Saturday, November 28, 2015

NAMNA YA KUMWITA,KWENDA NA KUMUOMBA MUNGU ILI AKUSIKILIZE.

Yeremia 29:12 “Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza”.

Utangulizi 

Watu wengi wamekuwa wakitamani maombi wanayoyapeleka mbele za Mungukusikilizwa.Watu wanaomba kila aina ya maombi inayowezakana maadam Mungu asikie na kuwaokoa kutoka kwenye shida waliyonayo au kuwapa haja za mioyo sawasawa na uhitaji wao.

Wapo wanaoomba na wanaona majibu yao yanajibiwa lakini pia lipo kundi jingine kubwa ambalo wanaona kama vile Mungu amenyamaza, amewaacha, hawasikii, au wanajiona kama vile Mungu amewakataa na kuziona ahadi za Mungu kwamba si za kweli na mbaya zaidi wengine wamefika mahali pa kumwacha Mungu kwa sababu ya kushindwa kuvumilia majibu kutoka kwa Mungu na hivyo kutafuta njia mbadala za kutatua matatizo yao. 

Wapo walioomba kuhusu watoto, ndoa zao, afya zao,ajira,biashara,Elimu zao nk. Walipoona katika fahamu zao Mungu hajibu basi wakaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji,wachawi na kwa miungu mingine kutafuta msaada huko.

Sasa ili Mungu aweze kusikiliza au kujibu maombi yako huenda kuna mambo mengi ya msingi ambayo mwombaji anapaswa kuyajua na kuyatendeakazi. Sasa baada ya kuona maombi mengi ninayoomba na pia ambayo wana wa Mungu pia wanaomba hayajibiwi ili nilazimu nimuombe Mungu anifundishe vizuri kuhusu hili neno.

Hivyo hayo ninayoenda kukushirikisha ni sehemu ya yale ambayo Mungu amekua akifundisha naamini na wewe yatakusaidia maana nimeona yakinisaidia binafsi pamoja na wale ambao Mungu amenipa kuwafundisha kwa njia nyingine.

Lengo la ujumbe huu ni kukupa maarifa yatakayokusaidia kuomba maombi ambayo wewe mwenyewe.Pindi unapoomba utakua na uhakika Mungu anakusikiliza kwa wakati  huo.Zaidi ujumbe huu umekusudia kukufundisha namna unavyoweza ukapeleka maombi mbele za Mungu.

Siku moja nikiwa chuoni mwaka wa kwanza majira ya tisa jioni,nilikua nikipandisha ngazi kuelekea chumbani kwangu ambacho kilikua ghorofa ya tatu juu kabisa.Wakati naanza kupandisha zile ngazi nikasikia mtu ananiuliza ndani yangu 

Je hivi Mungu huwa anaitwaje?Anaendwaje?Anatafutajwe?Anakaribiwaje? Nilipofika chumbani nikaanza kutafakari haya maswali na baadae ndipo nikapata hii mistari katika Yeremia 29:12-13 inayosema “Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza 13 nanyi mtanifuata na kuniona,mtakaponifuata kwa moyo wenu wote.”Baada ya kuisoma vizuri ndio nikagundua karibu maswali yale yote yalitoka hapa.

Mungu anasema nanyi mtaniita, sasa na mimi nikuulize swali, hivi umeshawahi kujiuliza Mungu tunamwitajemwitaje? Tunamwendeaje? Na tunamtafutaje. Usiishie kusema Mungu ameseam nikaribieni nami nitawakaribia, umneshawahi kujiuliza anaposema tumkaribie yeye yuko wapi? Na pia tunamkaribia kwa namna gani? Sasa hayo ndio maswali yaliokuwa yakinijia.

Picha ambayo Mungu alitaka niipate kwenye zile ngazi ni hii, nifikirie kwamba kile chumba kule juu ndiko aliko yeye yaani mbinguni. Sasa baada ya kufikiria hivyo ndio niwaze na nijiulize amesema nimuite nimwendee nimtafute n.k Sasa hivi ndio ninamwitaje, ninamwendeaje na ninamtafutaje? Nilipozidi kutafakari hiyo mistari roho mtakatifu akanifundisha yafuatayo:
kwanza alinionyesha makosa matatu ambayo watoto wake mara nyingi tumekuwa tukiyafanya wakati wa maombi. Na ningependa na wewe uyajue kwa maana itakusaidia ili bado unayafanya basi usiyafanye tena.


Kosa la kwanza, 
Kuomba kinyume au nje ya mapenzi ya Mungu.
1 Yohana 5:14 inasema Na huu ndio ujasiri tulionao kwake ,ya kuwa,tukiomba kitu sawa na mapenzi yake atusikia” Moja ya tafsiri za kiingereza inasema “We are certain that God will hear our prayers when we ask for what pleases him” Kosa kubwa ambalo tumekuwa tukilifanya mara nyingi ni kuomba vitu au mambo ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

Anaposema sawasawa na mapenzi ya Mungu maana yake ni lazima ujue kwanza nini ni mtazamo au mawazo ya Mungu juu ya hilo unalotaka kuliombea. Maombi ni kuzungumza au kusemezana na Mungu kwa Kumwambia yale ambayo amesema kwenye neno lake kuhusu haja zako wewe.

Kwa lugha nyingine usiombe kitu ambacho hujui nini Mawazo ya Mungu juu ya hicho kitu. Mawazo ya Mungu juu ya kila haja ujyonayo yako ndani ya Neno lake .Hivyo ni lazima Neno la Mungu likae kwa wingi ndani yako ili unapoomba uombe kulingana na ahadi zake na pia sawa na kile alichokisema.

Zaidi pia wengi wanapotaka kuomba huenda kuhusu ndoa,kanisa,Ajira,watoto ,biashara nk huwa wanomba kimazaoea. Maana yake ni hii wengi wamezoea ninpoombea ndoa nitaombea amani,upendo ,furaha nk Sasa sina maana hayo maombi hayafai ila ninachotaka ukipate ni hiki hoja unazozipeleka mbinguni hakikisha umefunuliwa na Mungumwenyewe.Maana yake Mungu ndiye akupe mambo ya kuombea kuhusu nchi ,ndoa,biashara yako nk.


Kosa la pili, 
Kukosa utulivu na uskivu wa rohoni wakati wa maombi na baada ya maombi.
Sikiliza Mungu anayo mambo mengi ya kukuambia wewe kuliko yaje wewe uliyonayo wewe kumweleza yeye. Chungu hakiwezi kumwambia mfinyanzi kwamba ulinumba kwa kazi hii tu, bali mfmyazi ndiye mwenye mengi kuhusu kile chungu. 

Ndio maana Yesu anasema si ninyi mlionichagua mimi bali ni mimi niliyewachagua njnyi (Yohana 15:16),Sasa watu wengi sana wana bidii nzuri ya maombi wanaweza wakakaa hata masaa matatu mfululizo na hata zaidi wanamuomba Mungu tu.

Katika mda huu wote wao ndio wanaojieleza na mara wanapomaliza ni kusema Ameni na kuondoka.Hii ni picha ya mtoto anayekuja kwako kama mzazi anasema baba/mama naomba hela ya daftari, nauli na ya kula shuleni, pia naomba uninunulie suruali nk. Sasa kabla wewe hujamjibu yeye ameshafungua mlango na kuondoka.sasa kibiblia ndiko kunaitwa kukosa utulivu na usikivu wa rohoni mbele za Mungu.


Mara zote unapoomba jifunze kuwa na wakati wa kutulia kusikiliza Mungu naye anasema nini.Kwenye utulivu ndiko Mungu anakosema sio kwenye kelele maana anjua hamwezi kusikilizana.Soma Isamwel 3:1-10 utaelewa ninachokisema hapa.Mungu alisema na Samweli alipotulia.


Kosa la tatu, 
Kumuomba Mungu wakati tayari umeshajitafutiajibu la shida uliyo nayo.

Hili ni kosa jingine kubwa ambalo wana wa Mungu wamekuwa wakilifanya. Wengi wana mahitaji mbalimbali.Wapo watu wengi ambao kweli wanaomba kwa kumaanisha mbele za Mungu na wengine hata kufunga kwa masaa mengi lakini tatizo lao katika fahamu zao wameshafanya uamuzi wa nini watafanya baada ya maombi yao.sasa hata Mungu akikushirikisha mawazo yake si rahisi ukamwelewa kwa sababu tayari kwenye nafsi na ufahamu wako kuna jibu na Biblia inasema Aonavyo mtu katika nafsi yake ndivyo alivyo.

Sambamba na hilo, kosa linalofanana na hili ni wale watu wanaomwomba Mungu afanye kama vile wao waonavyo kataka nafsi zao. Yaani wanamtaka Mungu akubaliane na Mawazo yao na njia zao juu ya shida au haja walizo nazo wao wenyewe.

Na jambo hili tunalielewa vizuri tunaposoma katika Kitabu cha Luka 9:12 -17 .Habari za wanafunzi wa Yesu pindi njaa ilipokuwa ikiwauma watu wakati Yesu anaendelea na mkutano. Wao walimwambia Bwana waage watu wakajijinunulie chakula vijijini na mashambani, wao walidhani hili ndilo jibu la njaa ya watu. Hawakufikiri kwamba sio wote wenye pesa za kununua chakula, Kuwaaga watu kungemaanisha Yesu aache kufundisha nk. Sasa jibu la njaa ya wale watu halikuwa kama wanafunzi walivyowaza na walivyotaka bali jibu lilikuwa kwa Yesu kufanya muujiza wa kubariki mikate mitano na samaki wawili vitosheleze watu wote 5000.

Sasa baada ya kuwa tumeona hayo makosa makubwa matatu tuangalie Mungu anaposema nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza ana maana gani?.

Katika mstari huu kuna mambo makubwa matatu yamezungumziwa.


Moja ni MTANIITA,mbiIi MTAKWENDA NA KUNIOMBA, tatu ni NAMI NITAWA

SIKILIZA.
Jambo la kwanza ni ,
Mtaniita.
Ukisoma kitabu cha Yeremia 33:3 anasema “Niite,nami nitakuitikia ,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua. Mungu ansema utakapomwita yeye atafanya mambo mawili.Moja atakuitikia na mbili atakuoyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua.

Maana yake ni hii, kukuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua ni kukufunulia mambo ambayo ulikuwa huyajui katika lile ulilomuita.Hivyo basi kumuita Mungu ni kumuomba au Kumtaka Mungu akufunulie mambo makubwa na magumu usiyoyajua kuhusu shida au hitaji au haja uliyonayo mbele zake. Mfano unamuita Mungu akufunulie ndoa yako jinsi ilivyo, nini kinaendelea usichokijua, nini ukiombee, nini hakijakaa sawasawa kwenye hiyo ndoa k.
 Hivyo basi unapotaka kuomba juu ya jambo lolote lile ni vizuri kwanza ukamuita Mungu juu ya hilo jambo.Maana yake muombe Mungu akupe picha kamili ya hilo unalotaka kuliombea,akufunulie jinsi lilivyo ili ujue uanzie wapi kuomba.,kama ni ndoa,nchi,mke au mme mtarajiwa,Huduma yako nk.


Jambo la pili 
Mtakwenda na kuniomba.
Sasa baada ya kuwa umemuita Mungu kinachofuata ni kwenda na kumuomba Mungu. Anaposema mtakweda na kuniomba ana maana mtaanza kuomba sawasawa na vile nilivyowaonyesha au nilivyowafunulia wakati mliponiita katika haja zenu.Hivi ulishawahi kujiuliza ni mambo gani makubwa na magumu ambayo Mungu atakuonyesha_pindi utakapomuita?. Kumbuka tulikotoka tumeona Kumuita Mungu ni kumfanya Mungu akufunulie mambo usiyoyajua kuhusu hitaji lako ili ujipange vizuri kuyaombea.

Sasa kwenda na kuomba maana yake ni kuomba sawasawa na vile Mungu alivyojifunua kwako kuhusu hitaji ulilonalo.Utakapoomba namna hii ndiko kunaitwa kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu maana yake unaombea mambo ambayo Mungu anataka uyaombee kwa wakati huo. Kwa lugha nyepesi jifunze kuomba mambo ambayo Mungu anakuongoza kuyaombea. Labda nitoe mifano michache ndio somo litaeleweka vema.

Mfano wa kanza huenda mnaombea mgonjwa au mtu aliyefungwa na mapepo. Ni kweli Biblia imesema mtaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya. Sasa si kila mgonjwa ni wa kuweka mikono na kuanza kukemea ugonjwa au mapepo, kuna magonjwa mengine yanasababishwa na mawazo yaani tatizo ni mtu mwenyewe, Mwingine huenda ni kwa sababu ya kujeruhiwa nafsi yake na mwingine huenda ni kwa sababu ya dhambi, na mwingine huenda mikataba aliyoingia mwenyewe na mapepo na huenda mengine ni Mungu mwenyewe ameruhusu Shetani aguse afya ya huyo mtu kama alivyomruhusu shetani kwa Ayubu nk..

Saa nafikiri mpaka hapa umeshaona si wagonjwa wote utakawawekea mikono watapona. Hivyo ni vema umuite Mungu akufunulie nini cha kufanya, mwingine atakuambia huyu anahitaji ushauri tu wala si maombi,mwingine anaweza kukuambia huyu ametenda dhambi hii na hii akizitubia nitamponya, na mwingine atakuambia huyu hicho ni kipimo chake mpe tu neno la uvumilivu na Ushindi,Mwingine atakuambia huyu ndugu mwenyewe au wazazi wake waliingia mkataba na mapepo hivyo vunja kwanza mktaba huo nk.

Mfano wa pili,huenda mnaombea kanisa lenu. Ni rahisi kusema tumuombe Mchungaji ndani ya kanisa,mara tuombee kamati ya ujenzi tuombe Mungu kuhusu ujenzi nk.Kweli ni maombi mazuri lakini una uhakika Mungu kwa wakati huo anataka muombee hayo mambo.Huenda kuna roho ya mpinga Kristo ina vamia washirika au kuna maajenti wanajiingiza kwa siri makanisani na kuwapofusha macho ninyi mnakazana kuombea ujenzi. Maana yangu ni hii ikiwa wewe ni mchungaji au kiongozi wa maombi katika kundi lolote lile ni vema kila wakati kumuita Mungu akupe mambo ya kuombea kwa wakati huo. Mungu atakufunulia nini unachotakiwa kuombea kwa wakati huo.

Nina ujasiri na ninachokisema kwa sababu siku moja tukiwa katika kambi la vijana.Nilikuwa kwenye timu ya maombi ya hilo kambi.Ndani ya hiyo timu tulikuwa na wajumbe wa shetani kutoka kuzimu yaani maajenti (vibaraka wa shetani).Hawa jamaa walikuwa wakiomba na kufimga kuzidi masaa yale tuliyokuwa tukifunga sisi.Na wakati wa kuomba walikuwa wanapendekeza tuombee na kukemea roho ambazo hazifanyi kazi katika lile eneotulilokuwepo. Na walikuwa wanajita watumishi wa Mungu.Nina uhakika wa habari hii kwani Mungu alinifungua macho tukaomba na nguvu za Mungu ziliposhuka mmoja wo akasema “sisi ni wajumbe wa shetani kutoka kuzimu,tulitumwa kuleta uharibifu lakini katika yale tuliyotumwa tumeshindwa kuyatekeleza”.

Nakuambia tangia siku hiyo ndipo nilipofunguka macho yangu ya ndani na kuanza kuhitaji uongozi wa Mungu katika yale tunayoomba kila siku.Hujawahi kuona Kiongozi wa maombi anasema jamani hee tutaombea hili na hili na hili,lakini mnapoanza kuomba unakuta Mungu anakuongza kuombea vitu vingine kabisa ?

Kumbuka siku zote katika kila unaloliomba ,mwambie Mungu nifunulie zaidi kuhusu mambo ya kuomba kuhusu hili jambo.lwe ndoa,kanisa,mkutano au semina,Watoto,elimu nk Sasa nimalizie kwa kusema kuomba kwa namna hii ndiko Kibiblia kunaitwa kumtafuta Bwana.Sikiliza huwezi kumtafuta mtu mahali asikopatikana.Unapomtafuta Bwana ni lazima umtafute kwenye maeneo yake yaani kule anakopatikana.Sasa kunaitwa kumtafuta Bwana kwa sababu umeomba kulingana na ufunuo wake

Ni imani yangu kuwa baada ya kuwa umesoma ujumbe huu basi naamini umeshapata maarifa ya kukusaidia katika kumtafuta Bwana na hivyo kwa jambo lolote utakalotaka kuomba siku zote utaomba kwanza ufunuo wa Mungu juu ya hili jambo.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nawe.
Na: Patrick Samson Sanga

JIFUNZE KUMILIKI MAJIBU YA MAOMBI YAKO

Yoshua 13:1-7
Utangulizi,
Katika dunia ya leo watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao mwingi ikiwa ni pamoja na kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuomba Mungu awabariki, awaponye, awalinde kwa kifupi awajibu mahitaji yao waliyonayo mbele zake siku zote. Wapo waliokuwa hawazai wamezaa, vipofu wameona, wasioajiliwa wameajiliwa, biashara za wengi zimefanikiwa, ndoa nyingi Mungu ameziponya, wapo waliotaka kuolewa au kuoa na Mungu amewapa waume na wake wazuri.
Sasa hao hao watu ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika kuomba Mungu awatendee miujiza katika maisha yao, imefika mahali wanaona yale ambayo yalikuwa ni majibu ya Moambi yao shetani ameyavamia na kuleta balaa zaidi na limekuwa pigo kubwa sana kwa wana wa Mungu. Na kwa sababu hiyo wamejikuta wakimlalamikia Mungu kama vile wana wa Israeli na imefika mahali pa wengine kuona kama Mungu hawezi na hivyo kumuacha.
Tatizo la haya yote ni kwamba wakristo wengi hawana tabia ya au mazoea ya kumiliki mujibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Huenda ulikuwa huna mtoto na Mungu amekupa kuzaa mtoto, sasa huyo mtoto ndiyo jibu lenyewe kutoka kwa Mungu. Sasa ni lazima ujifunze kumiliki huo muujiza wa mtoto, sasa si mtoto tu bali ni pamoja na ajira, ndoa, uponyaji, kanisa, Nchi, Biashara nk.

NINI NI MAPENZI YA MUNGU KWA MWANADAMU?

Mathayo 7:21 inasema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”
Naamini kabisa kama kweli wewe unahamu ya kuingia katika ufalme wa Mungu basi ni lazima utataka kujifunza yapi ni mapenzi ya Mungu kwako ili uyatende na uweze kuurithi uzima wa milele. Yesu anasema si kila mtu, sio watu, bali mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa Baba.…………kwa lugha nyepesi maana yake wapo wengi wenye kusema Bwana Bwana lakini hawataurithi ufalme wa milele kwa sababu ya kutotenda mapenzi ya Mungu.
Hivyo basi kwa sababu si kila mtu, aniambiaye………….., maana yake kwa kila mtu chini ya jua kuna mapenzi ya Mungu ya kutekeleza, na mapenzi ya Mungu maana yake ni yale ambayo Mungu anataka watu wake wayatende . Sasa lengo au shabaha ya ujumbe huu ni kujibu swali letu kwamba nini ni mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu na hivyo kukupa maarifa yatakayokusaidia kuyajua mapenzi ya Mungu katika maisha yako .
Baada ya kuwa nimemuomba Mungu anijulishe na kujifunza zaidi kuhusu mapenzi ya Mungu nilipata maarifa yafuatayo kuhusu mapenzi ya Mungu, Mapenzi ya Mungu unaweza kuyagawanya katika makundi makubwa mawili kama ifuatavyo;
(a) Ni mapenzi ya Mungu uongozwe na Roho Mtakatifu.
Ukisoma 1Wakorinto 12:3 Biblia inasema “kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema Yesu amelaaniwa wala hawezi mtu kusema Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu sasa ili uelewe vizuri soma kwanza mistari hii katika Isaya 46:9-10 ; “ Kumbukeni mambo ya zamani za kale, maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado nikisema , shauri langu litasimama , nami nitatenda mapenzi yangu yote” unaweza ukarudia tena kusoma hiyo mistari ndiyo tuendelee.
Mungu anasema yeye ndiye autangazaye mwisho tangia mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka. Maana yake ni hii Mungu anakujua vizuri kuliko unavyojijua. Pia tayari Mungu anayo ratiba kamili ya maisha yako tangia ulipozaliwa. Na anajua kwa nini alikuumba na anao wajibu au kusudi ambalo anataka ulitekeleze, na hii ina maana haukuzaliwa kwa bahati mbaya.
Sasa ili uweze kulitumikia kusudi/shauri la Bwana katika kizazi chako unatakiwa uongozwe na Roho Mtakatifu. Maana katika zaburi 32:8 anasema “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, nitakushauri jicho langu likikutazama’.
Mimi sijui kusudi la Mungu kwako ni nini?, ila ninachojua kwa mujibu wa Biblia kila mmoja ana wajibu wa kuutekeleza. Na Roho Mtakatifu ndiye mwezeshaji wa wewe kutekeleza huo wajibu uliopewa na Mungu chini ya jua. Ikiwa ni huduma, siasa, utawala, ofisi, biashara n.k. Anaposema nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea maana yake katika mambo ya rohoni na hata ya mwilini, Roho Mtakatifu atakuongoza kuyatenda yale ambayo ni mapenzi ya Mungu. Maana katika warumi 8:14 anasema ” kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho Mtakatifu hao ndio wana wa Mungu”.
Sasa kama hauongozwi na Roho Mtakatifu katika kulitumikia shauri / kusudi la Bwana katika maisha yako ya kiroho au kimwili maana yake unaongozwa na roho nyingine ya dunia hii ambayo nia yake ni mauti. Na mtu wa namna hii hata akitoa unabii au pepo kwa jina la Yesu atakataliwa maana anafanya hayo kwa kujikinai siyo Mungu Roho Mtakatifu anayemuongoza.
(b) Ni mapenzi ya Mungu ulitendee kazi neno lake.
, Warumi 2:13 inasema “Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki“. Tazama, haki ya kuurithi ufalme wa Mungu haiko kwa wale waliosikia au kusoma kwamba tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu kwa maana hapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao.Bali haki ipo kwa wale ambao siku zote wanatafuta kuwa na amani na watu wote na pia wale ambao wanaishi maisha ya utakatifu . Yakobo 1:22 inasema “Lakini iweni watendaji wa Neno wala si wasikilizaji tu, hali mkijidangaya nafsi zenu”. Neno la Mungu ni jumla ya mawazo na njia za Mungu kwa wanadamu za kuwasaidia kuishi katika mpango wa Mungu.
Limebeba mapenzi ya Mungu, hukumu, amri, mafunuo na maagizo ya Mungu kwa mwanadamu. Sasa kwa mfano imeandikwa usiue, usizini sasa si yule anayesikia kwamba usiue,au usizini ndiye anayehesabiwa haki bali ni yule asiyeua wala kuzini. Kushindwa kulitendea kazi Neno la Mungu ni kushindwa kuyatenda mapenzi yake maana hayo mapenzi yake yamebebwa kwenye neno la Mungu.
Anaposema enendeni kwa Roho, halafu wewe unaendenda kwa mwili na unajua nia ya mwili ni mauti ,Je unategemea kuurithi uzima wa milele? Kwa lugha nyingine na nyepesi maana yake ni mapenzi ya Mungu tuwe na imani yenye matendo. Ukisema nakiri na kuamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka ili niokolewe, maana yake unatakiwa kutekeleza yale ambayo Yesu anakuagiza maana Imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo.
Hebu soma habari hii. Yakobo 2:14 –26 Mstari wa 14 unasema “Ndugu zangu yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je ile imani yaweza kumwokoa? Na ule wa 24 unasema “Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa na haki kwa matendo yake, si kwa Imani peke yake”.
Kumbuka imani inafanya kazi pamoja na matendo yake, yaani kwa kushirikiana na matendo yake. Uzao wa Imani ni – kile ulichosikia (ulichoamini) + matendo yake.
Imani yeyote ile, iwe ni ya Mungu kukuagiza kufanya jambo fulani au iwe ya wewe kuiumba ina matendo yake. “Yakobo 2:22” . Ukitenda kinyume cha hayo matendo yake hautafanikiwa. Mfano:- kama Ibrahimu angemtoa sara kuwa dhabihu kwa Mungu asingehesabiwa haki na kuwa rafiki wa Mungu . Tendo la Imani ya Ibrahimu ilikuwa ni kumtoa Isaka. Ndiyo maana Mungu alimhesabia haki.
Mapenzi ya aina yeyote ile ya Mungu kwako yamebebwa katika makundi mawili niliyokutajia. Hivyo jifunze kutulia na kusikiliza uongozi wa Roho Mtakatifu na kisha pili ujifunze kutendea kazi yale ambayo Mungu amesema katika neno lake.
Mtu afanyaye hayo hakika hatakosa kuurithi uzima wa milele. Maana yeye mwenyewe amesema katika Zaburi 32:8 kwamba “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, nitakushauri jicho langu likikutazama”. Sasa akikufundisha na kukuonyesha njia Yesu maana yake anakuongoza katika njia ya uzima maana yeye alikuja ili uwe na uzima, kisha uwe nao tele Yohana 10:10.
Neema ya Bwana Yesu na iwe nawe siku zote.
Na;Patrick Samson Sanga.

KWA NINI MUNGU ANATAKA TUENENDE KWA ROHO?

Ukisoma katika warumi 8:14 Biblia inasema “kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” na pia Paulo kwa wagalatia anasema” Basi nasema Enendeni kwa Roho,wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili Wagalatia 5:16.
Hapa tunaona jinsi Paulo anavyosisitiza kwa makanisa ya Rumi na korinto kuhusu suala zima la kuongozwa na Roho Mtakatifu. Anawaambia warumi kwa kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu maana yake haijalishi ana umri gani, ni wa dhehebu gani, jinsia gani maadamu anaongozwa na Roho wa Mungu huyo ni mwana wa Mungu na bado anawaagiza wagalatia akisema Basi nasema enendeni kwa Roho………….. anaposema enendeni maana yake mkiongozwa na Roho, au mkimfuata Roho katika yale anayowaagiza. Maneno haya yanaonyesha zipo sababu za msingi kwa nini tunatakiwa kuongozwa na Roho sasa hapa sizungumzii kazi za Roho mtakatifu najua zipo kazi nyingi anazozifanya Roho Mtakatifu lakini mimi nazumgumzia sababu za kuongozwa na Roho Mtakatifu, ambaye ndio agano jipya la Mungu kwetu (Yeremia 31:31) katika hiyo Yeremia Neno linasema “Angalia siku zinakuja asema Bwana nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israel. Sasa ukiendelea kusoma mistari inayofuata utaona anazungumzia habari za kutia sheria yake katika mioyo ya watu.
Sasa hili ndilo agano jipya la Mungu pamoja na wanadamu. Sasa usipojua kwa nini unatakiwa kuongozwa na Roho na siyo akili zako, au mazoea, au taratibu za kwako n.k. hautajua umuhimu wa kuongozwa na Roho Mtakatifu na pili hautaona sababu za kuongoza na Roho Mtakatifu. Sasa lengo la ujumbe huu ni kukufundisha sababu za msingi za kwa nini unatakiwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na siyo akili zako au mawazo yako. Sasa baada ya utangulizi huo mfupi na tuangalie sababu hizo za msingi.
Moja,
Ili tusizitimize tamaa za mwili wagalatia 5:16
“Basi nasema enendeni kwa Roho , wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.Tunatakiwa tuenende kwa Roho ili tusizitimize tamaa za mwili. Siku zote mwili na Roho ni maadui nia ya mwili ni mauti na nia ya Roho ni uzima na amani (Warumi 8:7). Maana yake siku zote mwili utakuongoza kufanya mambo ambayo mwisho wake ni mauti ya kiroho na hata kimwili pia.
Utakuongoza katika tamaa zake, sasa usipoongozwa na Roho huwezi kujizuia kutekeleza tamaa za mwili na kwa sababu hiyo wewe si mwana wa Mungu na mtu wa namna hii hataingia mbinguni kamwe. Katika 1Wakorinto 6:9-10 anasema “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanyanyike, waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala walevi, wala watamanio, wala walevi wala watukanaji, wala wanyang’anyi.Sasa utakapoongozwa na Roho Mtakatifu utaratibu wake utakuacha huru mbali na hayo mambo ya mwili au nia ya mwili na utakuongoza katika uzima na amani na kulitenda tunda la Roho ambalo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu utu wema , fadhii, uaminifu, upole na kiasi “Wagalatia 5:22-23”.
Mbili,
Ili tupate kuyaelewa mafumbo ya Mungu na kuyafasiri mambo ya Rohoni kwa maneno ya Rohoni.
1Wakorinto 2:10 inasema “ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote hasa mafumbo ya Mungu” na ule mstari wa 13 unasema “ Nayo twayanena , si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya Rohoni kwa maneno ya Rohoni. Hapa najua walio wachungaji, walimu wa neno la Mungu au viongozi wa vikundi mbalimbali vya kiroho watanielewa zaidi.
sikiliza Roho Mtakatifu ndiye mwenye uwezo wa kuchunguza kilichopo kwenye ufahamu wa Mungu kuhusu wewe, ndoa yako, kanisa lako, biashara yako, masomo yako, nchi yako n.k. sasa akishachunguza ndiyo anakujulisha maana wewe ulikuwa hujui. Pia Roho Mtakatifu ndiye anayekusaidia kuyanena, kuyafundisha au kuyafafanua maneno ya Mungu kwa watu wake, anaposema kuyafasiri maana yake kuyafundisha mambo ya Rohoni kwa jinsi / namna ya Rohoni.
Hivyo kama wewe ni kiongozi au mwalimu wa neno la Mungu, ukiongozwa na Roho, yeye atakuongoza / atakusaidia kuwafundisha hao watu neno la Mungu kwa jinsi ya Rohoni yaani kwa mfumo wa Rohoni kulingana na watu ulio nao, maana yeye ndio mtunzi wa hilo Neno,soma mwenyewe 2Petro 2:21” maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Tatu,
Ili tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu na kuyapokea mambo ya Roho na Mungu .
Iwakorinto 2:12 inasema “Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu” na ule wa 14 unasema “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya Rohoni. Unapoongozwa na Roho Mtakatifu ndipo anapokusaidia kujijua wewe mwenyewe vizuri. Anaposema upate kuyajua yale ambayo Mungu amekupa katika maisha yako.Roho mtakatifu atakusaidia kujua aina ya vipawa ulivyonavyo, karama za Rohoni ulizonazo, huduma ulizonazo kama umeitwa huko, atakusaidia kujua vizuri unaweza kufanya nini na nini huwezi, kipi ufanye na kipi usifanye, atakusaidia kujua baraka zako za kiroho na kimwili pia. Kwa kifupi atakusidia kulijua kusudi la Mungu katika maisha yako na vipi ufanye ili uweze kulifikia hilo kusudi na zaidi atakupa upako/ nguvu za kuweza kuyapokea yale yote anayo kuagiza ili uweze kulifikia kusudi lake kwako na kuzirithi baraka zako maana katika zaburi 32:8 anasema “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoienda nitakushauri, Jicho langu likikutazama”.
Nne,
Ili atusidie kuomba yale tunayotakiwa kuyaomba kwa wakati huo.
Warumi 8:26” kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa”. Udhaifu unaozumgumziwa ni wa namna mbili moja si rahisi kwa jinsi ya mwili kuomba kwa muda mrefu kwa sababu mwili ni dhaifu na pili udhaifu tulionao ni kushindwa kuomba jinsi inavyotupasa kuomba.
Sasa tunapoongozwa na Roho, maana yake moja anatusidia tuweze kuomba na zaidi anatufundisha namna ya kuomba na kutuongoza yapi tuyaombee kwa wakati huo au kipindi hicho. Mfano wewe unaweza ukawa unaomba upako wa Roho Mtakatifu katika huduma na yeye Roho Mtakatifu, anajua kwamba ameshakutia mafuta na shida uliyonayo ni kutokujua namna ya kushirikiana na upako wake ulio juu yako. Hivyo yeye atakuongoza kuomba kwa habari ya kushirikiana na upako aliouweka juu yako. Kwa kifupi yeye kwa sababu ndiye mwenye maisha yako atakuongoza siku zote kuomba yale unayotakiwa kuyaomba kwa majira hayo iwe kuhusu masomo, ndoa, kanisa, nchi n.k.
Tano,
Ili atuongoze katika kufanya maamuzi.
2Wakorinto 3:17 Basi Bwana ndiye Roho, walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru” pia ukisoma warumi 8:1-2 inasema “sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti” kufanya maamuzi ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Yapo maamuzi mengi sana ambayo mwanadamu anatakiwa kufanya na hawezi kukwepa kuyafanya.
Sasa Mungu kwa kulijua hilo ametupatia Roho Mtakatifu ili atusaidie katika kufanya maamuzi. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana kwako, yaani mtawala, kiongozi ndipo anapokupa uhuru juu ya kufanya maamuzi katika maisha yako. Maana yake ulikuwa hujui nifanye nini? Niamueje ? Sasa yeye anakuletea uhuru ndani wa kufanya jambo ambalo anajua ni la mafaniko kwako. Kumbuka siku zote nia ya Roho ni uzima na amani.
Huenda ziko sababu nyingi ni kwa nini unatakiwa uenende kwa Roho, lakini hizi tano ndizo Mungu alizonipa tuweze kushirikiana kujifunza. Ni imani yangu kwamba utakapoamua kutaka na kupenda kuongozwa na Roho ndipo utakapoona Mungu akijifunua kwako .
Tuendelee Kuombeana
Na; Patrick Sanga.

Tuesday, November 24, 2015

MAMBO SITA YANAYO SABABISHA MAELFU YA WATU WA AINA MBALIMBALI KUINGIA KWENYE VIFUNGO VYA NGUVU ZA GIZA


1. Wapo waliopata watoto kwa njia za ushirikina
2. Kukubari huduma za kishirikina
3. Kuzindika nyumba
4. Matumizi ya hirizi na baadhi ya vifaa vya ushirikina
5. kuhuzuria au kuishi maeneo yenye utawala wa kipepo
6. Wengine majina yao yamewaingiza kwenye vifungo

Kwa kurithi watoto wengi wanao zaliwa kwenye familia ambazo kuna mambo ya uchawi au wanaabudu mizimu na kufanya mambo ya matambiko huwa wanatolewa kwa pepo au mizimu wangali bado wadogo kadri wanavyoendelea kukua ndivyo wanavyoendelea kuona kama mambo yanayo fanyika ni sahemu halali kwa maisha yao. Nakumbuka safari moja tukiwa kilimanjaro tulifanya huduma na kijana mmoja wa kidato cha pili aliyekuwa amefungwa na nguvu za giza , na tukiwa tunafanya nae maombi alitapika vitu fulani vyeupe vya kushangaza sana. Baada ya kufunguliwa na Bwana Yesu na yale mapepo kumuachia tukapata nafasi ya kukaa nae na kuzungumza nae, alitueleza kuwa yeye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kwenye familia yao na kuwa amekuwa akipelekwa kwenye makaburi na kufanya matambiko na wazazi wake kuanzia akiwa mdogo na akaeleza kuwa alikuwa akilishwa vyakula kama nyama za aina fulani kila alipofika makaburini kwa tambiko, sasa hii ina maana kama Bwana Yesu asinge mfungua angeendelea kuishi maisha ya ushirikina chini ya utawala wa nguvu za giza.namna watoto wanavyoingizwa kwenye vifungowazazi wengi wasio amini huwaingiza watoto wao kwenye vifungo vya ushirikina bila ya wao kujua. watoto wengi wakizaliwa hupelekwa kuchanjwa chale, kwa waganga wa kienyeji au wengine hupelekwa kwa Bibi zao kwa ajili ya mambo fulani ya kimira kama kuzika kitovu, kwa taratibu za kimila, kupewa jina chini ya taratibu za kiganga, zipo sara mtoto anaombewa kwa babu zake waliokufa wakati mwingine hizi sara hufanyika makaburini ‘mfano wa sara inayoombwa { mtoto wenu amekuja, mumkumbuke, mumsaidie, tunawakabidhi ni wa kwenu, maneno mengi sana yanatamkwa mara nyngi nkuwa kwa kiluga bila hata ya wao kujua ni nini wanafanya katika ulimwengu wa roho, kumbe katika ulimwengu wa roho yule mtoto anakabidhiwa chini ya falme na mamlaka za giza} Na ndio sababu ukisoma Kumb 18 :10 utakuta anasema Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au Binti yake kati ya moto’ ukiendelea mbele kidogo utakuta anasema ‘wala asionekane mtu aombae wafu sasa u mstari 12a utakuta anasema ‘kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana’Wakati fulani tukiwa na huduma mkoa wa Tanga nilipata nafasi ya kupita mitaani watu wanako ishi asilimia kubwa ya watoto nilio waona walikuwa wamevishwa Hirizi, na vitambaa vyeusi mikononi, shingoni,kwenye miguu wengine walikuwa wamevishwa shanga viunoni, japo hii aina maana mambo haya yako huko tu isipokuwa niliguswa sana nikiwa huko cha kushangaza leo hii hata wakristo wengi wamevalisha watoto wao hivyo vitu, wengine ukiwauliza hata yeye mzazi hajui kwa nini kamvalisha mtoto hicho kitambaa cheusi wengine ukiwauliza atakuambia Bibi yake alimvalisha.

Kwa kushiriki mambo ya uchawi na ushirikina wapo wakristo wengi leo hii ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha na mambo ya uchawi na ushirikina bila ya wao kujua mfano kuchangia tambiko, kuhudhuria ibada za wafu, kula nyama za kusongolewa, kunyoa nywele kwa ajili ya aliyekufa, kunywa dawa za kimila, kwenye misiba mingi ambayo watu huamini mambo ya ushirikina huwa wanakunywa Dawa wanafamilia au ukoo mara baada ya mazishi au msiba kuisha . lakini

Biblia imesema wazi kabisa kuwa ‘msishiriki ibada zao’ na ukisoma katika Kumb 14 :1 utakuta anasema ‘msifanye upaa kwa ajili ya aliye kufa.’ Sasa ni muhimu ukafahamu kuwa haya ni moja ya mambo yanayoingiza maelfu ya watu kwenye vifungo

1. Wapo waliopata watoto kwa njia za ushirikina

MASHAMBULIZI KUTOKA ROHO WAOVU






Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, nao hawakushinda, wala mahala pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na shetani, audanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye… kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari. Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu (Ufunuo 12:7 – 12).
Shetani hayuko hapa duniani kucheza. Yuko kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kwa hali na mali wewe usiingie mbinguni. Yeye anayo kazi moja tu, ya kupigana na wewe na akushinde. Yeye halali. Akikushindwa leo kesho anatafuta mbinu nyingine. Hivyo yako mashambulizi makali ya shetani, roho waovu mapepo na majini.
Mtu wa Mungu huwezi kuyashinda mashambulizi ya shetani bila kujifunza mbinu zake anazozitumia na huwezi kumshinda bila ya wewe kujifunza upiganaji. Wakristo wengi wameshindwa vita hii japokuwa bado wanaenda kanisani.
Baada ya mtu kuokoka, hupata passport ya kwenda mbinguni. Sambamba na passport hiyo Mungu humpa nguvu, uweza na mamlaka ya kumwezesha kupigana na shetani na kumshinda. Hivyo mkristo anatakiwa ajipiganie yeye mwenyewe na ashinde. Yesu ameshakupa passport ya kwenda mbinguni, hivyo ipiganie hiyo nafasi ili shetani asikumyang’anye, usipojipigania utaikosa mbingu.
Lakini pamoja na hayo, kuwa na nguvu, uweza na mamlaka, bila ya kuwa na ujuzi wa hali ya juu wa kuvitumia ni kazi bure kuwa navyo. Hili ndilo tatizo la wakristo, wanazo nguvu, uweza na mamlaka lakini hawajui mbinu ya kuvitumia. Ni sawa na raia asiyepitia mafunzo ya kijeshi, umpe mzinga, ndege ya kivita, n.k akapigane vita.
Shetani hushambulia kupitia njia kuu mbili. Njia ya kwanza ni kupitia roho waovu walioko ndani ya wazazi, na mababu zetu. Baada tu ya mtu kuzaliwa roho waovu walioko ndani ya wazazi na mababu huingia ndani ya mtu. Hii ni njia ya mapokeo, tunapokezana kutoka kwa wazazi. Wazazi walipokea kutoka kwa mababu. Hawa roho waovu tumeishi nao muda mrefu, hivyo wametutumikisha sana, sasa tumezoea kutumikishwa nao, maana wamekuwa nasi tangu kuzaliwa. Roho waovu hawa hata mtu baada ya kuokoka huendelea kumfuatafuata tu. Ni lazima wakufuate maana wamekuwa ni rafiki wa ukoo na familia yenu. Kama hutajua jinsi ya kupigana na hawa roho waovu wa mapokeo ni razima wakushinde tu. Hawa roho waovu wa mapokeo unaweza kuwashinda kwa kujifunza laana na kuivunja. Bila kuijifunza laana na kuivunja ni lazima wakushinde. (soma kitabu changu kiitwacho, ULIIVUNJA LAANA ULIPO AMINI?

JE NGUVU ZA GIZA ZIPO?

Wapo watu wachache ambao huwa hawaamini habari za utendaji wa nguvu za giza,. na wengine huamini kuwa wakisha okoka hawahusiki tena, na mambo yanayohusu nguvu za giza kitu ambacho si kweli, Je umeshawahi kujiuliza kwa nini Bwana Yesu kabla hajaondoka alituombea maombi haya Yoh 17 : 15 ‘Mimi siombi kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu’ ikiwa Bwana Yesu aliomba tulindwe na yule mwovu, hii inamaana kuwa alijua fika utendaji wa ibilisi na jinsi amabavyo maisha yetu yalihitaji ulinzi wa Mungu usiku na mchana. Na ndio sababu ukisoma ule mstari wa 12 ‘a’ anasema ‘nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa nikawatunza,,,,,’ unaweza ukaona jinsi ambavyo Bwana Yesu aliona umuhimu wa sisi kutunzwa, au kulindwa na ndio sababu alipokuwa akiondoka akaomba kwamba tulindwe na yule mwovu, hii ina maana kuwa alikuwa akitambua fika vifungo na manyanyaso ya Adui ambayo yalikuwepo ulimwenguni na ukiendelea kusoma ule mstari wa ‘20’ utakuta akiwaombea na wengine watakao amini au watakao okoka baadae yaani wewe na mimi tulioamini leo hii.na wengine wanao endelea kuamini anaseama ‘Wala si hao tu ninao waombea ;lakini na wale watakao amini kwa sababu ya neno lao’
Ukisoma katika ‘ Waefeso 6 :12’ anasema ‘kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama ;bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho’ Mtume paulo alipokuwa akiandika walaka huu alitaka tufahamu kuwa kushindana kwatu, au kwa tafsiri nyingine tungeweza kusema kupambana kwetu si kwa vita za mwilini isipokuwa ni juu ya falme na mamlaka za giza, moja ya tafsiri za kiingereza imetafsili hivi ‘against powers’ maana yake dhidi ya nguvu mbalimbali za kuzimu falme za nguvu za giza inaweza kuwa na maana {Utawala wa ibilisi ambao chini yake kuna mapepo, majini pamoja na na vinyamukela vya kuzimu } huko ndiko tunakotakiwa kupeleka mashambulizi yatu, tena akaendelea kusema juu ya wakuu wa giza hili maana yake watawala wa giza { ambao ni wachawi, washirikina, na waganga wa kienyeji } akaendelea kuelezea jinsi amabvyo tunatakiwa kupambana dhidi ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Sasa akisema majeshi ya pepo wabaya uelewe hivyo hivyo majeshi maana kuna maelfu na maelfu ya mapepo ambayo yanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha yanavuruga mipango mizuri ya Mungu kwenye maisha ya watu
Sasa hii inaweza kukupa kuwa na hakika kuwa nguvu za giza zipo na kuwa unahitaji kujipanga kwa maombi kila wakati ili kukabiliana nazo.
`
Hivyo basi ni muhimu kuamini tu kuwa nguvu za giza zipo na zina nguvu na kuwa zinatenda kazi Duniani mchana na usiku na hii sasa ndio sababu kuna vitu vinaitwa [vifungo vya nguvu za giza} {maagano ya mizimu} mambo ya uchawi na ushirikina, watu kuhangaika na mambo ya kuagua ,kutambika mizimu, ibada za wafu, na mengineyo mengi
Na mambo haya ndiy’o yanayosababisha maisha ya vifungo kwenye maisha ya watu wengi
Nakumbuka nikiwa na fanya huduma ya ukombozi katika mkoa fulani na Dada mmoja aliyekuwa amepagawa na roho za giza, tukiwa katika maombi zile roho za giza zilianza kupiga kelele zikieleza ‘Mama yake alitukabidhi huyu tumtunze alipozaliwa , tumemuoa, ni mke wetu, huwa tunakuja saa nane usiku tunafanya nae tendo la ndoa, hatuwezi kumuacha tumetoka nae mbali {yaani hujawahi kuona roho za giza zikilia kwa uchungu na kumngangania mtu,} haikuwa rahisi sana maana huyu Dada alikuwa chini ya mikataba mikubwa ya nguvu za giza, alikabidhiwa na mama yake pasipo ya mama yake kujua, Asante kwa Yesu aliyetupa mamlaka yote Mbinguni na Duniani maana kwa jina lake yule binti alifunguliwa, ndugu unayefuatilia mafundisho haya tunapoendelea na mafundisho haya utazidi kujua namna watu wanavyoingia kwenye vifungo na jinsi unavyoweza kumuingiza mwingine pasipo ya wao kujua.
----Siku moja mara baada ya kufundisha somo hili katika kongamano la wanafunzi wa sekondari na vyuo Dada mmoja alinieleza jinsi alivyoanza kumpenda sana kaka fulani bila hata ya yeye kujua kwa nini alimpenda kiasi kile, anasema gafra alikuwa hawezi tena kusoma na kuelewa darasani, kiasi kwamba angekuwa teyari kufanya jambo lolote ambalo yule kaka angeamua walifanye, nikamuuliza kama aliwahi kuwa na urafi wowote na yule kaka akasema hapana isipokuwa siku moja walikutana kwenye kongamano fulani la vijana yule kaka alimsalimia yule Dada, na aliposalimiwa anasema hakukuwa na kitu chochote kilichotokea na kuwa hakuwahi kumfikili huyu kaka ila anasema, siku moja kuna nguvu ilimshukia gafra, akajikuta anamkumbuka sana na kumpenda isivyo kawaida ndipo nikamuuliza kama baada ya pale kuna kitu chocho aliwahi kupokea kwa yule kaka ndipo makasema kuna siku tu nilisha ngaa maana aliniletea picha yangu ambayo inaonyesha alinipiga ila sikumbuki alinipiga wapi nilipoipokea tu ndipo hali ilipozidi kuwa mabaya zaidi na baada kuichukua ile picha nilianza kuumwa na kitovu kwa nguvu, hii ni sehemu tu ya ushuhuda kitu nilitamani ukifahamu ni kuwa kama hutatambua kujifunika katiaka ulinzi wa Bwana Yesu kila wakati na kila mahali ni rahisi tu kukamatwa, baadae tukatambua kuwa huyu kaka alipiga hii picha bila huyu Dada kujua na kuipeleka kwa wakuu wa giza ili aweze kumpata kwa kutumia madawa maana yule bint alionekana kuwa na misimamo Ashukuliwe yesu aliye mfungua binti huyu
Kumbuka hili siku zote jitahidi kukaa mkao wa kujilinda kila wakati maana unahitaji msaada wa Mungu siku zote usiku na mchana Biblia imesema wazi kabisa 1yoh 5 :18 ‘twajua ya kuwa kila aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda’ wala yule mwovu hamgusi.
Ni muhimu ukafahamu kuwa unahitaji kujilinda kwa maombi kwa kulisoma neno kwa kukaa makao wa kumuhofu Mungu kila wakati hii itamfanya adui asipate nafasi kwenye maisha yako na ndio sababu Biblia ikasema Yakobo 4 :7 ‘Basi mtiini Mungu. mpingeni Shetani, nae atawakimbia ninyi’ sasa basi kule kumtii Mungu, kutembea na hofu ya Mungu ndiko kunakokutengenezea imani na ujasiri wa kumpinga shetani kwenye eneo lolote la maisha yako nae akukimbie, maana watu wengi leo wameishi maisha ya vifungo tu kwa sababu ya utumwa wa dhambi, na ndio sababu Biblia ikasema 1yoh 5 :14 ‘Na huu ndio ujasiri tulionao kwake ya kuwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,atusikia,,,,,,’ sasa waweza kujiuliza swali kuwa ni kwa nini akaanza na huu ndio ujasiri tulionao kwake, hii ina maana ya kuwa huwezi ukawa na ujasiri wa kusimamia Nguvu za Mungu katika kumpinga ibilisi kama hauja kaa kwa Mungu kwa miguu yote miwili
Mungu awabariki sana,

JE MTU ALIYEOKOKA ANAWEZA AKAVAMIWA NA ROHO ZA GIZA ?

1. Je, anaweza kuwa chini ya vifungo, wakati Yesu alimaliza yote Msalabani?
Ndugu mpendwa unayefuatilia mafundisho haya, kila mahali ambako Mungu amenipa neema ya kufundisha masomo haya ya ukombozi nimekuwa nikiulizwa hili swali.na inawezekana hata wewe unashauku ya kujua mengi kuhusiana na hili,
Mpendwa unayefuatilia mafundisho haya, ni kweli kabisa kuwa hata mtu aliyeokoka anaweza akavamiwa na roho za giza.
Na zika athiri mambo yake, kama biashara yake, uchumi wake, ndoa yake na hata maisha yake kwa ujumla na bado akawa anaenda kanisani, anaomba, anaimba, na kufanya baadhi ya mambo,
Kumbuka adui mkubwa wa ibilisi ni yule aliyempokea kristo, na ndio maana wakati mwingine kuokoka kumetamkwa kama kutangaza vita, mtu aliyeokoka anafananishwa na mtu ambae yuko vitani na kuwa amezungukwa na maadui kila mahali, na kila adui anatamani kama angelimmaliza yeye maana anasababisha matatizo makubwa kwenye ufalme wa adui bila ya yeye kujua.
Watu wengi kwa sababu ya kutokuyasoma maandiko hudhani ya kwamba kuokoka ni kumaliza kila kitu ikiwa ni pamoja na uhakika wa kufika mbinguni na kumbe kuokoka ni kuanza safari ya maisha mapya katika ulimwengu wa mapambano, na ndio sababu Biblia ikasema katika 2kor 10 :12 kwamba ‘kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke, sasa ukiufuatilia huu mstari utagundua Biblia inatutaka tuwe waangalifu, maana Adui ni kama simba aungurumae anaye tafuta mtu apate kummeza, wakati huo huo ukisoma Yakob 4 :7 utakuta anasema ‘basi mtiini Mungu mpingeni shetani nae atawakimbia’ sasa kwa nini Biblia inakutaka umpinge shetani ndipo nakukimbie, hii ina maana usipompinga atakukimbilia wewe.
Ulinzi wa Mungu unakuwa juu ya mtu, tu pale anapokuwa Hodari katika Bwana huku akiutafuta uweza na nguvu zake, Efeso 6 :10 ‘Hatimae mpate kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake’
Nini maana ya kuwa hodari katika Bwana, huku ni kukaa kwenye maombi, kuwa na neno la Mungu ndani yako, kujifunza kuutafuta uso wa Mungu kwenye maeneo Mbalimbali ya maisha yako, kwa kadiri utakavyokuwa ukiendelea katika hali hii ndivyo utakavyo kuwa ukiuona uweza na nguvu za Mungu kwenye maisha yako ukiendelea mstari wa 11 utakuta anasema ‘vaeni siraha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani’ sasa hii inakupa kujua kuwa unatakiwa kupingana na hila za shetani kila siku maishani mwako na hauwezi ukazipinga tu hivi hivi ni mpaka umevaa siraha zote za Mungu, ikiwa ni pamoja na neno la Mungu kujaa kwa wingi ndani yako, kuwa muombaji, na kweli ya Mungu kuwa kwenye maisha yako,
Hii inaweza kuwa moja ya mirango ya adui kwa mtu aliye okoka
Fitina, kule kumfitini mtu au kumsengenya mtu na hauoni shida kufanya hayo, na kule kushindwa kabisa kumtoa mtu moyoni mwako,kushindwa kuachilia,kusamehe, kuendeleza kinyongo, kuacha uchungu uendelee kujaa ndani yako inaweza ikampa ibilisi mrango na ukavamiwa na roho za giza, maana ukiwa kwenye hali hii huna mda wa kuomba, ila unamda wa kulaumu na kunungunika, ikiwa ni pamoja na kujisemea vibaya au kumsemea mwingine.
Kiburi, kule kujaa kiburi na ukaidi, kutokutaka kusikiliza ushauri, kuwaona wengine wote hawana kitu isipokuwa wewe au fulani, na hivyo kutokunyenyekea, wala kushuka kitu ambacho kimesababisha roho za ukengeufu kwa watu wengi leo{uasi} hii imesababisha mirango kwa nguvu za giza.
Tendo la ndoa kabla ya ndoa, au nje ya ndoa kumbuka mtu anapoamua kutoa nguo zake kwa mtu amabaye si mke wake halali, kwa tafsiri ya rohoni anautoa utukufu wa Mungu, au anauvua, hivyo basi anauvua ulinzi, na kwa sababu hiyo Roho za giza zinakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kumvaa mtu huyu
Na ndio sababu watoto wa kuhani heli Hofsini na Finehasi walipofanya uzinzi na wanawake waliokuwa wakitumika malangoni pa hema ya kukutania, utukufu wa Mungu uliondoka, na ulinzi wa Bwana ukaondoka na lile sanduku la agano likatekwa, habari hizi utazipata vizuri samweli wa kwanza na kuanzia sura ya pili, kitu nilitaka uone ni jinsi ambavyo utukufu wa Mungu ukiondoka juu ya mtu na ulinzi wa Mungu ukiondoka kwa sababu ya dhambi uwezekano wa mtu kuvamiwa na aroho za giza unakuwa ni mkubwa zaidi.
Kukata tamaa ile hali ya kujikatia tamaa, kuvunjika moyo, kupoteza kabisa matumaini hata kujisemea maneno ya laana, inafungua mirango kwa roho za giza kuvamia maisha yako. Ndio sababu Biblia ikasema Filip 4 :6 msijisumbue kwa neno lolote ; Bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. sasa kule kulaumu kulalamika, kujilaani haja zako zinajulikana na mapepo na sio Mungu. Iyo ndio inayompa adui nafasi kwenye maisha ya watu wengi leo.

Wednesday, November 18, 2015

MTUME MUHAMMAD ALISALI NA VIATU MSIKITINI

Ndugu msomaji,
Leo ningependa tujikumbushe na kujifunza kuhusu kusali na viatu katika nyumba za ibada.
Waislam mara nyingi wamekuwa wakiwashutumu Wakristo na kuwakejeli kuwa, eti wanasali na viatu Kanisani. Je, Mtume wa Allah aitwaye Muhammad alivaa viatu alipo kuwa anaswali Msikitini?
Hebu tuangalia ushahid huu hapa:
Ukisoma kitabu cha Al-u-lu wal-marjan Uk. 179
14. Mlango:
Ruhusa ya kusali na Viatu.
325. Hadithi ya Anas Bin Malik (R.a) kutoka kwa Said Bin Yazid Al-Azid (r.a) amesema, Nilimuuliza Anas Bin Malik (r.a) “Hivi Mtume (s.a.w) alisali huku amevaa viatu vyake?” Akanijibu, “Ndiyo” (Bukhari, Hadithi N. 383, Juzuu ya 1)
Hapo tunamuona Muhammad akisali na Viatu, na mlango hapo umesema, Ruhusa ya kusali na Viatu, maana yake waislamu hapo wameruhusiwa kusali na Viatu, pia haikuishia hapo, Muhammad akasema tena kuwaambia Waislamu.
Ukisoma kitabu kinachoitwa “TAFSIRI YA BULUGH AL-MARAM MIN JAM’I ADILLATIL AHKAM
Ukurasa wa 101 Hadithi Na. 171
Abu Said (r.a) amesimulia: Mtume (S.a.w) amesema: “Ye yote miongoni mwenu atakapoenda msikitini kusali, basi atizame, akiona uchafu au najisi katika viatu vyake aondoe kisha aswali navyo”. Abu Dawud Ibnu Khuzaimah ameipa daraja ya Sahih.
*Murad wa kutwaharisha viatu:
Iwapo mtu amekanyaga najisi kwa kiatu, atakitwaharisha kwa kusugua chini mchangani*
Hapo kwa mtu mwenye akili zake timilifu, hawezi kukomaa na kuanza kuwalaumu Wakristo, eti kwa nini wana Sali na viatu? Wakati Muhammad mwenyewe, alisali huku amevaa viatu, na pia akawaambia waislamu wanapoenda kusali, basi watazame viatu vyao kama kuna najisi, basi wavisugue chini mchangani, labda waislamu watuambie wao kusali na viatu, ni Uviviu wa kusugua viatu mchangani? Au mazingira yao wanayoishi hayana mchanga?
Tena Muhammad akakazia zaidi kuhusu Viatu, aliponukuliwa katika Hadithi hii.
Kasema Mtume (S.a.w) “Atakaepata (ona) nge nae anasali, basi amuue kwa kiatu cha kushoto” (Mkweli Mwaminifu, Juzuu ya 1-2, Hadithi Na. 188, Uk, 88)
Muhammad anawataka Waislamu wakimuona Nge basi wamuue kwa kiatu cha kushoto, sasa jiulize, wewe umevua viatu, unaswali peku peku (kama bata) Halafu amekatiza nge, unaweza kweli kumkanyaga kwa mguu? Nachoweza kusema ni uvivu tu wa waislamu katika kusugua mchangani viatu vyao vilivyo na najisi, kwani wameshapewa ruhusa ya kusali navyo.
Kumbe Mtume Muhammad alikuwa anavaa viatu alipo kuwa ndani ya Msikiti.
Kumbe Mtume Muhammad alisali na viatu Msikitini.
Hakika Uislam ni dini bandia.
Max Shimba Ministries

Sunday, November 15, 2015

POSA SABA (7) ZA MUHAMMAD ZILIZO KATALIWA


1. Kwanini baadhi ya wanawake walikataa posa za Muhammad?
2. Kwanini muhammad aliendelea kuomba/toa posa na huku zikikataliwa?
Ndugu msomaji,

Leo nitakua ushahid kadhaa kuonyesha jinsi Muhammad alivyo penda wanawake lakini wengine walikataa posa zake na kuto jali utume wake alio pewa na Mkewe.

Muhammad alimwomba amuoe Ghaziyyah kwa sababu ya uzuri wake, lakini alikataliwa. Tabari anadai kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu lakini hatoi ushahidi. al-Tabari juzuu ya 9 uk.136. Hakuna ushahidi kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu na kwamba Muhammad hakuwa makini kwa kutokumwadhibu, au kwamba hakuwa mwaminifu na Muhammad alimwadhibu.

Layla aligusa bega la Muhammad tokea nyuma na kumuomba amuoe. Muhammad alikubali. Ndugu za Layla walisema, "Ni jambo baya kiasi gani ulilolifanya! Wewe u mwanamke anayejiheshimu, lakini Nabii ni mpenda wanawake. Tafuta kujitengua toka kwake." Layla alikwenda kwa Nabii na kumuomba aikane ndoa hiyo na aliafikianana na hilo [ombi]." al-Tabari juzuu ya 9 uk.139.

Kutoka al-Tabari juzuu ya 9 uk.140-141, Muhammad alimposa lakini aliishia kutokumuoa:
1) Umm Hani’ bin Abi Talib [Hind] kwa sababu alikuwa na mtoto.
2) Duba’ah binti ‘Amir lakini alikuwa mzee sana.
3) Inaripotiwa kuwa alimposa Saffiyah binti Bashshamah, mateka. Alitakiwa achague mmoja kati ya Muhammad na mume wake, na alimchagua mume wake.
4) Umm Habib bint al-‘Abbas lakini kwa kuwa al-‘Abbas alikuwa kaka wa kulelewa pamoja naye kwa hiyo isingeruhusiwa kisheria kwa hiyo Muhammad aliamua kujiondoa.
5) Jamrah binti Al-Harith. Baba yake alida isivyo sahihi kuwa alikuwa anasumbuliwa na kitu Fulani. Aliporudi, alikuta ameisha kumbwa na ukoma.

Haielezwi kwa kauri moja endapo Umm Hani’ alikuwa muislam kabla au baada ya Muhammad kumwomba amuoe. al-Tabari juzuu ya 39 uk.197 na rejeo chini ya ukurasa 857 uk.197.

Ndugu msomaji ambaye ni mfuasi wa dini ya Uislam, je, unaweza tumabia kwanini posa 7 za Muhammad zilikataliwa?

Max Shimba Ministries

Muhammad’s Fear Of Judgment Day

  Muslims beware! The next  eclipse  could be the  Day of Judgment .  This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...

TRENDING NOW