Friday, May 13, 2016

KUMBE ALLAH ANAYE MSAIDIZI


UTATA NDANI YA KURAN KUHUSU UTAMBULISHO WA ALLAH!!
KUMBE ALLAH ANAYE MSAIDIZI
Je, Allah anaye Msaidizi, mbona anatumia wingi katika kujieleza?
Hebu rejea kwenye Kuran kwanza:
Suratul Anbiyaa 91. Na mwanamke aliye linda uke wake, na TUKAmpulizia katika roho YETU, na TUKAmfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu
.
Ndugu zanguni, Allah ameanza vituko vyake hapa. Katika Koran Allah anadai kuwa hana msaidizi Suratul Baqarah: aya 106 ― 107 Lakini katika aya tuliyo isoma hapo mwanzoni - Suratul Anbiyaa 91 tumeona kuwa Allah anatumia wingi alipo kuwa akielezea jinsi alivyo mpa ujauzito Maryam.
ALLAH ANAMUUMBA ISA BIN MARYAM KWA KUTIMIA WINGI
Kuran imejaa utata, hebu soma hapa Suratul Attahriim 12. Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na TUKAmpulizia humo kutoka ROHO YETU, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu.
HAPA: Allaha anasema kwa undani zaidi TUKAmpulizia ROHO YETU. Hivi huyu Allah ni kweli alikuwa Mungu au ni madai ya Muhammad na rafiki yake Jibril? Mbona alisema kuwa yeye hana msaidizi wala Mwana? Kivipi Allah anatumia wingi katika kumuumba Isa Bin Maryam?
Aya zaidi kuhusu Maryam na kupata ujauzito za Isa: Suratul Anbiyaa 91.
Endelea hapa tena:
ALLAH ANAMUUMBA BINADAMU KWA KUTUMIA WINGI:
Suratul Hijr 26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
HAPA tumesoma kuwa Allah anamuumba Binadamu kwa kutumia wingi" Nukuu: Na TULIMUUMBA MTU"
Endele hapa tena
ALLAH ANAUMBA MAJINI KWA KUTUMIA WINGI:
Suratul Hijr 27. Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.
Allah anaendelea kutumia wingi katika uumbaji. Sasa anasema kuwa "TULIWAUMBA MAJINI" Allah anaendelea kutumia wingi katika uumbaji.
Je, unafikiri kuwa labda Allah alijisahau au fanya makosa pale alipo sema kuwa yeye hama msaidizi.
Wadhalimu wa dini ya Kiislam wamekuwa mstari wa mbele kusema kuwa, eti Wakristu wana miungu mingi na wao wana Mungu Mmoja tu naye ni Allah. Leo tumejifunza kuwa, Allah hayupo peke yake maana sasa anatumia wingi katika kazi zake ikiwa pamoja na ya uumbaji wa Binadamu na Majini.
Nukuu zingine ambazo ALLAH anatumia wingi: S. 3:44, S. 3:145, S. 17:1, S. 6:114, S. 19:40-42, 50-53, 56-74 Arberry, S. 2:252-253 , S. 3:108 Y. Ali; cf. S. 45:6, S. 37:161-166 Pickthall, S. 37:170-182 Y. Ali, S. 23:12-14 Arberry, S. 19:16-2, S. 66:12 Pickthall, S. 15:26-29 Pickthall.
Ndugu zanguni nimeweka ushaidi wa kutosha kutoka Quran yao kuhusu wingi ambao Allah amekuwa anautumia kila mara kwenye Quran yake.
Je, Allah anaye Msaidizi? Je, Allah anaye Mwana ambaye na yeye ana wadhifa wa KiAllah? Kwanini Allah anatumia wingi huku tukifahamu kuwa Allah hafananishwi wala hana msaidizi?
Hakika kuna shaka kubwa kubwa kwenye Quran ya Allah ambayo sasa inasema kwa kutumia wingi.
Biblia inasema kuwa Mungu anaye Mwana na anaitwa Yesu, zaidi ya hapo Biblia inatuambia kuwa kuna Mungu Roho Mtakatifu na hao wote ni WAMOJA katika Roho.
Karibuni kwa Mungu wa Biblia ambaye amesema kiuwazi kuwa yeye ni Baba na ana Mwana ambaye na yeye ni Mungu. Kumbuka hawa ni wamoja kwa kupitia Mungu Roho Mtakatifu.
Katika Huduma yake.
Max Shimba Ministries Org.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW