Ndugu msomaji,
Katika kijarida hiki kifupi, nitakuwekea sababu tano (5) kwanini Wakristo wanaabudu siku ya Jumapili.
Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-
1) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].
2) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].
3) Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO 2:1]
4) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].
5) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.
Hakuna andiko lolote linalosema mtu yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi. Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].
KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA
Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13].
Wokovu wetu siku hizi uko ndani ya Kristo, siyo kwa kushika Torati ya Musa. Kuna watu wasiijua Biblia tena hawaelewi hata Agano Jipya. Hawaelewi KWA NINI Yesu alikufa. Kwa mfano wanaposema, ‘Imeandikwa katika Kutoka 20:8-11 lazima tushiike sabato!’ Je! ina maana mtume Paulo alifundisha uongo? Au alitaka kutudanganya? Au Unafikiri Biblia inajipinga yenyewe? Je! Unaamini Biblia siyo neno la Mungu? Au kwa nini watu wanapenda kujizika katika Agano la Kale?
Najua kuwa narejea kwenye mambo yale yale ambayo tayari nimekwisha yaandika hapo juu. Lakini mambo hayo ni ya kimsingi. Ni lazima tuyaelewe mambo hayo pale tunapoyaangalia maisha ya watu wa Agano la Kale! Kwa kupitia Biblia nzima tunajifunza sasa juu ya Yesu Kristo na wokovu wake. Lakini kama Biblia ni neno la Mungu (na ndivyo lilivyo) kwa nini basi waopo watu wanaopinga mpango wa Mungu kupitia mwanae Yesu Kristo ili waweze kubakia katika mpango wa kale ambaop Mungu mwenyewe ameuondoa?
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo… Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.”
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 16, 2016
April 16, 2016
6 comments:
Unajibu kisiasa zaidi. Na ni wapi Yesu aliposema kuwa kwa kuwa amefufuka siku fulani basi muabudu siku hiyo.. Ebuu tuchunguze maandiko siku ya kwanza ya juma (Jumapili) imeonekana mara nane tu kwenye agano Jipya lakini hakuna sehemu inayoonyesha kuwa siku hiyo ilkuwa maalumu kwa mitume hao. Wala hakuna hata moja ya mafungu kati ya hayo linalodokeza kuwa wale mitume waliazimu kuacha kuitunza Sabato ya siku ya Saba. Hizo ni sababu tu ulizojitungia logically. Ila amri za Mungu zipo milele, sasa wewe sema eti haokoki kwa kushika siku wakati wewe mwenyewe hapo umetoa sababu ya kuishika Jumapili. Acha siasa mzee!
Kwahyo wanaosali jumapili mbinguni hawaingii
Uthibitisho wa kibiblia unaonesha kuwa, siku ya Sabato ni Jumamosi kama leo inavyojulikana. Angalia!
Mathayo 28:1 Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
Marko 16:2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;
Marko 16:9 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.
Luka 24:1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Yohana 20:1 Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
Yohana 20:19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Yesu alifufuka siku ya jumapili ambayo Biblia inaiita kuwa ni siku ya kwanza ya juma. Kama Yesu alifufufuka siku ya kwanza ya juma(jumapili), Sabato itakuwa lini??
Jibu: Jumamosi
Marko 6:2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
Luka 4:31 Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;
Luka 13:10 Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.
Luka 6:6 Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.
1. 6. Je, kanisa la awali lilikutana siku ya Sabato kuabudu?
Jibu: Ndiyo. Mitume wa Yesu na mitume waliofuata walikutana siku ya sabato kuabudu.
Ushahidi wa Biblia:
Matendo ya Mitume 13:14 Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi.
Matendo ya Mitume 13:27 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.
Matendo ya Mitume 13:42 Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.
Matendo ya Mitume 13:44 Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.
Matendo ya Mitume 15:21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.
7.Je, Mungu ana watu wake maalumu tu?
Jibu :Ndiyo
Math 7 :21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Je, mapenzi ya Baba yake ni yapi ?
Zaburi 40 :8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
1. 8. Je, mtu anaweza kumpenda Yesu bila kushika Amri zake 10?
Hasha!! Yeye anasema;
Yoh 14:15(mkinipenda mtazishika amri zangu)
Yohana 14:21 (Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake).
Yohana 15:10 (Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake).
1. 9. Je, inawezekana kushika Amri 9 tu isipokuwa Sabato?
Hasha!! Haiwezekani kabisa, Biblia inasema;
Yakobo 2:10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
1 Yohna 2:3-5 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
1 Yohana 5:2-3 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
. Je, Sabato itakuwepo hadi mbinguni ?
Jibu : Ndiyo
Nabii Isaya alioneshwa watakatifu wakienda mbele za Mungu kuabudu siku ya Sabato mbinguni. Yohana naye alioneshwa sanduku la Agano (la Amri 10 ikiwemo sabato) liko hekalu la mbinguni.
Isaya 66 :22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
Ufunuo 11 : 19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
Post a Comment