Saturday, August 22, 2015
YESU NI UPENDO (SEHEMU YA NNE)
Ndugu yangu, wajua yakwamba Yesu Kristo anakupenda ? Wajuwa yakwamba alisulubiwa kwa ajili ya watu wote: Wanaume na Wanawake, Watoto, Vijana na Wazee? Yesu Kristo alikufa kwa ajili yako.
Yesu anakupenda sana, inawezekana kuna mtu anakupenda sana ila Yesu anakupenda zaidi ya wote duniani hivyo nakushauri ukate shauri umfuate yeye maana atakupa kustarehe milele na kuurithi ufalme wa mbinguni pamoja naye.
TAFAKARI: “Yesu anakupenda upeo, amepoteza kila kitu, na kufa kifo cha aibu ili asikupoteze.”
JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mnyanganyi, mwizi, mwongo, muuaji, usiye kuwa na ukweli? Yesu anakupenda na anataka kukuponya.
JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mlozi mkubwa mwenye kutumikia Shetani, tangu ujana wako unazuru wanadamu wengine, unaua watoto, wanawake hata wanaume, unaharibu mavuno, unatawanya magonjwa toka jamaa kwa ingine, unaua hapa na pale.Unapopita ni woga mtupu na kukimbia mbali sababu ya mapepo mabaya yako. Mara na mara unajiuliza nini ulikuja kufanya hapa duniani, ukitafuta kujua sababu ya mabaya yote unayoyatenda. Unajiuliza namna gani uliweza kufikia hapo. Fahamu neno moja tu, hata unaishi mabaya haya yote : Yesu anakupenda na anataka kukuponya.
JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
…Wewe ni mkoma,tangu miguu hadi kichwani. Ulipoteza vidole, sikio, pua, ukageuka kilema kwa namna fulani; fahamu jambo hili: Yesu anakupenda na anataka kukuponya.
JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI HILI?
… Wewe ni msichana, waonekana kuwa ni mrembo sana na wakati wako wote unavunja jamaa za wengine. Unapotosha rafiki zako za darasa, za shule lako, za ofisi ao za mtaa wako. Mara nyingine ulitoa mimba, ulitafuta kupatia wengine sumu, ao uligonganisha wapenzi wako: wamoja wafariki ao wangali wagonjwa sana sababu yako, sababu ya unyofu wako, na sura yako nzuri sana. Sasa wajiuliza mengi kuhusu maisha yako: uliweza kutambua mabaya yote uliyotenda na unajiuliza nini Mungu atakayokutendea.
Unapatwa na woga wakati unawaza haya yote sababu unaambiwa yakuwa siku moja Mungu atahukumu matendo ya watu.Unaishi katika uasi, unajua ya kwamba JEHENAMU ndiyo inakungojea na unajifariji ukisema kwamba ni maneno yasiyokuwa na msingi hata unasema : Mungu hayuko!
…Wewe ni kijana uliyetenda mambo sawasawa na yale na mwisho ukafikia kusema hivyo. Unajitia kwa mstari ya wale wasiosadiki kuwa Mungu yuko, ili ujitulize.
Ndugu yangu, rafiki yangu, Shetani anakupoteza. Unajuwa ni nini inayokungojea. Hata ikiwa hivyo, ninataka kukujulisha ya kwamba wakati ungali wa kugeuza yale yote, kwani katika upendo wake Mungu alituma Mwana wake wa pekee ili akuondoshe katika maisha yale. Yesu anakupenda, anataka akuokowe kwa damu yake na uwe safi mbele ya Mungu.
…Wewe ni mwanaume, mwanamke, mtoto unayelala kitandani katika hospitali sababu ya ugonjwa, ya msiba wa barabarani, ya ulozi; ili ujue neno hili: Yesu ni karibu yako na anakupenda na anataka akuponye.
… Ulifanya kosa fulani na kwa sasa unapatikana katika mateso ya gereza: Yesu anapatikana hapo kwa kukuponya.
…Wewe ni mtumishi, kiongozi, uliyepata cheo kikubwa kwa njia ya madawa na ulozi, kuua na kusengenya, uongo na vibaruwa vya uongo: ulipita juu ya wengine ili ufikiye pahali ulipo, sasa maneno haya ni mkononi mwako: usifikiliye ni kwa bahati tu. Yesu anakuambia ya kwamba anakupenda hata ulipitia kwa njia hizo. Ulisoma mistari hii na unashangaa ukigundua kwamba hata ukiwa mwenye kutenda mabaya kama hayo, Yesu anakupenda pia.
Sikiliza anayosema Mwokozi wako:
“Watu wenye afia njema hawahitaji muganga, ila wenye ugonjwa tu.. Sikuja kuita wenye haki bali wenye zambi”( Marko 2.17) .
Unasikia hayo? Yesu anasema ya kwamba alikuja kwa ajili ya watu kama wewe.Unaona mlango wa kutoka mahali ulipo sasa, ni Yesu Kristo mwenyewe.
…Mara nyingine wasema: mimi si Muisraeli anayeambiwa maneno hayo ya Yesu ! Mimi ni Muafrika, Muasia,Muamerika…jua ya kwamba maneno hayo ni kwako pia na usikilize asemayo:
“Muniangalie, na muokolewe, miisho yote ya dunia;kwani mimi ni Mungu,na hapana mwengine.” ( Isaya 45:22).
Wasikia zaidi ya hayo? Ulizani kwamba ulifikia mwisho, ukitesa wanadamu wengine, unajisikia hakuna tena kukaribia Mungu. Ulisema haya na yale kuhusu zambi zako. Na Yesu anakuambia:
“Leo kama mtasikia sauti yangu, msifanye migumu mioyo yenu.”( Waebrania 4.7).
Una maneno haya mkononi mwako, jua ya kwamba ndiyo “leo” yako hii na Mungu anasema: Usifanye moyo wako kuwa mgumu.
Kwa kumaliza, Roho Mtakatifu anakupa ujumbe huu:
“Basisisi,! Tutapona namna gani, tusipochunga wokovu mkubwa namna huu?” (Waebrania 2.3).
Ndugu, rafiki, wajua sasa ya kwamba Mungu anakupenda, wajuwa kuwa Mwana wake Yesu ni tayari kukuponya. Haupatikane tena katika kutokujua. Mungu anataka kukufungua macho kwa maneno haya na anasema:
“Kwa maana Mungu alivyopenda ulimwengu, hata kutoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu akimwamini asipotee, bali apate uzima wa milele” (Yoane 3.16).
Chaguo ni lako: amini na uokolewe ao kutoamini na kuhukumiwa. Ndiyo, katika neema yake kubwa, Mungu anakuonyesha wazi njia ya kupitia. Anasema:
“Nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; kwa hivi chagua uzima ili uwe hai.” (Kumbukumbu la torati 30.19).
Unapenda kumusikia Mungu? Ama kama asemavyo mtume Paulo:
“Ao unazarau utajiri wa wema wake na saburi na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu unakupeleka kwa toba? Lakini kwa ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya asira kwa siku ile ya asira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu” (Warumi 2.4-5), na inaandikiwa tena “Basi, zamani wakati huu wa ujinga, Mungu hakuangalia ; lakini sasa anaamuru watu wote wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki,kwa mtu yule aliyemuweka kwa kazi hii; naye amewapa watu wote hakika ya mambo haya kwa kumfufua toka wafu” (Matendo ya mitume 17.30-31).
Pamoja na mtume Paulo:
“Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kama kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu” (2 Wakorintho 5.20) kabla wakati haujapita.
Pokea upatanishi unaopewa na Mungu. Kwa hivyo unaombwa kukiri makosa yako, ukitambua ya kwamba wewe ni mwenye zambi.
Kumbuka kuwa Yesu anakupenda,
Max Shimba
Max Shimba Ministries 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Muhammad’s Fear Of Judgment Day
Muslims beware! The next eclipse could be the Day of Judgment . This warning comes from none other than Muhammad himself. During the l...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment