Monday, April 11, 2016

KWANINI MUHAMMAD ALIMILIKI WATUMWA NA MATEKA WA KIAFRIKA?

Ndugu msomaji,
Leo tujikumbushe kidogo kuhusu kazi ya Muhammad nabii wa Allah.
"Anas bin Malik alisimulia: Mtume wa Mungu alikuwa safarini na alikuwa na mtumwa Mwafrika aitwaye Anjasha, na alikuwa akiendesha ngamia..." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 95 na.182 uk.117.
"Anas alisimulia: ... Na Anjashah, mtumwa wa Nabii [Muhammad], alikuwa akiendesha ngamia..." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 111 na.221 uk.142.
"Jabir bin ‘Abdullah alisimulia: Mtu mmoja miongoni mwetu alitanganza kuwa mtumwa wake angepewa uhuru baada ya kifo chake. Nabii alimwita yule mtumwa na akamuuza (1) Mtumwa yule alikufa mwaka uleule." Rejeo chini ya ukurasa (1) inasema "Mtoaji uhuru alikuwa na shida, kwa hiyo Nabii alimuuza mtumwa kwa niaba yake na kumruhusu kuiondoa ahadi yake ya kumpa mtumwa uhuru baada ya kifo chake." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 45 (Kitabu cha Rehani kwenye Sehemu Zinazomilikiwa na Wakazi wa Kudumu ‘The Book of Mortgaging in Places Occupied by Settled Population’) sura ya 9 na.711 uk.427.
"Kisha mtu aitwaye Rifa’a bin Zaid ... alimleta mtumwa aitwaye Mid’am kwa Mtume wa Allah" Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 78 (Kitabu cha Viapo na Nadhiri) sura ya 33 na.698 uk.455.
"Kuuzwa kwa Mudabbar (yaani mtumwa aliyeahidiwa na bwana wake kuachiwa huru baada ya kifo cha bwanawe." (433) Jabir alisimulia: Nabii alimuuza Mudabbar (kwa niaba ya bwana wake aliyekuwa bado hai na anahitaji hela)." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 (Kitabu cha Mauzo yaani Kujadiliana Juu ya Bei) sura ya112 juzuu ya 433 na kabla ya uk.238.
"Mtu wa Ansari alimfanya mtumwa wake Mudabbar na hakuwa na mali nyingine yoyote isipokuwa yeye. Nabii aliposikia hilo, alisema (kwa washiriki wake), ‘Nani anataka kumnunua (yaani mtumwa) kwa ajili yangu?’ Nu’aim bin An-Nahham alimnunua kwa Dirham mia nane." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 79 (Kitabu cha Fidia za Viapo Visivyotimizwa) sura ya 7 na.707 uk.464.
"‘Ammar alisimulia: Nilimwona Mtume wa Mungu na mahali pale hapakuwa na mtu yoyote isipokuwa watumwa watano, wanawake wawili, na Abu Bakr (yaani hao ndio waliokuwa watu pekee waliobadili dini na kuwa Waislam kwa wakati huo)." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 57 (Washiriki wa Nabii) sura ya 6 na.12 uk.8.
" [Ibn Az-Zubair] alimtumia [‘Aisha] watumwa kumi ambao aliwaacha huru kama fidia kwa (kutotimiza) nadhiri yake. ‘Aisha aliwaacha huru watumwa zaidi kwa lengo hilohilo mpaka aliwaachia watumwa arobaini. Alisema, ‘Ningejua ningeeleza bayana jambo la kufanya iwapo nitashindwa kutimiza nadhiri yangu nilipokuwa naiweka ili kwamba niweze kuitimiza kirahisi.’"(1)
Rejeo la chini ya ukurasa (1) linasema, "‘Aisha hakueleza bayana nini angefanya endapo angeshindwa kutimiza ahadi yake, hii ndio sababu aliwaachia huru watumwa wengi sana ili aweze kujirahisishia utoshelevu wa kiapo chake." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Maadili na Matendo Mema ya Nabii na Washiriki Wake) sura ya 2 na.708 uk.465.
"Na ‘Ata hakupenda kuwaangalia hao wajakazi waliokuwa wakiuzwa Maka isipokuwa alipokuwa anataka kuwanunua." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 74 (Kitabu cha Kuomba Ruhusa) sura ya 2 na.246 uk.162.
Tendo la Ndoa na Watumwa na Mateka:
"Je mtu anaweza kusafiri na mjakazi bila kujua kama ni mjamzito au la? Al-Hasan hakuona shida kwa mwenye mtumwa kumbusu au kumpapasa kwa mahaba mjakazi.
Ibn ‘Umar alisema, ‘Kama mjakazi afaaye kuhusiana naye kimwili ametolewa kuwa zawadi kwa mtu mwingine, au ameuzwa, au ameachwa huru, bwana wake hatakiwi kufanya naye tendo la ndoa kabla hajapata hedhi moja ili kupata uhakika wa kutokuwepo kwa mimba, na hakuna haja hiyo kwa bikira.’
‘Ata alisema, ‘Hakuna madhara yoyote kumpapasa kimahaba (1) kijakazi mjamzito bila kufanya naye tendo la ndoa. Allah alisema: ‘Isipokuwa kuwapapasa kimahaba wake zao na (mateka wanawake) ambao mikono yao ya kuume inawamiliki (kwani katika hali hii hawastahili kulaumiwa).’" Rejeo chini ya ukrasa (1) linasema, "Mjamzito na mtu mwingine, siyo bwana wake wa sasa." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 (Kitabu cha Mauzo yaani Majadiliano ya Bei) sura ya 113 baada ya na.436 uk.239-240. (Sehemu hiyo hiyo ‘Ata kama hapo awali.)
"Abu Sai’id Al-Khudri alisema kuwa wakati alipokuwa amekaa na Nabii wa Allah alimwambia, ‘Oh Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tunapata mateka wanawake kama sehemu yetu ya nyara, na tunapendezwa na bei zao, una maoni gani kuhusu [tendo la ndoa la] kukatiza kujamihiana na kumwaga nje?’ Nabii alisema, ‘Je unafanya hivyo kweli? Ni vema kwako kutokufanya, Hakuna nafsi ambayo Allah ameifanya kuishi isipokuwa itakuja kuishi." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 (Kitabu cha Mauzo, yaani Majadiliano ya Bei) sura ya 111 na.432 uk.237.
"Ibn Muhairiz alisimulia: Niliingia msikitini na nikamwona Abu Sa’id Al-Khudri na kukaa pembeni yake na nikamuuliza kuhusu Al-’Azl (yaani kukatiza kujaminiana). Abu Sai’id alisema, ‘Tulitoka na Mtume wa Allah kuelekea Ghazwa [vita] ya Banu Al-Mustaliq na tulipata mateka miongoni mwa mateka Waarabu na tuliwatamani wanawake na useja ukawa mgumu kwetu na tulipenda kufanya ngono ya kukatiza kujamihiana. Basi tulipokusudia kufanya ngono ya kukatiza kujamihiana, tulisema, ‘Tunawezaje kufanya ngono ya kukatiza kujamihiana kabla ya kumuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyepo miongoni mwetu?’ Tulimuuliza kuhusu jambo hili na akasema, ‘Ni vema kutokufanya hivyo, kwa sababu nafsi yoyote kama iliandikwa kuishi itaishi mpaka Siku ya Kiama." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 31 na.459 uk.317. Sehemu hii inasema sawa na Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 77 (Kitabu cha al-Qadr) sura ya 3 na.600 uk.391. Kwa maneno mengine, chochote kitakachokuwa kitakuwa, hivyo usizuie kwa namna isiyokuwa kawaida. Muhammad hakuwahi kukosoa kuwasumbua kingono mateka au watumwa ambao mtu anawamiliki.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 9, 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW