Sunday, February 28, 2016

KWANINI MASHAHIDI WA YEHOVA WANAPOTOSHA KWA MAKUSUDI KUHUSU UUNGU WA YESU?

Mashahid wa Yehova wanadai kuwa:
1. Yesu alikuwa Malaika aliyeumbwa.
2. Yesu hakuwa Mungu na mwanadamu wakati ule – “God incarnate”.
Mashahidi wa Yehova wanasema kuwa Yesu hakuchanganya au kushiriki tabia za kiungu na za kimwili alipokuwa duniani. Wanadai alipokuwa duniani alikuwa mwanadamu mkamilifu tu, ikimaanisha, hakuwa na adhama ya Uungu. Na tangu kufufuliwa, yeye ni nafsi kamili ya kiroho tu.
3. Yesu alishindwa kuwakomboa wanadamu.
4. Mwili wa Yesu haukufufuliwa.
5. Mwanadamu Yesu amekufa kwa hiyo haishi tena.
6. Kabla ya kufa Yesu alikuwa mwanadamu tu, bali baada ya kufufuliwa alikuwa na hali ya kiungu (malaika).
7. Yesu si mpatanishi wetu.
Je, madai ya hawa Mashahidi wa Yehova ni ya kweli?

LAKINI BIBLIA INATUFUNDISHA NINI KUHUSU YESU?
Biblia inakataa na kuvunja hoja zote dhaifu za Mashahidi wa Yehova kama ifuatavyo:
1. Yesu si malaika kama wanavyo dai hawa Mashahidi wa Yehova. Soma-Waebrania 1:1-8. Yeye ni bora. Pia soma Yohana 1:1-3; 8:58; Ufunuo 1:8; 21:6; 22:13 – Yesu hakuumbwa bali yeye mwenyewe ni mwumbaji aliye wa milele.
WAEBRANIA MLANGO WA 1: 1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; 4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao. 5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana? 6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu. 7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto. 8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio. 10 Na tena, Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako; 11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo,
1. Aya ya 2: Inakiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu.
2. Aya ya 3: Inakiri kuwa Yesu alimaliza deni la dhambi na yupo upande wa Kuume wa Ukuu huko juu.
3. Aya ya 4: Yesu ni Mmbora kupita mailaka, hivyo basi hawezi kuwa ni Malaika Mikaeli kama wanvyo dai Mashahdi wa Yehova.
4. Aya ya 5: Mungu Baba anakataa kuita Malaika Mwanae.
5. Aya ya 6: Malaika wote wanamsujudia Yesu, pamoja na Mikaeli na Gabrieli.
6. Aya ya 7: Inakiri kuwa Yesu ndie aliye umba Malaika.
7. Aya ya 8: Yesu ndie mwenye Kiti cha Enzi, zaidi ya hapo Yesu anaitwa Mungu na Baba yake.
8. Aya ya 9: Yesu kwa mara nyingine tena anaitwa Mungu na Baba yake.
9. Aya ya 10: Yesu anaitwa Bwana na kukiri kuwa yeye ndie aliye weka Misingi ya Nchi na Mbingu. Ni kazi ya mikono ya Yesu.
10. Aya ya 11: Yesu ni wa milele.
2. Isaya alitabiri kwamba Mungu angeishi kimwili-Isaya 7:14; Mathayo 1:23. Mariamu pia alikuwa na mimba kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu, mwili wa Yesu alitoka kwa Mariamu lakini Roho kwa Mungu. Kwa hiyo Yesu alikuwa asili zote mbili--kimwili na kiroho, Mathayo 1:18-20. Katika Filipi 2:6-7 tunaona kwamba Yesu alifanyiwa kuwa mfano wa Mwanadamu, Filipi 2:6-7; Waebrania 2:16. Pia tunaweza kusoma katika Ynoha 1:1-2, 14; 16:28; 1 Timotheo 3:16. Pia tunaweza kumwona Petro alikiri katika Mathayo 16:18, Yesu ni nani? Na kama kuna mtu ambaye anatufundisha ya kuwa Yesu hatokani na Mungu, mwambie asome 1 Yohana 4:3 na 2 Yohana 7.
Isaya Mlango 7: 14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Aya inakiri kuwa Yesu ni Imanueli.
3. Mashahidi wa Yehova wanasema Yesu si mkombozi wetu. Tusome Yohana. 1:29; Mathayo. 10:28; Rum. 5:11; Waebrania 10:3-14.
Yohana 1: 29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
Sasa Je, Nani ni mwongo hapa, Mungu au Mashahidi?
4. Wanadai mwili wa Yesu haukufufuliwa. Yesu alisema kwamba atafufuka, Yohana 2:19-22 [Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha] na pia alionyesha mwili wake (uliofufuliwa) kwa Tomaso, Yohana 20:24-28.
5. Wanadai mwanadamu Kristo alikufa asiwe hai tena. Lakini Biblia inasema katika Zaburi 16:10, hapa Daudi alitabiriwa kuwa Yesu atafufuka. Na Petro alidai kwamba Kristo alifufuka, Matendo ya Mitume 2:30-31, wakati alipokuwa anahubiri siku ya Pentikoste alikuwa anaongozwa na Roho Mtakatifu. Na katika Matendo ya Mitume 1:1-3, Yesu alithilibitisha sana kwamba alikuwa hai.
6. Pia Mashahidi wanadai Yesu hakuwa na hali ya kimungu isipokuwa baada ya kufufuliwa. Katika Yoh.
1:1-3; 17:5 tunaona Yesu alikuwa Mungu tangu mwanzo. Katika Flp. 2:6, Yesu alikuwa sawa na Mungu, na Kristo na Mungu ni kitu kimoja, Yohana. 14:11; 17:21.
Kwa hiyo wanasema kuwa Kristo aliyekufa na yule aliyefufuliwa sio mtu yule yule, wale ni watu wawili tofauti. Lakini Biblia inasema ni yule yule kabla ya kufufuka na baada ya kufufuliwa, Matendo ya Mitume 1:11; Waefeso. 4:10; Waebrania 10:12.
7. Mwisho wanadai Yesu siye mpatanishi wetu. Tusoma gazeti lao, “Watch Tower” Toleo 15/9/1909, uk. 283. “Katika toleo lao la 1906, ukarasa wa 26, walisema, ‘Bwana wetu Yesu, kati ya Baba na nyumba ya waaminio, katika kipindi cha Injili.’ Usemi huu si kweli. Hakuna maandishi yanayosema hivyo. Ni sehemu ya mwisho ya kipindi cha giza, ambao tunafurahi kuufuta kutoka machaoni mwetu.”
Mashahidi ni waalimu gani? Wanaobadili mafundisho yao? Nani anaweza kuamini wameongozwa na Mungu ikiwa wanasema wenyewe kuwa wamekosa katika kufundisha kwao? Lakini, ukweli ni kwamba Yesu ndiye mpatanishi wetu, 1 Timotheo 2:5; Waebrania. 9:15; 1 Yohana 2:1.
YESU NI MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Tito 2:13
….tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Yesu Kristo ni Mungu Mkuu!!
Shida KUU ya Mashahidi wa Yehova ni hii: Wanampima Mungu kwa vigezo vya kibinadamu. Mungu anasema: Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? (Yeremia 32:27)
Jibu liko wazo. HAKUNA!
Hebu tusome Wafilipi 2: 5-11 INASEMA:
5 Tuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu. 6 Yeye ingawa alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho, 7 bali alijifanya si kitu, akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la mwanadamu. 8 Naye akiwa na umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba! 9 Kwa hiyo, Mungu alimtukuza sana na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, 10ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, vya duniani na vya chini ya nchi 11 na kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
NENO la "Kuwa sawa na Mungu" kwa Kigiriki ni MORPHE-: Iikimaanisha Yesu alikuwa na adhama zote za Kimungu na Mungu. Hivyo basi katika ushaidi huu wa katika kitabu cha Wafilipi tunasoma kuwa Yesu hakuwa mtu wa kawaida bali alikuwa ni Mungu pamoja nasi yaani Imanueli.
Ni maombi yangu Mungu ayafungue macho ya Mashahidi wa Yehova kwa ukweli wa injili na mafundisho ya kweli ya neno la Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW