Saturday, April 30, 2016

ALLAH SIO JINA LA MUNGU (SEHEMU YA PILI)


Ndugu msomaji,
Katika mada iliyo pita, tumethibitisha kuwa Mungu wa kwenye Biblia ana jina/majina na Allah wa kwenye Quran naye ana majina 99 kama ilivyo shahidiwa kwenye vitabu vyake angalia link hii:http://www.islamicity.com/mosque/99names.htm .
ZAIDI YA HAPO, NIMETHIBITISHA KUWA ALLAH SIO JINA BALI NI WADHIFA TU KAMA ILIVYO "RAIS" "MFALME" nk. Hayo maneno "Rais", "Mfalme" sio majina bali hao wenye huo wadhifa wanayo majina yao na ndio maana huwa tunasema Rais "fulani" kasema hivi au Mfalme fulani kasema hivi na vile, Lazima tuweke jina la huyo Rais au Mfalme katika maelezo yako.
Kwenye hii mada tunaendelea kumuuliza Allah mswali na kuwauliza Waislam maswali kuhusu huyu Allah mwenye jina lisilo tambulika na au halipo kwenye Taurat, Zaburi, na Injili.
SASA TUANZE MADA YETU:
Waislam hupenda kuanza kusema maneno haya katika hotuba zao: Nukuu: "KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU"
Hayo maneno yanatuambia kuwa "Mwenyezi Mungu" anaye tamkwa na Waislam ana Jina, kama sio "majina".
Swali la kwanza: Kwa ndugu zetu Waislam ni hili hapa. "Mnaweza tuambia hilo jina la Mwenye Mungu ambaye ni mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu ni lipi" Tafadhali tujibuni kwa kutumia aya.
Swali la pili kwa Waislam:
Kama "Allah" ni jina la Mwenyezi Mungu wa Waislam, tunaomba mtupe aya kutoka Quran yenu ambayo Mwenyezi Mungu ambaye ni mwingi wa rehema na mwenye kurehemu anasema kuwa "ALLAH" ni jina langu.
Ndugu Waislam, hakuna haja ya kuchukia wala kutuletea lugha chafu kama ilivyo utamaduni wenu baada ya kusoma maswali yetu mawili ya kwanza ambayo yameenda shule. Kitu cha muhimu ni nyie Waislam mtuletee aya ili tufahamu JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEM ambaye mnamtaka kila mnapo anza khutbah zenu Msikitini.
LAKINI KILA NINAPO ISOMA BIBLIA, MUNGU WA KWENYE BIBLIA ANAJITAMBULISHA KWA MAJINA YAKE KITU AMBACHO NI TOFAUTI NA ALLAH WA KWENYE QURAN AMBAYE MPAKA HII LEO HATUJUI JINA LAKE NI NANI.
Kutoka 3: 13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini? 14Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.
Nilipo endelea kuisoma Biblia Takatifu ambayo imekamilika, Mungu alimwabia Musa katika Kutoka 6:2, 3Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. https://www.wordproject.org/bibles/sw/02/6.htm#0
Ndugu msomaji, hata wewe ambaye ni binadamu unalo jina au majina, lakini kitu cha kushangaza Allah ambaye mwenye Majina 99 tofauti kabisa na Mungu wa Musa na Ibrahim na Daudi na Yesu, yeye ameweka "aina za nomino" na kudai hayo ni majina yake. Huu ni msiba mkubwa sana kwa Waislam.
Kusoma juu ya majina tofauti tofauti ya Mungu kunaweza kutusaidia katika kutambua jinsi Mungu alivyo. Baadhi ya Majina yenyewe ni kama yafuatayo:
Elohim – Mwenye nguvu, mtakatifu (Mwanzo 1:1)
Adonai – Bwana, ikiashiria uhusiano wa mtumishi na bwana wake (Kutoka 4: 10, 13)
El Elyon – Aliyetukuka, mwenye nguvu kupita wote (Mwanzo 14:20)
El Roi – Mwenye nguvu kupita wote na aonaye (Mwanzo 16:13)
El Shaddai – Mwenyezi Mungu (Mwanzo 17: 1)
El Olam – Mungu wa milele (Isaya 40:28)
Yahweh – BWANA “NDIMI”, yenye maana ya Mungu wa milele adumuye kwa uwezo wake mwenyewe (Kutoka 3:13, 14).
Unaona raha iliyo katika Ukristo? Mungu wetu anajitambulisha kwa Majina yake ambayo yanaamanisha na au yatatufundihsa jinsi Mungu alivyo.
Sasa nategemea kuwa umeanza kuelewa kuwa Allah sio jina la Mungu bali ni kitu kingine kabisa na wala hana Uhusiano wowote ule na Mwenyezi Mungu ambaye ni Yehova, Mimi Niko Ambaye Niko wa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 30, 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW