Monday, April 11, 2016

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA TATU)

Je, Isa bin Mariamu ni mwana wa Mungu?
Kama kuna jambo ambalo Allah mungu anayeabudiwa na Waislamu analikataa sana kupitia Quran basi jambo hilo si lingine bali ni YESU KUWA MWANA WA MUGU. Allah ansema hivi.
Sura 6:101 – Yeye ndiye muumba wa mbingu na ardhi, inamkinikaje awe na mwana, hali hana mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.
Quran 9:30 – Na Mayahudi wanasema ‘uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ na ‘wakristo wanasema Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale walilkufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa?
Hili ni agizo la kutisha kwamba Wakristo na Wayahudi tuangamizwe kwa kuwa tunaamini Mungu ana Mwana, au wana, lakini Wakristo tunaoamini hivyo kwa sababu Mungu wetu:-
- Yehova alifundisha kuhusu Bwana Yesu hivi:
Kutoka 4:22…Israeli ni Mwanangu Mimi……
Mathayo 17:5……Huyu ni Mwanangu Mpendwa wangu….
Malaika wa Mungu alisem hivi.Luka 1:30-31, 35 – Malaika akamwambia usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kuvuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.
Hivyo basi Isa wa kwenye Quran siyo Mwana wa Mungu lakini Yesu wa kwenye Biblia ni Mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.
Leo tumejifunza tena kuwa, katika Quran Allah kakiri kuwa yeye hana Mwana, lakini kwenye Biblia Yehovah anasema kuwa Yesu ni Mwana wake.
Mungu awabariki sana na tuendelee kujifunza tofauti za Isa wa Quran na Yesu wa Biblia.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 9, 2016

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW