Thursday, March 3, 2016

MUHAMMAD AKIRI KUPATA UTUME KWA KUCHEZEWA NAFSI YAKE NA SHETANI

Ndugu msomaji,
Kwanza ningependa tujifunze maana ya neno Nabii:
Nabii ni mtu gani?
Nabii ni mtu aliyeteuliwa rasmi kwa vigezo vya Kiungu ili kuleta ujumbe wa Mungu kwa wanadamu, kwa maneno mengine nabii ni msemaji wa siri za Mungu.
Mitume wote na manabii wote wa Biblia waliwai ongea na Mungu. Lakini, Mtume wa Allah "Muhammad" hakuwai ongea na Mungu HATA MARA MOJA. Je, utume wake tutauamini vipi maana hakuwai ongea na aliye mtuma?
Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu aliye Mtuma? Maana ya neno Mtume kwa kifupi: Ni Mtu aliye tumwa.
HEBU TUANGALIE, HUYU MUHAMMAD ALIZALIWAJE NA KUUPATAJE UTUME WAKE?
1. MUHAMMAD ALIKUWA NA SHETANI TANGU KUZALIWA KWAKE,
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa "Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa na shetani tangu alipozaliwa, (Fat'hul Baary Juzuu ya 6 Uk. 389).
Je, kuna ushahid wowote ule kuwa Muhammad alitolewa Shetani ALIYE KUWA NALO TANGU KUZALIWA KWAKE? Kama upo Basi Waislam, tuleteeni tuuone.
2. MUHAMMAD AKIRI KUPINGWA NA KUBANWA MBAVU ZAKE NA KIUMBE AKIWA PANGONI,
Katika kitabu kiitwacho: Maisha Ya Nabii Muhammad s.a.w uk 16-17 kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy, tunasoma kama ifuatavyo;-
Hata siku moja- katika mwezi wa Ramadhani mwezi 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 ½ wa umri wake- mtume alimwona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumwona wapi katokea, akamwambia; “soma”. Mtume akamjibu; “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujifundisha kusoma.” Akaja akamkamata akambana, akamwambia tena; “soma,” Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tau akamwambia; “soma- Iqraa Bismi Rabbik.” Akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake. Kisha mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika Qur’an, ingawa haijawekwa mwanzo.
Mara, yule mtu (Malaika) akaondoka machoni mwake- asimwone kenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake-khofu imemshika. Alipofika nyumbani, Bibi Kadhija alidhani ana homa, akamfunika maguo gubigubi na akakaa mbele yake akimsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia alimweleza Bibi Kadhija yote yaliyomtokea; na Bibi Kadhija akamtuliza moyo wake, akamyakinishia ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu akaondoka akenda kwa jamaa yake – Bwana Waraqa bin Naufal- akampa habari yote iliyompata mumewe. Naye akamwamrisha amwite. Na mtume akenda akamweleza habari yake yote. Bwana Waraqa akamwambia; “ Huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa. Basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu, nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako; Inshaallah nitakuwa mkono wako wa kulia” Wakarejea kwao na khofu yote imemtoka”.
Alipokuwa pangoni alichezewa na Shetani: Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
3. MUHAMMAD AKIRI KUCHEZEWA NAFSI YAKE NA SHETANI
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na Shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
Katika tukio hili lililompata Muhammad akiwa pangoni , ndipo Waislamu wote ulimwenguni wanapolieleza kuwa hapo ndipo Muhammad s.a.w alipoletewa wahyi (ufunuo) na kupewa unabii na utume. Lakini unapotafakari juu ya ujumbe huo utaona kuwa hata yeye mwenyewe hajui nini kilichokuwa kimemtokea kule pangoni. Ndiyo maana tunasoma kuwa alipofika nyumbani kwake mkewe Bi. Khadija alimfunika nguo mumewe akidhani ana homa. Muhammad alimweleza mkewe kilichomtokea kuwa ni “Shetani” hakumsema malaika yeyote kama Waislamu wanavyotaka kutuaminisha leo. Kwa sababu kama angekuwa ni malaika kama tunavyosoma ndani ya Biblia ,asingesita kujitambulisha kwa Muhammad kuwa yeye ni nani.
KUFUATANA KITABU CHA MAISHA YA NABII MUHAMMAD, tunajifunza kuwa Muhammad kwa mara ya kwanza kabisa alipata utume wake pangoni baada ya NAFSI YAKE KUCHEZEWA NA MASHETANI.
Wahyi (ufunuo) uliokuja kwa Muhammad alisikia makengele, uso kuwa mwekundu, jasho kumtoka. Katika Bukhar, Hadithi na 2, Juzuu na 1,Al-Lu’lu Kitabu cha 3.Uk. Na.874 Hadithi na 1505 “Hadithi ya Aisha r.a mama wa waumini amesema, kuwa Al Harith ibn Hisham r.a alimuuliza mtume wa Allah s.a.w ‘ Ewe mtume wa Allah hivi wahyi (ufunuo) hukujia vipi?’ Mtume wa Allah s.a.w akajibu, “ Wakati mwingine hunijia kama mlio wa kengele, na aina hiyo ndiyo ngumu zaidi kwangu, inaondolewa hali hiyo kwangu wakati tayari nimeshapata wahyi. Na nyakati nyengine malaika anakuja kwangu akiwa katika mfano wa mtu, kwa hiyo ananieleza na ninayazingatia aliyoyasema.” Aisha r.a alisema , Na hakika nilimwona unamshukia wahyi siku ya baridi kali na ilipomuondoka hali hiyo, paji lake la uso lilichuruzika jasho.”
Muhammad akiwa Medina aliulizwa na Wayahudi ikiwa ufunuo wake umetoka kwa Mungu wa Kweli kwa kumtaka atoe sifa za manabii. Akijibu swali hilo alisema:
Mkweli Mwaminifu Juzuu 3-4 Uk.63.Hadithi Na. 880. “Kasema Mtume (s.a.w):- (Mambo) mane ya sheria za mitume (Kuwa na) na haya,na kujipaka mafuta mazuri,na kuowa (wake),na kupiga mswaki.
Hizi si sifa za Ki-Mungu kwa nabii na mtume bali ni za kibinadamu tu.
4. QURAN INASEMA KUWA, NABII LAZIMA AFANYE MIUJIZA; MUHAMAMD AKIRI KUWA YEYE NI MTUME BANDIA NA HAKUFANYA MIUJIZA
Qur’an nayo inathibitisha kuwa manabii na mitume ni lazima wafanye miujiza.
Qurani 40:78 Suratul Al-Muumini [Waumini] inasomeka “Na kwa yakini tumewatuma mitume kabla yako wengime katika wao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia na haikuwa kwa mtume yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”
Muhammad hakupewa kufanya muujiza wowote ili kuthibitisha madai ya unabii na utume wake.
Qur’an 29:50 Suratul Al-Ankabuut (Buibui). “Na walisema “Mbona hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa Mola wake? Sema miujiza iko kwa Mwenyezi Mungu tu (akitaka atakuteremshieni na kama hataki basi),nami hakika ni mwonyaji mbainishaji (dhahiri tu).” (Taz. Qur,an 6:35-37 13:7,)
MASWALI:
(i). Kama Jibril ndie alitumwa na Allah, na huyo Allah ni Mungu, kwanini Muhammad alisema kuwa nafsi yake imechezewa na MASHETANI baada ya kukutana na Jibril?
(ii). Kama Jibril alitoka kwa Allah, kwanini Muhammad alipo toka pangoni alisema kuwa Jibril AMEMZUGA AKILI YAKE?
(iii) Je, wapi katika Injili au Taurat au Zaburi tunasoma kuwa Manabii na Mitume katika Biblia walipata kwa njia ya homa na kukiri kuchezewa na mashetani kama Muhammad wa kwenye Quran?
(iv) Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu aliye Mtuma? Maana ya neno Mtume kwa kifupi: Ni Mtu aliye tumwa.
3. KUROGWA KWAKE MUHAMMAD
Zaidi ya hayo tunaona Muhammad alirogwa. Kurogwa ni hali ya mtu kuathirika na nguvu za giza yaani uchawi. Je nabii au mtume wa Mwenyezi Mungu wa Kweli anaweza kurogwa?
Amesema Mwanaisha Mkewe Mtume kuwa "Yahudi Mmoja aitwaye Labiid bin Al'answan alimroga Mtume Muhammad, ikawa Mtume baadhi ya Nyakati huchanganyikiwa na kuanza kuita Ovyo ovyo na kupiga makelele. (Sahih Muslim J. 4 uk. 38-39)
Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha kuwa utume wa Muhammad una utata.
MASWALI:
(a) Hivi, kuna Mtume au Nabii yeyote yule ambaye alikiri kurogwa kama Muhammad?
(b) Hivi Allah alikuwa wapi wakati Muhammad anarogwa? [Ingawa Quran inakiri kuwa aliye teremsha uchawi/urogi ni Allah]
(c) Wapi tunasoma kuwa Muhammad aliombewa na kutoa huo uchawi/urogi aliofanyiwa na Labiid bin Al'answan?
YAANI INA MAANA MUNGU ALIKOSA MTU WA KUTUMA MPAKA ATUME MTU ALIYECHEWA NA MASHETANI KAMA HUYU?
Ndugu msomaji,
Muhammad hakuwa Mtume wa Mungu na wala hana sifa za KITUME.
1. Muhammad hakuwai ongea na Allah aliye mtuma.
2. Muhammad alikuwa na Shetani tokea kuzaliwa kwake.
3. Muhammad alikiri kuchezewa na Shetani wakati wa kusimikwa utume wake Pangoni.
4. Muhammad alikiri kuwa Shetani amechezea akili na nafsi yake.
5. Muhammad alikiri kuwa alirogwa na Labiid bin Al'answan.
SASA WAISLAM, NIONYESHENI, wapi kwenye Taurat, au Zaburi au Injili kama kuna Mtume aliye na sifa za ajabu kama za Muhammad.
Karibuni kwa Yesu ambaye ndie Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW