Sunday, March 20, 2016

KUMBE FIRAUNI A.K.A FARAO ALINYENYEKEA NA KUWA MUISLAMU



Ndugu msomaji,
Kutokana na ushahid wa Surat Yunus aya ya 90-92, iliyo teremka Makka na kufanyiwa turjuma na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani inakiri kuwa Farao aka Firauni alisilimu na kuwa Muislam.
Surat Yunus 90. Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea!
91. Ala! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi!
92. Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu
Aya hizo hapo juu kama zilivyo kwenye Surat Yunus zinatufahamisha kuwa Farao aka Firauni alisilimu na kuwa Muislam, lakini nilipo endelea kuisoma Quran kwa makini, nikakutana na shaka kubwa sana ndani ya Quran. Hebu soma kwanza ......aya kutoka Surat An Nisaai amabazo zinapinga aya kutoka Surat Yunus hapo juu.
Surat An Nisaai 17. Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima.
18. Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu.
Allah kupitia Surat An Nisaai analeta shaka na utata kwa kusema kuwa, toba inayo kubaliwa ni ile uliyo fanya dhambi kwa ujinga, lakini wote tunafahamu kuwa Farao yeye alikuwa anajua nini anafanya, hivyo hawezi kuingizwa kwenye kundi la wajinga.
ENDELEA KUSOMA UTATA NDANI YA QURAN
Surat Ghaafir 83. Walipo wajia Mitume wao kwa dalili zilizo wazi walijitapa kwa ilimu waliyo kuwa nayo. Basi yakawazunguka waliyo kuwa wakiyafanyia maskhara.
84. Walipo iona adhabu yetu walisema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee, na tunaikataa miungu tuliyo kuwa tukiishirikisha naye.
85. Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao wamekwisha iona adhabu yetu. Huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu ulio kuwa kwa waja wake. Na hapo walio kufuru walikhasiri
Allah anaendelea kupinga ya zake mwenye kwa kusisitiza kuwa, yeye huwa hasamehi watu ambao wamekwisha ionja adhabu, lakini cha kushangaza, WAISLAM HAWA HAWA, huwa wanaombea Maiti msamaha wa dhambi, sasa Allah atawasamehe vipi maana teyari wamesha ionja adhabu ya kifo?
Kufuatana na wasomi wa dini ya Uislam, wengi wao nakubali kuwa Allah alimuokoa Farao na kumsamehe dhambi zake na kuwa Muislam. (Muhammad Asad, The Message of the Qur'an [Dar al-Andalus Limited, 3 Library Ramp, Gibraltar 1993], p. 306, fn. 112)
Ndugu zanguni, kila ninapo isoma Quran, huwa napata na kukutana na utata mkubwa sana kiasi cha kujiuliza, hivi ni kweli Allah aliumba na yeye ni mjuzi wa yote? Mbona Quran yake imejaa shaka na utata mkubwa?
Nawasihi Waislam wote duniani, mje kwa Yesu ambaye yeye hana utata wala hana shaka ndani yake. Maana Yesu ni JIBU, NJIA NA YEYE NI MWOKOZI WETU NA MUNGU MKUU.
Je! Unataka kumpa Yesu maisha yako sasa hivi ili akuokoe na kukupatia uzima wa milele? Je! Unajua maana ya kumpokea Yesu maishani mwako?
Kumpokea Yesu maana yake ni KUKIRI kwamba Yesu ni MWOKOZI, na pia hakuna mwingine awezaye kuokoa isipokuwa Yesu pakee. Biblia Takatifu inatuambia kwamba:
“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” (Matendo 4:12)
Kama unataka kuokoka sasa hivi; Tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa kutamka kwa kinywa chako sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu yote. Ninatubu kwa dhati ya kweli kutoka rohoni mwangu. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho Wako – Uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Nakuomba unifanye niwe vile utakavyo mimi niwe. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina."
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zote zimesamehewa kabisa. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
Baada ya kuokoka
Unapoanza maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:
(a) Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7).
(b) Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11).
(c) Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17).
(d) Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6).
(e) Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25).
(f) Ikemee dhambi na ujitenge nayo. Ukiamini, kwa jina la Yesu unaweza kuishi maisha matakatifu (Yakobo 4:7-8).
(g) Jidhihirishe wazi kwa watu kwamba wewe umeokoka na pia shuhudia kwa watu injili (Mathayo 10:32-33; Warumi 1:16).
Hongera kwa kuokoka, tangu sasa umekuwa kiumbe kipya. Nakutakia baraka tele katika jina la Yesu Kristo, amina.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 20, 2016

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW