Friday, May 6, 2016

WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI?

(SEHEMU YA KWANZA)
Ndugu msomaji,
Leo tunaanza na mada hii kubwa ambayo inauliza na kuwaomba Waislam watuletee uthibitisho wa Muhamamd akisilimu na kuwa Muislam.
Tunaposoma kitabu cha maisha ya Muhammad S.A.W. kilichoandikwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa Kenya na Zanzibar Sheikh Farsy ukurasa wa 5 kuna maneno haya…
Pale pale alfajiri alipokwisha kuzaliwa mtume alikwenda kuitwa babu yake kuja kumwona mjukuu wake. Babu huyu alifurahi sama na akamfunika maguo mjukuu wake, akajikongoja naye mpaka kwenye Al-ka’ba akafungua mlango akaingia ndani, akasimama, akamwombea dua kwa mashairi mazuri ya kiarabu aliyoyatunga mwenyewe wakati ule ule, kisha akarejea naye na jua bado halikuchomoza.
Hapa tunaona Babu yake Muhammad akimchukua mjukuu wake Ndani ya alkaaba alfajiri kwenda kumfanyia ibada, kumkabidhi kwa Mola wake, kutia wakfu.
Lakini je Kuna nini Hapa cha kuzingatia?
(1) imani ya Abdul muttalib ilikuwa hii.
Katika kitabu " Acha Biblia Iseme" kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu wa kiislamu aitwae Ali muhsin Barwani ukurasa wa 153 tunasoma maneno haya; “hapakutokea mwarabu ambaye alipewa jina hilo(Muhammad) na babu yake tangu kuzaliwa kwake, na huyo babu hakuwa Mkristo bali alikuwa akifuata mila za kishirikina.” Na wala hakujua taurati wala injili." mwisho wa Nukuu
Ushahidi wa wazi unaothibitisha kuwa babu yake Muhammad Abdul muttalib pamoja na kuomba miungu haswa mungu Hubaal sanamu kuu ndani ya alkaaba; vilevile aliomba dua kwa Allah; Mungu atakayerithiwa baadaye na mjukuu wake katika uislamu; ushahidi tunaupata tunaposoma utangulizi wa suratul al-fyl ulio katika juzuu ya ukurada wa 946 Qurani iliyotafsiriwa kwa kiswahili chapa ya nane tunasoma maneno hayo. “chifu mkuu wa makka zama hizo alikuwa Abdul muttalib, alikwenda al ka’ba pamoja na baadhi ya machifu wa kikuraish na akilishika komeo la chuma la mlango wa al-ka’ba, akamwambia Allah (S.W.0 kuilinda nyumba yake pamoja na wahudumu wake. Zama hizo kulikuwa na masanamu 360 ndani na kando ya Al- ka’ba.”
Ndugu zetu kiuanadamu waislamu Wanadai kwa mujibu wa Quran 30:30 sote tunapozaliwa tunazaliwa Hali tukiwa waislamu ila wazazi wetu uja na kutuondoa kwa uislamu Ima kwa Mfano kubatiswa na kadhalika. Hivyo na Hapa tunaona Mtoto huyu alipozaliwa mwanzo alipewa Jina na babu yake aliyekuwa mshirikina Kisha babu huyu Zamani za kabla ya uislamu alijikokota na mjukuu wake hadi alkaaba na alfajiri Ile kumtoa wakfu.

Sasa tukija kwa kufikia umri wake wa Miaka 40 usiku wa manane ramadhan ya mwaka wa 610 kuna kiumbe kilimpiga kabari (kumbana) Na akapata homa. Habari hizi tunazipata kwenye Vitabu vinavyoelezea Historia na maisha yake Muhammad, kabla ya kuzaliwa, baada ya kuzaliwa, kufa kwake, na mazishi yake, tukisoma kitabu cha Historia ya Muhammad, kilichoandikwa na Sheikh Abdulla Saleh Farsy, Ule Uk 16, Paragraph 4, ambapo kuna habari ya Muhammad kukimbilia katika pango la Jabari Hiraa, ambako huko ALIENDA AKIWA NA MIAKA 38, mwaka wa pili alipokuwa humo pangoni, ndipo alipopewa kibano kilichopeleka kupata homa, na kujibashiria ni mtume,
Tunaambiwa:
Hata siku moja katika mwezi wa ramadhani, mwezi 17 jumatatu katika mwaka wa 40 unusu wa umri wake, mtume alimuona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumona wapi katokea, akamwambia:
“Soma” MTUME AKAMJIBU, “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujifundisha kusoma”
Akaja akamkamta akambana, akamwambia tena “Soma” mtume akamjibu jawabu ile ile. Hata mara ya tatu akamwambia, “Soma Iqra Bism Rabbik” akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake, kisha mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hiyo ndiyo sura kwanza kushukua katika Quran ingawa haijawekwa mwanzo. Mara yule mtu akaondoka machoni mwake, asimwone wapi kaelekea, na Mtume akarejea kwake khofu imemshika.
SHEIKH ABDULLA SALEH FARSY ANAZIDI KUTUFAHAMISHA KILICHOTOKEA KWA MAUHAMMAD BAADA YA KUTOKA PANGONI ALIKOPIGWA KABARI, NA KISHA KULAZIMISHWA KUSOMA WAKATI YEYE ALIKUWA MBUMBUMBU ASIYEJUA KUSOMA WALA KUANDIKA, FARSY ANASIMULIA KATIKA KITABU CHA WAKEZE MTUME WAKUBWA NA WANAE, ULE UK 12 PARAGRAPH YA 3, ANASEMA:
Basi mtume akafanya khofu akarejea kwa mkewe na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda , akataka afunikwe na maguo, mara akawa anatetemeka kwa nderema, na anaweweseka na kusema: “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na mashetani, na kuniharibu akili yangu na kunizuga” Bibi Khadija pale pale, alimdakiza akamwambia, “Wacha hayo siyo yatakayokuwa hayo, wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako, wewe unatazama vema jamaa zako unachukua mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa nzuri ambazo hakuna mwenye nazo, unafanya hivi, na unafanya hivi, furahi ndugu yangu tua moyo wako, Wallahi mimi mkeo, naona umekwisha kuwa Mtume”.
KWA HIVYO MUJIBU wa ushahidi huu Muhammad Kapaa homa, baada ya kubanwa na kiumbe huko pangoni, kiumbe ambacho akikujitambulisha na Muhammad mwenyewe amesema kuwa ni anahofia ni shetani, ndiye aliyemchezea, na kumzuga, na kumharibu akili yake, shetani ambaye Muhammad kazaliwa akiwa nae, kwa mujibu wa Kitabu cha Fat’hul Baary, Uk 6 Hadithi Namba. 89 Kinasema,
Abu Huraira amesimulia kuwa, “Mtume Muhammad (S.a.w) alikuwa na shetani tangu alipozaliwa”
Lakini mkewe katika kumtuliza mumewe wakiwa chumbani kitandani, akaamua kumriwadha na maneno matamu, ambayo kwa kweli hata kama ni wewe mwanaume lazima ulainike, mwisho wa mariwadho hayo, Bi KHADIJA ambaye hakuwa na Dini, hamjui Mungu, anamtangaza Muhammad mumewe kuwa ni mtume, na baada ya hapo sasa Habari zikaenea, na Waandishi wa vitabu vingine wakakoleza zaidi kwa kusema huyo aliyembana huko pangoni Muhammad, ni Malaika Jibril imani ambayo ipo kwa waislamu mpaka leo, wakati Muhammad mwenyewe amejieleza kuwa Shetani ndiye kamfanyizia, huko Pangoni mpaka kumtia homa, na mwisho kujibashiria utume, hapo ni kabla ya Quran kuwapo.
Sasa tukija zama za baada ya matukio Aya ya pangoni , Tunazidi kusoma kwamba Mtu wa kwanza kusilimu alikuwa na Khadija.
Katika ukursa wa 18 sheikhy Farsy anaelezea maneno yanayo husu mke wa muhammad khadija binti khuweylid nayo yanatuhadithia hivi…
Akarejea kwa mkewe bibi khadija, akamsimulia habari hii. Palepale bibi huyu akamwamini, akawa ndiye mtu wa awali kabisa kushehedusha shahada ya uislamu. Basi mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke.
Katika kitabu hicho hicho cha maisha ya nabii muhammad ukurasa wa 18 kifungu c. wametajwa waislamu wa awali kabisa nao ni hawa…
(i) Mwislamu wa kwanza
Bibi Khadija bint Khuweylid
Mtume aliamrishwa kufundisha dini siku ya jumatatu na bibi huyu alisilimu siku hiyo hiyo akafanya ibada na mtume usiku ule ule kabla ya mtu yeyote ulimwenguni huyu ndiye aliyefuzu kwelikweli.
(ii) Mwislamu wa pili
Sayyidina Ali bin Abi Talib bin Abdul Muttalib
Alipomwana mtume na bibi Khadija usiku ule wanafanya mpya aliwauliza, “hii ni ibada gani?” mtume alimfahamisha na akamtaka awe pamoja nao lakini yeye alikataa kwanza akasema mpaka niende nikamshauri baba yangu”. Mtume akamkataza kuitoa siri ile nje. Mara asubuhi ya usiku ule ule, kijana huyu akaja kwa mtume akampa habari kuwa yeye yu pamoja nao. Akawa ndiye islamu wa pili duniani. Aliposilimu alikuwa kijana wa miaka 10 hivi.
(iii) Mwislamu wa tatu na wa nne.
Zayd bin Haritha Al Ka’bi na Bibi Aymana.
Huru wa mtume na mwanawe wa kupanga alikuwa akikaa pamoja na mtume na akasilimu kama sayyidina Ali mchana wa jumane. Alisilimu yeye na mkewe, bibi ummu Aymana yaya wa mtume.
Hawa wote ndio waislamu wa awali kabisa ambao walisilimu mara baada ya muhammad s.a.w. kuleta dini ya uislamu ambayo alianzisha rasmi hapa duniani jumatatu ya siku ya 17 ya mwezi wa ramadhani sawa sawa na 27th Disemba ya mwaka wa 610 baada ya Kristo.
NDIO MAANA BADO NAULIZA WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI?
Umeletwa kwenu na Mwalimu Chaka wa Musa

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW