Sunday, May 22, 2016

ALLAH NA MUHAMMAD HAWAPENDI WANAWAKE WA KIAFRIKA WA KIISLAM

Leo nina maswali matatu tu kwa wanawake wa Kiislamu.
Kabla sijawauliza maswali kwanza niwashirikishe ahadi za Yesu ambaye amekuwepo zaidi ya miaka 570 Kabla ya Muhammad, yeye alisema:-
Luka 20:34 Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa;
35 lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi;
36 wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.
Yesu anasema kuwa katika ufalme wa Mungu, watu hawataoa wala kuolewa, watakuwa sawa na malaika kwa sababu Malaika hawaoi wala kuolewa, na pia katika kuurithi ufalme wa Mungu sawasawa na Ibrahimu, hakuna upendeleo wa mwanaume au mwanamke, maana wote ni sawa mbele za Mungu,
Wagalatia 3:27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Wanaume na wanawake ambao wamemwamini Yesu na kubatizwa kisha wakafanya mema, hao watakuwa warithi sawasawa bila kuwekwa daraja kwa wanaume kuwa juu kuliko wanawake au wanawake kuwa juu kuliko wanaume, katika ufalme ambao watu wa Kristo tutakuwa pamoja na Ibrahim na manabii wote wa kweli.
Mathayo 8:11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
Ufalme ambao wafanyao udhalimu watatupwa nje wakitaka kuingia, Yesu atawazuia kwa sababu hawakutaka kuwa Watakatifu,
Luka 13:27 Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
29 Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.
Huo ndo ufalme wa Mungu wa kweli ambao watu waliomwamini Yesu wataingia, usio na Upendeleo.
Maswali yangu matatu yanatokana na aya za Quran ambazo zilisemwa na Muhamnad, kuhusu pepo, akitoa ahadi kwa wanaume, Ilisemwa, 👇🏻
Quran 52 SUURATUR RAHMAAN

ﻓِﻴﻬِﻦَّ ﻗَﺎﺻِﺮَﺍﺕُ ﺍﻟﻄَّﺮْﻑِ ﻟَﻢْ ﻳَﻄْﻤِﺜْﻬُﻦَّ ﺇِﻧﺲٌ ﻗَﺒْﻠَﻬُﻢْ ﻭَﻟَﺎ ﺟَﺎﻥٌّ
56. Watakuwamo wanawake watulizao macho, mtu yeyote hajawagusa kabla yao wala jinni.
Katika pepo hiyo watakuwemo wanawake ambao hawajaguswa yaani hawajaingiliwa na watu wala jini, wa ninyi wa hapa duniani tayari mmeshaingiliwa, mmezaa mna watoto na wengine hamna watoto ila mneshaguswa na wanaume wa kibinadamu, na baadhi yenu majini, ila hao wa peponi wenyewe hawajawahi kuishi duniani, tena wanaume wataozeshwa. wanawake hao wakiwa na sifa kuu mbili za macho,
1) Wana macho makubwa ya Vikombe.
Quran 52
SUURATUT TUUR
ﻣُﺘَّﻜِﺌِﻴﻦَ ﻋَﻠَﻰ ﺳُﺮُﺭٍ ﻣَّﺼْﻔُﻮﻓَﺔٍ ﻭَﺯَﻭَّﺟْﻨَﺎﻫُﻢ ﺑِﺤُﻮﺭٍ ﻋِﻴﻦٍ
20. Wakiegemea juu ya viti vya fahari vilivyopangwa safu, na tutawaoza wanawake weupe wenye macho ya vikombe (makubwa)
Wanawake hao watakuwa weupe hakuna mwanamke mweusi, ni wanawake maalum ambao hawajawahi kuguswa na mwanadamu wala jini.
2) Wana macho makubwa kama mayai ya mbuni.
Quran 37 SURATUL AS-SAAFAT
ﻭَﻋِﻨْﺪَﻫُﻢْ ﻗَﺎﺻِﺮَﺍﺕُ ﺍﻟﻄَّﺮْﻑِ ﻋِﻴﻦٌ
48. Na pamoja nao watakuwa wanawake wenye macho mazuri matulivu makubwa
ﻛَﺄَﻧَّﻬُﻦَّ ﺑَﻴْﺾٌ ﻣَّﻜْﻨُﻮﻥٌ
49. Hao wanawake hao kama mayai yaliyohifadhiwa.
Hizo ndiyo ahadi za wanaume wa kiislamu za kupewa wanawake wa namna hiyo, maana ninyi hakuna hata mmoja wenu ambaye ana macho makubwa kama ya vikombe, wala mwenye macho makubwa kama mayai ya mbuni.
Sasa nawaombeni kwa utulivu bila jaziba nijibuni maswali yangu haya matatu.
a) Je! ndani ya Quran kuna aya ye yote ambayo imesema kuwa na ninyi wanawake weusi mtaolewa peponi?
b) Kuna aya yo yote ndani ya Quran ambayo imesema kuwa ninyi mkiingia peponi mtapewa wanaume ambao hawajawahi kuwaingilia wanawake wala majini?
c) Ndani ya Quran kuna aya yo yote ambayo imesema kuwa, ninyi nanyi mtabadilishwa muwe na macho ya vikombe makubwa au mayai ya mbuni ili muwe sawa na wale wanawake ambao hawajawahi kuguswa na watu au majini?
Kama hakuna basi karibuni kwa Yesu ambako katika ufalme wake hakuna ubaguzi wala upendeleo maana pepo hiyo watakuwa wamependelewa wanaume tu.
BILA YA JAZBA. TAFADHALI LETENI MAJIBU YENYE AYA KUTOKA QURAN.
Watakabahu.
Max Shimba Ministries Org

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW