Monday, March 28, 2016

UTATA NDANI YA QURAN. "AYA ZA QURAN ZAPINGANA"



Ndugu msomaji,
Leo tutaangali utata mkubwa uliopo kwenye Quran kama ifuatavyo:
Sura Al-Baqara 2:109
109. Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Hapa quran inaongelea watu wa kitabu (yaani Wakristo), na kusema:
Wengi wa watu wa kitabu, kutokana na wivu wao, wanatamani kuwarudisheni kwenye kutoamini baada ya kuwa mmeamini, pamoja na kwamba ukweli umeshadhihirishwa wazi mbele yao. Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake. Yeye ana nguvu juu ya kila kitu.
Quran pia inawaagiza Waislamu katika sura Al Imran 3:20 kwamba:
Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata. Na waambie walio pewa Kitabu na wasio na kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu basi wameongoka. Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake.
Yaani:
... kama wasipowasikiliza, basi ninyi kazi yenu pekee ni kuwaonya tu.
Kwa hiyo, kutokana na aya hizi mbili, yaani Al-Baqara 2:109 na Al Imran 3:20, tunaona mambo yafuatayo:

1. Ni wajibu wa Waislamu kuhubiri dini yao lakini si wajibu wao kuwalazimisha watu kuamini dini yao.
2. Allah kwa wakati wake atawafunulia wale wasioamini ukweli wa mambo.
3. Ni wajibu wa Waislamu kutoa maonyo tu kwa wale wanaowahubiria.
LAKINI, HEBU TAZAMA AYA ZIFUATAZO JINSI ZINAVYO PINGA AYA ZA WALI:
Al-Nisa 4:101
...... Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.
Yaani,
Wale wasioamini ni maadui zenu wakubwa. Akimaanisha Wkaristo na Wayahudi ni maadui wakubwa wa Waislam.
Vilevile inasema katika sura Al-Tawba 9:3
Proclaim a woeful punishment to the unbelievers.
Yaani:
Tangazeni mapigo makuu (ya ole) kwa wasioamini.
Pia quran inasema katika sura Al-Anfal 8:39
Make war on them until persecution is no more and Allah’s religion reigns supreme.
Yaani:
Fanyeni vita juu yao hadi kusiwepo na mateso tena na hadi pale dini ya Allah itakapokuwa imetawala.
Maswali:
1. Je, aliyempa Muhammad maneno ya 2:109, 3:20 na yale ya 4:101, 9:3, 8:39 ni huyo huyo au ni wawili tofauti?
2. Iweje aseme kuwa usiwalazimishe watu kuamini bali waonyeni na kuwavumilia tu, kisha anageuka sehemu nyingine na kusema walazimisheni, tena kwa vita?
3. Je, hii si ishara ya tabia ya usahaulifu ambayo si tabia ya Mungu bali ni ya mwanadamu?
4. Kama ni huyo huyo, je, aya hizi zinafanana au zinapingana?
5. Kama zinafanana, ni kwa vipi?
6. Kama zinapingana, huu si ushahidi tayari kuwa quran haitoki kwa Mungu wa kweli kama ambavyo quran yenyewe imeweka kigezo cha kujua hilo? Maana Mungu wa kweli hawezi hata kidogo kusahau jambo alilolisema kabla halafu aje aseme kitu tofauti. Ni viumbe tu ndio wanaweza kusahau na kukosea.
Hakika Quran si kitabu cha Mungu. Waislam nawakaribisha kwa Mungu wa Biblia ambaye alimtuma Mwanawe kuja Duniani kwa ajili ya dhambi zetu.
Karibuni kwa Yesu.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 28, 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW