Friday, February 5, 2016

JE BIBLIA IMETIWA MIKONO (CHAKACHULIWA)?

Neno Biblia ni neno lenye asili ya Lugha ya kiyunani nao huita “Biblos” neno hili linapotamkwa humaanisha “Maktaba” au Mjumuiko, Mkusanyiko wa vitabu”.

Biblia ni kitabu kilicho andikwa na waandishi wasio pungua “arobaini”ambao walikuwa sehemu na mahala tofauti lakini kwa uongozi wa Roho Mtakatifu waliweza kuandika maneno yaliyowiana.

Matendo 11;19wanafunzi wa Yesu walitawanyika baada ya ile dhiki

1Petro 1:20 walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Isaya 34:16 tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome.

Pamoja na hayo siku hizi za karibuni kumeibuka vikundi mbalimbali vinavyoendesha mikutano,inayojulikana kwa jina la “mihadhara” vikundi hivyo vimeibua mafundisho yasiyo sahihi kwa kudai kuwa Biblia imetiwa mkono na si kitabu cha kweli, hivyo kupitia uchambuzi huu tutaangalia mada mbalimbali kwa kuanza na mada hii tete juu ya ukweli wa Biblia, ambapo vitabu vyote yaani Biblia na Qur an vitasaidia kutoa ufumbuzi.


VIGEZO VYAO VYA KUDAI KUWA BIBLIA SI YA KWELI
Yeremia 8:8-9 inasema kuwa “kalamu ya waandishi imeifanya kuwa uongo.”

Jibu kwa kifupi

Katika kujibu swali hili, ni muhimu kuanza kwa kuangalia makosa ya kiusomaji yaliyofanywa na wajenga hoja wa mada hii. Kwa kutolichunguza kwa makini andiko hilo ili kuelewa muktadha wake, hebu tuchunguze….!

Yeremia 8:8
Mwasemaje sisi tuna akili na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini tazama kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

JIBU LA KWANZA
Katika aya hiyo, yako mambo ya kimsingi ambayo kamwe wajenga hoja hawayazingatii jambo la kwanza. Nabii Yeremia anasema “Torati ya Bwana tunayo pamoja nasi” hivyo kabla ya kujenga swali lolote ingepaswa kujulikana kwamba Torati haikuwa kwingine bali ilikuwa mikononi mwa manabii, hivyo ilikuwa salama.

JIBU LA PILI
Sehemu ya pili, ni pale andiko linaposema “lakini tazama” kauli hii uhashiria kuwepo kwa upande wa pili wa watu au kundi lililo anzisha jitihada nyingine pinzani mbali, pindi Torati ikiwa imehifadhiwa na manabii ambapo jitihada hizo zililenga kuikosoa Torati ambayo ilihifadhiwa na kutunzwa na manabii.

JIBU LA TATU
Na sehemu ya mwisho ni ile kauli inayosema kalamu ya uongo ya waandishi “imeifanya kuwa uongo” kauli hii kamwe hailengi kuonyesha kuwa kulifanyika tendo la kuivuruga au kuibadilisha torati yenyewe la hasha” hapo limetumika neno “imeifanya” kuwa uongo, hii inamaana kuwa torati yenyewe ni ya kweli lakini wao walianzisha jitihada zao za kuikosoa …….

MIFANO HAI
Chukulia mfano mtu akikwambia “wewe unanifanya mimi kuwa mjinga? Je- tayari umekuwa mjinga? Jibu – hapana”. Isipokuwa yeye anafanya mambo Fulani ili kufanya uonekane hivyo na hali sivyo ulivyo.

Je waandishi waliifanyaje Torati kuwa uongo na kwa namna gani?

Kwa kadri ya msingi wa maandiko ya Biblia tendo la kuifanya torati kuwa uongo huhashiria “kutamka” au “kuandika maneno yanayo pingana na torati ya Bwana”.

Biblia inaonyesha kuwa kulikuwa na watu waliojaribu kutunga na kuweka sheria zao zilionekana zikipingana na zile halali za Mungu Yehova, hivyo huko ndiko kuifanya torati au sheria halali ya Mungu kuwa uongo na si badala yake kuiharibu sheria yenyewe ya Mungu kwenye kitabu husika, fuatilia ushahidi ufuatao:-

Isaya 10:1 Ole wao wawekao amri zisizo haki na waandishi waandikaoManeno ya ushupavu ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake………

Yohana 19:5 Wayahudi wakajibu sisi tunayo sheria na kwa sheria hiyo amestahili kufa kwakuwa alijifanya mwana wa Mungu.
Maandiko hayo yanonyesha vile ambavyo wanadamu nao walivyokuwa na jitihada za upande wao wa kuasisi sheria na taratibu zao ambazo kwa kadri ya maandiko zinaonekana kupingana na zile za halali za Mungu,hivyo hizo ndizo sheria “torati” za uongo.

Pia kama nilivyokwisha eleza kuwa kwa upande mwingine tendo hilo la Kalamu ya uongo ya waandishi kuifanya Torati kuwa uongo humaanisha kutamka au kufundisha yaliyo kinyume na Torati hiyo ya Bwana, lakini huenda hoja ikawa ni kuwepo kwa neno kalamu ya uongo ambalo hufanya kuwepo na maana moja tu ya kuandika, katika hili Biblia inaweka wazi kuwa hata mdomo huweza kuwa kalamu pia ”waswahili wanasema maneno uumba” unapoongea uongo ni sawa na kuandika uongo huo kwenye bongo za wengine. Hivyo maneno ni kalamu.


Tukio linganifu katika mafunuo ya Qur-an
Katika mafunuo ya Qur-an maelezo na picha hiyo ya kibiblia tuliokwishaiona huonekana pia, tatizo la kuibuka kwa makundi ya watu waliojaribu kugeuza au kuyafanya maneno ya Mungu au vitabu vilivyoaminiwa na jamii fulani kuwa uongo linaonekana kutawala katika pande zote za kidini. Hebu tupitie aya kadhaa za Qur an:-


KUMBE QURAN NI MKUSANYIKO WA UONGO
Qur –an 15:91 “Ambao wameifanya Qur an kuwa mkusanyiko wa uongo alioukusanya nabii Muhammad akadai kuwa ni maneno ya
Mwenyezi Mungu.”


KUMBE WATU WANAPINDA NDIMI KWENYE QURAN
Qur an 3:78 “ Kuna watu wanaopinda ndimi zao kwa kusoma vitabu ili tufikiri

kuwa maneno yao hayo ni ya kitabu cha Mwenyezi Mungu hali
hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu nao wanamsingizia
Mwenyezi Mungu uongo mkubwa……”

Kwa ushahidi huo wa maandiko ya Qur an tunaweza kupata picha ya jumla juu ya hoja hii nyeti, maandiko hayo ya Qur an hususani ile aya ya kwanza yanaonyesha tukio linganifu na lile la Kibiblia, hapo pia inaonekana kuwepo kwa makundi ya watu fulani waliokosoa na kuibeza Qur an kuwa ni mkusanyiko wa uongo tendo linalolingana sawia na lile la Torati ya Bwana.
Qur an inasema kuwa watu hao waliifanya Qur an kuwa ni mkusanyiko wa uongo.


Hoja ya msingi:
Je’nisahihi kutumia ushahidi wa andiko kuthibitisha mapungufu ya Qur an?

Endapo jibu si sahihi vivyo hivyo hakuna usahihi wowote wa madai ya kupotoshwa kwa Biblia kwa kutumia maneno hayo ya Yeremia kuwa kalamu ya waandishi ‘imeifanya kuwa uongo’ maneno ambayo ndiyo yanayotumiwa na Qur an pia katika muktaza uleule, kimsingi maneno hayo yanaonyesha tu upidhani uliolikabili neno hilo la kweli toka wa waandishi na watunzi wa maneno na vitabu vya uongo na siyo kupotoshwa kwa neno lenyewe.


MASWALI:
Maswali ya kujibu Kwa wanaodai kupotoshwa Kwa Biblia
Nani alifanya upotoshaji huo?

Wapi na ni lini upotoshaji huo ulifanywa?

Yako wapi magombo ya asili ambayo hayakupotoshwa ili kusaidia kujua maeneo ya vifungu vilivyopotoshwa?

Kulikuwa na sababu zipi zilizofanya Mungu anyamaze na kutolinda mafunuo yake ya wokovu kwa wanadamu wake?

Je nini ukweli na maana ya Mungu kutoa maelekezo yanayoonyesha uhakika na kutokuwepo uwezekano wa
kubadilishwa kwa mafunuo yake matakatifu?


Fuatilia Aya zifuatazo kuona uhakika wa Biblia:-
Mathayo 5:18 “yodi wala nukta ya torati haitaondoka…………..
Zaburi 15:4 “ameapa hayabadili maneno yake……………..
Qur-an Surat Ban Israel17:77 Ndiyo desturi ya wale tuliowatuma (tuliowapa utume) kabla yako katika mitume wetu. Wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu.

Qur-an Surat Fatir 35 : 43 Wala hutapata mahadiliko katika kawaida(desturi) ya Mungu (allyoiweka)wala hutakuta mageuko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu.

Ushahidi huo wa maandiko ya vitabu vyote viwili unaonyesha na kuthibitisha vile ambavyo hoja zinazo tolewa kwa kudai kuwa Biblia imeharibiwa si hoja za kimsingi na zaidi ya yote ni hoja zinazoonekana kushusha nguvu na uwezo wa Mungu wa kulinda na kusimamia mambo yake,lakini zaidi ya yote ni kutaka kumfanya mwongo pale alipoahidi kulinda maneno yake na kutokubali mageuzi katika mafunuo yake.


“Kamwe Biblia haijapotoshwa na haiwezi kupotoshwa”.
Qur- an Sura ya 87:18

“Hakika hayo mnayoambiwa humu (ndani ya Qur- ran) yamo katika vitabu vilivyotangulia. Vitabu vya Ibrahim, Musa, Isa na manabii wengine………………..”


Maneno hayo ya Qur-an yanatupatia Mwangaza unaotupa msingi wa kuichunguza vyema mada hii ya muhimu, maelezo ya Qur-an katika Aya hiyo yanaonyesha kuwa msingi wa mafunuo hayo ya Qur-an unategemea sana na kujengwa juu ya yale yaliyokwisha funuliwa awali katika vitabu vilivyo katika mkusanyiko wa “Biblia takatifu” hata hivyoMaandiko ya Qur-an kwa uwazi huyataja na kuyathibitisha mafunuo hayo ya kibiblia kwa kadri ya Aya zifuatazo:-


1. Torati - Musa
Qur-an 2:53 Natulimpa Musa kitabu (Torati) cha kupambanua na kuongoa ………
Qur-an 28:48 “Mnayakataa alopewa Musa”


2. Zaburi – Daud
Qur-an 4:163 Na Dawdi tukampa “Zaburi”
Qur-an 17:55 Dawd tukampa “Zaburi”


3. Injili-Bwana Yesu
Qur-an 5:47 watu wa “Injili” wahukumu kwa yale aliyotelemsha Mwenyezi Mungu ndani yake.


Mafungu hayo ya Qur-an kwa uwazi mkubwa yanaonyesha uzito na ukweli wa vitabu hivyo vya kale, kwa maana nyingine ndiyo maana Qur-an inaweka wazi kuwa mafunuo hayo (ya Qur-an) yanatokana na msingi wa Biblia (87:18).


BIBLIA NI ZAIDI YA QURAN
Biblia Mhimili wa Qur-an
Pamoja na mafunuo hayo mapya ya Qur-an bado mtume Muhammad aliendelea kuonyesha umuhimu na nafasi ya “Biblia” katika imani yake hiyo ya uislam.


Mafungu na Aya kadhaa tutakazozipitia zitatusaidia kuoana ukweli huu utakao tupa mwelekeo wa kuelewa vile Biblia ilivyo tegemeo (Mhimili) mkuu wa Qur-an. Kwa kadri ya Aya kadhaa za Qur-an inaonyesha dhahili kuwa Qur-an si kitabu kinachojitegemea chenyewe, badala yake kinapaswa kupimwa na kusaidiwa na mafunuo ya Biblia takatifu


Fuatilia nukuu zifuatazo za Qur-an ili kupanua ufahamu wa hoja hii ya msingi:-

Qur-an 10:94… “Ukiwa na shaka katika haya tuliyo kutelemshia nenda ukawaulize
watu wasomao vitabu kabla yako…………….”


Hoja za msingi
Ikiwa Qur-an ni kitabu chenye kujitosheleza chenyewe kuna haja gani ya kuwauliza waliyosoma vitabu vya kabla ya Qur-an?
Qur an 16:43 … Nendeni mkawaulize wenye kumbukumbu za vitabu vya


Mwenyezi Mungu vya kale ikiwa ninyi hamjui


Jifunze kupitia mfano
Katika dunia yetu Hospitali mbalimbali zinazotibu magonjwa ya kila aina humo wapo Madaktari bingwa, kwa kawaida ili kumtambua Daktari bingwa (Mhimili) ni pale tu unapopata ugonjwa na kwenda katika hospitali unayo iamini lakini hatimaye mwisho wa yote una taarifiwa kuhamishwa na kupelekwa katika hospitali nyingine kwa uchunguzi zaidi, “bila shaka huko ndiko kwa daktari bingwa”.


Ni wazi kama utakuwa msomaji mwaminifu katika sehemu hii tutakubaliana na kupata jibu kuwa “Biblia takatifu ni Mhimili wa Qur-an” na kwamba hakuna usahihi wa mafundisho yanayosikika kudai kuwa kitabu hiki kitakatifu kimetiwa maneno ya uongo au kuharibiwa kwa namna yeyote ile.

“Bwana akubariki kwa uelewa huu, na unapochukua hatua kuelimisha wengine.”

For Max Shimba Ministries

By permission

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW