Friday, April 1, 2016

ALIYEKUFA SIKU YA BIRTHDAY YAKE NA KUFUFUKA ASHUHUDIA KANISANI

Waumini waliofika katika ibada ya shukrani iliyoandaliwa na kanisa la Glory of christ ministries international maeneo ya Tottenham jijini London jumapili iliyopita wameweza kusikia ushuhuda kutoka kwa mchungaji Catherine Mganga ambaye aliwahi kufariki kwa muda wa masaa mawili na kuchukuliwa mbinguni nakuonyeshwa maeneo mbalimbali na kurudishwa tena duniani

akishuhudia mbele ya waumini kanisani hapo mchungaji Catherine amesema mnamo mwaka 1975 wakati anaadhimisha siku ya kuzaliwa kwake(Birthday) akiwa na dada yake pamoja na ndugu jamaa na marafiki walikuwa wanasifu na kuabudu mara alijikuta akiangalia angani na kuona malaika akishuka kwenye kaa la moto,akiwa anapaa aliona mwili wake mwingine ukiwa bado sakafuni, anasema alipofika mbinguni alichukuliwa na malaika hadi sehemu ambayo watu duniani wakiomba maombi yao yanazuiwa na ibilisi, anasema kuna giza kuu
Mchungaji Grace Gwajima akifafanua maana ya ibada ya shukrani kanisani hapo

Waumini wakimsikiliza mchungaji Grace Gwajima

amesema mara baada ya kutoka hapo malaika akawa anamchukua kumpeleka jehanamu,amesema akawa anakataa kwenda akijua malaika anakwenda kumuacha huko pia kwasababu ya giza lilivyokuwa akazidi kuogopa lakini malaika akamwambia twende ukaone ili upate kuwashuhudia watu duniani,amesema alianza kulia na kumuomba malaika kurudi sehemu ambayo iliwafanya waumini waliokuwepo kanisani hapo kutaka kusikia kilichoendelea kutokana na kilio chake.
Mchungaji Grace akimkaribisha mchungaji Catherine kwa ushuhuda

Mchungaji Catherine Mganga akishuhudia

pia waumini waliweza kusikia shuhuda kutoka kwa watu wengine akiwemo mama Melisa ambaye alishuhudia juu ya binti yake huyo mwenye miaka saba kwamba mwaka jana alikuwa anafanya maombi kwamba mama anunue nyumba mpya,hata akiwa anajiandaa kwenda shule asubuhi maombi ni hayohayo Mungu amwezeshe mama yake anunue nyumba mpya na kweli Mungu akafanya miujiza  mama yake akanunua nyumba mpya,lakini mambo yakabidilika gafla kwa Melisa amesema akaanza kupata malalamiko kutoka shuleni kwamba Melisa kamchapa kibao mwalimu wake,ni mbishi pia kuna wakati anabadilika kabisa muonekano wake ukimwangalia,kwa mujibu wa mama yake anasema hakuwa akiamini maneno yote kwakuwa binti yake hana tabia hizo,ndipo uongozi wa shule walipomshauri kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi zaidi, jibu alilopewa ni kwamba inawezekana ni uchovu kwahiyo anahitaji muda wa kutosha kupumzika kitu ambacho mama huyo alikipinga


Mama Melisa akiwa na Melisa akitoa ushuhuda ambapo pia walimaliza kwa kuimba wimbo

amesema alimhamisha shule lakini kilichotokea huko pia hakuamini baada ya kusikia mwanae amemkwangua mwalimu pia ameangusha kabati la vitabu kitu ambacho hata walimu wa shule hiyo hawakuamini kwamba ni Melisa aliyefanya yote hayo,lakini siku moja akiwa darasani peke yake alipiga kelele akipinga jambo "no noooooooooooo" mwalimu wake alipomtazama alimuona kakaa peke yake alipomuuliza kulikoni hakujibu, ndipo mama yake akajua kuna kitu kinaendelea kwakuwa hata binti yake hakuwa akipenda kuingia chumbani kwake kama ilivyokuwa zamani kisa kikiwa ni maombi ambayo alikuwa akiyafanya ndipo rafiki yake na mama melisa alipomchukua kumpeleka kwa mchungaji Grace Gwajima lakini kabla ya kuondoka nyumbani Melisa alikuwa hawezi kumtazama mama yake machoni alikuwa kama anayeona aibu, baada ya maombi Melisa akabadilika na kuwa kama awali

Ndipo mama yake alipomuuliza visa vyote vilivyotokea Melisa akamwambia mama yake kuwa kuna sauti ilikuwa ikimwamuru kufanya hivyo hata kuwapiga wenzake ikiwa pamoja na mwalimu,hata siku alipopiga kelele darasani ilikuwa inamlazimisha kufanya tukio ambalo yeye anasema alikuwa analipinga kukawa na mtu ambaye anamtisha ila watu wengine walikuwa hawawezi kumuona, baada ya maombi anasema huyo mtu pamoja na sauti haijarudi tena na amesharudi katika hali yake ya maombi
Watoto nao walisimama na kuzungumza mistali mbalimbali ya Biblia
Baadhi ya wasumini waliokuwepo ibadani

jumapili hiyo kulikuwa na wengi ambao walishuhudia shuhuda zilizowagusa wengi,Gospel kitaa inaahidi kukuletea shuhuda zote ikiwa pamoja kumalizia shuhuda ya Mchungaji Catherine Mganga ambaye kwasasa amejiunga rasmi na kanisa hilo ambapo jumapili ijayo atakuwa kanisani hapo kumalizia ushuhuda wake ikiwa ni pamoja na kuhubiri wakiwa pamoja na mchungaji Grace Gwajima
waumini wamekuwa wakiongezeka katika kanisa hilo kutokana navile Mungu anatenda miujiza na kuwafungua watu wenye matatizo mbalimbali ikiwa ni miezi mitano tangu kuanza kwa huduma hiyo. ambapo ibada wanafanyia katika ukumbi wa shule ya sekondari Peak view huko Tottenham,Langham Road, N15 3RB
moja ya jengo la shule hiyo ambapo ibada zinafanyika

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW