Wednesday, February 24, 2016

MAJINA KUMI NA MBILI YA ROHO MTAKATIFU

 
Katika kijarida hiki, tutajikumbusha majina kumi na mbili ya Roho Mtakatifu na kazi zake.

Haya ungana nami moja kwa moja na tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anamajina mengi na wasifa mwingi, mengi yao kama sio yote yanaeleza kazi na huduma yake. Hapa chini ni baadhi ya majina na wasifa wake kama yalivyo semwa katika Biblia kuhusu Roho Mtakatifu.

1.   MWANDISHI WA NENO (Author of Scripture)
2 Petro 1:21; 2 Timotheo 3:16. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 
Roho Mtakatifu ndie aliye weka pumzi katika vitabu vyote vya Biblia 66. Hivyo basi, waandishi wa Biblia walipewa nguvu/upako na Roho Mtakatifu na wakaandika Biblia bila ya makosa.

2.   MSAIDIZI/WAKILI/MSHAURI WETU (Comforter / Counselor / Advocate)
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.
Isaya 11:2; Yohana 14:16, 15:26; 16:7.
Maneno yote matatu yanatokana na neon la Kigiriki Parakletos, amabalo linatupa Paraclete. Jina linguine la Roho. Yesu alipo ondoka duniani, Wafuasi wake walijisikia vibaya sana kwasababu awalikosa mfariji. LAKINI Yesu aliwapa ahadi ya Roho ambaye atawafariji, Washauri, Wawakilisha na kuwa Msaidizi wao wale ambao wapo katika Kristo. Roho Mtakatifu vile vile yeye Ushuhudia roho zetu kuwa sisi ni watoto wa Mungu na utuhakikishia wokovu wetu.
KUMBE BASI, ROHO MTAKATIFU akama aya zinavyo sema atakuwa nasi MILELE.


3.   MHAKIKISHI WA DHAMBI (Convictor of Sin)
Yohana 16: 7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 
8 
Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 
10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 
11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. 
Roho Mtakatifu yeye ndio anakuonyesha au kufunulia UKWELI kuhusu Mungu katika akili zetu na roho zetu. Ukweli huu ndio utatuhumu kwa kuwa tutafahamu kuwa sisi ni watenda dhambi na hatuto weza pinga huo ukweli. Hufanya hivi kwa kuweka hatiani Moyo wako kwamba sisi ni watenda dhambi mbele ya Mungu Baba, na kwamba tunahitaji haki yake (righteousness) na kwamba kwahakika siku moja hukumu itakuja kwa watu wote. Wale ambao wanapinga ukweli huu, basi wanapinga ukweli wa Roho Mtakatifu.

        4. AMANA/MHURI/BIDII (Deposit / Seal / Earnest)
2 Wakorintho 1:22; 5:5; Waefeso 1:13-14. Roho Mtakatifu ni Mhuri kwa watu wa Mungu. Yeye hutujali sisi kama watoto wake. Zawadi ya Roho Mtakatifu ni kama malipo ya amana kwetu sisi kwa urithi wa mbinguni, ambao Kristo alituahidi baada ya kazi ya pale Msalabani. Ni kwasababu ya Roho Mtakati ambaye ameweka Mhuri kwetu ndio maana tuna uhakika wa Wokovu. Hakuna mwenye uwezo wa kuvunja hii “SEAL” ya Mungu.

5.   KIONGOZI (Guide)
Yohana 16:13. Kama ambavyo Roho alivyo waongoza waandishi wa Biblia katika kweli yote, vivyo hivyo ametuahidi kutuongoza wote tuaminio katika Kristo. Ukweli kuhusu Mungu ni jambao la mzaha kwa watu wa dunia na Makafiri, kwasababu hawana macho ya rohoni na hawamweli Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 2:14)  Wale walio katika Kristo ndani yao wana Roho Mtakatifu ambaye anatuongoza katika yote tunayo hitaji. Wale ambao hawana Roho Mtakati wao ni kama yatima, maana hawana kiongozi na hawata weza elewa maneno ya Mungu, wao baba yao ni Yule muovu, IBILISI.

6.   ANAMAKAZI NDANI YA WAAMINIO (Indweller of Believers)
Warumi 8:9-11; Waefeso 2:21-22; 1 Wakorintho 6:19) Roho Mtakatifu anaishi katika mioyo ya waaminio/watu wa Mungu, na huku kuishi ndani ya kila mtu kwa wakati mmoja (omnipresence) ni sifa mojawapo pekee ya Mungu. Akiwa ndani ya Waaminio, huwaongoza, huwafundisha, kuwafariji, na ni mshawishi na zaidi ya hapo huzalisha matunda ya Roho (Wagalatia 5:22-23) Hutoa uhusiano wa karibu kati ya Mungu na Watoto wake “Intimate connection” Wakristo wote walio okoka wana Roho Mtakatifu ndani yao/katika mioyo yao.


     7. MWOMBEZI (Intercessor)
Warumi 8:26 Kazi na au huduma moja ya muhimu sana ya Roho Mtakatifu kwa walio kombolewa na damu ya Yesu ni kuwaombea “interceding”
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

    8. MFUNUAJI/ROHO WA KWELI (
Revealer / Spirit of Truth)
Yohana 14:17; 16:13; 1 Wakorintho 2:12-16.
Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 
17 
ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 
Roho Mtakati yeye ndie anatufunulia yote ambayo Yesu aliyafanya na yote ambayo Yesu anataka tuyaelewa. Ndio maana watu ambao hawa Roho Mtakatifu wao huona mambo tunayo funiliwa si ya maana.

1 Wakorintho Mlango wa 2 :12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. 
13 
Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. 
14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. 
15 Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. 
16 Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

.         9. ROHO YA MUNGU/BWANA/KRISTO (Spirit of God / the Lord / Christ)
Mathayo 3:16; 2 Wakorintho 3:17; 1 Petro 1:11 Katika vitabu hivyo tunahakikishiwa kuwa Hakika Roho Wa Mungu ni sehemu ya Utatu na Hakika yeye Ni Mungu kama alivyo Mungu Baba na Mungu Mwana. Alisemwa kwa mara ya kwanza wakati wa uumbaji, ikifuatiwa na Yesu ambaye aliumba kila kitu. Yohana 1:1-3. Tunaona Utatu huohuo katika Yesu wakati alipo kuwa anabatizwa, wakati Roho alipo shuka na tukasikia sauti ya Mungu Baba.

   10. ROHO YA UZIMA (Spirit of Life)
Warumi 8:2 Neno Roho ya Uzima maana yake kuwa ni Roho Mtakatifu ambaye anatupa na au umba UZIMA, haimaanishi kuwa anasaidia wewe kuoka, bali anakufanya wewe kuwa umeokoka. Bila ya Roho Mtakatifu hakuna wokovu. HAPA VILE VILE tunaona Utatu katika Kazi ya Mungu. Tumeokolewa na Mungu Baba kupitia kazi ya Mwana wake Yesu, na wokovu unaedelezwa “sustained” na Roho Mtakatifu.

11.MWALIMU (Teacher)
Yohana 14:16; 1 Wakorintho 2:13.  Yesu aliahidi kuwa Roho atawafundisha kila kitu na kuwakumbusha yote ambayo aliwafundisha wakati alipo kuwa nao. Waandishi wa Agano Jipya waliongozwa na Roho Mtakatifu ndio maana walikumbuka kila kitu ambacho Yesu alisema na kufanya.
Yohana 14: 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 

12.SHAHIDI (Witness)
Warumi 8:16; Waebrania 2:4; 10:15 Roho anaitwa SHAHIDI kwasababu YEYE anatuhakikishia na kutushuhudia kuwa sisi ni watoto wa Mungu, na kwamba Yesu na Wanafunzi wake walitumwa na Mungu Baba na kuwa Biblia ni Neno la Mungu. Zaidi ya hapo, Roho hutupa Zawadi ya Roho Mtakatifu, na utushuhudia sisi na dunia kuwa sisi tulio okolewa na Damu ya Yesu ni watoto wa Mungu.
Warumi Mlango wa 8:16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 
17 
na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. 

Nakushauri uendelee kumwomba Mungu aliki aendelee kukufulia mambo makuu kupitia Roho Mtakatifu. Kumbu, bila ya Roho Mtakatifu, Wokovu wetu unakuwa wa mashaka. Ndio maana lazima tumfahamu huyu Roho Mtakatifu aliye ahidiwa kuja na Bwana wetu Yesu Kristo aliye kufa kwa ajili ya dhambi zetu.

Basi mpendwa, Mungu aendelee kukubariki.

Ni mimi, Mtumishi wake Max Shimba.

Katika huduma yake

Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW