Thursday, February 25, 2016

MALAIKA GABRIEL WA BIBLIA NI TOFAUTI NA JIBRIL WA KWENYE QURAN


Ndugu msomaji,
Tokea kuanzishwa Kwa dini ya uislam, waislamu duniani wanaamini na kuifundisha jamii kuwa malaika aitwae ‘Gabriel’ Kama maandiko matakatifu ya Biblia yanavyofundisha ndiye malaika ‘Jibril’ Kama Quran inavyosimulia.
Swali la muhimu je ni kweli kuwa malaika “Gabriel” ndiye “Jibril” nakusihi fuatilia somo hili ili kujua ukweli….
HOJA ZA WAISLAMU ZA KUAMINI KUWA MALAIKA GABRIEL NDIYE JIBRIL
Waislam wanalinganisha kwa kusoma aya za Quran na Biblia na kusema kuwa malaika Gabriel ndiye Jibril wanasoma aya hizi….
QURAN 19:16-17 SURAT MARYAM
16. Na mtaje Mariamu kitabuni (humu) alipojitenga na jamaa zake (akenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti) 17. Na akaweka pazia kujikinga nao.Tukampelekea muhuisha sharia yetu (jibril) - akajimithilisha kwake kwa sura ya Binadamu aliye kamili.
LUKA 1:26-28
26. Mwezi wa sita, malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti. 27. Kwa mwana mwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake Yusufu wa mbari ya Daudi. Na jina lake Bikira huyo ni Mariamu 28 Akaingia nyumbani kwake akasema, salamu uliyepewa Neema, Bwana yu pamoja nawe.
“Mbali na kusoma aya hizi, pia wanaendelea kusoma kitabu cha maisha ya nabii Muhammad kilichotungwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa Kenya marehemu sheikh Abdallah Saleh Al-Farsy katika ule ukurasa wa 17 kifungu (A) kuna maneno haya...
NAMNA YA KULETWA WAHYI…
Waislamu wanaitikadi kuwa Quran ni maneno ya Mwenyezi Mungu na vilevile Taurat ya nabii Musa na injili ya nabii Isa, na Zaburi ya nabii Daudi. Vyote pia ni vitabu vyenye maneno ya mwenyezi Mungu. Lakini Mungu haonekani Kwa macho wala hayupo mahali mahsusi. Basi vipi hao mitume wamepata maneno haya? Jawabu yake ni hii wao huyapata ima kwa Jibril malaika mkubwa kuliko malaika wote wa Mwenyezi Mungu.
QU-RAN 53:2-6 SURATUL NAJM (NYOTA)
2. Kwamba mtu wenu huyu Nabii Muhamad (hakupotea Kwa ujinga) na wala hakukosa (na hali ya kuwa anajua) 3. Wala hasemi Kwa matamanio (ya nafsi yake) 4. Hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake) 5. Amemfundisha (malaika) mwenye nguvu Sana 6. Mwenye uweza na yeye (huyu jibril) akalingana sawa sawa.

Waislamu kwa kusoma aya hizi, wanaamini Malaika Gabriel ndiye jibril lakini aya hizi zinaonyesha tofauti kwani malaika Jibrili alipelekwa na Allah aende kwa Mariamu ambaye alikua msikitini na Quran haikutaja mji wala nchi aliyoenda jibril, lakini tunaona Biblia inafundisha kuwa, malaika Gabriel aliingia nyumbani kwa Mariamu na tena biblia inatufundisha kuwa ufunuo wa unabii uliletwa kwa muongozo wa Roho Mtakatifu (2 Petro 1:20-21) na wala si malaika jibril kama Qurani inavyosimulia.
JE, MALAIKA NI VIUMBE WA NAMNA GANI?
WAEBRANIA 1:13-14.
13. Je, yuko malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapo waweka adui zako chini ya nyayo zako? 14. Je, hao wote si “roho”watumikao walitumwa kuwahudumu wale watakao urithi wokovu?
Ni wazi tunaona kuwa malaika ni vyumbe ambao ni nafsi ya roho ambao wanauwezo wa kuwajia watu kwa umbo la wanadamu eg (Mwanzo 18:1-19:12) kama tunavyoona walipomwendea Ibrahim na lutu.Malaika alimwendea Musa katika sura ya kijiti kinacho waka bila kuteketea (kutoka 3:1-5)
JE, MALAIKA WOTE NI WEMA NA HAWAMKOSEI MUNGU?
Tukisoma Quran tunaona Allah mungu anayeabudiwa na waislamu anasimulia malaika kuwa ni viumbe wenye sifa hii.
QURANI 16:93 SURATUL AL-NAHL (NYUKI)
Na Mwenyezi Mungu angalitaka kwa yakini angalikufanyeni “kundi moja tu” (mnamtii nyote kama alivyowafanya “malaika” lakini kakuachieni mfanye mtakavyo) lakini anamuachia kupotea anayemtaka na anamuongoa anayemtaka na hakika mtaulizwa kwa yale mliokuwa mkifanya.
QUR-AN 32:13 SURAT AS-SAJDAH (KUSUJUDU)
Na tungalitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (Kwa lazima Kama tulivyowapa malaika…..
UFAFANUZI WA AYA YA 13 ULIO NDANI YA QUR-AN NI HUU…
Angetaka mwenyezi Mungu angemuumba Binadamu Kama malaika hawezi kufanya mabaya, maumbile yake ni kufanya mema tu; kwa hiyo halipwi kwa mema yake hayo kwani hayaonei taabu katika kufanya. Lakini binadamu ameumbwa Kwa uweza wa yote mawili sawasawa na raha yake zaidi ni kufanya mabaya.
Kadiri ya aya hizi Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu anasema kuwa malaika ni wema na hawawezi kufanya mabaya na wako kundi moja tu na wote wanamtii Allah. Lakini tukirejea kwa Biblia tunaona Mungu wetu Jehovah amefunulia mitume wake kuwa malaika wako hivi…
2PETERO 2:4
Kwa maana Mungu hakuwaachia “malaika waliokosa” bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza walindwe hata ije siku ya hukumu.
Hao malaika waliokosa wapo chini ya ibilisi, mbali na hao waliokosa lakini pia wapo malaika wa namna hii…
MATHAYO 25:31
Hapo atakapokuja mwana wa adamu, katika utukufu wake na malaika watakatifu wote pamoja naye; ndipo atakapo keti katika kiti cha utukufu wake.
Kadri ya aya hizi tunaona wazi wazi kuwa Mungu wetu anafundisha makundi mawili ya malaika, wema (yaani Watakatifu) na wabaya (yaani waliokosa) Fundisho ambalo Allah halielezei kwani yeye Allah anasema malaika ni wema tu hawawezi kufanya mabaya “hali hii inatufundisha kuwa Allah siyo Yehova”.
MAANA YA NENO GABRIEL
Neno au jina “Gabriel” asili yake ni lugha ya kiebrania na maana ni “Mjumbe wa Mungu” katika Biblia jina hili Gabriel limetajwa mara “nne” (4) (Tazama Danieli 8:16 na 9:21, Luka 1:19 na 1:26) kuhusu malaika Gabriel mara nyingi Biblia inaonyesha kuwa Mungu anamtuma ili alete habari njema zinazohusu wokovu wa wanadamu na hutoa maneno ya kuwafariji wale aliowatokea akisema “usiogope”katika Biblia limetajwa mara (366) aidha tunaposoma Biblia tunaona pia malaika huyu anaitwa malaika wa Bwana (The angel of the Lord) Neno hili katika biblia limetajwa mara (65) katika aya zipatazo (61) iwapo sehemu hizo zote zinahusika na malaika Gabriel basi malaika huyo atakuwa ametajwa mara nyingi.
NAMNA YA KUJUA TOFAUTI YA MALAIKA GABRIEL NA JIBRIL
1 TIMOTHEO 4:1
Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani WAKISIKILIZA roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.
(Tazama pia Mathayo 7:15-20)
1YOHANA 4:1, 3, 15
1. Wapenzi msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; Kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani 3. Na “kila roho isiyomkiri Yesu” haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmeisikia kwamba yaja, na sasa imekwisha kuwako duniani 15. Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake naye ndani ya Mungu.
Jambo la muhimu ni la kujaribu kati ya jibril na Gabriel ni nani aliye mkiri Yesu kuwa ni Mwana wa MUNGU endapo fundisho lao ni moja basi pia watakuwa siyo malaika wawili bali mmoja- wakitofautiana itakuwa siyo mmoja bali ni malaika wawili walio tofauti kabisa..
JE, CHEO CHA MALAIKA GABRIEL NI SAWA NA JIBRIL?
MALAIKA GABRIEL ALIYETUMWA NA MUNGU YEHOVA ANASEMA HIVI…
Malaika akajibu akamwambia Mimi ni Gabriel, nisimamaye mbele za Mungu, nimetumwa niseme nawe na kukupasha habari hizi njema (Tazama Luka 1:19)
Kwa mujibu wa ayah ii malaika Gabriel anaeleza kuwa husimama mbele za Mungu hivyo ni wazi kuwa cheo chake ni mjumbe asimamaye mbele ya Mungu. Je, malaika jibril anayetumwa na mungu aitwaye Allah cheo chake ni hiki hiki cha Gabrieli?
QURAN 81:19-21 SURATUL AT-TAKWIR (JUA LITAKAPO KUNJWA KUNJWA)
19. Kwa hakika hii (Qurani) ni kauli aliyo kuja nayo mjumbe mtukufu (jibril) 20. Mwenye nguvu, mwenye cheo cha heshima kwa Mwenyezi Mungu 21. Anayeitiiwa huko (mbinguni na malaika wenziwe) kasha mwaminifu.
UFAFANUZI WA AYA YA 19-21 ULIO NDANI YA QUR-AN NI HUU…
Mjumbe mtukufu na mwenye kutiiwa huko mbinguni ni “jibril” ambaye ndiye “mkubwa wa malaika wote.”
JE, MALAIKA MKUU WA YEHOVA NI NANI?
YUDA 1:9 “Lakini Mikael malaika “mkuu” aliposhindana na Ibilisi….. Katika ayah ii tunaona Mungu wetu tunayemwabudu wakristo aitwae Yehova malaika wake mkuu ni Mikaeli na Mungu anayeabudiwa na waislamu aitwaye Allah malaika wake mkuu ni Jibril. Hivyo Jibril siyo Gabriel. Tukirejea kwa malaika mkuu “Michael” hili ni jina lenye asili ya lugha ya “kiebrania” na maana yake ni “Nani sawa na Mungu” hii kwa sababu ndiye aliyewaongoza malaika wenziwe kumpiga shetani na kumtoa kule mbinguni pale alipojikweza na kutaka kufanana na Mungu (Tazama Ufunuo 12:7-12 na Danieli 10:13,21na12:2)
MAFUNDISHO YAO KUHUSU UWANA WA MUNGU
(A)MALAIKA GABRIEL WA MUNGU YEHOVA ALIFUNDISHA HIVI..
LUKA 1:26-35 Nanukuu aya ya 35 tu
Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu “Mwana wa Mungu”
(B)MALAIKA JIBRIL WA MUNGU AITWAYE ALLAH ANASEMA HIVI…
QURAN 18:4-5 SURATUL AL-KAHF (PANGO)
4. Na kiwaonye wale wanaosema “mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto 5. Wala hawana ilimu juu ya (jambo) hili wala Baba zao (hawana ujuzi juu ya jambo hili ila wanajisemea tu) Ni neno kubwa hilo litokalo katika vinywa vyao hawasemi ila uwongo tu
Maneno haya aliyafundisha malaika jibril (QURAN 53:5-6) ni ya kumkufuru Mungu wetu Yehova (Tazama kutoka 4:22) Mungu anasema “Israeli ni Mwanangu Mimi” na malaika wake Gabriel, alifundisha uwana wa Mungu.
MAFUNDISHO YAO KUHUSU ROHO MTAKATIFU
LUKA 1:34-35 “Malaika Gabriel anamwambia Mariam hivi…
34. Mariam akamwambia malaika litakuaje neno hili maana sijui mume? 35. Malaika akajibu akamwambia Roho mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli- Roho Mtakatifu ni Mungu (Matendo 5:3-4) Na wala siyo malaika ndio maana malaika alisema atakujilia.
QUR-AN 16:102 SURATUL AL-NAHL (NYUKI)
Sema Roho Takatifu yaani jibril ameiteremsha kutoka kwa mola wako kwa haki ili kuwathubutisha wale walio amini…
QUR-AN 2:87 SURATUL AL-BAQARAH (NG’OMBE)
Na hakika tulimpa Musa kitabu na tukawafundisha mitume (wengine) Baada yake na tukampa Isa mwana wa Mariam hoja zilizo waziwazi na tukamtia nguvu kwa roho mtakatifu (jibril)
UFAFANUZI WA AYA YA 87 ULIO NDANI YA QURAN NI HUU
Kwa waislamu Roho mtakatifu ni “Malaika Jibril” si Yule wanaodai wakristo kuwa ni mmoja wa asili ya utatu (Trinity). Hapa tunaona malaika Gabriel hasemi kuwa yeye ndiye Roho Mtakatifu mahala popote lakini Jibril anasema eti, ndiye roho mtakatifu- hivyo Gabriel siyo Jibril.
JE, MALAIKA JIBRIL ALIPELEKA UTUME KWA WAYAHUDI?
QUR-AN 2:97 SURATUL AL-BAQARAH (NG’OMBE)
Sema anayemfanyia ushinde jibril kwa kuwa ndiye aliyemletea utume nabii Muhammad (asiwapelekee wayahudi) (ni bure hana kosa Jibril) hakika yeye aliteremsha Quran moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
UFAFANUZI WA AYA YA 97 ULIO NDANI YA QUR-AN NI HUU...
“Mayahudi katika hila zao za kumkataa mtume Muhammad walimwuliza “malaika gani anayekuletea wahyi? Mtume akasema “Jibril” wakasema “Lo! HUYO NI ADUI YETU, HATUMTAKI lau kuwa malaika mwingine ndiye anayekuletea wahyi (yaani ufunuo) tungekufuata. Jibrili hajapeleka utume Kwa wayahudi; Isitoshe malaika huyo Jibril anafundisha kuhusu wayahudi hivi….
QUR-AN 5:82 SURATUL AL-MAIDAH. (MEZA YA CHAKULA)
“Hakika utawakuta walio “maadui” zaidi kuliko watu (wengine) kwa waislam ni “mayahudi” Na wale mushirikina.”
Hapa tunaona Jibril anawafundisha waislamu kuwa maadui zao zaidi ni wayahudi. Kuwa adui wa wayahudi ni kuwa adui wa wokovu kwani Bwana Yesu anatufundisha hivi...
YOHANA 4:19-22 Nanukuu aya ya 22 tu
Ninyi mnaabudu msicho kijua, sisi tunaabudu tukijuacho kwa kuwa, “wokovu watoka kwa wayahudi.”
Isitoshe manabii wote ni wayahudi kutoka kwa Musa, Daudi, Isaya, Ezekieli, Daniel, Hosea, Mika, Malaki, Yohana mbatizaji na hata Yesu.
JE, NAMNA MALAIKA GABRIEL ANAVYOTOKEA WATU NI SAWA NA JIBRIL?
(A)JIBRIL
QUR-AN 19:16-26
16. Na mtaje Mariam kitabuni (humu) alipojitenga na jamaa zake (akenda) mahali upande wa (mashariki wa msikiti) 17. Na akaweka pazia kujikinga Nao. Tukampelekea muhuisha sharia yetu (jibril) - akajimithilisha kwake (Kwa sura ya) binadamu aliye kamili 18. (Mariamu) akasema hakika Mimi najikinga kwa (Mwenyezi Mungu) mwingi wa rehema aniepushe nawe. Ikiwa unamuogopa Mungu (basi ondoka nenda zako) 19. (Malaika) akasema hakika mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu 20. Akasema nitawezaje kupata motto, hali hajanigusa mwanamume (yeyote Kwa njia ya halali) wala mimi si (mwanamke) mwenye kuzini 21. (Malaika) akasema ni kama hivyo( unavyosema lakini mola wako amesema haya ni sahali kwangu ili tumfanye muujiza kwa wanadamu na rehema itokayo kwetu (ndio tumefanya hivi) na hili ni jambo lililokwisha kuhukumiwa 22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali 23. Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende (akawa anazaa na huku) anasema,”laiti ningekufa kabla ya haya ningekua niliye sahaulika kabisa 24. Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia) “ usihuzunike hakika mola wako amejalia (ameweka) kijito cha maji chini yako 25. Na litikise kwako shina la mtende litakuangushia tende nzuri zilizo mbivu 26. Basi ule na unywe na litue jicho lako.
JINSI JIBRIL ALIVYOFANYA ALIPOMTOKEA MUHAMMAD NI HIVI…
Hata siku moja- katika mwezi wa Ramadan mwezi 17 jumatatu katika mwaka wa 40 unusu wa umri wake- Mtume alimuona mtu kasimama mbele yake bila kumwona wapi katokea, akamwambia,”soma” mtume akamjibu “Mimi sijui kusoma “kwani sijapata kujifundisha kusoma –“Akaja akamkamata” akambana,akamwambia tena “soma” Mtume akamjibu jawabu yake ile ile.Hata mara ya tatu akamwambia tena “soma –igraa Bismi rabbik” akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake kasha mtume akaisoma kama alivyosomewa.Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika kurani. Ingawa haijawekwa mwanzo. Mara Yule mtu (malaika) akaondoka machoni mwake-asimuone kenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake-khofu ikamshika. Alipofika nyumbani bibi Khadija alidhani ana homa, akamfunika manguo gupi gupi na akakaa mbele yake akamsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia alimweleza Bibi Khadija yote yaliyomtokea na Bibi Khadija akamtuliza moyo.Akamyakinisha ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu akaondoka akenda kwa jamaa yake-Bwana Waraga Bin Naufal-akampa habari yote iliyompata mumewe; naye akamwambie amwite, na mtume akenda akamweleza habari yake yote. Bwana Waraga akamwambia “huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa... Basi jibashirie kuwa wewe ni Mtume wa umma huu. Nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako inshallah nitakuwa mkono wako wa kulia wakarejea kwao na hofu yote imemtoka.
Habari hii inapatikana katika kitabu cha maisha ya Nabii Muhammad (S.a.W) mtungaji ni Sheikh Abdulla Saleh Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar baadaye akawa Kadhi Mkuu wa Kenya, katika ukurasa wa 16-17
(B)MALAIKA GABRIEL ALIVYOWATOKEA WATU ALIFANYA HIVI…
LUKA 1:19 Alijitambulisha Kwa kusema, “Mimi ni Gabriel.”
DANIEL 8:15-16 Au muhusika ambaye alimtokea hujulishwa kwanza
DANIEL 8:17-21
LUKA 1:13, 30…
Gabriel anamsadia mtu pale anapopatwa na hofu na anasema usiogope. Tabia za malaika Gabriel ni huruma na kumfahamisha mtu kwa upole, lakini malaika Jibril wa Allah yeye hukamata, kumbana mtu, jambo lililompelekea Muhammad apate homa. Swali je, huyo jibril ni Nani?
JE, ALLAH MUNGU WA WAISLAMU ANAWATUMA VIUMBE GANI?
QUR-AN 19:83 SURATUL MARYAMU.
Je, huoni yakwamba tumewatuma mashetani juu ya makafiri wanaowachochea (kufanya mabaya) “Na namna hii tumemfanyia kila Nabii maadui (Nao ni) mashetani katika watu na (mashetani katika) majini. Baadhi yao wanawafunulia wenzi wao maneno ya kupambapamba ili kuwadanganya. (QUR. 6:112 suratul Al-An’am)
SHETANI ANA UWEZO WA KUJIGEUZA AWE MFANO HUU… 2 WAKORINTHO 11:10-15, NA NUKUU AYA YA 14 TU “Wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa Malaika wa nuru.”
“Kila akiriye kuwa Yesu Ni Mwana WA Mungu, Mungu hukaa ndani yake, tena roho ya kukiri hivyo imetoka kwa Mungu (1 Yoh 4:1-3, 15). Malaika Gabriel amekiri kuwa Yesu Ni mwana WA Mungu, Jibril hakukiri hivyo “Luka 1:35” (Qur. 9:30). Je, Jibril ni nani?
NINI MWISHO WA VIUMBE HIVYO ANAVYOVITUMA ALLAH
Allah hutuma mashetani, maandiko matakatifu ya Biblia yanatufundisha mwisho wa viumbe hao hivi;
MATHAYO 25:41 “Bwana Yesu atawaamuru hivi…
Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, ondokeni kwangu mliolaaniwa; mwende, katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.
Ndugu mpendwa ni matumaini yangu katika BWANA WETU YESU KRISTO kuwa umeweza kujua wazi wazi kuwa Malaika Gabriel wa Mungu wetu Yehova siyo malaika Jibril wa mungu aitwaye Allah anayeabudiwa na waislamu BWANA akubariki Sana ueneze ujumbe huu kwa watu wa mataifa ili wamgeukie Bwana Yesu wapate kuokolewa.
Amina!
By permission Max Shimba Ministries Org

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW