Saturday, April 30, 2016

MAJINA YA MUNGU WA BIBLIA


MSIFU MUNGU KWA MAJINA YAKE.
Majina ya Mungu, hueleza sifa za Mungu, Tabia za Mungu au Matendo ya Mungu. Mfano; Wayahudi wanamwita Mungu El‐Shaddai. Ni neno lenye majina mawili ndani yake. ‘El’ maana yake Mungu, na ‘Shaddai’ lenye maana itokanayo na neno ‘Shad’ yaani Titi (Ziwa) la mama anyonyeshaye.
Kutokana na ukweli kwamba, titi/ziwa la mama anyonyeshaye, linampa mtoto mchanga kila kitu anchohitaji. Maziwa ya mama yake, humpa mtoto kila kitu mtoto anachohitaji. Ndani ya maziwa kuna vitamini, protini, wanga, mafuta, madini, maji, na kila kitu mtoto anachohitaji. Maziwa ya mama, yanamtosheleza mtoto kwa kila kitu. Hivyo, Waisraeli wanapomwita Mungu El‐Shaddai, wanamaanisha kuwa, kama ziwa linavyo mtosheleza mtoto, vivyo hivyo, Mungu ni ‘Mtoshelezi’ kwetu. Halleluyah!
Hivyo, kila jina la Mungu, linabeba aidha Sifa yake au Tabia yake au Matendo yake. Ndio maana Mfalme Daudi anasema
“Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu … Mpeni Bwana utukufu kwa jina lake. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.” (Zab 29:1‐ 2) Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni Jina lake, kwakuwa lapendeza.(Zaburi 135:3).
Na Bwana Yesu alitufundisha kuanza sala namna hii;
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako tukutuzwe, hakafu Ufalme
wako uje hapa duniani.
Kwahiyo, unaweza pia kumsifu Bwana kwa majina yake. Majina ya Mungu, hueleza aidha sifa za Mungu au tabia za Mungu au Matendo makuu ya Mungu. Yafuatayo hapa chini, ni baadhi ya majina ya Mungu kwa lugha ya Kiebrania, yatakayokusaidia kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu.
MAJINA YA MUNGU NA UKUU WAKE.
MUNGU akubariki sana na msingi wa somo letu uko katika Zaburi 83:18 inayosema ''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.''
1: JEHOVAH ADONAI =MUNGU Mwenye Enzi Yote (Mwanzo 15:2-8 )
2: JEHOVAH EL – SHADAI =MUNGU Ututoshalezae MUNGU Mwenyenzi (Mwanzo 17:1)
3: JEHOAH EL-OHEENU =BWANA MUNGU Wetu (Zaburi 99:5,8,9)
4: JEHOVAH EL- GIBBOR= MUNGU Mwenye Nguvu ( Isaya 9:6-9)
5: JEHOVAH EL-OLAM =MUNGU wa Milele (Mwanzo 21:23)
6: JEHOVAH EL-OHEEKA= BWANA MUNGU Wako (Kutoka 20:2,5,7)
7: JEHOVAH EL-ELYON= MUNGU Aliye Juu Sana (Mwanzo 14:18)
8: JEHOVAH EL-OHIM =Muumbaji wa Milele (Mwanzo 1:1)
9: JEHOVAH SABAOTH =BWANA wa Majeshi (1 Samweli 1:3)
10: JEHOVAH TSIDKEMU= BWANA ni Haki Yetu (Yeremia 23:6)
11: JEHOVAH RAPHA= MUNGU Nikuponyae (Mwanzo 15:26)
12: JEHOVAH MEKADDISHKEM =BWANA Niwatakasae (Kutoka 31:13)
13: JEHOVAH ROHI =BWANA Mchungaji Wangu( Zaburi 23:1)
14: JEHOVAH JIREH= MUNGU Atupaye /Atoaye (Mwanzo 22:14)
15: JEHOVAH HOSEENU= BWANA Aliyetuumba (Zaburi 95:6)
16: JEHOVAH NISSI= BWANA ni Bendera(Beramu) yangu (Kutoka 17:15)
17: JEHOVAH SHALOM =BWANA ni Amani Yangu (Waamuzi 6:24)
18: JEHOVAH SHAMMAH= BWANA Yupo Hapa (Ezekiel 48:35).
MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka yaani hujampokea BWANA YESU awe ni BWANA na MWOKOZI wa maisha yako ndugu hakikisha unampokea leo maana wokovu ni sasa.
Namna za kumshukuru, kumsifu, na kumwabudu Mungu wetu.
Kwahiyo, katika maisha yetu sisi, kama waumini, tunatakiwa kumpa Mungu wetu ibada, (kumshukuru, kumsifu na kumwabudu) kwasababu ya mambo yote hayo niliyoyataja. Tunatakiwa kumtukuza Mungu kwasababu ya sifa zake,
na kwasababu ya tabia zake, na matendo yake na fadhili zake na ahadi zake kwetu.
Sasa basi, hapa chini, nimekuwekea njia kuu tatu ambazo unaweza kumsifu na kumtukuza Mungu kwazo. Utengapo muda wa kwenda mbele za Mungu, unaweza kutuia njiia kuu zifuatazo; Kumtukuza Mungu kwa,
1. Kumwimbia nyimbo za kumsifu na kuwabudu
2. Kumweleza au kusimulia kwa maneno
3. Kumtolea Mungu sadaka na dhabihu
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 30, 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW