Sunday, May 22, 2016

MWINJILISTI UMAR MULINDE ALIYEHARIBIWA KWA TINDIKALI BAADA YA KUHAMA UISLAMU, AMSHUKURU MUNGU KWA UPONYAJI -


Ikiwa takribani miaka mitano ipite tangu mwinjilisti Umar Mulinde kujeruhiwa vibaya kwa kuharibiwa mwili kwa tindikali aliyomwagiwa na watu wanaosadikiwa kuwa waumini wa dini ya kiislamu waliokuwa wakipinga hatua yake ya kubadili dini na kuwa Mkristo, hapo juzi mwinjilisti huyo alifanya ibada maalumu ya shukrani kukumbuka namna tukio hilo lilivyotokea na kumuharibu kabisa sura yake yenye mvuto. Katika jumble wake kupitia okras wake wa Facebook mwinjilisti huyo aliandika namna ambavyo kupitia nguvu ya maombi na neema ya Mungu ilivyomponya katika tukio hilo la kuogofya, bila kusahau kutaja madaktari waliomuhudumia huko nchini Israel ambako alihamishiwa kupata matibabu yaliyokwenda sambamba angalau kurudisha sura yake kwenye muonekano mzuri. Mwinjilisti Umar Mulinde raia wa Uganda ambaye baba yake ni imamu wa msikiti nchini humo, alikuwa mmoja wa vijana waliokuwa na imani kali ya uislamu na hata kufikia hatua ya kuwachukia kupita kiasi waumini wa dini ya Kikristo likiwemo taifa la Israel, hata hivyo mambo yalibadilika baada ya kukutana na Yesu ambaye alimbadilisha maisha yake ambapo aliapa kutorudi nyuma kamwe licha ya tukio hilo kubwa na vitisho anavyopata kutoka kwa waumini wa dini aliyokuwepo awali. Unaweza kutazama na kusoma zaidi habari za mwinjilisti huyu kuanzia alipomwagiwa tindikali mpaka hali aliyonayo sasa kwa Kubonyeza HAPA. https://www.facebook.com/mulinde.umar

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW