Saturday, April 2, 2016

MAKOSA MAKUBWA YA KISAYANSI KATIKA UISLAM KUHUSU JUA



1. MUHAMMAD NA ALLAH WANASEMA ETI JUA LINAZUNGUKA
2. MUHAMMAD ASEMA JUA LINASUJUDU KWA ALLAH
3. MUHAMMAD ASEMA JUA LINAVAA VAZI/NGUO, ETI NDIO MAANA USIKU KUNA GIZA
Ndugu msomaji,
Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa Allah hakuumba, lakini Waislam wamekuwa wagumu kukubali na kuanza kunitukana. Leo nawaletea uthibitisho mwingine kuwa Allah hakuumba na Muhammad ni mtume bandia.
Muhammad na Waislam wa Mwanzo Walisema Nini kuhusu Jua?
Utakwenda wapi kutafuta maana sahihi ya Kurani? Zamakhshari? al-Tabari? Baidawi? Kama ungekuwa Muislam wa mwanzo ungeweza kwenda kwa Muhammad mwenyewe! Sikia jinsi Muhammad alivyoeleza, kwa mujibu wa Bukhari na al-Tabari.
"Abu Dhar alisimulia: Nabii aliniuliza wakati wa machweo ya jua, ‘Unafahamu mahali ambako jua linakwenda (wakati wa kuchwa)?’ Nilijibu, ‘Allah na Mtume wake wanafahamu vizuri zaidi.’ Alisema, ‘Linakwenda (yaani linasafiri) hadi linasujudu chini ya kiti cha enzi, na linapata kibali cha kusimama tena, na linaruhusiwa na kisha (muda utakuja ambapo) litakuwa linakaribia kusujudu lakini kusujudu kwake hakutakubaliwa …’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441 uk.283.
MUHAMMAD ANASEMA JUA LINASUJUDU KWENYE KITI CHA ENZI CHA ALLAH
Tafsiri nyingine ya kifungu hicho hicho cha al-Bukhari inasema:
"Abzur Ghifari (ra) alisimulia: siku moja Nabii Muhammad (amani na iwe juu yake) aliniuliza, ‘Abzar unafahamu jua linakwenda wapi baada ya kuzama?’ Nilimjibu, ‘Sifahamu, Mtume wa Allah ndiye yeye tu anayeweza kusema vizuri zaidi.’ Kish Nabii (SA) alinijibu, ‘Baada ya kuzama, jua hubaki likisujudu chini ya Aro’sh (kiti cha enzi cha Allah) na linasubiri amri ya Allah ili lichomoze tena upande wa mashariki. Siku itakuja wakati ambapo jua halitapata ruhusa zaidi toka kwa Allah ya kuchomoza tena na Qeyamot (Siku ya Kiyama) itakuja duniani.’"
MUHAMMAD ABADEILKA NA KUSEMA KUWA JUA LINAZAMA KWENYE MBINGU
MUHAMMAD ASEMA JUA LINAVAA VAZI/NGUO

al-Tabari juzuu ya 1 uk.231 inasema, "Nilimuuliza Mjumbe wa Mungu [Muhammad] ‘[Jua] linazama wapi?’ Alinijibu: ‘Linazama mbinguni na kisha linachomoza kutoka mbingu kwenda mbingu nyingine hadi linachomoza kwenye mbingu ya juu zaidi, mbingu ya saba. Hatimaye, linapokuwa chini ya kiti cha enzi, linaanguka chini na kusujudu, na malaika wanaolisimamia wanasujudu pamoja nalo. Kisha jua linasema, Bwana wangu, ni wapi unakoniamuru nichomozee, ni upande ule nilikozamia au nilikochomozea?’ Aliendelea. Jambo hili ndilo (linalokusudiwa na) neno la Mungu: ‘Na jua: Hukimbilia mahali linapotakiwa kuwepo (usiku)’ linaposhikiliwa chini ya kiti cha enzi – ‘Jambo hilo limeamriwa na Yeye Mwenye Nguvu na Mwenye Kujua’ Bwana kwa mamlaka yake ya kifalme, Bwana ambaye ‘anavijua’ viumbe vyake. Aliendelea, Gabriel alileta kwenye jua vazi lenye kung’aa tokana na mwanga utokao kwenye kiti cha enzi, kwa kufuata vipimo vya saa na siku. Ni refu zaidi wakati wa majira ya joto na fupi zaidi wakati wa majira ya baridi, na lenye urefu wa wastani wakati wa majira ya kupukutisha majani na wakati wa majira ya kuchipua majani. [Mitindo ya majira ya kuchipua majani, kupukutisha majani na majira ya baridi!] Aliendelea. Jua huvaa vazi hio, kama mmoja wenu anavyovaa zavi lake. Kisha, huwa huru kuzunguka kwenye anga la mbinguni mpaka linapochomoza kutokea upande linaochomozea. … Njia hiyo hiyo hufuatwa na mwezi wakati wa kuchomoza kwake … Lakini Gabriel huuletea vazi kutoka kwenye mwanga wa miguunil. Hivi ndivyo neno la Mungu (linavyomaanisha) ‘Amelifanya jua kuwa angavu na mwezi kuwa mwanga.’"
Jua na mwezi ni alama za Allah. Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 na.1173 uk.304;
Sunan Nasa’i juzuu ya 2 na.1462,1464 uk.272; juzuu ya 2 na.1465, 1466 uk.273; juzuu ya 2 na.1475 uk.278; juzuu ya 2 na.1477 uk.280; juzuu ya 2 na.1481 uk.283; juzuu ya 2 na.1485-1486 uk.286-287; juzuu ya 2 na.1488-1489 uk.287,289; juzuu ya 2 na.1500 uk.297; juzuu ya 2 na.1502 uk.299; juzuu ya 2 na.1505 uk.300; juzuu ya 2 na.1506 uk.301.
Dhu al-Qarnaiyn [Zul Qarnain] "alishuhudia kuzama kwa jua kwenye sehemu yake ya kupumzikia kwenye bwawa lenye ute mweusi na wenye harufu mbaya sana." al-Tabari juzuu ya 5 uk.173-174 (Tazama Sura 18:82-97).
al-Tabari juzuu ya 1 uk.234 pia inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi yenye matope. Msemo "yenye matope" ni hami’ah, unaomaanisha udongo mweusi wa mfinyanzi, lakini hamiyah ni neno lenye kufanana nalo linaloweza kumaanisha kitu cha moto. (Tazama rejeo la 442 chini ya uk.234).
" [Muhammad] Aliendelea. Wakati jua linachomoza, linainuka juu ya kibandawazi (kinachokokotwa na farasi) toka kwenye moja ya chemchemi hizo likiwa pamoja na malaika 360 …. Wakati Mungu anataka kuvijaribu jua na mwezi, ili kuwaonyesha watumishi wake ishara na kwa njia hiyo kuwataka waache kutokumtii Yeye na kuanza kutii, jua huporomoka ghafla toka kwenye kibandawazi na kuanguka kwenye kina cha bahari, ambacho ni cha mduara. Wakati Mungu anataka kuongeza umuhimu wa ishara kuwatisha zaidi watumishi wake, jua lote hunguka, na hapawi na sehemu yake yoyote inayobaki kwenye kibandawazi. Huko ndiko kupatwa kukamilifu kwa jua, wakati ambapo mchana hujiwa na giza na nyota hutokeza." al-Tabari juzuu ya1 uk.236.
Bibliografia: Tafsiri za Kurani
1. Arberry, Arthur J. The Koran Interpreted. Macmillian Publishing Co., Inc. 1955.
2. Dawood, N.J. The Koran. Penguin Books. 1956-1999.
3. Malik, Farooq-i-Azam. English Translation of the Meaning of AL-QUR’AN : The Guidance for Mankind. The Institute of Islamic Knowledge 1997.
4. Pickthall, Mohammed Marmaduke. The Meaning of the Glorious Koran. Dar al-Islamiyya (Kuwait) (tarehe haijaonyeshwa).
5. Rodwell, J.M. The Koran. First Edition. Ivy Books, Published by Ballantine Books. 1993.
6. Shakir, M.H. The Qur’an. Tahrike Tarsile Qur’an, Inc. 12th U.S. Edition 2001.
7. Sher Ali, Maulawi. The Holy Qur’an. Islam International Publications Limited (Ahmadiyya) 1997.
8. Yusuf ‘Ali, Abdullah. The Holy Qur-an : English translation of the meanings and Commentary. Revised & Edited by The Presidency of Islamic Researches, IFTA. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (Al Madina Saudi Arabia) 1410 BH.
Marejeo Mengine
Campbell, Dr. William. The Qur’an and the Bible in the Light of History and Science (2nd edition). Arab World Ministries 2002.
The Translation of the Meanings of Sahih Al-Bukhari Arabic-English Vol.1 by Dr. Muhammad Muhsin Khan. Islamic University, Al-Medina Al-Munawwara AL MAKTABAT AL SALAFIAT AL MADINATO AL MONAWART
Tarehe haijaonyeshwa, hakina haki miliki.
The History of al-Tabari : An Annotated Translation. Ehsan Yar-Shater, General Editor. State University of New York Press, 1989.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 2, 2016

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW