Sunday, June 19, 2016

KWANINI ALLAH AMBAE SIO YEHOVA ALIOGOPA KUYAAMRISHA MAJINI YAISIKILIZE TAURAT, ZABUR NA INJILI?

ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI MACHAFU YALITUMWA KWA MUHAMMAD ILI KUSIKILIZA QURAN
ALLAH HUYO HUYO ALISEMA KUWA KILA WATU WALIPEWA KITABU CHAO. HAPO TEYARI KUNA SHAKA KWENYE QURAN YA MUHAMMAD AMBAYO SASA INAKABIDHIWA MAJINI MACHAFU.
Allah kasema katika Suratil Ahqaaf aya ya 29 mpaka 32, “
]وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِنْ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنْصِتُوا فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَى قَوْمِهِمْ مُنْذِرِينَ * قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنْزِلَ مِنْ بَعْدِ مُوسَى مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَى طَرِيقٍ مُسْتَقِيمٍ * يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِي اللَّهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ * وَمَنْ لا يُجِبْ دَاعِي اللَّهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الأرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِنْ دُونِهِ أَولِيَاءُ أُوْلَئِكَ فِي ضَلالٍ مُبِينٍ[
Maana yake, “Na (wakumbushe) wakati tulipowaleta kundi la Majini kuja kwako kusikiliza Qurani. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana): “Nyamazeni! (Msikilize maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha somwa walirudi kwa jamaa zao kwenda kuwaonya. Wakasema “Enyi watu wetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya (Nabii) Musa, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake na kinachoongoza kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka. Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mlingani, (Muitaji) wa Mwenyezi Mungu na muaminini, atakusameheni (Mwenyezi Mungu) dhambi zenu na atakukingeni na adhabu iumizayo. Na wasiomuitikia Muitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatamshinda (asiwapate) hapa katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele Yake. Hao wamo katika upotofu ulio dhahiri.”
Na kisa kingine ni cha Majini waliosikia Qurani kutoka kwa Mtume S.A.W wakati alipokuwa akiwasalisha Masahaba wake Sala ya Alfajiri. Na hii ilikuwa bila ya yeye kuwa na habari mpaka Mwenyezi Mungu S.W.T. alipomjulisha. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Jin aya ya 1 na ya 2, “
]قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِنْ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا[
Maana yake, “Sema: “Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la Majini lilisikiliza (Qurani) likasema: “Hakika sisi tumesikia Qurani ya ajabu. Inaongoza katika uwongofu; kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote tena na Mola wetu.”
Makala haya yametolewa katika kitabu changu kiitwacho, "Hakika ya Majini."
MASWALI KUHUSU MAJINI:

1. Wapi katika Taurat tunajifunza kuwa Majini yaliumbwa ili kumwabudu Mungu?
2. Wapi katika Zaburi Tunafundishwa kuwa Majini yaliumbwa ili ya mwabudu Mungu?
3. Wapi katika Injil tunafundishwa kuwa Majini yaliumbwa ili kuwamudu Mungu?
JE, BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU MAJINI?
Biblia Inasema nini kuhusu uhusiano na Mapepo au Majini
Mungu ametuonya kutokuwa na uhusiano na pepo. Imeandikwa, Mambo ya Walawi 19:31 "Msiwaendee wenye pepo wala wachawi, msiwatafute ili kutiwa unajisi na wao mimi ndimi BWANA Mungu wenu."
Ilikuwa kawaida ya watu wa zamani enzi za Biblia kusali pepo. Mungu aliwaonya wana wa Israeli kuhusu uombaji wa pepo na uchawi. Imeandikwa katika Kumbukumbu la torati 18:9-12 "utakapokwisha ingia katika nchi akupayo BWANA Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto wala asionekane mtu atazamaye mbao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala msihiri wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo wala mtu apandishaye pepo wala mchawi wala mtu awaombaye wafu kwa maana mtu atandaye hayo ni chukizo kwa BWANA kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA Mungu wako anawafukuza mbele yako."
Biblia yatupa mwanga kuhusu hali ya pepo. Imeandikwa, katika Matendo ya mitume 16:16-18 "Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu wenye kuwahubiria njia ya wokovu akafanya hayo siku nyingi lakini Paulo akasikitika akageuka akamwambia yule pepo nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu akamtoka saa ili ile."
Pepo ni wale malaika waliomwasi Mungu kule mbinguni na kutupwa hapa duniani. Imeandikwa katika Ufunuo 12:7-9 "Kulikuwa na vita Mbinguni Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na Shetani adanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye."
Kwa sababu pepo za husiana na Shetani, mtu katika israeli angeonekana akifanya pepo ilibidi auawe. Imeandikwa, katika Mambo ya walawi 20:27 "Tena mtu mme au mke aliye na pepo au aliye mchawi hakika atauawa watawapiga kwa mawe damu ya itakuwa juu yao." Isaya 8:19 yasema "Na wakati watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndeye na kunong'ona je haiwabasi watu kutafuta habari kutoka kwa Mungu waoje! waende kwa watu walio kufa kwa ajili ya watu walio hai?."
JILINDE DHIDI YA MAJINI NA SHETANI
Unaweza kujilinda jinsi gani dhidi ya roho waovu-Majini-Mapepo-Mashetani? Biblia inajibu hivi: “Jitiisheni kwa Mungu; lakini mpingeni Ibilisi, naye atawakimbia ninyi.” (Yakobo 4:7) Tunatii agizo hilo tunapoishi kupatana na mafundisho yaliyo katika Biblia, kitabu pekee kitakatifu ambacho kinamfichua Shetani, roho waovu, na “hila” zao. (Waefeso 6:11; 2 Wakorintho 2:11) Pia, Biblia inatuambia kwamba roho waovu pamoja na wote wanaompinga Mungu, hawatakuwapo milele. (Waroma 16:20) “Wanyoofu ndio watakaokaa duniani, na wasio na lawama ndio watakaobaki ndani yake,” inasema Methali 2:21.
JE, UMEJIULIZA HIVI?
● Je, Mungu ndiye aliyewaumba roho waovu?—2 Petro 2:4.
● Je, unaweza kuzungumza na wafu?—Mhubiri 9:5, 6.
● Unaweza kujilinda jinsi gani dhidi ya roho waovu?—Yakobo 4:7.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW