Friday, February 12, 2016

YESU ANAKIRI KWA MDOMO WAKE KUWA YEYE NI MUNGU. (SEHEMU YA PILI)

Ndugu Msomaji,
Leo nitaleta ushahidI zaidi wa Yesu akisema kwa mdomo wake kuwa yeye ni Mungu.
Waislam wamekuwa na tabia ya kusema na kuuliza, wapi Yesu kasema "Mimi Yesu ni Mungu" . Waislam wanasisitiza kuwa, lazima wapewe aya yenye maneno hayo. Leo kwa mara nyingine tena nitawapa aya ambayo Yesu anasema YEYE NI MUNGU.
YESU ANAJARIBIWA NA SHETANI.
Kwenye aya hapa chini, utasoma kuhusu Ibilisi alivyo mchukua Yesu na kwenda kumjaribu. SASA SOMA:
Mathayo 4: 5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Kwenye hizo aya hapo juu, tumesoma kuwa Ibilisi anamjaribu Yesu, Ibilisi anasema kwa Yesu kuwa, ajitupe kutoka juu ya kinara, hilo lilikuwa ni jaribu la Ibilisi kwa Yesu. Ibilisi alitaka kuona kama Yesu atamsikiliza na kutenda hayo. Ingawa Yesu angewaza kujitupa kutoka huo mnara na kuwaamuru Malaika wake wangemchukua kutoka mikononi mwao, lakini KAMA ANGEFANYA HIVYO, basi angekuwa ametenda matakwa ya Shetani na kufuata maamrisho ya Shetani.
SASA SOMA NINI YESU ALIMJIBU SHETANI HAPA CHINI,
Mathayo 4: 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
YESU ANATOA JIBU AMBALO WENGI WENU HAMKUWAI LIFIKIRIA.
1. Kumbuka Ibilisi alikuwa anamjaribu Yesu.
2. Kumbuka kuwa katika hayo majaribu, walio kuwepo ni (a) Mjaribu ambaye ni Ibilisi na (b) Mjaribiwa ambaye ni Yesu.
SASA BASI, MJARIBIWA AMBAYE NI YESU ANAMJIBU MJARIBU-SHETANI KUWA USIMJARIBU BWANA MUNGU WAKO.
Maswali ya kujiuliza:
1. Kwanini Yesu alisema usimjaribu Bwana Mungu wako, huku tukifahamu kuwa anaye Jaribiwa ni Yesu?
2. Kwanini Ibilisi hakupinga madai ya Yesu kujiita "BWANA MUNGU", huku Ibilisi akifahamu kuwa anaye mjaribu ni Yesu?
3. Kwanini Yesu hakukataa kuitwa Mwana wa Mungu katika aya ya 6?
4. Kwanini Ibilisi alimuita Yesu Mwana wa Mungu?
MJARIBIWA AMBAYE NI YESU, ANAMWAMBIA MJARIBU-SHETANI kuwa USIMJARIBU BWANA MUNGU WAKO?
Kwanini Yesu anaye jaribiwa na Shetani alisema umsimjaribu "BWANA MUNGU" na hakusema kuwa usinijaribu mimi Yesu?
Nivigumu sana kupinga Uungu wa Yesu, maana hata Shetani aliye kuwepo zama kwa zama, anakiri kuwa Yesu ni Mungu , na zaidi ya hapo, anamuita Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu "aya ya 6". Kwanini SHETANI HAKUMSHTAKI YESU kwa kujiita BWANA MUNGU?
Leo kwa mara nyingine tena nimejibu swali, wapi ilipo aya ambayo Yesu anasema yeye ni Mungu. Sasa swali langu kwa WAISLAM, je mpo teyari kumpokea Yesu aliye sema yeye ni Mungu?
SASA, nawakaribisha mje tujadili hii mada kwa utulivu na kwa kutumia aya za Biblia tu. Maana hicho ndicho kitabu pekee cha Mungu.
YESU KASEMA KUWA YEYE "BWANA MUNGU"
Mungu awabariki sana.
Max Shimba
For Max Shimba Ministries

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW