Friday, June 3, 2016

ALLAH ANASEMA YEYE NI MWENYE HILA NA MUONGO (Sehemu ya Kwanza)


Ndugu msomaji,
Kama kichwa cha habari kinavyo sema hapo juu kuwa Allah amejaa hila.
Maana ya Hila:
Hila maana yake ni udanganyifu na ujanja.
SASA TUANZE KUSOMA HILA ZA ALLAH:
Sasa hapa naomba sana Waislamu wanisaidie mimi: katika Sura ya 13:42 Surat Al Rad panasema “Hila” zote ni zake Allah. Tena katika Sura ya 10:21 Surat Yunusi inasema: Allah ndiye mwepesi wa kufanya hila.
Swali ambalo watu wote tungejiuliza hivi hila ni nini?
Na je mtu anafanyaje,hila anakubalika na jamii?
Nasema hivyo kwasababu katika lawama ambazo marafiki zangu wa Kiislamu waminitwishwa wiki iliyopita na kuniita mpumbavu mtu nisiyejua kitu ni kitendo kile cha kusema Allah siye Mungu aliyeumba. Kuitwa Allah kwa maana ya Mungu au God au Mulungu hakumuharalishi kuwa Mugu muumbaji iko miungu mingi lakini yuko Mungu mmoja tu muumbaji aitwaye YEHOVA. Huyu si muongo hana hila maana hila haikai ndani mwake na watu wake pia wanatakiwa wasiwe na hila.
Kama nilivyo sema, hila maana yake ni udanganyifu na ujanja. YEHOVA alitufundisha kuwa tujiepushe na hila na ujanja wa aina yeyote uliyo na uovu ndani yake. Katika Mithali 12:20 tunasoma haya: “Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu bali wafanyao mashauri ya amani kwao kuna furaha”.
Kwahiyo ninaposema Allah siyo Mungu wa kweli ninasema nikijuacho.
Katika Sahihi Muslim Vol iv hadithi nambari 2667 Abuu huraira amekariri Muhammad akimuelezea Allah kuwa ndiye awatiaye wanadamu wote katika tamaa mbaya, uongo na uasherati kila mmoja kwa kipimo chake maalumu.
Waislamu wote duniani huamini kuwa Mungu anapaswa kuabudiwa ni yule ambaye Makureshi walimtambua kuwa aliitwa Allah, hawachunguzi wala hawajiulizi huyu "mungu" aitwaye Allah asili yake ni nini? Biblia inasema msiamini kila roho bali zichunguzeni kama zimetoka kwa Mungu aliye hai. 1Yoh 4:1
Kwa kule kusema Allah hana mfano wa kitu chochote je kwatosha kuthibitisha Uungu wake? Maana tumesikia na tumezoea kuambiwa na Waislamu kuwa Allah hana mfano wala hafananishwi na kitu chochote hakuzaaa wala hakuzaliwa. Nami nikafanya utafiti wa kutosha katika Qur’an na vitabu vingine vya Kiislamu kuona ukweli huo.
Je, ni kweli au kuna hila inayotumika katika jambo hili?
Katika Qur’an ya kiingereza iitwayo THE NOBLE QUR’AN nilitafuta maana ya neno Allah, hiyo ikaishia kusema ni neno lililotumika ndani ya Qur’an zaidi ya mara 3000 hakuna zaidi kilichosemwa. Lakini ndani ya GLORIOUS QUR’AN Tafsiri ya Mohamed Marmaduke pickth neno Allah limetafsiriwa hivi:-
(The word Allah the stress is on the last syllable) has neither feminine not plural and has never been applied to anything other than unimaginable supreme being.
Tafsiri yake neno Allah mkazo hasa kwenye silabi ile ya mwisho. Halina ukike wala halina wingi na halijatumika kwa ajili ya kitu chochote zaidi ya uwepo wa ukuu usiofikirika. Hii ndiyo imani ya Waislamu wote.
Tafsiri hii pia inaonesha kuwa Allah hana mfano wa kitu chochote tukijuacho au tunachokiwaza kwa akili.
Hii inafanana na Tauhidi ya Kiislamu ambayo msingi wake ni Sura ya 112:1-4 ya Surat ikhlas. Katika sura hiyo aya ya mwisho inahitimisha kuwa Allah hana mfano. Hapa Waislamu husimama na kuwabeza Wakristo katika maneno yaliyomo katika Mwanzo 1:26 yasemayo “Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu” Waislamu kwa kukosa kujua hufikiri Mungu aliposema hivyo anafanana nasi kwa njia gani. Basi tukijifunza tutajua ukweli. Nilipokuwa nikitazama katika Qur’an kitu ambacho Waislamu wanakiamini kuwa kitabu cha Mungu wao nikasoma katika Sura ya 24:35 Surat ana Nuru nikaona maneno haya:
“Mwenyezi Mungu nuru ya mbingu na ardhi. Na mfano wa nuru yake ni kama kishubaka kilichomo taa…….”
Sijui kama Waislamu wanaisoma aya hiyo! Aya inasema mwenyezi Mungu ni nuru yaani Allah ni nuru ya mbingu na ardhi. Nataka nijue ewe Muislamu kama ingekuwa ni somo la darasani ukiulizwa Mwenyezi Mungu ni nini kwa mujibu wa Sura 24:35 Surat an nuru kama hatasema Mwenyezi Mungu ni nuru ya mbingu na ardhi usishangae ukikosa.
Kwahiyo kila mwenye ufahamu atajua kuwa nuru ya mbingu na ardhi ina mifano mingi sana. Tazama sentensi inayofuatia aya hii nayo inatoa mfano wa huyo Mwenyezi Mungu kwamba nuru yake ni kama taa ya kandili. Kumbe Allah ana mfano isipokuwa hila imetumika Sura 112:1-4 kuwapumbaza watu wajue kuwa Allah hana mfano. Labda Waislamu wangenisaidia kujibu swali hili. Je, Waislamu wanamuabudu Allah yupi yule asiye na mfano kwa mujibu wa Sura 112:1-4 au yuleAllah mwenye mfano kwa mujibu wa Sura ya 24:35?

Radio imani inawaita Wakristo makafiri jina baya lakini kwa maana halisi ni mtu asiyeamini sisi hatumuamini Allah mwenye kutunga hila, hatumuamini Allah ambaye ni kigeu geu.
Katika Sura 69:17 Surat al-Haaqqah tunasoma maneno haya:
“Na malaika watakuwa kandoni mwake na malaika wa namna nane watachukua kiti cha enzi cha Mola wako juu ya…”
Tena katika Sura 85:15 Syrat Buruj inamtaja Mungu wa Waislamu aitwaye Allah kuwa yeye ndiye mmiliki wa kiti cha enzi.
Swali ambalo napenda kuwauliza Waislamu wote Allah kumiliki kiti cha enzi.
Je, kiti hicho anakifanyia nini? Huenda watu wakanishangaa. Nasema hivyo nikiwa na maana ya je, Allah naye anakaa katika kiti kama wakaavyo wanadamu?
Je, ana miguu kama mwanadamu kama anakaa kama mwanadamu katika kiti cha enzi, basi haikosi hana tofauti na mwanadamu.
Angalia katika Sura ya 69: 44-45 Surat Al-haqqah twasoma.
“Na kama (mtume) angelizuia juu yetu baadhi ya maneno tu bila shaka tungalimshika kwa mkono wa kuume”.
Aya hii inaonesha kuwa Allah ana mkono wa kuume. Na kama Allah ana mkono wa kuume atakosaje mkono wa kushoto? Na kama Allah anasema atakosaje mdomo? Basi ondoeni dhana ya kwamba Allah hana mfano.
Unaposoma kwa makini imani ya Kiislamu na kumuangalia Allah mwenyewe utakubaliana nami bila mashaka kuwa Allah hana sifa ya Uungu. Maana katika Luka 1:37 Malaika akimpasha habari Mariamu juu ya kupata mimba aliposhangaa Malaika akamwambia hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Kwake YEHOVA hakuna lisilowezekana, anaweza kujitokeza mbele ya wanadamu vile apendavyo. Yeye hana mpaka wala haongozwi na matakwa ya wanadamu awaye yote. Katika Uislamu Allah ana mipaka ya kufanya kazi zake.
Jambo lingine ambalo Waislamu wanawabeza sana Wakristo ni juu ya Biblia. Wao hudai eti Qur’an ni kitabu pekee chenye ukweli.tena ni kitabu chenye lugha moja tu ambayo Allah ameiridhia. Ndiyo maana sala zetu tunaendesha Kiarabu, vitabu vyetu vimendikwa Kiarabu. Lakini je kuna ukweli gani kwamba humo ndani ya Qur’an aya zake zimeandikwa katika lugha moja?
Nina mashaka hila imetumika katika aya hizi. Waislamu wengi wanaposoma aya hizi huamini kuwa ni kweli kwa mfano katika Sura 26:193-195 inasema:-
“Ameteremsha haya muhuisha sharia mwaminifu juu ya moyo wako ili uwe miongoni mwa waonyaji kwa lugha ya Kiarabu wazi wazi”.
Aya nyingine ni 12:2 na 39:28 pamoja na 42:7 kwa mujibu wa aya hizi zinapelekea Waislamu wengi waamini kuwa maneno yote ya Qur’an ni ya Kiarabu na hakuna hata neno moja ndani yake lililo katika lugha ya kigeni.
Wasomi wa Kiislamu nao wameshindwa kuwaeleza ukweli waumini wa Kiislamu ukweli wa jambo hili. Radio imani na nyinginezo zingetoa fursa ya kuwafundisha uwazi wa dini yao ili wapate kuutambua Uislamu lakini ajabu wamezama kuwaeleza Waislamu wasiosoma juu ya Ukristo na imani yao. Basi ni vizuri mimi sasa niwafundishe Waislamu wote wapate kujua ukweli katika jambo hili na hila iliyotumika kudai Qur’an imeandikwa au ina maneno ya Kiarabu tu. Hebu nikumbushe jambo ambalo unalijua katika kitabu cha Siratw Rasullah Saifa ya 260 kimemuelezea Mkristo mmoja aitwaye Jabir ambaye alikuwa mtumwa wa Amiri Ibn Al-hadrami. Kijana huyu alipoachiwa huru alikaa Makka kenye kibanda kilichokuwa karibu na Al-marwa. Imeelezwa pia baada ya Muhammad kujibashiria utume alionekana katika kibanda cha Jabir akimfundisha habari za torati na injili.
Katika Sahihi Al-Bukhar Vol vi hadithi nambari 507 na 510 inaonesha kuwa wakati aya ya Qur’an ziliponakiliwa mara ya pili Seyidina Uthuman aliagiza jopo la waandishi aliloliteuwa kwa kazi hiyo kuwa waingize maneno ya Kiarabu kila walipohitarafiana wajumbe wake. Katika yale yaliyokuwa katika nakala ya kwanza ya Qur’an ambayo iliandikwa na Zaid bin thabit.
Hii inaonesha kuwa nakala ya mwanzo ambayo ndiyo ORIGINAL zilikuwepo aya ambazo maneno yake yalikuwa siyo ya Kiarabu. Hii inathibitishwa na kitabu cha Al-itgan kilichoandikwa na Jaladu Dyn Suyut ambacho chaonesha kuwa licha ya Sayidina Uthuman kutoa agizo lile bado maneno ya kigeni yaliyobaki kwenye Qur’an na bado yangalimo mpaka leo.
Juzuu ya pili ya kitabu hicho mlango wa Fiyma waga-a Fiy-hi BIGHAYR Lughat L-Arabu. Yaani yaliyowekwa katika lugha ya Kiarabu. Inaonesha ni kwa jinsi gani maswahaba wa Muhammad walivyotatizwa na maneno ya lugha za kigeni. Baadhi ya lugha hizo zinatajwa kuwa ni Kihabeshi (Ethiopic), Kiajemi, Kiebrania, Kiaramu, Kitarig, Kinnabatw. Pamoja na Qur’an kukanusha Muhammad kufundishwa na Jabir lakini mpaka leo Qur’an ina maneno ya Kirumi ndani yake.
Je, ni maneno gani hayo ya lugha nilizozitaja ambayo yamo katika Qur’an? Fuatana nami katika makala haya kujua usiyoyajua.
Ndiyo maana Waislamu wanapowabeza Wakristo kwa mambo yasiyo sahihi tunaashangaa. Lakini pia tunawashangaa wanapokasirika wanapofundishwa ukweli, ifuate kweli ili hiyo kweli ikuweke huru.
Barikiwa sana,

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW