Wednesday, April 13, 2016

MUNGU AMETUONYA KUTOKUWA NA UHUSIANO NA MAJINI



1. LAKINI ALLAH KASEMA MAJINI NI MAISLAM
2. ALLAH AKIRI KUWA MAJINI MACHAFU YANAMWABUDU YEYE
3. YEHOVA KASEMA WOTE WENYE UHUSIANO NA MAJINI WATAINGIA JEHANNAM
Ndugu msomaji,
Je, Biblia Inasema nini kuhusu uhusiano na Mapepo au Majini
Mungu ametuonya kutokuwa na uhusiano na pepo. Imeandikwa, Mambo ya Walawi 19:31 "Msiwaendee wenye pepo wala wachawi, msiwatafute ili kutiwa unajisi na wao mimi ndimi BWANA Mungu wenu."
Ilikuwa kawaida ya watu wa zamani kusali Majini na Pepo. Mungu aliwaonya wana wa Israeli kuhusu uombaji wa pepo na uchawi. Imeandikwa katika Kumbukumbu la torati 18:9-12 "utakapokwisha ingia katika nchi akupayo BWANA Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto wala asionekane mtu atazamaye mbao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala msihiri wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo wala mtu apandishaye pepo wala mchawi wala mtu awaombaye wafu kwa maana mtu atandaye hayo ni chukizo kwa BWANA kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA Mungu wako anawafukuza mbele yako."
Biblia yatupa mwanga kuhusu hali ya pepo. Imeandikwa, katika Matendo ya mitume 16:16-18 "Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu wenye kuwahubiria njia ya wokovu akafanya hayo siku nyingi lakini Paulo akasikitika akageuka akamwambia yule pepo nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu akamtoka saa ili ile."
SASA BASI, NILIPO ENDELEA KUSOMA VITABU VYA DINI YA UISLAM NIKAKUTA KUWA, ALLAH WA UISLAM YEYE ANAABUDIWA NA MAJINI NA ZAIDI YA HAPO, MAJINI YALISILIMU NA KUWA MAISLAM.
HILI NI JAMBO LA KUSHANGAZA, MAANA KWENYE BIBLIA YEHOVA KASEMA NA KUTUONYA KUTOKUWA NA UHUSIANO NA MAJINI.
QURAN INAKIRI KUWA MAJINI NI MAISLAM NA YALISILIMU PALE QURAN ILIPO TEREMSHWA KWA MUHAMMAD.
Majini wanatajwa sana katika dini ya Kiislamu kwa kuwa ni waislam kwa kusilimu, kwa kuiamini Quran tukufu aliyopewa mtume Muhammad.
Majini walisilimu na kuwa Waislamu mwaka 610 AD (Baada ya Yesu) SOMA 72:1-14 QURAN. Hivyo basi, unapotumia neon jinni maana yake unatumia lugha ya Kiarabu ukimaanisha Pepo mchafu. Ni kama Spoon/kijiko, vyote ni kitu kimoja. Ndani ya Quran, neon “PEPO” limetumika kama Paradiso, mbinguni. Lakini pia, tunapata neon jingine liitwalo AKHERA ila neno hilo halimaanishi PARADISO, bali kwa lugha ya Kiarabu neno hili “AKHERA” lina maana ya KUZIMU.
Lakini pia ukiangalia ndani ya SURALJINN ( QURAN 72:1-2, 8-9, 12 ) Mapepo hawa wanajieleza waziwazi kabisa kuwa mwanzo waliishi Mbinguni, walipogeuka kwa kuasi, walitegwa na Mungu. Linganisha na maandiko haya katika Biblia ( UFUNUO WA YOHANA 12:7-9; YUDA 1:6-8; UFUNUO 20:10; UFUNUO 21:8 ). Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, hawa majini ( Mapepo ) waliotegwa na Mungu Mbinguni wakiwa Malaika huko na kutupwa Duniani baada ya kuasi huko, sasa, wakati wa mtume Muhamad katika safari yake ya kurudi Taif mwaka 620 AD (baada ya Yesu) wapo walioamini na kuona kuwa Quran ni ya ajabu ya kuwatangazia neema ya kuabudu. Katika vol 8-9, husema , wanapojaribu kwenda Mbinguni ( walikotoka zamani ), hukuta ile Mbingu imezungushiwa vimondo vya moto. Hivyo, hudai kuwa mbingu yao iko Akhera, yaani Kuzimu, maana Mbingu ya juu ina moto na hawana uwezo wa kwenda huko. SOMA (QURAN 72:9), Mbingu ina utisho wa moto ila Akhera ( kuzimu ) hakuna shida kwao.
MAJINI YANAMWABUDU ALLAH
Hivyo basi, kulingana na jinsi Allah asemavyo ndani ya Quran kuwa nimeumba binadamu na majini ili muniabudu ( QURAN 57:58 ; 51:56) na kuwa , mbinguni mwao Majini wanaabudu (Majini waliosilimu mwaka 620 AD) ,SOMA QURAN 72:14, ambao ni wema wanaosafiri na kurithi uzima wa milele upatikanao Akhera ( Kuzimu ). Lengo kubwa la Shetani na Majini ni kufanya urafiki na wanadamu wengi ili kwa wingi huo apate watu wengi wa kwenda nao JEHANAMU ( QURAN 6:128 ). Jambo la muhimu kujua hapa ni kwamba moto wa milele hakuwekewa Mwanadamu bali ni Shetani na malaika zake wote ( Majini au mapepo ). Hawa, hawana nafasi tena ya kuungama au kutubu.
LAKINI YESU ANAYAAMURU MAJINI KUTOKA NDANI YA WATU
Yesu Kristo anayetambuliwa na Waislam kama Mtume tu, hakuwa na urafiki wowote na Shetani wala Mapepo ( Majini ). Aliyaamuru Majini kutoka ndani ya watu waliokuwa wakiteswa nayo ( MATHAYO 8:29: MARKO 5 N,K )
Wakati Yesu anaondoka hapa duniani, alichukuliwa na wingu na kupaa kuelekea juu. Mbinguni ni juu kama Quran inavyothibitisha. Yesu aliweza kupaa na kuingia Mbinguni lakini Majini ( Mapepo ) walioslimu wakijaribu tu, wanakutana na moto mkali. Tumeona kuwa Majini ambao ni Waislamu kwa kusilimu, wanaishi AKHERA yaani Kuzimu. Je, Waislamu wengine unadhani wataishia wapi milele? Katika imani ya Kiislam huamini kuwa, Muislam akifa anakuwa na Majini wawili wa Kumlinda humo Kaburini.
Pepo ni wale malaika waliomwasi Mungu kule mbinguni na kutupwa hapa duniani. Imeandikwa katika Ufunuo 12:7-9 "Kulikuwa na vita Mbinguni Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na Shetani adanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye."
Kwa sababu pepo za husiana na Shetani, mtu katika israeli angeonekana akifanya pepo ilibidi auawe. Imeandikwa, katika Mambo ya walawi 20:27 "Tena mtu mme au mke aliye na pepo au aliye mchawi hakika atauawa watawapiga kwa mawe damu ya itakuwa juu yao." Isaya 8:19 yasema "Na wakati watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndeye na kunong'ona je haiwabasi watu kutafuta habari kutoka kwa Mungu waoje! waende kwa watu walio kufa kwa ajili ya watu walio hai?."
KILA MUISLAM ANA JINI KATIKA MWILI WAKE. HILI NI JAMBO LA AJABU SANA, MAANA YESU YEYE ALIYATOA MAJINI NDANI YA WATU.
Majini wamepewa ruhusa ya kukaa katika mwili wa Muislam yeyote, hivyo kila Muislam ana Jini kuanzia moja na kuendelea. Vile vile Majini wameruhusiwa kukaa katika nyumba za Waislam. Katika nyumba yoyote ya Muumini wa dini hiyo, kuna Jini au Majini wanaokaa humo. Ni ukweli usiopingika kuwa bila Majini hakuna Uislamu kama vile pasipo Roho Mtakatifu hakuna Ukristo. Majini ndiyo yaliyomchukua mtume Muhamad kwa muda wa siku 40 akiwa Mabondeni walikompeleka na kuanza kumuagiza kuhusiana na kuanzisha imani hiyo ya Kiislamu.
Sasa inakuwaje Yesu atoe Majini ndani ya watu kama ilivyo sema kwenye Luke 11:14, Matthew 8:16, Mark 1:34, Luke 4:41, Matthew 8:32, Mark 5:8, nk huku Allah yeye akiwajaza Waislam Majini?
Katika Walawi 19: 31, Mungu ametuonya kutokuwa na uhusiano wowote ule na Majini, LAKINI Allah anasema katika Quran kuwa, ameteua Mtume kwa kila kiumbe mpaka Majini machafu. Hebu soma aya hapa chini
ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI YANA MTUME WAO
Quran 6: 130. Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri.
Ndugu msomaji, natagemea baada ya kusoma hiki kijarida kifupi kuwa umeelewa na kufahamu Allah wa Quran sio Mungu wa Biblia anaye kataza uhusiano na Majini.
Mawali la kujiuliza:
1. Kwanini Mungu wa kwenye Biblia anakataza uhusiano na Majini LAKINI Allah wa Quran anaruhusu uhusiano na Majini?
2. Kwanini Mungu wa Biblia anatoa Majini ndani ya Watu, LAKINI Allah wa Quran anawajaza watu Majini?
3. Kwanini Mungu wa Biblia nasema kuwa Majini yote yataingia Jehannam LAKINI Allah wa Quran anasema kuwa Majini yalisilimu na ni Maislam?
Ndugu msomaji, ushahid wa aya umesha usoma mwenye. Nakushauri umchague Mungu wa Biblia anye kupenda na kulinda kutoka hizo nguvu chafu za Majini.
Karibuni kwa Yesu ambaye ndie Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 13, 2016

1 comment:

Unknown said...

unaongea usenge tu

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW