Thursday, March 3, 2016

MASHAHIDI WA YEHOVA WANAPINGA WOKOVU KWA KUMKIRI YESU KRISTO

i. Wanadai kuwa kuna Nafasi ya Pili Kuokolewa.
ii. Wanadai kuwa si nia ya Mungu kuwaokoa watu sasa.
iii. Wanadai kuwa Mavuno ya Injili yamekwisha.
Ndugu msomaji,
NINI MAANA YA KUOKOKA?
KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani. Ambavyo jamii yetu maneno haya tunayatumia sana,
NINI MAANA YA WOKOVU?
Watu wengi neno hili wamelitafsiri vile wa pendavyo au waonavyo sasa Swali hili acha lijibiwe na maandiko matakatifu, na maneno haya yasibadilishwe kwamba ni wakati gani wa kuokoka kitendo kikishamalizika cha kukiri kifuatacho ni uwokovu kwa mjibu wa neno, fuatilia hapa chini, “Kwasababu ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Warumi 10:9-10.)
LAKINI, MASHAHIDI WA YEHOVA WANASEMA KUWA ILE FIDIA ALIYOTOA YESU KWA WANADAMU WOTE HAITHIBITISHI UZIMA WA MILELE WALA HAIWEZI KUKUOKOA:
Kitabu chao cha “Studies in the Scriptures” Vol. 1, uk. 150, cha Mashahidi wa Yehova kinasema, “Ile ‘fidia kwa watu wote’ aliyoitoa yule ‘mwanadamu Kristo Yesu’ haitoi wala kuthibitisha uzima wa milele wala baraka kwa mtu ye yote; bali inamthibitishia kila mtu nafasi nyingine au jaribu la kupata uzima wa milele.”
MASHAHIDI WA YEHOVA WANADAI KUWA KUNA NAFASI YA PILI YA KUOKOLEWA
Katika uk. 143, wanasema, “Nafasi ya pili itakuwa bora kuliko nafasi ya kwanza kwa sababu ya mazoezi yaliyopatikana katika matokeo ya jaribu la kwanza.” Tena, katika uk. 130, 131 wamesema: “Wote walihukumiwa mauti kwa sababu ya kuasi kwake Adamu, na wote watafurahia (katika maisha hayo au yanayokuja) na nafasi kamili kupata uzima wa milele kwa masharti mema ya Agano Jipya.”
LAKINI, MAFUNDISHO YA BIBLIA YANASEMA NINI KUHUSU WOKOVU?
HAKUNA NAFASI YA PILI KUOKOLEWA KAMA WANVYODAI MASHAHIDI WA YEHOVA!!!!!
Soma Waebrania. 9:27, “Kufa mara moja na baada ya kufa hukumu.”
Luka. 9:59-60, “Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao.”
Matendo. 13:44-46 “Kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele.” Je, alisema hapa kwamba wata pata nafasi ya pili! Hata siku moja!
Waebrania. 10:26, “......haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi.”
Kwa hiyo tumeona kwa urahisi kwamba Biblia inatufundisha kwamba tutaishi na tutakufa mara moja tu na bada ya kufa hukumu!!
Lini unatakiwa ufanye uamuzi huu muhimu?
Hebu MUNGU na aseme nawe kupitia maneno yake ambayo ni amina na kweli anasema:
Warumi 13:11 Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
2Wakorintho 6:2 "Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa"
Biblia inaonya kuwa "tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa" yaani wakati huu unaposoma hapa ndio wakati wako wa kutubu na kumgeukia Mungu kwa njia ya kristo kama bado haujafanya hivyo kwani huu ni uamuzi ambao kila mwanadamu lazima aufanye.Mungu ana kalenda yenye miaka mingi lakini kwenye swala la kuukiri wokovu wa kristo wakati ni sasa..Ninakuomba umpe kristo maisha yako,ili hata kama ukifa muda wowote akupokee na uishi naye milele.
MASHAHIDI WA YEHOVA WANAENDELEA KUFUNDISHA KUWA SI NIA YA MUNGU KUWAOKOA WATU KATIKA KIPINDI CHA INJILI BALI ULIMWENGU UTAOKOLEWA KATIKA KIPINDI CHA UTAWALA WA MIAKA 1000.
Mafundisho ya Biblia yanasema nini kuhusu Wokovu:
Yesu mwenyewe alifundisha katika Marko. 16:15-16, kwamba tuhubiri Injili ili watu waokolewe. Na tangu siku ya Pentekoste wakovu umehubiriwa, Matendo. 2:38, 40; 13:26, 47. Pia Paulo alisema, “LEO NI SIKU YA WOKOVU”, katika 2 WaKorintho. 6:2; Wafilipi. 2:12. Na katika Waebrania. 2:3-4, mwandishi anatuambia kwa urahisi kama tunakataa wokovu hatuwezi kukwepa adhabu!!! Kwa hiyo ina maana tunaweza kukosa wokovu leo!
Na tunakosa kwa kutotii injili, katika kipindi cha Injili.
LAKINI, MASHAHIDI WA YEHOVA WANADAI KUWA, “MAVUNO” YA INJILI YAMEKWISHA.
Katika kitabu chao, “Studies in the Scriptures,” Vol 2, uk. 245, Mashahidi walisema: “Miaka arobaini ya mavuno ya kipindi cha Injili itakoma Oktoba 1914, na vivyo hivyo, upenduzi wa Ukristo, kama unavyoitwa, lazima tutegemee kuuona mara.” Hivyo wanasema kuwa hakuna mtu awezaye kuokolewa baada ya Oktoba 1914, BK. Tena, Ukristo (maana yake madhebehu yote isipokuwa kanisa lao) utapinduliwa mara baada ya mwake ule.
BIBLIA INAWAJIBU MASHAHIDI WA YEHOVA KUWA:
Mwaka 1914 umekwisha kupita zamani; mbona madhehebu bado yapo? Isitoshe, ikiwa mavuno ya kipindi cha Injili yalikwisha mwaka 1914, basi Mashahidi wenyewe walio hai leo wamechelewa!
Imekuwaje wao kudai kuwa wamejua tareje na majira hali Yesu amesema hakuna ajuaye mambo hayo?
(Marko. 13:32; Matendo. 1:7).
WOKOVU NI HAPA DUNIANI
Usikubali uongo wowote wokovu ni hapa duniani na baada ya kufa ni hukumu na hukumu hii itategemea uliishije hapa duniani.” Na Kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, baada ya kufa hukumu, Waebrania 9:27”
“Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo Watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima na wale waliofanya mabaya kwa ufufuo wa hukumu Yohana 5:28-29”
Kwa hiyo maisha yetu ya hapa duniani ndiyo yatakayoamua hukumu yetu itakavyokuwa.
Mungu amezibitisha mwenyewe kuwa kuna Watakatifu Duniani.”Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, Nao ndio nliopendezwa nao, Zaburi 16:3”
Kataa uongo wowote tunaokoka hapa duniani na tunaishi Maisha ya utakatifu yanayompendeza Mungu.
SALA YA TOBA
Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako. Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.
Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa wewe kuokoka. Lakini napenda kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma Wakolosai 1:13,14 na Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na Yohana 3:7. Ni vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.
Kwa hiyo kama unataka kuokoka - tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa sauti sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Baada ya kuokoka
Unapoanza maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:
1.Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3.Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4.Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5.Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
Ukipenda unaweza kuniandikia kwa anwani hii hapa chini juu ya uamuzi uliofikia leo wa kuokoka, ili tumshukuru Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia, tukutumie maandiko mengine ya kukusaidia: maxshimbaministries@gmail.com.
Ni maombi yangu Mungu ayafungue macho ya Mashahidi wa Yehova kwa ukweli wa injili na mafundisho ya kweli ya neno la Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW