, au Kula Yamini, kunamaanisha kumthibitishia, kwa kutumia Jina la Mwenyezi Mungu, kwamba jambo fulani linaloapiwa – na ambalo halina ushahidi wazi wazi- ni kweli na sahihi kama linavyodaiwa na mwenye kula kiapo hicho na hivyo basi ni budi kusadikiwa madai hayo kwani Mdhamini Mkuu ni Mwenyezi Mungu, Mjuzi Pekee wa ukweli au uwongo wa mambo yaliyofichika nyoyoni!
katika Hadithi iliyopokelewe na Abdallah bin `Umar R.A.A. na iliyotolewa na L-Bukhari, “
"إِنَّ اللَّهَ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ ، فَمَنْ كَانَ حَالِفًا فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ أو فَلْيَصْمُتْ"
Maana yake, “Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu, atakaeapa aape kwa Mwenyezi Mungu au anyamaze
Sasa tumsome Allah ambaye sio Yehova "Yahuh", je yeye anaapa kwa nani?
SURAT ASH-SHAMS 1-3
1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..
Hivi mtu anaye apa kwa mwengine anakuwa Mungu au binadamu? Je, nani kaumba hapo. Maana Allah anaapa katika aliye umba, na kuumba ni sifa ya Mungu. Kumbe Allah ambaye sie Yehova hakuumba.
Zaidi ya hapo, Allah anaapa kwa usiku. Kumbe usiku una mamlaka zaidi ya Allah. Allah anaapa kwa mchana, kumbe mchana una mamlaka zaidi ya Allah.
Mbona katika SURAT ASH-SHAMS Allah anaapa kwa (1) Usiku (2) Mchana (3) kwa aliye umba kiume na kike?
Je, ni nani huyu aliye umba Kiume na Kike ambaye Allah wa Islam anaapa kwake? Endelea kusoma...kutoka Biblia Takatifu….
Yeremia 27: 5 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.
Sasa tunamsoma Yehovah ambaye ni Mungu wa Biblia kuwa yeye ndie aliye umba kila kitu, pamoja na Kiume na Kike ambacho Allah wa Islam anaapa kwake. Kwahiyo, Jehovah aliumba kiume na kike, na Allah wa Islam anaapa kwake, sasa jaza mwenyewe nani ni Mungu?
Je, Mungu anaweza kuapa kwa Mwengine? Endelea kupata elimu …
Waebrania 6:13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.
Jehova anasema hakuna Mkubwa wangu wa kuapa kwake, lakini Allah katika Kuran anasema kuwa yeye anaapa kwa aliye umba kiume na kike.
Hivyo basi leo tunafahamu kuwa aliye umba ni Jehona na Allah anaapa kwa Jehovah Mungu wa Biblia na Wakristo.
Mungu awabairiki sana
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa yesu Kristo
Copyright © Max Shimba Ministries 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW