Wednesday, December 9, 2015

MAOMBI YA HATARI


UTANGULIZI
Maombi ya hatari ndiyo ni sahihi. Kichwa cha habari kinaogopesha katika mtazamo wa kwanza, lakini maelezo yake ni matamu, naamini matamu kuliko asali. Huwezi kueeleza kwa undani maana ya maombi ya hatari mpaka utakapokua unafanya. Haya ni maombi ambayo ulimwengu mzima umekuwa ukiyatamani, kila mtoto wa Mungu anapaswa kuomba haya ili kuweza kumweka shetani pamoja na mapepo yake kule wanakostahili.
Unapokuwa umeomba maombi haya katika Roho na kweli, utakuwa unamwambia shetani 'IMEKWISHA'' mimi niko nje ya kambi yako. Hebu turudi kwenye jarada hili la kitabu hiki tuone kwanza nyundo nzito na yenye hatari inavyoharibu kijibanda kwa nguvu isiyo kifani na utaweza kuona kufuli (kitasa) na mlango wa kijibanda vinavunjwa vipande vipande kwa ile nyundo. Ukitazama kwa uangalifu zaidi, utamwona mtu akikimbia kutoka kwenye kibanda akiwa huru kabisa.
Hivi ndivyo maombi haya ya hatari yalivyomweka mtu huru kutoka kwenye vifungo vya shetani na mapepo yake. Maombi ya hatari ni nguvu na uwezo mkuu wa Roho Mtakatifu unaona hivi na kuangamiza nguvu za giza zilizopo dhidi yako. Maombi haya ukiyatumia, utakuwa huru kutokana na vigongo na mashambulizi ya kishetani yanayo kuzunguka. Kamwe usinisifu mimi, baada ya maombi haya, bali mpe Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu utukufu wote, ambao ndiyo walioniwezesha kuyafahamu maombi haya.
Kabla ya maombi yako hayajawa na hatari unapaswa kwa mtu wa hatari unapokuwa mtu wa hatari ndipo utakapoweza kuomba maombi ya haraka na utakapoomba maombi ya hatari UPAKO WA HATARI uatanza kutiririka, na mambo ya hatari yataanza kufanyika katika ulimwengu huu na katika ulimwengu wa Roho.
MAPAMBANO YA KIHEKIMA
Kama tutajua nafasi yako ndani ya Kristo, ndipo utakapojua haki yako. Ukijua haki yako unauwezo wa kutumia haki yako, shetani na mapepo yake watakimbia.
Maombi ya hatari yanashambulia kiini cha matatizo yako. Hii ni njia nzuri ya kufanya nashambulizi. Unapokishinda kiini cha matatizo, sehemu nyingine ya hilo tatizo huwa inakufa. Unapotaka kuua mmea, unachotakiwa ni kung'oa shina lake na mti huo utakufa. Ikiwa tu utakata matawi, bila kung'oa shina hilo shina unaweza kuchipua tena. Hivyo inachotakiwa ni kuikata mizizi na mmea utakufa kabisa.
Maombi ya hatari ni aina ya maombi ambayo yanamlazimisha shetani na majeshi yake kuhama kwa nguvu na Roho Mtakatifu, hata kwama hawataki kuhama. Maombi haya yanaangamiza nguvu zote za shetani kuanzia ngazi za chini hadi ngazi za juu. Maombi ya hatari kama yanavyoitwa humfanya mtu wa Mungu kuwa huru kutokana na kutawaliwa na nguvu za shetani. Maombi haya huleta ukombozi kwa kila mtu wa Mungu
Maombi ya hatari huondoa na kuharibu kila laana maagano na makubaliano dhidi ya mtu wa Mungu. Tukitumia ujasiri tunaopata kwa njia ya Roho Mtakatifu, tunaweza kujiletea ukombozi sisi wenyewe tuapoomba maombi haya.
Maombi ya hatari hayampi shetani nafasi ya kuaingilia maisha yetu au maendeleo yetu. Maombi ya hatari ni maombi ya nguvu yanayopaswa kuombwa na watu wa Mungu wenye nguvu. Maombi ya hatari hutangaza VITA dhidi ya nguvu za giza zinakuzunguka na ufalme wa shetani mwenyewe.
Maombi haya yanakufanya kuwa zaidi ya mshindi; kila mtu wa Mungu anahitaji maombi haya ili awe mshindi wakati unaposhindwa kuishi maisha ya ushindi.
Fellowship, vikundi bya Kikristo, Makanisa na huduma zinahitaji aina hii ya maombi kwa ajili ya ushindi na kuwafanya waumini wake kukombolewa kwa jina la Yesu.
i. Biblia inasema utakuwa kiumbe kipya kiroho (2 Wakoritho 5:17)
ii. Ni lazima uwasamehe wote wakikukosea
Kama ulivyokwesha kujulishwa maombi ya hatari ni nini? Inakufahamisha juu ya maombi haya kwa uangalifu, maombi haya siyo ya mkato bali ni maombi yenye nguvu, kwa sababu ufalme wa Mungu hutekwa na wenye nguvu (MATHAYO 11: 12)
JINSI YA KUOMBA MAOMBI HAYA
• Usipige magoti unapoomba maombi haya
• Usimame na ujiandae kama askari
• Ukishike kitabu hiki mikononi mwako na kukisoma chote
• Unaweza kuomba haya mchana na usiku
• Maombi haya yanafanyakazi wakati wowote lakini ni vyema zaidi yawe walati wa usiku.
UHAI NA MAUTI vipo katika uwezo wa ulimi wako.
HATUA YA KWANZA: Jifunike wewe mwenyewe, nyumba yako, familia yako au jamii yako, wapendwa wako mali zako, familia yako au ya Yesu Kristo, kabla hujaanza kuomba.
HATUA YA PILI: Ukiri mapenzi ya Mungu kwako (yaani maandiko yaliyo mapenzi ya Mungu) endapo baada ya maombi unapatwa na mashambulizi ya kiroho, omba tena . Mashambulizi hayo ni kwa sababu tayari umekwisha TETEMESHA na kuharibu kitu fulani katika ufalme wa giza.
HATUA YA TATU: Endelea na maombi haya, maana kwa hakika ………………………. Kwenye nguvu katika roho. Katika mashambulizi makali ya kishetani, vipingamizi endelea kwa siku saba (7) za masisitizo (mfululizo) wa maombi haya kuanzia saa 6.00 usiku wa manane hadi saa 9.00 alasiri kwa kufanya hivi, utawasumbua na kuwazuia maadui kufanya mkutano dhidi yako, na wengine kwa ujumla kwa ajili ya usumbufu huu utakao kuwa unaendelea kufanya utasababisha wao kuliondoa jina lako katika orodha ya wale wanaotakiwa kushambuliwa. Kwa kuondolewa jina katika orodha ya watarajiwa moja kwa moja unapata uhuru na ufumbuzi wa matatizo yako.
Maombi haya hayatoshelezi kukufana uombe kuanzia usiku wa saa 6.00 hadi alfajiri saa 9 inabidi uongeze maombi mengine juu ya hayo. Unaweza ukaomba mara mbili au zaidi katika muda huo wa masaa matatu ya maombi ya msisitizo (hivyo haimaanishi kwamba unarudia bali unazidi kuchochea moto zaidi mahali ambapo tayari pana moto dhidi ya shetani)
Omba mara kwa mara ukimaanisha na kueleweka ni nini unachokisema. Epuka na kupaaza sauti zaidi ikiwa upo wenye nyumba yenye watu wengi. Sauti isije ikawasumbua wengine hivyo omba kwa sauti ya kwaida ya utulivu. Lakini pia kutunza siri ya za maombi haya ya vita na hatari, mawakala wa shetani wanaweza kuwa wanasikiliza maombi.
MAOMBI KWA KUKIRI NENO
MATAYO 16:19
Imeandikwa nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni na lolote utakalo lifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni na lolote utakalo lifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.
UKIRI WA MUNGU
Baba sasa ninazipokea funguo zote za ufalme wa mbinguni ili kufungua milango ya mambo yasiyowezekana chochote nitakacho, nitakacho kifungua sasa kitafunguka milele katika jina la Yesu, Amen.
WAFILIPI 4:13
Imeandikwa nayaweza mambo yote katika Yesu Kristo anitiaye nguvu. Katika jina la Yesu, Amen.
LUKA 1:37
Imeandikwa kwamba hakuna Neno lisilowezekana kwa Mungu.
UKIRI WA MUNGU
Baba upo pamoja nami sasa na hakutakuwa na chochote ambacho hakitawezekana kwangu katika jina la Yesu-Ameni.
ZAKARIA 4:6
Imeandikwa ''si kwa uwezo wala si kwa nguvu bali ni kwa Roho yangu asema Bwana wa Majeshi''
UKIRI WA NGUVU
Baba vita si vya kwangu bali ni kwa Roho yako utanipigania katika jina la Yesu-Amen!
ISAYA 41:10
Imeandikwa, usiogope kwa maana mimi ni pamoja nawe, usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako, nitakutia nguvu, naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
UKIRI WA NGUVU
Baba ninakushukuru kwa kuwa upo pamoja nami kwa ajili ya kunitia nguvu, kunisaidia, kunishika na kuwa na Mungu wangu, moyo wangu umetiwa nguvu, katika vita hii katika jina la Yesu, Amen!
ZABURU 105: 15
Imeandikwa, msiwaguse masikini wangu wala msiwadhuru ''masikini wangu''
UKIRI WA NGUVU
Nimefunikwa kwa Damu ya Yesu Kristo shetani huwezi kunigusa kwa sababu mimi ni mpakwa mafuta na nabii wa Mungu maisha yangu yako mikononi mwa Yesu Kristo na ninayo chapa yake. Nimetiwa muhuri wa Roho Mtakatifu katika jina la Yesu Amen!
ISAYA 54:17
Imeandikwa, kila silaha itakayo fanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndiyo urithi watumishi wa Bwana na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.
UKIRI WA NGUVU
Katika jina la Yesu ninaharibu kila silaha ya shetani iliyofanywa dhidi yangu, silaha ya kiroho au ya kimwili ninaulaani na kuufunga kila ulimi utakaoinuka dhidi yangu katika hukumu, kwa kuwa huu ni urithi wangu kama mtumishi wa Mungu, ni haki yangu kwa Bwana.
KUMBUKA: sasa wewe uko tayari umeiva kwa kuomba maombi ya hatari umejaa nguvu na upakwa mafuta mapya na nguvu, kuzishinda nguvu zote za shetani.
UWEZO KATIKA ULIMI WAKO
Mauti na uzima huwa katika ulimi (mithali 18:21) lakini neno liko karibu nawe sana. Likini kinywa chako na moyo upate kulifanya (kumbu la torati 30: 14) uwezo wa Mungu uko katika ulimi wako sasa, tamka maneno nayo yatafanyika. Omba maombi ya hatari katika nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu na shetani na mapepo yatainua mikono juu.
PIGANA NA UWE HURU SASA
Uwepo wa Bwana
Katika jina kuu linalotikisa falme na mamlaka la Bwana wetu Kristo wa Nazareth, katika jina litendalo maajabu la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi, Baba wa Mbinguni; Ninaita uwepo wako mahali hapa, ninaita uwepo wa Bwana. Asante Mungu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu kuniunga mkono katika vita hivi katika jina la Yesu Kristo Amen.
ROHO MTAKATIFU
Roho Mtakatifu ninaomba uwe pamoja nami katika vita dhidi ya shetani na wajumbe wake. Roho Mtakatifu wewe ni mfariji wangu. Pigana vita hivi kwa ajili yangu na unifariji katika jina la Yesu. Siwezi kuomba kama vile uombavyo wewe. Nakusihi sema sasa ukitumie kinywa changu katika Jina la Yesu.
Roho Mtakatifu uniongoze na unilinde, unifundishe jinsi ya kuomba nitumie kama shoka lako katika vita hivi, dhidi ya shetani na wajumbe wake. Roho Mtakatifu wewe ni mfariji wangu. Pigana vita hivi kwa ajili yangu na unifariji katika jina la Yesu siwezi kuomba kama vile uombavyo wewe. Nakusihi sema sasa ukitumia kinywa changu katika jina la Yesu.
Roho Mtakatifu uniongoze na unilinde, unifundishe jinsi ya luomba nitumie kama shoka lako katika vita hivi vya adui. Uje katika nguvu na uwezo wako na ukaonyeshe ukuu wako dhidi ya shetani na wajumbe wake katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth, Amen.
WARUHUSU MALAIKA WA VITA
Katika jina lenye nguvu la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi. Ninaruhusu malaika wa vita kutoka ufalme wa Mungu ninawaamuru enyi wote kukaa kwenye nafasi zenu dhidi ya shetani na mapepo yote, sambaeni kila mahali sasa, mjieneze katika Anga, Nchi na Bahari, muangamize nguvu zote za giza katika Anga, Nchi na Bahari, muangamize nguvu za giza katika anga za nchi kavu na baharini mpige shetani bila kukoma, haribuni mipango yote waliyoifanya dhidi yangu. Ninawamuru enyi malaika na Bwana mnizunguke kama wigo sasa. Mnizunguke mimi katika jina la Yesu Kristo-Amen.
DAMU YA YESU KRISTO
Ninajifunika kwa damu ya Yesu Kristo. Ninawaloweka watu wa familia yangu, ndugu zangu, nyumba yangu, ofisi yangu, chakila changu, fedha zangu, kiwanja changu, rafiki zangu, majirani zangu, n.k katika damu yenye nguvu ya Yesu Kristo wa Nazareth. Ninalifunika anga lote, nchi yote na bahari yote kwa damu ya Yesu Kristo; shetani imeandikwa katika ufunuo 12: 11 ''Nao wakamshinda shetani kwa damu ya Mwanakondoo na kwa Neno la ushuhuda wao '' nimetumia damu ya Yesu kukushinda sasa na hata milele katika jina la Yesu!
FUNGA MAPEPO YOTE YANAYOZUIA MAOMBI
Katika jina la Bwana wangu Yesu Kristo ninakemea, ninafunga na kuyaangamiza mapepo yote yanayozuia maombi Angani, katika nchi na Baharini. Pia naharibu kila pepo anayeninginia, kila pepo arukaye na wale walionyimwa chakula. Ninawatuma hadi kuzimu katika jina la Yesu. Ninaharibu vipingamizi vyenu vyote vya maombi yangu, ninawatupa katika giza la milele. Ninawafungia huko hata siku ya Bwana ya hukumu. Pia ninakemea, na kufunga na kuharibu mapepo yote yanayozuia ukombozi wangu, mafanikio yangu na miujiza. Ninaharibu kazi zenu dhidi ya maisha yangu, ninawatupa wote katika giza la milele na kamwe msiweze kuinuka tena hata siku ya hukumu ya Bwana. Ninawatumia moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote katika jina la Yesu Kristo, Amen!
UKUNGU WA KIPEPO
Ninatumia moto wa Roho Mtakatifu na Damu ya Yesu kuharibu ukungu wa kipepo unaofunika anga. Ninaharibu kila mfuniko ambao, umenifunika katika jina la Yesu Amen. Ninaharibu kila kifuniko, minyororo, mafundo na uchawi dhidi yangu. Ninauamuru moto wa Roho Mtakatifu kuviteketeza vyote na kuvifanya majivu kabisa. Ninauzimisha moshi wangu shetani dhidi ya maombi yangu. Ninatumia damu ya Yesu kuviharibu vyote, katika jina la Yesu, Amen.
Shetani, imeandikwa katika kitabu cha LUKA 1:13 kusema ''Hakuna lisilo wezekana kwa Mungu.
JIFUNGUE (JIWEKE HURU)
Katika Jina la Yesu ninavunja nguvu zote za giza zilizonifunga. Ninajiweka huru kutoka kwenye nguvu za giza dhidi yangu. Ninajiweka huru kutoka kwenye vifungo vya Uchawi, Waume wa Kipepo, Wake wa kipepo, Watoto wa kipepo, Makazi ya kipepo, Mali za Kipepo, Mapepo ya kurithi, Majini Bahari, Maruhani, Misukule na Mizimu, Subians, Maruani, Zakuani.nk.
Sikiliza enyi nguvu za giza, imeandikwa katika kitabu cha Matayo 18:18 kusema Amini nawaambia yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni na yoyote mtakayo yafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. NInasimama juu ya neno hili na kujifungua kutoka kwenye aina zote za giza na nguvu zote za kipepo katika jina la Yesu, Amen!
T. V ZA KIPEPO (SPIRITUAL SCREENS)
Ninavunja vipande vipande T. V zote za kipepo ambazo shetani anazitumia kunifuatilia. Ninavunja vioo vyote vya kipepo, mikanda ambavyo shetani amevitega dhidi yangu.
Ninayakemea ninayavunja na kuyaamuru mapepo yote ya angani na duniani yapate kuniachia kwa jina la Yesu. Amen. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote. Ninafunga wote kwa ufunguo wa hukumu na msiinuke kamwe hadi siku ya Bwana ya hukumu nisikilize sana shetani imeandikwa katika Isaya 54:17 kwamba hakuna silaha itakayofanyika dhidi yangu ambayo itafanikiwa, na kila Ulinzi utakaoinuka juu yangu nitauhukumu kwa makosa. Ninasimama juu ya Neno hili na ninazilaani silaha zako zote ulizozifanya dhidi yangu, nitaziharibu kwa jina la Yesu, Amen!
MITANDAO MINGINE YA KIPEPO (Ndege, Simu, Vifaru, Roketi/ Radi/Pisto)
FUNGE SHETANI
Ninakukemea shetani, ninakwenda kinyume chako kwa damu ya Yesu na kwa moto wa Roho Mtakatifu. Shetani ninakushinda. Ninaukanyanga ufalme wako. Ninakunyanganya kila kilicho changu. Ninakiamuru kuviacha vitu vyangu katika jina la Yesu. Mimi ni balozi wa Bwana, mimi ni masihi wa Bwana Yesu Kristo amenipa nguvu, mamlaka na uwezo wa kuzikanyaga nguvu, mamlaka na uwezo wako shetani wala hakuna kitakacho nidhuru.
Kumbuka imeandikwa katika zaburi 105:15 kusema usimguse masihi wangu na wala usimdhuru nabii wangu; malaika wa Bwana wananizunguka hakuna silaha yoyote itakayofanyika juu yangu, itakayofanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yangu katika hukumu, nitaukumukua mkosa, kwa Jina la Yesu, Amen.
Nisikilize shetani, mimi ni kapteni wa jeshi la Bwana ninasikiliza amri kutoka kwa Amiri Jeshi wangu tu Yesu Kristo wa Nazareth ambaye vyote viliumbwa kwa yeye ninakuamuru uhame katika Jina lipitalo majini yote Yesu Kristo wa Nazarethi popote pale unapojificha, naamuru moto wa Roho Mtakatifu ukuunguze usiku na mchana hata milele. Amina!
FUNGA FALME NA MAMLAKA N.K.
Ninazikemea, ninazifunga na kuziharibu falme na mamlaka ya wakuu wa giza hili, majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote, katika jina la Yesu. Ninawagonga wachawi wote, majini, mizimu, majini, baharini wakuu wa giza, roho wa udhaifu na roho chafu zote zilizo dhidi ya maisha yangu na maendeleo yangu. Ninayaaharibu maficho yako na kila mbinu unayoitumia kujihami na moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote katika Jina la Yesu. Ninawatupa wote kuzimu ninawafungia katika giza milele
ninawafungia wote hata siku ya hukumu ya Bwana na wala msiinuke tena, katika jina la Yesu, Amen.
MANENO MACHAFU YOTE
Ninayafuta na kuyaharibu maneno yote mabaya niliyowahi kuyatamka ambayo shetani anayatumia dhidi yangu. Ninaungama na kutubu na kuyafuta, maneno hayo popote yalipo, Ardhi, Baharini, Angani, Mwezini, kwenye Nyota au kwenye Jua katika Jina la Yesu. Ninaugeuza ukiri wangu mbaya na ulio kinyume na maagizo ya Mungu ili uwe ukiri mwema katika utukufu wa Mungu Mwenyezi. Ninatumia damu ya Yesu kuyafuta maneno ya ikiri mbaya na wa kinyume katika Jina la Yesu, Amen!
MALI ZA MASHETANI
Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi, naharibu kila kitu nilicho nacho ambacho ni mali ya shetani, ninakiharibu kila kilicho cha Shetani, na vitu vyote vyenye uhusiano na shetani, vyenye nguvu za shetani ambavyo nimevinunua kwa fedha zangu au kupewa kama zawadi.
Ninazitakasa nguo zangu zote kwa Damu ya Yesu wa Nazarethi. Ninaharibu kila kitu nilicho nacho ambacho ni mali ya shetani ninakiharibu kila kilicho cha shetani na vitu vyote vyenye uhusiano na shetani vyenye nguvu za shetani, ambavyo nimevinunua kwa fedha zangu au kupewa kama zawadi. Pia ninaharibu mali zangu zote katika uimwengu wa Roho popote penye mfano wangu, mali zangu, fedha zangu, jina langu, sehemu yoyote ya Mwili wangu, Kucha, Nywele zangu na yoyote yanayotokana na hayo ambavyo viko Baharini, Angani, Duniani, kwenye Mahekalu ya Sanamu au Madhabahu za Shetani, ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kuwaunguza wajumbe wote washetani wanaofanya vitu dhidi yangu vyote, jamii yangu kwa damu aya Yesu Kristo wa Nazarethi.
VIFUNGO VYA (MOYO NAFSI NA MAWAZO)
Katika jina la Yesu Kristo wa Nazarethi, Baba wa Mbinguni, ninakuinulia mkono wangu wa kuume mimi mwanao/ binti yako …(Taja jina) nitazame Bwana maana nguvu na uwezo wote unatoka kwenye kiti chako cha enzi kama ilivyoandikwa katika zabauri 52:11-12. Kusema ''mara moja amenena Mungu mara mbili nimeyasikia haya, ya kwamba nguvu zina Mungu na fadhili ziko kwako ee Bwana, maana ndiwe umlipaye kila mtu sawa sawa na haki yake. Baba wa mbinguni , ninapokea nguvu kutoka kwako sasa katika jina la Yesu. Ninatumia nguvu hizi kufuta ,kuvunja,
kuharibu na kujitenga mwenyewe kutoka kwenye laana zote na maagano yote yaliyofanywa dhidi yangu.
Ninaamuru laana zote pamoja na mapato na mazindiko yaliyofichwa popote dhidi ya maisha yangu kujidhihirisha sasa katika Jina la Yesu. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu na Damu ya Yesu kuwadhihirisha wote. Ninaziharibu nguvu zote katika jina la Yesu Kristo-Amen.
DHAMBI ZA MABABU
Baba wa Mbinguni ninaleta dhambi zote za mababu zangu mbele zako. Ninatubu na kuziungama dhambi zao zote kwa maana walikutenda dhambi. Ninaziungama dhambi zote za kuuwa binadamu wenzao, kuabudu sanamu na kuwanunua wanadamu, kafara za watu kwa miungu ya sanamu, kula nyama za watu na kila matendo mengine ya kishetani walioyafanya.
Baba pia ninaungama dhambi za wazazi wangu na uovu wao walioutenda mbele zako. Baba ninakusihi uwe na rehema katika Jina la Yesu Kristo ninawasamehe makosa yote walionitendea katika jina la Yesu. Ninaomba uzisahau dhambi na makosa na uovu wao kwa hiyo ninajitenga mwenyewe kutoka kwenye adhabu ya makosa hayo, katika jina la Yesu.
DHAMBI AU LAANA ZA WAHENGA (WAKALE)
Katika jina lenye nguvu na uwezo la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi ninatubu dhambi zilizofanywa na hao wazee wetu wa kale (wahenga) ambazo kwa hizo laana imepata kuniandama hata hii leo mimi na uzao wangu. Ninavunja na kuharibu laana zote zilizosababishwa na uovu wowote waliofanya; ninaziharibu kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazarethi. Laana zote mapatano na matambiko katika upande wa baba yangu na mama yangu ninaziharibu na kuzivunja katika Jina la Yesu. Bila kujali na aina gani ya laana iliyowekwa juu yangu; bila kujali na maagano gani wahenga wangu wamefanya na shetani; na bila kujali ni wapi wamefanya mambo ya matambiko, mazindiko juu yangu, angani duniani, baharini, ninayaharibu yote katika Jina la Yesu, Amen.
Pia ninavunja laana, maagano na matambiko, niliyofanyiwa na Baba yangu na Mama yangu na Wazazi wao (Babu na Bibi) kutoka kizazi chochote kwa upande wa Baba yangu na Mama yangu, bila kujali laana, matambiko, Mazindiko, Mapatano na
ushirikano na ushirikiano uwao wote yalifanyika wapi. Ninaamuru yote kuvunjika na kuharibiwa katika Jina la Yesu Kristo, Amen.
KUTOKA KWANGU MWENYEWE
Katika Jina la Yesu ninakwenda kinyume na laana zote nilizozisababisha mimi mwenyewe, juu ya maendeleo yangu na maisha yangu, kwa kujua na kutokujua. Ninakuvunja wewe laana popote pale ulipojificha, angani duniani na baharini, ninakuharibu na kuzivunja nguvu zako zote katika Jina la Yesu.
Ninakuja kinyume cha maagano niliyofanya na miungu ya sanamu, pepo wachafu, maruahani, majini bahari, wanaume wa kipepo, wake wa kipepo, Watoto wa kipepo, Mizimu n.k katika Jina la Yesu, mazindiko yote niliyojifanyia ninayaharibu yote. Ninajiondoa katika mazindiko hayo. Ninalifuta jina langu kwenye kitabu cha shetani. Ninajitangazia uhuru leo katika Jina la Yesu Amen. Ninajifunika kwa damu a Yesu Kristo wa Nazarethi.
KWA KUTO MTII MUNGU
Ninaungama na kutubu dhambi zangu kwa jina lako baba, katika jina la Yesu, ziondoe laana (Malaki 3: 8-12) nzige, tanutu na viwavi kutoka kwangu. Ninyeshee mvua za mwanzo na za mwisho. Nijaze tena baraka zako, katika Jina la Yesu, Amen.
KUTOKA KWA SHETANI NA WAJUMBE WAKE
Katika Jina la Yesu ninavunja na kuzimisha laana zote. Maagano na mazindiko ya shetani na wajumbe wake walio dhidi yangu. Ninaharibu uchawi, laana, maagano kutoka kwa miungu ya uongo, wachawi waganga wa kienyeji, na majini ya bahari, mizimu, wanaume au wanawake wa kipepo, watoto wa kipepo makazi ya kipepo, mali za kipepo, kutoa mimba, kutiwa maji, mikutano ya wachawi, Mahekalu ya kipepo, kutoka Angani, Nchi na Baharini (Hes.22).
Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kuteketeza na kuharibu mipango yenu yote iliyopangwa dhidi yangu, katika Jina la Yesu Kristo wa NazarethI, Amen.
LAANA YA NCHI
Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazarethi na laana ya nchi yangu, mji wangu, na kijiji changu ninavunja laana zote, matambiko maagano na mazindiko yaliyofanywa dhidi ya watu wangu na ninaharibu nguvu zote zilizofanyika dhidi yao, katika jina la Yesu Kriso. Ninavunja laana ya mauti, kichaa, tama, umaskini,
masongwa, kutaka kujua, kuachana, utasa, kutokuoa, au kutokuolewa n.k. Ninajitenga sasa kutoka kwenye laana hizo, maagizo na mazindiko katika Jina la Yesu, Amen.
Ninaharibu nguvu zote na mipango ya wachawi, Miungu ya uongo, Miti mibaya, Mito, Mapori mabaya n.k katika mji wangu na kijiji changu. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kuviharibu vyote katika Jina la Yesu, Amen.
AINA YA MAKUBALIANO
Ninavunja maagano na mazindiko yaliyofanywa kwa ajili yangu, nchini na baharini pia ninaharibu maagano na mazindiko yaliyofanywa kwa niaba yangu kwa miungu ya uongo, miti, mivinjo (shrine) mito na vijito.(Funga na haribu mito yote mibaya, miungu ya uongo, vijito na wachawi) katika kijiji changu au mji wangu ninajitenganisha sasa kutoka kwenye laana hizo, maagano na mazindiko katika Jina la Yesu, Amen.
MASHAMBULIZI YA NDOTO
Katika jina la Yesu wa Nazarethi ninavunja nguvu zote za giza dhidi yangu zinazokuja ndotoni. Ninayafunga na kuyatupa mapepo yote yanayonishambulia kwa njia ya ndoto. Ninakuja kinyume na ndoto zote za kipepo dhidi ya maisha yangu. Ninawakemea, ninafunga na kuharibu mapepo yote yanayonipa chakula kwenye ndoto, wanawake na wanaume wa kipepo wanaofanya mapenzi nami katika ndoto, mahoka yote, yanayonijia katika ndoto, mapepo yote yanayofanya kuogelea kwenye mto, mapepo yote yanayonioa katika ndoto,(majinamizi). Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote katika Jina la Yesu, Amen.
Katika jina la Yesu Kristo wa Nazarethi, ninavunja Roho zozote chafu juu yangu, roho ya kiburi, hasira, uchungu, kukataliwa, makosa, uasi, uvivu, chuki, mashaka, kuchanganyikiwa, kujidharau, kutokuamini, anasa, ukaidi, mashindano, mateso, umaskini, ukosefu wa usingizi, mauti, uoga, uongo, kutokusamehe, uasherati, uzinzi, uchafu, kutokutii, wivu, uuwaji, ulevi, n.k ambao zinanikandamiza roho yangu nafsi yangu, moyo wangu, mawazo yangu na hali ya mazingira yangu.
Ninazikemea na kuzifunga, na kuzitoa nje roho hizo kwa jina ka Yesu. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kuwateketeza wote popote pale mlipojificha, angani, nchini na baharini. Ninatumia damu ya Yesu Kristo kujifunika ili msiweze kurudi tena kwangu katika jina la Yesu, Amen.
SHEREHE ZA MIJI NA MILA ZA KIFAMILIA
Katika jina la Yesu Kristo ninakemea na kuharibu mila zote za kipepo sherehe na matukio yanayotendeka na jamii yangu au mji wangu. Ninayaharibu mapepo yote yanayoabudiwa katika sherehe hizo, ninatumia damu ya Yesu kutangaza vita dhidi yenu katika Jina la Yesu. ( Kumbuka, ujiepushe kushiriki sherehe hizo maana kwa kufanya hivyo utakuwa unayapendeza mapepo hayo na kuyaabudu.)
ULINZI WA KIPEPO (SPIRIT GUARDS)
Ninayafunga kwa minyororo na kuyatupa katika shimo la giza mapepo ya ulinzi yanayolinda laana za maagano, mazindiko, uchawi na mahirizi n.k dhidi ya maisha yangu. Ninaziharibu hati za makubaliano, nawafunga wote katika giza la milele. Naamuru moto wa Roho Mtakatifu kuwatesa mchana na usiku katika jina la Yesu. Ninatumia damu ya Yesu kuziba nafasi mlizokuwa mmekalia, kwa jina la Yesu, Amen.
JITENGE MWENYEWE
Baba wa Mbinguni, ninajishusha na kujitenganisha na laana zote, maagano, mazindiko n.k niliyofanyiwa mimi niko huru sasa, hivyo ninayo haki ya kuchagua nitakayemtumikia. Ninachagua kumtumikia Baba wa mbinguni, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. Mimi ni kiumbe kipya na ni mpya kila siku ya maisha yangu. Roho Mtakatifu yu juu yangu sasa. NInayaweza mambo yote katika Yesu Kristo anitiaye nguvu (Fil 4:13)
Neno la Mungu linasema kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.
(Mathayo. 12:37) Baba nifanye kuwa na haki kwa maneno ya kinywa changu kwa kuwa uzima na mauti vimo katika uwezo wa ulimi (Mithali 10:21).
Basi mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli (Yohana. 8:36) kamwe sitateswa tena na Shetani pamoja na wajumbe wake kwa maana mimi tayari niko huru, katika jina la Yesu Kristo. Amen.
Pastor Justice Lutashobya For Tanzani Prayer Mission Programme: 2008-2014

No comments:

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW