Tuesday, April 26, 2016

ROHO MTAKATIFU NA UTUKUFU WA MUNGU



( Shekinah, Kabod, Gloria)
Utukufu Wa Mungu Yahweh.
Yohana 17:22, Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja;
Yesu atawapa utukufu wake waliokombolewa.
Matendo ya mitume 7:55, Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akatazama juu mbinguni, akauona utukufu wa Mungu na Yesu amekaa upande wa kulia wa Mungu.
Stefano, katika dakika zake za mwisho, kabla hajauwawa na wayahudi, aliona utukufu wa Mungu JUU mbinguni.
Musa pamoja na wana wa Israeli, pia waliona utukufu wa Mungu na macho yao.
Kutoka 16:7, 10.
Ms. 7, na asubuhi ndipo mtakapoona utukufu wa BWANA; na sisi tu nani, hata mkatunung´unikia?......
Ms. 10, Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa BWANA ukaonekana katika hilo wingu.
Kutoka 40:34-35:
Ms. 34, Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.
Ms. 35, Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.
Tazama pia, Kutoka 29:43. Mambo ya walawi 9:4,6,23. Hesabu 14:10, 16. Hesabu 16:19,42.
Hesabu 20:6.
1 Wafalme 8:10-11.
Ms.10, Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya BWANA ikajaa wingu.
Ms.11, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya BWANA ilikuwa imejaa utukufu wa BWANA.
2 Mambo ya nyakati 5:11-14:
Ms.11, Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu,.......
Ms.12, tena walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao,na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoaazi na vinanda na vinubi......
Ms.13, hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipasa sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA.
Ms.14, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya BWANA ilikuwa imejaa utukufu wa BWANA.
2 Mambo ya nyakati 7:1-2:
Ms. 1, Basi Suleimani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa BWANA ukajaza nyumba.
Ms. 2, wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa BWANA, kwa sababu kwa kuwa utukufu wa BWANA umeijaza nyumba ya BWANA.
Isaya 58:8:

Ms. 8, Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Isaya 59:19:
Ms. 19, Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.
Utukufu wa BWANA ni – Roho wa BWANA!
Isaya 60:1-3:
Ms. 1,Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
Ms. 2, Maana, tazama, giza litafunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.
Ms. 3, Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kkjia mwanga wa kuzuka kwako.
Ezekiel 3:23, Basi, nikaondoka, nikaenda uwandani, na tazama, utukufu wa BWANA ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.
Ezekieli aliuona utukufu wa Bwana:
Ezekieli 1:28, Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA.
Ezekieli 8:4, Na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwapo hapo, sawasawa na maono yale niliyoyaona katika uwanda.
Ezekieli 10:4, Utukufu wa BWANA ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa BWANA.
Ezekieli 43:2, 4,5
Ms 2, na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling,aakwa utukufu wake.
Ms.4, Na huo utukufu wa BWANA ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile lielekealo upande wa mashariki.
Ms. 5, Kisha Roho ikaniinua, ikanichukua mpaka ua wa ndani; na tazama, utukufu wa BWANA uliijaza nyumba.
Ezekieli 44:4, Kisha akanileta, kwa njia ya lango la upande wa kaskazini, mbele ya nyumba; nikaangalia, na tazama, huo utukufu wa BWANA uliijaza nyumba ya BWANA, nikaanguka kifudifudi.
Maandiko katika Agano Jipya kuhusu utukufu wa Mungu:
Matayo 17:1-6, Ms.1,Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.Ms.2,Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang`aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Ms.3, Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye. Ms.4, Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya." Ms.5, Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni." Ms.6,Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
Katika kitabu cha Luka tunasoma kwa wafuasi waliingia katika mawingu. Lk 9:34.
Luka 2:8-9,Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao.Ms.9, Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
Utukufu ulingáa, na wakaweza kuiona na macho yao.
Stefano ahubiria wayahudi:
Matendo ya Mitume 7:2, Naye Stefano akasema, "Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni! Mungu alimtokea baba yetu Abrahamu alipokuwa kule Mesopotamia kabla hajaenda kukaa kule Harani.
Stefano aliuona utukufu wa Mungu!
Matendo ya Mitume 7:55, Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akatazama juu mbinguni, akauona utukufu wa Mungu na Yesu amekaa upande wa kulia wa Mungu.
Matendo ya Mitume 9:3-4, Lakini alipokuwa njiani karibu kufika Damasko, ghafla mwanga kutoka angani ulimwangazia pande zote.Ms.4, Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia: "Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?"
Tazama jinsi Saulo alivyoielezea wakati alipoilinganisha tukio hili na hali zingi mbili baadaye:
Matendo ya mitume 22:6, 11,…Ms. 6,.. Basi, nilipokuwa njiani karibu kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwangu mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote. Ms. 11,.. Kutokana na ule mwanga mkali sikuweza kuona na hivyo iliwabidi wale wenzangu kuniongoza kwa kunishika mkono mpaka nikafika Damasko
Matendo ya Mitume 26:13-14, Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.Ms.14,..Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: `Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama punda anayepiga teke fimbo ya bwana wake.`
Utukufu wa Bwana ni Roho wa Bwana:
Warumi 6:4, Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya.
“Utukufu wa Baba” ni nini?.
Warumi 8:11, Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa uzima miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.
Ufunuo 15:8, Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia Hekaluni mpaka mwisho wa mabaa makubwa saba ya wale malaika saba.
Ufunuo 21:23, Mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuangazia, maana utukufu wa Mungu huuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo.
Tazama vile neno la Mungu linaelezea Neno la Mungu kama: wingu, mwangaza, mwanga, ng,aa, moshi na Roho wa Mungu, ijapokuwa utukufu wa Mungu kwa hakika haielezeki.
Daudi alisema kwamba mwishowe Mungu atampokea katika utukufu:
Zaburi 73:24, Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
Tunafahamu nakala ya Petero kuhusu unabii wa Yoeli wakati wa pentekote:
Matendo ya mitume 2:17-18, `Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.Ms.18, Naam, hata watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, nitawamiminia Roho wangu, siku zile, nao watautangaza ujumbe wangu.
Lakini tazama kile aliendelea kusema:
Matendo ya mitume 2:19, Nitatenda miujiza juu angani, na ishara chini duniani; kutakuwa na damu, moto na moshi mzito;
Wengine wanatafsiri hii kama bomu zinazoanguka duniani, lakini siyo hivi bwana aongea juu yake, Anatangaza UMWAGIKAJI wa ROHO WAKE na UTUKUFU.
Damu! – Damu ya Yesu.
Moto! – Moto wa Roho mtakatifu! Ndimi za moto zikashuka na kukaa juu ya kila mmoja wao.
Yesu alipaa mawinguni, ambayo ni wingu wa utukufu.
Matendo ya mitume 1:9, Baada ya kusema hayo, wote wakiwa wanamtazama, alichukuliwa mbinguni; WINGU LIKAMFICHA wasimwone tena.
Yesu atarudi duniani akishuka kutoka wingu wa utukufu.
Matendo ya mitume 1:11,…. wakasema, "Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mliivyomwona akienda mbinguni."
Mungu mwenyewe, utukufu wake unangáa ndani ya mioyo yetu.
2 Wakorintho 4:6-7, Mungu ambaye alisema, "Mwanga na uangaze kutoka gizani," ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu uangazao katika uso wa Kristo. Ms.7, Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo, ili ionekane wazi kwamba nguvu hiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisi wenyewe.
Mambo mengine makuu yalikuwa ya kuvutia kama nuru ya ajabu ndani ya mioyo zao.
By permission Vagn Rasmussen Ministries.
Anwani: rasmussenvagn@hotmail.com
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 26, 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW