Monday, August 3, 2015

USHUHUDA: MWANASHERIA MKUU WA SHERIA ZA KIISLAM WA IRAKI AMPOKEA YESU

BADO
HUJASTAHILI



KUTOKA:

KWENYE GIZA LA UDANGANYIFU WA KIISLAMU

HADI:
KWENYE NURU YA UTUKUFU WA YESU



-UKWELI-



Ushuhuda wa Lazaro


Nakala ya Bure




Ni furaha yangu kubwa katika Bwana kwamba nimeweza kukushirikisha ushuhuda wangu binafsi. Jinsi Bwana alivyonichagua mimi na jinsi nilivyokuja kwenye miguu ya Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi.
MAISHA YANGU YA ZAMANI
Mtu fulani aliniuliza, “Mchungaji waweza kunieleza upi ni muujiza mkuu unaoukumbuka katika umri wako huu?” Nikamjibu “katika ufahamu wangu muujiza mkuu katika umri huu ni kwamba katika mwaka 1988 nilikuwa Maulvi (Msomi wa Kiislamu) na leo mimi ni Mchungaji.” Nilisoma kozi ya juu kabisa ya kidini (Maulvi Fazil, Alam Fazil, Fazil-e-Ijaz). Baada ya kuhitimu shahada yangu ya Uzamili ya Sanaa katika Kiarabu kutoka Lahore nilikwenda Iraq kwa masomo ya juu zaidi.
MASOMO YA JUU KULE IRAK NA SAUDI ARABIA
Kutoka mwaka 1974 hadi 1978 nilisoma Chuo Kikuu cha Irak. Nilitunukiwa shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Sheria za Kiislamu katika Kiarabu na Uajemi (Mufti) kwa sababu nilikuwa naenda kuwa Maulana (mufii wa Kiislamu). Lugha yangu ya kwanza ni Punjabi. Nilisoma kwa Kiarabu hadi nikatokea kufanya mitihani ya falsafa ya udaktari (PhD) kwa lugha ya Kiarabu. Pamoja nami katika darasa walikuwepo wanafunzi ambao lugha yao kuu ilikuwa Kiarabu. Nilipata alama 995 kati ya alama 1000 ambapo nilivunja rekodi katika Chuo Kikuu cha Irak hadi siku ya leo(mwaka1995). Nilisoma sheria za kiislam kuanzia mwaka 1978 hadi 1980 katika mji Mtakatifu wa MAKA (Saudi Arabia). Niliteuliwa kuwa mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu nchini Saudi Arabia kuanzia mwaka 1980 hadi 1984.

NCHINI ISLAMABAD KAMA MWANASHERIA MKUU WA MAHAKAMA YA SHERIA
Nilirudi nchini mwangu mwaka 1985 na nikateuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu wa Islamabad (1984-1989). Nilirithi chuki ya kumchukia Kristo na Wakristo kutoka kwa mababu zangu. Niliwatesa Wakristo na nilikuwa kinyume na Yesu. Nilijaribu kwa nguvu zangu zote kukomesha mikutano yao ya dini, niliwaadhibu na kuwanenea mabaya kwa uwezo wangu wote. Kama mtuhumiwa wa Kikristo angeletwa mbele yangu mahakamani, angearifiwa na wanasheria kwamba huyu hakimu atakuhukumu kifo tu. Akijua kuwa wewe ni Mkristo inatosha, hata hitaji maelezo zaidi. Atakapo fungua faili lako na kusoma kwamba wewe ni Mkristo inamtosha kukuhukumu kifo.


YESU NDANI YA OFISI YANGU

Katika asubuhi mwanana ya Aprili 26 mwaka 1989, nilikuwa nimekaa ofisini mwangu nikiwa na katibu wangu (mwanamke) akiwa anafanya shughuli fulani za mambo ya dini. Mara majira ya saa 5.30 asubuhi ofisi yangu ilianza kujawa na mwanga wa ajabu na wa kushangaza ambao ulikuwa mwangavu na unaong’aa kuliko jua. Wakati huo nilikuwa nimefuga ndevu ndefu zilizonifikia tumboni na nywele ndefu zilizonifika mabegani. Katibu wangu alikuwa akihofia mpira huu wenye mwanga usio wa kawaida ambao nuru yake ilizidi kuwa angavu, na alianza kuniuliza mimi “Maulana (msomi wa Kiislamu) ni nini kinachotokea ofisini kwetu?” Mimi binafsi nilikuwa naogopa na ili kuficha woga wangu nilimwambia aende nje ya ofisi. Baada ya dakika chache ule mwanga ulitoweka, lakini katikati ya ofisi yangu nilimwona mtu aliyekuwa amesimama. Na ndevu za rangi ya dhahabu na nywele za rangi ya dhahabu ndefu hadi mabegani akiwa amevalia vazi ling’aalo sana. Nilikuwa nikimtazama ana kwa ana. Alianza kuongea na mimi na kuniambia “Angalia Maulana umenitesa mno lakini upo kwenye mipango yangu tangu milele” Niliwaza huyu alikuwa Malaika wa Mauti na leo ndio siku yangu ya mwisho ulimwenguni. Nilikuwa nikitetemeka ndani yangu na kuyaogopa sana haya mazingira kwa sababu nilikuwa na uhakika huyu alikuwa Malaika wa Mauti na kwamba leo ndio mwisho wangu duniani. Katika hofu yangu ya kutisha nilihisi shinikizo kubwa ndani ya nafsi yangu na nikaanza kumlalamikia. Nikamwuliza “wewe ni nani na umedirikije kuingia ofisini mwangu? Walinzi wa usalama wako wapi? Kwanini hawakukuzuia? Unataka nini toka kwangu?” Ndani ya sekunde moja nilimwuliza swali zaidi ya moja. Nikamwambia, “Jitambulishe” Akajibu “Nimekukomboa wewe (Fidiya) na kujitoa sadaka kwa ajili yako (Qurbani), wakati neno “kujitoa sadaka” (Qurbani) linapozungumzwa linaeleweka kirahisi zaidi na Muislam. Kwa mujibu wa sadaka Hazrat-I-Ibrahim (Abraham) ya kumtoa mwanae Ishmael kutokana na Imani ya kiislam. Nilitiwa moyo na jibu hili na kwa haraka nikamwuliza “Je, wewe ni Hazrat-I-Ibrahim aliyemtoa sadaka mwanae Ishmael?” Akajibu “Hapana nimeyatoa maisha yangu kwa ajili yako na kwa ulimwengu mzima msalabani (Saleeb) lakini wewe umenitesa mno. Hii ndio sababu Mimi mwenyewe nimekuja nikufanye uwe wangu.”

Nikiwa kama Msomi wa Kiislamu sikuwahi kusoma Biblia au maandiko mengine yeyote ya Kikristo na wala sikuwa na hamu na Kristo wala Ukristo. Lakini baada ya kusikia neno ‘msalaba’ (saleeb), niligundua kuwa huyu ni nabii ISSA (Yesu). Nikawaza moyoni mwangu, “Huyu ni mtu wa namna gani? Ninamtesa, ninamtukana na kumnenea maneno mabaya na yeye binafsi anakuja ofisini mwangu.” Kwa kila mtu kuna moyo wa ndani uitwao dhamiri. Sauti yangu ya ndani ilikuwa ikiniambia “Maulana acha usumbufu wako, yule unayemtesa anaongea na wewe. Achana na usumbufu wako na uadui na umpokee Yeye.”
Namshukuru Mungu kwamba sikumpokea Kristo baada ya kusoma Biblia au baada ya kuzidiwa nguvu na wasomi wa Kristo kwenye mdahalo. Mshahara wangu kwa mwezi ulikuwa rupia za Pakistani 120,000 (kadiri ya dola za Marekani 3,000). Mshahara wangu ulikuwa ukitumwa kwangu moja kwa moja kutoka Falme za Kiarabu za Saudia. Mimi nilikuwa ni mtu niliyezoea kulala peke yangu kwenye kitanda kikubwa (master bed). Haikuwa rahisi kwangu kukalia kochi la mtu mmoja. Nilikuwa mkubwa sana kiasi kwamba walizoea kunitengea kochi la watu wawili nikalie. Kwa kitambo niliwaza juu ya faraja na anasa zote ulimwenguni nilizokuwa nikizipata kama Mwanasheria Mkuu wa Sheria za Kiislamu ndipo nilipomjibu “Sikuamini, sina chochote cha kufanya na wewe wala msalaba wako.”

DINI YANGU YA ZAMANI NA UDHURU
Nilimpa udhuru mwingi kulingana na imani yangu na nilimwambia nabii wangu ni mkuu kuliko manabii wote. Lakini Akaniambia “Njoo toka nje ya ofisi yako.” Sielewi jinsi nilivyokwenda kwenye ubaraza wa ghorofa nikipaa pamoja naye angani, kisha toka kwenye ubaraza wa ghorofa nikaona mbingu zimefunguka. Akanionyesha Nabii wangu na vitu vingi vinginevyo. Kisha tukarudi ofisini na akaniambia. “Inabidi unifuate, nataka nikufanye mtumishi wangu, nataka nikufanye shahidi wangu.” Dhamiri yangu ikaanza “Maulana mpokee, ni kweli yeye ni Mkuu na mtukufu. Kubali ukweli huu kwamba wewe upo kinyume nae na umemtesa lakini anakupenda.” Nikamjibu “Sawa Issa Masih, kuanzia leo na kuendelea wewe ni wangu na mimi ni wako.” Na huyu Issa Masih akaenda zake toka ofisini mwangu kwa njia ile ile aliyojia.

KUJIUZULU KWANGU
Mara moja niliandika barua ya kujiuzulu na kuituma Saud Arabia kwa njia ya fax. Baada ya kupokea fax yangu Imam wa Khana-e-Kaba, Sheikh Abdala, alipanda ndege ya kwanza na kuja Islamabad na akaja moja kwa moja ofisini mwangu. Aliniuliza kwa mshangao mkubwa katika lugha ya kiarabu “Je, wewe si kichaa?” Nikamjibu, “Mimi sio kichaa lakini mimi ni Mkristo.” Alifahamu vyema kwamba natoka katika familia ya Kiislamu ambapo wote ni wasomi wa Kiislamu, na kwamba mimi ni wa 8 katika mlolongo wa wasomi wa Kiislamu baada ya baba yangu na mababu zangu waliotutangulia. Ndipo Sheikh akatoa amri kwa wenye mamlaka, “Anapaswa kuadhibiwa vilivyo kwa sababu ameukataa Uislamu na mtume wetu, kama akienda nje na kuwaeleza watu wengine imani yake mpya, itakuwa kufuru kwetu sisi. Mpeni wakati mgumu gerezani ili kwamba kwa wakati ujao asiwepo yeyote atakaye diriki kutumia jina hili ‘Ukristo’ tena.”
MATESO KWA KUMPOKEA YESU
Mara moja nilikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi. Usiku walinipeleka mahabusu. Nilipigwa kikatili sana kule jela na asubuhi nikaambiwa “Oh maulana, kujiuzulu kwako hakujakubaliwa. Tafadhali rudi kwenye kiti chako na uendelee na kazi yako” Nikajibu, “Hapana mimi ni Mkristo”
JINSI FAMILIA YANGU ILIVYOLICHUKULIA
JAMBO HILO
Baba yangu alifariki mwaka 1978 lakini wakati hayo yaliponitokea mama na kaka yangu walikuwa bado hai. Kwa sasa wote wawili wameshafariki. Walikuja gerezani na walisema, “Tumekupatia elimu nzuri namna hii na kutumia hela zetu nyingi kwa ajili yako. Tulikupeleka Irak kwa ajili ya masomo ya juu, kwanini sasa unaenda kuwa kafiri? (neno linalotumika kwa wale wanaoukataa uislam). Tafadhali rudi ofisini kwako uchukue nafasi yako.” Nikajibu, “Amme (mama) Hapana. Tangu jana nimekuwa Mkristo.” Shangazi yangu aliyekuwa amesimama pamoja nao alianza kunitukana. Alidhani labda nikishasikia maneno hayo mabaya ningerudi nyuma kwenye Uislamu. Alisema “Mpeni ndoo ya takataka na ufagio mrefu mikononi mwake halafu mwacheni akaishi na wafagizi (Wakristo).” Kwasababu Waislamu wengi wa Pakistani hudhani Wakristo ndio wafagizi, lakini wanasahau kwamba hata kule Saudia Waislamu hufanya kazi ya ufagizi na kazi nyingine nyingi za ajira ndogo. Nikamjibu, “Kama ni kwa ajili ya Masihi (Kristo) natakiwa kuifanya kazi hii nitaifanya. Kwa sababu yeye alikuja kwangu moja kwa moja na kuongea nami, alinionyesha utukufu wake na nguvu iliyopo Mbinguni ambayo sasa inakaa katika chembechembe zote za damu yangu. Sasa Anaishi ndani yangu siwezi kumwacha.” Wakasema “sawa” na wakaondoka.

KULE GEREZANI
Adhabu yangu ya kwanza ilianza kwa kucha za vidole vyangu kunyofolewa kwa kuvutwa. Baada ya kupigwa kwa mara ya pili nilipelekwa hospitali. Pale hospitalini nilipewa maumivu mengine makali ya akili. Nilisikia kwamba mke wangu na mtoto wote wawili walikufa kwenye chumba cha uzazi wakati wa kujifungua. Kwanza madaktari walikuwa wakijaribu kuokoa maisha ya mtoto na ndipo wakati huo mke wangu alipofariki. Kisha baada ya masaa 4 mtoto wangu naye akafariki. Ndugu zangu wote, majirani na marafiki walikuja wakaniambia, “Unaona, Allah amekuadhibu. Mkeo na mtoto wamekufa. Kucha zako zimenyofolewa. Lakini bado muda wa kurudi nyuma upo.” Jibu langu pekee lilikuwa, “Hapana sasa anaishi ndani yangu.” Kwa wakati ule sikuwa najua kwamba huu ulikuwa mstari wa Biblia kwa sababu hakukuwepo mtu katika familia yetu nzima aliyekuwa anaifahamu Biblia. Hata mimi kama msomi wa kiislamu sikuwahi kujifunza ama kusoma Biblia. Kwa sasa nalijua andiko linalosema,“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Mungu hukaa ndani yenu” (1Kor 3:16).

Pili nilikuwa nimening’inizwa miguu yangu ikielekea chini lakini si kwa kamba wala minyororo. Safari hii walizitumia nywele zangu ndefu, na nilikuwa nikibembea mle chumbani kama mpira. Uzito wangu wote ulikuwa katika nywele zangu. Nilining’inizwa namna hii hadi damu kutoka kichwani ikaanza kudondoka sakafuni. Unaweza kufikiria wazi kwamba damu ili idondoke sakafuni nguo zangu zote zilikuwa zimeloa damu. Walidhani ningekufa kwa sababu kutokana na mateso uso, macho yangu yalivimba hadi macho yalifunikwa kabisa. Nilikuwa mnene na aliyezidiwa uzito, nilikuwa siwezi kufumbua macho yangu au hata kumwona mtu. Tena waliniuliza, “Sasa Maulana unawaza nini kuhusu dini yako mpya?” Nikawajibu, “Kristo ni wangu na mimi ni wake.” Leo sisi ni watumwa wa mapokeo ya wahenga wetu. Pale ambapo wahenga wetu walitufikisha, hatutaki kupaacha, wala dini zao. Hata hivyo wahenga wangu wote walikuwa Maulvi na wasomi wa Kiislamu na kwa sababu ya hilo ilikuwa ngumu kwao kumpokea Yesu.
KUVUNJWA MBAVU
Nilikaa miaka miwili katika gereza la Hari Pur Hazara. Mshtuko mkubwa wa tatu ambao niliupata gerezani ni kwamba mbavu zangu zote za pande mbili zilivunjwa kwa mateke ya askari polisi na maofisa. Naweza kukuonyesha mbavu zangu na mtu yeyote aliye na taaluma ya udaktari anaweza kuzikagua mbavu zangu wakati wowote. Baada ya kuzivunja mbavu zangu na kunipiga mateke bila huruma wakasema tena, “Tutakugharamia matibabu yako yote na tutakupeleka hospitali kama utarudi kwenye Uislamu.” Nikajibu, “Wala kamwe msiniambie jambo hili tena. Lolote mnalotaka kunifanyia mnaweza kufanya lakini siwezi kusikiliza maneno yanayonitaka nirudi nyuma kwenye dini yenu ya kizamani. Hata kama ningetaka kurudi nyuma siwezi kurudi nyuma kwa maana Yesu anaishi ndani yangu siwezi kumwacha.” Nilipelekwa hospitali madaktari waliamua kunifanyia upasuaji na walikuwa wakipanga kuniwekea vitu fulani kama chuma ambavyo vingekaza mbavu zangu tena. Wangenipeleka kwenye chumba cha upasuaji asubuhi ambayo ingefuata. Jinsi nilivyokuwa na maumivu makali ya kufa, ilipofika saa 10:30 alfajiri nilimwona Yesu Kristo tena ana kwa ana akiwa amesimama upande wangu. Nikamwambia, “Masihi (Yesu) wamenipiga na kunitesa bila huruma.” Yesu akajibu, “Bado hujastahili kunitumikia.” Nilifadhaika sana kwamba niliacha nafasi kubwa ya heshima kubwa namna ile, mke wangu na mtoto wamekufa, nimeiacha familia yangu, mali zangu zote zimechukuliwa, kucha zangu nazo zimeng’olewa, nilitundikwa kutumia nywele zangu, sasa hata mbavu zangu zimevunjwa na kile Yesu anachoniambia ni kitu kisicho cha kawaida kabisa.

YESU NI MPONYAJI

Nikalalamika tena, “Masihi (Yesu) wamezivunja mbavu zangu.” Aliposikia malalamiko yangu akasema, “Mbavu zangu hazikuvunjwa nilipokuwepo ulimwenguni kwa hiyo sitaruhu mbavu zako ziendelee kuwa zimevunjwa.” Halleluya. Mara moja nikamwita muuguzi nikamwambia anifungue vitambaa nilivyofungwa kifuani mwangu. Akaniambia, “Una kichaa? Kesho asubuhi tutakufanyia upasuaji, siwezi kufanya hivyo.” Nikamwambia “Kama hutafanya hivyo basi mimi nitafanya hivyo.” Akakimbilia kwa daktari. Daktari akaja na akanipa karatasi ya kuweka sahihi. Akaniambia hii ni kwa sababu kama ukifa baada ya kuzifungua hizo plasta hatutahusika na kifo chako. Sikuwa naweza kuweka sahihi lakini niliweka sahihi. Wakanifungua plasta zangu lakini daktari akasema siamini kile ulichosema, nataka nikupige picha ya eksirei (x-ray) kwenye kifua chako. Waliponipiga picha ya x-ray waliona mstari pande zote mbili za kifua changu katikati ya mbavu zangu. Hata sasa kama ungependa kufanya hivyo tena utashuhudia mistari miwili katika pande zote mbili za mbavu zangu. Daktari alinikimbilia na kusema, “Mbavu zako hazijavunjika tena zimepona zenyewe ghafla.” Nikasema hapana hazijapona zenyewe ghafla bali kuna mtu ameniponya. Nikamweleza kuwa mtu kipofu hakuweza kupona mwenyewe ghafla, kuna Nguvu ya Kiungu nyuma ya uponyaji wangu. Baada ya miaka miwili gerezani wakanirudisha tena mahakamani. Kule gerezani maofisa wa polisi walikuwa wakilalamika mara kwa mara, “Wewe ni mfungwa wa namna gani hakuna wageni wanaokuja kukuona kwa kipindi cha miaka miwili.” Nikajibu, “Mheshimiwa kama kuna mtu anayekuja kunitazama au hakuna mimi sijali, lakini kuna mgeni ambaye yupo ndani ya moyo wangu na ninaongea naye kila ninapohitaji kuongea naye. Mgeni huyu hafungwi na muda wenu wa kutembelea wafungwa yaani saa 10-12 jioni, ila yeye ni mgeni aliye huru na naweza kuongea naye masaa 24 kwa siku.”

MWANASHERIA MKUU WA SHERIA ZA KIISLAMU
MBELE YA HAKIMU WA DARAJA LA CHINI
Baada ya miaka miwili gerezani nilipelekwa mahakamani na nilikuwa mbele ya hakimu. Mahakama ikatoa amri ya kifo changu. Walinichukua na wakaniambia, “Kesho asubuhi majira ya saa 10 alfajiri utatundikwa, lakini tunakupa nafasi ya mwisho. Je, ungependa kurudi kwenye dini yako ya zamani?” Jibu langu lilikuwa, “Fanyeni mtakayo kufanya siwezi kumwacha Masihi.” Tena wakaniuliza, “Hili ndilo jibu lako la mwisho?” Nikasema, “Ndio.” Wakaniuliza, “Ungetamani nini cha mwisho?” Nikawauliza, “Mnaweza kuitimiza hamu yangu ya mwisho?” Wakadhani nilitaka kurudi. Hivyo wakasema, “Tuambie hamu yako ya mwisho.” Nikawaambia, “Hamu yangu ya mwisho ni kwamba ninyi nyote mliopo hapa mahakani mngempokea Yesu na kuwa Wakristo.” Wakasema, “Haiwezekani.” Nikawaambia, “Mmeniuliza na nikawaambia, sasa kutimiza au kutotimiza hilo ni juu yenu.” Mahakimu, wanachuo wenzangu walizoea kuniambia, “Oh Maulana wewe ni mtu wa namna gani, kabla ulikuwa unawahukumu watu na sasa unaenda kutundikwa.” Sikuwa na la kujibu, nikamuuliza Yesu, “Ee Bwana hawa mahakimu wenzangu wananiuliza hivi niwajibu nini?” Yesu akanitokea tena na kuniambia, “Bado hujastahili kunitumikia.” Nikamjibu, “Lakini siku moja nitastahili kukutumikia.” Nilikuwa na hamu hii moyoni mwangu kwamba hadi wakati atakaponiambia, “Unastahili kunitumikia.” Kabla sitamtumikia lakini nilijua kwamba siku moja hakika atasema, “Unastahili kunitumikia.”
Aliniambia niwaambie, “Kabla nilikuwa hakimu aliyewahukumu wanadamu tu lakini sasa nimepandishwa cheo na kuhamishiwa kwenye mahakama nyingine na Yesu. Mimi bado ni Mwanasheria Mkuu, lakini kutokana na kupandishwa cheo sasa nitakapoenda mbinguni nitawahukumu Malaika kule mbinguni.” Sikuwa nalijua jibu hili kwa sababu sikujua kuwa hili limeandikwa kwenye Biblia. Niliwajibu tu kama alivyoniambia. Wakasema, “Baada ya kusikia hukumu ya kifo sasa unaanza kuzungumza kwa hamaki?”

YESU ANA NGUVU JUU YA MAUTI
(USHINDI WA KWELI)
Mapema siku iliyofuata alfajiri nilipelekwa sehemu ya kutundikwa. Wakaifunga ile kamba ya kunyongea shingoni mwangu wakati huo huo jalada (faili) likawasilishwa kwenye mikono ya maofisa wa polisi, na kutokana na jalada hilo hukumu yangu ya kifo ilikwisha. Kwa nyongeza katika jalada hilo ilikuwepo rufaa aliyopewa hakimu kutoka kwa mahakimu wenzangu, kwa hiyo hakimu alitoa agizo hukumu yangu ifutwe. Hawa mahakimu wenzangu niliosoma nao wote walikuwa Waislamu lakini walitaka kuniokoa ndipo walipokata rufaa mahakamani ili niachiliwe. Katika rufani hiyo waliandika sababu zifuatazo za mimi kuachiliwa: “Kutokana na sheria za kiislamu huyu mtu hajafanya kufuru yeyote dhidi ya Uislamu, wala dhidi ya Korani tukufu au Nabii Muhammad. Alichokisema tu ni kwamba alimpokea Yesu kwa sababu kufuatana na maneno yake mwenyewe, Yesu mwenyewe alikuja ofisini mwake. Pakistani ni nchi ya kidemokrasia na katika bendera ya nchi hii kuna rangi nyeupe ambayo inawakilisha walio Wachache.”

KURA 4 ZA WAKRISTO NA WAPAKISTANI
Rufani iliendelea, “Ni kwa sababu ya Wakristo kwamba Pakistani imetokea kuwepo. Walipiga kura zao kwa Shirikisho la Kiislamu la Pakistani badala ya kupiga kura zao kwa Chama cha Siasa cha India kama Wahindu na Singasinga walivyofanya. Katika uchaguzi wa mwaka 1947 singasinga na Wahindu waliwapa kura zao Chama cha Siasa cha India lakini Wakristo kura zao waliwapa Shirikisho la Waislamu wa Pakistani. Kura moja iliyobakia ilikuwa ile ya Wakristo. Kama kura hii isingekuwepo kwa Shirikisho la Waislamu basi Chama cha Siasa cha Wahindu kingeshinda uchaguzi na NDOTO za taifa la Kiislamu katika bara ndogo iliyo ndani ya bara kubwa ingefikia ukingoni. Ndio maana rangi nyeupe ikawekwa katika bendera ya nchi yetu. Hivyo tunaomba achapwe viboko, kama akifa wakati wa kuchapwa viboko 10 sawa, vinginevyo na aachiliwe.”

VIBOKO
(Kama mtu akichapwa vizuri ipasavyo basi baada ya kiboko cha 4 au cha 5 hakika anakufa.) Nilichukuliwa sehemu hiyo na nikafungiwa kwenye nguzo. Wakati ule nilimwona Yesu amesimama mbele yangu. Nikafurahi lakini akasema, “Bado hujastahili kunitumikia.” Wakati walipokuwa wakinichapa niliona vipande vya nyama ya mgongo wangu vikiruka hewani , hadi kiboko cha 6 nilikuwa kwenye ufahamu wangu lakini baada ya kiboko cha 6 sikutambua nilipokuwa. Walidhani nilishakufa, nikalazwa hospitalini lakini madaktari wakatangaza nilikuwa hai. Nilipofumbua macho yangu nilijikuta nipo hospitali.

MALI NA SHAMBA DHINI YA NGUVU NA
MAMLAKA YA MBINGUNI
Baada ya kulazwa hospitali kwa majuma 2 nilirudishwa tena mahakamani. Nikajulishwa kwamba mali zangu zote na shamba langu nimenyang’anywa. Waliniambia, “Sasa upo huru lakini hutapewa chochote ila hizo nguo ulizovaa. Unatakiwa kuweka sahihi hapa kwamba hutakuwa na madai yoyote juu ya mali ya wahenga wako.” Nikajibu, “Nitawajibu kesho kwamba nitaweka sahihi au la.” Wakadhani sasa atafikiri juu ya mali ya baba yake na atarudi kwenye Uislamu. Wakati wa usiku nikamwambia Yesu, “Masihi ningeweza nikaweka sahihi zile karatasi wakati uleule lakini hebu niambie, je, niwajibu kwanza halafu niweke sahihi kwenye zile karatasi au unaniruhusu niweke sahihi bila kuwaambia chochote kuhusu wewe?” Sikuwa na ufahamu juu ya Injili na sikuwa nimegusa Biblia katika maisha yangu yote. Masihi akanijibu, “Nenda ukawaambie wakati wanafunzi wangu walipoanza huduma yao mtu mmoja aliona nguvu na mamlaka ya wanafunzi wangu. Akaenda nyumbani akaenda kuleta kiasi cha fedha ili anunue nguvu yangu na mamlaka kwa pesa yake. Mwanafunzi wangu akamwambia ‘Hela yako na ipotelee mbali na wewe.’” Wakati ule sikujua kwamba ule mstari ulikuwa umeandikwa kwenye Biblia, zaidi ya hayo niliiambia mahakama, “Sina chochote cha kufanya na mashamba na mali.” Baada ya kuweka sahihi mlinzi wa gereza akaniambia “Naenda kuvua sare zangu kwa sababu nitakusubiri nje ya gereza nikukaribishe kwangu.” Nikamwambia, “Hii haina haja mheshimiwa, umesema hilo na nimelipokea lakini yupo mmoja nje pale aliyekwisha kuwa tayari kunipokea. Ananisubiri nje ya gereza mmoja aliyefanya mambo yasiyowezekana katika maisha yangu kuwezekana na kuniokoa kutoka katika mauti ambayo yeyote asingeweza. Alifanya katika maisha yangu.”

“NENDA KAHUBIRI”
Baada ya kutoka gerezani nilimkuta tena amesimama nje ili kunikaribisha. Nimemwona mara saba katika maisha yangu. Akaniuliza, “Umechoka?” Nikamjibu, “Hapana Masihi, sasa niko huru, sasa maoni yako juu yangu ni nini?” Akasema, “Hujastahili kunitumikia.” Nikamjibu, “Sawa siku moja nitastahili kukutumikia, wewe shikilia maneno yako na mimi nishikilie maneno yangu.” Nilienda moja kwa moja nyumbani kwangu baada ya kufungua mlango kaka yangu akaja na ubao mkubwa wa kukatia nyama na akanipiga nao kwenye paji la uso wangu. Wakaniambia, “Usithubutu kuja kwenye nyumba hii tena, kwetu sisi wewe umekufa.” Nikaenda hospitali ya serikali karibu na Chandni Chock iliyopo Rawalpindi. Safari hii nilishonwa nyuzi 17 ili kuzuia damu isiendelee kuvuja. Unaweza kuona kovu hili kwenye paji la uso wangu. Baada ya kutibiwa usiku ule nililala kwenye njia ya uchochoro. Nilikaa siku 4 usiku na mchana katika msitu wa Islamabad karibu na msitu wa Bury Imam. Baada ya siku ya 4 Yesu alikuja na nikalalamika, “Masihi angalia kidonda kipya kinachovuja damu usoni mwangu.” Kwa mara ya kwanza maishani mwangu alinyanyua mkono wake akanielekezea na kusema, “Angalia ee Maulana kuanzia leo jina lako ni Lazaro halitakuwa tena Al Haj Maulana Zeid Hussen Mufti, lakini kuanzia sasa na kuendelea jina lako litakuwa Lazaro. Kulikuwa na Lazaro niliyemfufua kutoka kwa wafu baada ya kufa siku 4 na nakufufua wewe kutoka kwa wafu baada ya miaka 36. Nakuamuru uende KUHUBIRI Injili na niko pamoja nawe.” Nikamwuliza, “Masihi hutasema ‘hustahili kunitumikia?’” Kisha akasema, “Hapana nenda na ukaihubiri injili. Hii ni amri yangu kwako na niko pamoja nawe.” Kisha akasema, “Uangalie mwili wako.” Wakati nilipokuwa najitazama mara hiyo hiyo majeraha niliyokuwa naumwa niliyoyapa baada ya kumpokea, nikahisi kwa sekunde majeraha yote yaliponywa. Akaniambia, “Lazaro niombe lolote unalotaka toka kwangu.” Nikamjibu, “Masihi tayari unafahamu ninayohitaji.” Akasema, “Niombe nami nitakupa.” Nikasema, “Yesu nataka uniwekee NENO (kalaam) lako moyoni mwangu ili niweze kwenda kulihubiri neno lako kwa watu wote.” Akasema, “Lazaro, tayari nimeshakupatia, nimekuambia uende na kuhubiri Injili yangu ulimwenguni. Hii ni amri yangu na niko pamoja nawe.”

WAKRISTO WALINIKATAA
Baada ya hili nilienda kwa Wakristo kwa sababu isingewezekana kuhubiri Injili bila kuwa nayo. Nikawaambia Wakristo ushuhuda wangu lakini jibu likawa hili, “Nenda zako ee Maulana, wewe unataka kufa lakini kwanini wewe unataka sisi tufe pamoja nawe?” Nikarudi tena pale kwenye msitu na hii ikawa mara ya mwisho kumwona Yesu ana kwa ana. Hata sasa bado humwona kwani hukutana na mimi. Wakati ninaposikiliza wahubiri wa Mungu, Yesu hukutana nami kupitia neno lake. Wakati mtu fulani anapokuwa anaomba namwona Yesu katika maono yangu. Lakini sijawahi kumwona tena ana kwa ana kama nilivyomwona katika zile mara 7 za awali. Nilikuwa nimekaa juu ya jiwe wakati alipokuja akaniambia, “Lazaro amka na uhubiri Injili yangu.” Nikamwambia, “Masihi hawanikubali mimi na ushuhuda wangu.” Akaniambia “Wewe nenda, kwa sababu kuanzia sasa na kuendelea hutahitaji kuwatafuta wao ndio watakao kuwa wakikutafuta wewe.” Nikamwuliza, “Masihi, nianzie mahubiri yangu Rawalpindi?” Akasema, “Hapana nenda Karachi na uanze pale, kwa sababu nabii hapati kibali nyumbani kwake.”

KWENDA NJIA ZA VICHOCHORO ZA JIJI LA KARACHI
Nilikuja Karachi na kwa miezi 18 nilikuwa nikilala kwenye njia za vichochoro za Saddar karibu na bustani ya Jahangir. Sikuwa na nguo yeyote ya kuvaa. Vazi langu pekee lilikuwa lile nililokuwa nalo tangu nilipotoka Gerezani. Watu walikuwa wakidhani kuwa mimi ni kichaa
Kwa sababu ndevu zangu na nywele zilikuwa ndefu sana na sikuwa na viatu miguuni. Sikuwa na fedha ya kununua chakula nilikuwa nakaa na njaa kwa siku nyingi sana, sikuwa na Biblia. Hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa tayari kunipatia Biblia na sikuwa na uwezo wa kuinunua. Nikaenda kanisani nikachukua Biblia bila hata kumweleza mtu yeyote. Nikatoka nje na kuanza kuisoma. Roho mtakatifu alinisaidia kuielewa Biblia na neno la Mungu lilizungumza na mimi. Siku moja nilikuwa na njaa sana kwa sababu kwa siku 4 nilikuwa sijala kitu. Nikamwomba Mungu, “Leo sifungi tafadhali nipatie kitu nile.” Nikaona mgahawa nikaingia humo nikiomba, “Yesu yakupasa ulipe gharama zote.” Mhudumu akanijia na alikuwa akinitazama kwa kejeli. Nilikuwa naonekana kama ombaomba. Akanikejeli. “Ee mheshimiwa unataka kula nini?” Nikawaza kwa kitambo kidogo Yesu anatakiwa kulipa gharama yote kwa hiyo nikaagiza kuku wa kukaanga kwa binzari ambayo ilikuwa ikigharimu rupia 25 kwa wakati ule.

Wakati nilipokuwa nakula chakula keshia (mpokea fedha) akanijia akiwa ananiogopa sana. Akaniuliza, “Mheshimiwa wewe ni mchawi, Mkuu au Sufi?” Nikasema, “Hapana kwanini unaniuliza hivi?” Akasema, “Wakati nilipokuwa nimekaa kwenye meza yangu ya kupokea hela nilimwona Roho akinijia akanipa rupia 50 na kusema ‘Chukua rupia 25 kwa ajili ya chakula cha yule mtu na kisha umpe rupia nyingine 25 zinazobaki.’” Nikamshukuru Mungu nikachukua rupia 25 nikaenda sokoni. Nikanyoa ndevu zangu, nikakata nywele nikanunua viatu jozi moja na Shalwar Kameez mpya. Tena nikaomba, “Bwana hii ni Karachi kutokea sehemu gani unataka mimi kuanza kuhubiri hapa Karachi?” Akasema “Nenda eneo la Kashmir.” Pale kwenye njia ya miguu nilikutana na mchungaji Akram ambaye anatokea Sahiwal, Bilal Pura. Akaniambia niishi pamoja naye kwenye nyumba yake lakini nikamwambia, “Samahani sipendi kuchukua fadhila ya mtu yeyote, kama nikiruhusu hili leo yawezekana kesho wengi wakasema, ‘tulikuwa sisi tuliomchukua na kumtoa kwenye njia za vichochoro.’” Sasa mchungaji Akram anaishi Sahiwal na unaweza kumuuliza kwa mara ya kwanza ulimkuta wapi mchungaji Lazaro. Nilikuwa nimelala pembeni ya njia ya miguu kwenye mkokoteni wa punda uliokuwa mali ya Mpatheni ambae duka lake la mbao lilikwapo pale. Wakati huo kuhani maarufu wa kanisa maarufu pale Karachi alinijia na kuniuliza, “Umesema umemwona Yesu lakini unalala kwenye mkokoteni wa punda?” Nikamwambia, “Mheshimiwa nenda nyumbani kasome Biblia kwa sababu huduma hii ilianzia kwenye hori la ng’ombe, wakati malango yote yalipokuwa yamefungwa, milango ya hori ilikuwa wazi na kumpokea Kristo.”

SEMINARI YA BIBLIA
Wakati bado naishi kwenye vichochoro nilijiunga naseminari pale Karachi. Profesa Br. Samwel Jutt na mchungaji Samwel Hasrat walikuwa waalimu wangu wa mwanzo kwenye seminari hiyo. Marehemu mchungaji Sohan Lal Paulos aliyekuwa mwasisi wa misheni ya Kipentekoste pale Pakistani alikuwa mhudumu mwenza wa Profesa Samweli Jutt.Kanisa lao wakaliita kanisa la Injili la Ulimwengu katika miaka ya mwishoni mwa muongo ulioanzia 1950. Kanisa hili bado li hai katika Pakistani. Wengi wa watu waliokuwa pamoja na mchungaji Sohan Lal katika siku za mwanzo walimwacha katika siku za mwisho za uhai wake, lakini Profesa Samweli alikuwa nae hadi kifo chake. Namshukuru Mungu kwamba hata katika dunia hii alinipeleka kwa watu kama hawa ambao ni waalimu wa kweli wa Injili. Mwezi oktoba tarehe 13,1995, nilimuoa msichana wa Kikristo mjini Karachi. Tarehe 13 Julai 1996 Mungu akatupatia mtoto wa kike.

FAMILIA YANGU YA KIKRISTO
      Binti wa kaka yangu mkubwa ni Rubani katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Pakistan(PIA). Ni mwanamke maarufu sana kule Pakistani. Nilikuwa nikimpenda sana kwa hiyo nilipokaribia sherehe ya kufunga uchumba nilimwendea na kumwambia. “Binti, hakuna mtu yeyote wa familia yangu anayenitazama, kwahiyo kama ukija kwenye sherehe yangu ya kufunga uchumba nitajisikia kama familia yangu yote imehudhuria.” Akasema, “Umeacha dini ya wahenga wetu na umekuwa kafiri, usidiriki hata kuniita binti yako kwa sababu sikujui. Mimi sio mpwa wako kwa sababu jina la baba yangu ni Maulana Abdul Latif.” Nilikuwa nikishuka ngazi za kiwanja cha ndege cha Karachi nikilia. Nikaomba, “Bwana, baada ya harusi tafadhali nipe mtoto wa kwanza binti ambaye anaweza kukua na kusema jina la baba yangu ni mchungaji Lazaro.” Wakati mke wangu alipojifungua nilienda hospitalini. Kwa vile yule daktari mwanamke aliyajua maisha yangu ya zamani na alikuwa ni rafiki wa karibu wa mke wangu, aliniletea mtoto. Nikamuuliza, “Daktari, ni muda gani binti yangu alipozaliwa?” Akasema, “Sio binti yako ni mwana wako (mtoto wa kiume).” Nikasema, “Hapana ni binti.” Akasema, “Ulikuwepo kwenye chumba cha kujifungulia?” Nikamwambia, “Nilimwomba Mungu na najua amejibu maombi yangu kwa hiyo ni binti yangu wala sio mwana wangu.” Daktari akanikaribia akanikumbatia na kusema, “Mchungaji wewe ni mtu wa Mungu.” Sawasawa na mapenzi ya Mungu nilianza huduma yangu bila kuchukua msaada wowote kutoka kwenye kundi au kanisa lingine. Wengi walinikaribisha nijiunge nao lakini Mwokozi wangu alinitaka nimtumikie binafsi kwa utukufu wake. Nataka kutii amri zake na sio amri za binadamu. Tafadhali iweke huduma yangu, familia yangu na kanisa letu katika maombi yako ya binafsi.
Juni 1999




JIUNGE NA JESHILISILOMWAGA DAMU!
Ushiriki taabu pamoja nami kama askari mwema wa Kristo Yesu.(2 Timotheo 2:3)

WOKOVU? NDIO, YESU KRISTO NI HALISI!
Mpendwa Yesu, nakuja mbele yako pamoja na dhambi zote nilizofanya na ninakuomba unisamehe. Nakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi na siwezi kujiokoa mwenyewe. Tafadhali nisafishe mwili wangu nafsi yangu na roho yangu kwa damu yako ya thamani. Nahitaji msaada wako na nakuomba uje uishi ndani ya moyo wangu. Nataka kukutumikia, kutii amri zako na kufanya yapasayo. Nataka niishi kwa ajili yako kila siku. Tafadhali niongoze na kunilinda kwa Roho wako kwenda kwenye haki. Asante Yesu kwa kunisikia na kunijibu maombi yangu. Amen!
“Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.”
 Mdo 2:21
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipoteee bali awe na”
KUUKANA UISLAMU
Bwana Yesu nakuja kwako nikiamini katika rehema zako. Ninatubu dhambi zangu zote kwa ujinga wangu na uasi dhidi ya ukweli. Nakuomba unikomboe kutoka katika uongo wa kikatili wa Kiislamu. Sasa ninaichukua damu yako ya thamani katika fahamu zangu, mwili wangu na ninaamuru nguvu zote za shetani na nguvu za mapepo zifungwe na kukosa nguvu kabisa katika maisha yangu. Sasa rasmi na hata milele ninakana mahusiano yote na viapo katika dini ya Kiislamu na mtume wake Mohamed.Ninavunja laana zote za uongo, kuabudu sanamu, uchawi wa Kiislamu na laana nyingine nilizoingia kutokana na kujihusisha na Uislamu katika jina la Yesu. Ninaikana Korani na mapepo yote madanganyifu ya kidini yanayoambatana nayo. Nazikana roho zote za hofu, na vitisho vyote vya mambo ambayo mtu anaweza kunifanyia kwa kule kuukana Uislamu na nawaamuru warudi kule kifuani kwa aliyewatuma. Aksante Bwana Yesu kwa kuniweka huru kutoka katika vifungo vya dini. Tafadhali unijaze sasa na Roho Mtakatifu wa utukufu aliye kweli. Nina yaweka maisha yangu wakfu kwa huduma yako. Tafadhali niongoze na kunilinda katika njia ya Uzima wa Milele. Amen

Tunatoa aina nyingi sana za vitabu, vijitabu, vipeperushi, kanda za video na za kaseti zinazofunua na kuthibitisha kuwa mafundisho yale makuu ya Kiislam si ya kweli.  
Masomo kama Jihad, Utumwa,Wanake katika Uislam, Majaliwa ya Muasi, Mwanzo wa Koran, na Maisha binafsi ya Muhammad, mbali ya shuhuda za mageuzi; ni uhakika wa kujibu maswali unyoweza ukawa nayo juu ya Uislam.

Saidia kueneza ukweli kuhusu mafundisho ya mapepo yaitwayo Uislam. Maandiko yote yanatolewa bure ukiagaiza kwenye tovuti yetu.



Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW