Wednesday, February 17, 2016

ASILIA MBILI YA YESU KRISTO “MUNGU NA BINADAMU”

Tokea Dunia ianze, hapajawai toke Mtu yeyote alieishi kama Yesu Kristo. Yesu ni mtu wa maana sana ambaye ni Mwokozi, Mungu katika Mwili “Emanueli” (Isaya 9:6). Yesu sio Nusu Mungu na Nusu Binadamu kama watu na au imani nyingi zinavyo sema. Yesu yeye ni Mungu na ni Binadamu kwa wakati mmoja. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa na asilia Mbili tofauti ambazo ni Mungu na Binadamu kwa wakati mmoja.

Biblia inasema kuwa, Yesu ni “Neno” ambaye ni Mungu na alikuwa kwa Mungu na akafanywa kuwa Mwili na kuishi nasi, soma Yohana 1:1 na 14. Hii inamaanisha kuwa, mtu huyu mmoja ambaye ni Yesu alikuwa ana asilia mbili za Mungu na Binadamu.

Hii asilia ya Mungu haikubadirika pale ambapo “NENO” lilipo kuwa Mwili (Yohana 1:1, 14). Badala yake, Neno liliunga ubinadamu (Wakolosai 2:9). Hivyo basi, Umungu wa Yesu Kristo haukuharibika na au badirika. Zaidi ya hapo, Yesu hakuwa mtu tu ambaye alikuwa na Mungu ndani yake au Mtu aliye fanya kazi ya Mungu pekee, la hasha, Yesu ni Mungu katika Mwili na ni sehemu ya Pili katika Utatu Mtakatifu. Biblia inatuambia katika Waebrania 1 aya ya 3kuwa: Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno Lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni. Hivyo basi, asilia hizi mbili za Yesu Kristo haziwezi kuchanganywa (Eutychianism), vile vile haziwezi kuwa pamoja na kuwa Mungu-Mtu (Monophysitism). Hizi asili mbili ni tofauti na zinajitemea na wakati huohuo ni moja katika Yesu (person of Jesus). Huu muungano unaitwa Hypostatic Union.

Jedwari lifuatalo litakusaidia uone hizi asilia mbili za Yesu Kristo:
MUNGU
BINADAMU
Yesu anaabudiwa (Matayo. 2:2, 11; 14:33)
Yesu anamwabudu Mungu Baba (Yohana 17)
Yesu anaitwa Mungu (Yohana  20:28; Waebrania 1:8)
Yesu anaitwa Mtu/Binadamu (Marko 15:39; Yohana 19:5)
Yesu aliitwa Mwana wa Mungu (Marko 1:1)
Yesu aliitwa Mwana wa Adam (Yohana 9:35-37)
Anaombwa/prayed(Matendo ya Mitume7:59)
Anamwomba Mungu Baba (Yohona 17)
Yesu hana dhambi/sinless (1 Petro. 2:22; Waebrania 4:15)
Yesu alijaribiwa (Matayo. 4:1)
Yesu anafahamu kila kitu (Yohana 21:17)
Yesu alikuwa na Hekima (Luka 2:52)
Yesu anatoa uzima wa milele (Yohana 10:28)
Yesu Alikufa (Rom. 5:8)
Adhama zote za Mungu zipo ndani ya Yesu (Wakolosai 2:9)
Alikuwa na Mwili na Mifupa (Luka 24:39)

USHAHIDI ZAIDI WA ASILIA MBILI YA YESU

Mafundisho ya muungano wa Hypostatic ni ya “communication idiomatum” (Ni maneno ya Kilatini “Communication of properties”). Haya ni mafundisho ya adhama mbili za Yesu Kristo za Mungu na Binadamu zote zipo ndani ya Yesu Mtu “person of Jesus”. Hii inamaanisha kuwa, binadamu Yesu alikuwa na haki ya kusema kuwa “Alikuwa na utukufu na Baba Mungu kabla ya dunia kuumbwa soma Yohana 17:5), vile ile kudai kuwa  alitoka Mbinguni (Yohana 3:13), na kudai kuwa alikuwa kila mahalai “omnipresence (Matayo 28:20). Haya madai yote ya Yesu ni adhama za Mungu na kuwa yeye Yesu alikuwanayo.
Moja ya Makosa makubwa sana yanayo fanywa na wasio Wakristo ni kushindwa kwao kuelewa kuwa Yesu alikuwa na ASILIA MBILI. Kwa mfano, Mashahidi wa Yehova wao wanamwangali Yesu kama Binadamu na kupuuza adhama zake za Umungu. Mara zote wao hutumia zile aya ambazo zinakiri Ubinadamu wa Yesu na kuzipambanisha na aya ambazo zinasema kuwa Yesu ni Mungu. Kwa upande mwingine, Masayantisti wa Kikristo wao hufanya kinyume chake. Wao wana angalia zaidi upande wa Yesu ni Mungu na kusahau kuwa, Yesu alikuwa Binadamu vile vile.

Ili kumwelewa Yesu vyema, basi kila mafundisho ambayo yanamuhusisha Yesu, hayana budi kuzumgumzia Yesu kama Mungu na Yesu kama Binadamu. Hizo asilia Mbili ni zake. Kumbe ndio maana Yesu katika Luka 2:52 inasema: Naye Yesu akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu. Na wakati huo huo alikuwa kila kitu “omniscient” Soma Yohana 21:17. Yesu ni Neno la Mungu aliye kuwa Mwili/Binadamu (Yohana 1:1, 14).
Zaidi ya hapo, Biblia inamhusu Yesu (Yohana 5:39. Mitume wote walimtabiri Yesu (Matendo ya Mitume 10:43). Mungu Baba anatoa ushahidi kuhusu Yesu, Soma Yohana 5:37; 8:18. Roho Mtakatifu naye anato Ushahidi kuhusu Yesu, Soma Yohana 15:26. Kazi zake Yesu nazo zinashuhudia kuhusu Yesu Soma Yohana 5:36; 10:25. Makundi ya watu nayo yanashuhudia kuhusu Yesu, Soma Yohana 12:17. NA YESU anajishuhudia mwenyewe Soma Yohana 14:6 ; 18:6.
Kuna aya nyingine nyingi ambazo zinamshuhudia Yesu kuwa ni Mungu nazo ni
Yohana 10:30-33; 20:28; Wakolosai. 2:9; Wafilipi. 2:5-8; Waebrania 1:6-8; na 2 Petro. 1:1.
1 Timoteo 2:5 inasema , " Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani, mwanadamu Kristo Yesu, 6. aliyejitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wanadamu wote, jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake "   Hivi sasa, kuna Mtu Mbinguni ambaye yupo katika kiti cha Enzi. Yeye ni Mpatanishi wetu kwa Mungu Baba (1 Yohana 2:1). Ni Mwokozi wetu (Tito 2:13). Ni Bwana wetu (Warumi 10:9-10) Huyo Mtu anaitwa YESU.
Hakika Yesu Ni Mungu.
Kwa Maswali zaidi wasiliana nasi katika maxshimbaministries@gmail.com
Imeletwa kwenu na Max Shimba
Kwa Max Shimba Ministries Org.

@2015, April.  

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW