Friday, May 13, 2016

ALLAH KASEMA HOMA YA SIKU MOJA INAFUTA MADHAMBI YA MWAKA MMOJA





1. • Muislamu akipatwa na Homa ya siku moja anafutiwa dhamb
2 • Mwiba Huondoa Dhamb
3 • Mtu aliyefiwa watoto watatu anafutiwa dhamb
4 • Tendo la Ndoa linakufutia dhamb
5 • Kuoga siku ya ijumaa kunakufutia dhamb
Ndugu msomaji,
Leo hebu tuangalie baadhi ya mambo ambayo muislamu akiyafanya yeye anaamini amesamehewa dhambi zake.
1 • Muislamu akipatwa na Homa ya siku moja:
Katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu kilichoandikwa na Sheikh Said Moosa Mohammed al-Kindy wa Muscat Oman. Juzuu 3-4 uk 74 hadith na 924 inasema
“Homa ni bahati ya kila Muislamu kwa (adhabu ya) moto. Na homa ya siku moja inafuta (madhambi ya) mwaka (mmoja) kamili.
2 • Mwiba Huondoa Dhambi:
Katika Sahih Bukhari na Muslim juzuu ya 7 Hadith 544
“ Hadith ya Aisha (r.a), mke wa mtume (SAW) alisema mtume wa Allah amesema “Hakuna tatizo litakalompata Muislamu isipokuwa Allah atafuta madhambi kwa tatizo hilo kwake, hata kama ni mwiba utakaomtoboa” (al lu’lu war-marjan vol.3 H.1663 UK.969)
3 • Mtu aliyefiwa watoto watatu:
Katika sahih Bukhar na Muslim juzuu ya 9 Hadith 413
“Hadith ya Abu Said Al-khudri (r.a) amesema, alikuja mwanamke fulani kwa Mtume wa Allah! Na akasema kumwambia mtume wa Allah (SAW) “ Wanaume ndio pekee wenye kufaidika na mafundisho yako, kwa hiyo tutengee siku moja, tunakuja, unatufundisha katika katika aliyokufundisha Allah. Mtume (SAW) jikusanyeni siku kadha wa kadha mahala kadha wa kadha, wakajikusanya. Mtume wa Allah (SAW) akawaendea akafundisha katika aliyomfundisha Allah kisha akasema, Hakuna Mwanamke miongoni mwenu atakayetanguliza watoto wake watatu, isipokuwa watakuwa pazia ya kumkinga na moto, Mwanamke mmoja katika wao akauliza, Ewe mtume wa Allah, Wawili je? Yule mwanamke akalirudia swali lake mara mbili, Mtume (SAW) akasema wawili na wawili na wawili.
4 • Tendo la Ndoa:
Katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu juzuu 1-2 cha Mohammed al-Kindy uk 206 Hadith 467 inasema
“ Hakika Mwanamme akimtazama mkewe (kwa matamanio ya kuingiliana) nae (mke) akamtazama mumewe (kwa ajili hiyo) basi anawatazama Mwenyezi Mungu utazamaji wa rehema, (mume) akimshika mkewe kwa mkono wake ( kwenda kutimiza haja yao) basi yanadondoka (yanatoka) madhambi yao kwenye vidole vyao”
5 • Kuoga siku ya ijumaa:
Katika Kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu kilichoandikwa na Sheikh Moosa Mohammed al-Kindy Juzuu ya 1-2 Hadith no 66 uk 41 inasema
“ Ogeni siku ya ijumaa, kwani anaeoga siku ya Ijumaa basi inakuwa kafara kwake (yanafutwa madhambi yake) baina ya Ijumaa mpaka Ijumaa, na nyongeza siku tatu”
Lakini tunaposoma Biblia Takatifu Yer 2:22 “Maana ujapojiosha kwa magadi na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu asema Bwana MUNGU”
Hivi ndivyo mafundisho ya Kiislamu yanavyofundisha kuhusu kuondoa dhambi.
Jambo ambalo ningependa ulijue katika Uislamu , mbali ya kufanya swala mara tano kama walivyoamriwa, bado Muislamu huyu hana uhakika wa Msamaha wake wa dhambi.
Muhammad ambaye ndiye kiongozi, mpaka siku aliyokufa tarehe 8/6/632 B.K alikuwa hana uhakika kama amesamehewa dhambi zake au hapana na hivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa wafuasi wake hata leo.
Na Mwalimu Chaka wa Musa
For Max Shimba Ministries Org

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW